South Korea nayo ilitawaliwa, na ni kama rika moja na Tanganyika, lakini imeshaiacha Tanzania mbali sana kimaendeleo!
Singapore ilipata uhuru mwaka 1965 lakini leo hii iko wapi kimaendeleo?
Nimekunukuu au Fanya quoting...
Nimeona umetaja Nchi mbili au mataifa mawili Singapore na Korea ya kusini.
Kura tatu ya Tanganyika wakati wa Nyerere itakupa picha njinsi Ukoloni ulivyokuwa na matabaka ya kutisha.
Mtu mweusi alikuwa tabaka la chini/Mwisho katika Utawala wa kikoloni.
Hivyo ukoloni ndani ya Singapore haukuwa sawa na Africa Black nations, Mtu mweusi alichukuliwa kama mnyama tu., (Brutal Colonialism).
Singapore na South Korea ulizozitaja, mosi zimepiga hatua kipindi Human rights , IMF, World bank na WTO hazina nguvu sana na chupa ya democrasia ilikuwa Bado haija jaa pomoni.
Mfano Lee Kuan yew ambaye huitwa kama baba wa Taifa Singapore aliitwa majina kibao, Kiongozi katili, Asiye penda democrasia, Asiye na utu.. na majina kibao.. Huma rights na wauumini wa democrasia kimataifa walikuwa wanamuundama Kila mahala katika shughuli za kuiletea maendeleo Singapore.
Jambo kubwa jamaa alikuwa smart sana kichwani na Kila hatua... Na alijua njinsi ya kumega tonge na watu wa West.
Na Singapore kwa kutambua yakuwa hawana maliasili/Resources walijikita katika Human capital/skills na Uwekezaji.
Na Singapore ni Taifa dogo sana lenye eneo la kilomita za mraba 735 , Tanzania kilomita za mraba laki 9.4, Tabora kilomita za mraba Elfu 76. Japo udogo sio excuse.
Mwaka Jana, dk Moleli kipindi yupo katika mahojiano ya star tv The big ajenda anasema kwa ucheshii na utani ya kuwa lami Kutoka Dar mpaka kigoma.. nchi kama Singapore unasambaza yote mpaka chooni, bafuni..
Hivyo wengine humuiitaa Lee Kuan Yew -Benevolent dictator.
Ya,benevolent dictator & intelligent anatakiwa kwa nchi maskini ili walau kupiga hatua.
Taifa la Korea ya kusini kipindi linapiga hatua ulikuwa ukikamatwa tu na Jojo kutoka nje ya nchi unafungwa jela au faini ya kutisha.(Kulinda viwanda vichanga vya ndani na kupenda bidhaa za nyumbani)
Hicho ni kipindi ambacho free market policy's, WTO, IMF & World,Human rights zilikuuwa hazina nguvu sana na ushawishi..
Na viongozi wake walikuwa ni watata kweli kweli.. tajiri unaamlishwa, fungua kiwanda Cha simu, Magari.. ukibisha unatishiwa kufilisiwa, walau wanachokuahidi viongozi ni ruzuku.
Mpitie huyu mchumi Ha joon Chang kutoka Korea kusini ambaye baba yake ni moja wapo wa watu waliokuwa katika wizara kipindi Korea kusini inatoka katika umaskini.
Anasimulizi nzuri na fundishii,
Na si lazima ukabaliane na kilajambo alilosema lakini anatoa mwanga Mkubwa kuhusu Korea kusini, Singapore, Japan, china na mataifa yaliyo endelea na yanayoendelea.