Maduka ya Vodacom kuwa wazi kwa masaa 24 kuanzia tarehe 20

Mchakato wa kusajili laini za simu kwa alama za vidole bado ni mgumu sana kwa sababu kadhaa. Moja na kubwa ikiwa ni ya NIDA kushindwa kutoa vitambulisho kwa wakati kulingana na idadi ya watu pamoja na mahitaji na muda uliopangwa. Pamoja na kuwa siku za kukamilisha usajili ziliongezwa, bado kuna changamoto kubwa ya watu ambao bado hawajasajiliwa.

Ukiacha taarifa ya usalama wa pesa za watu watakaofungiwa laini zao - yaani pesa zitakuwa salama kwa miezi mitatu tu na baada ya hapo mmiliki wa laini atatakiwa kufuatilia kwenye kampuni husika - Vodacom pia imekuja na mbinu itakayowezesha mchakato wa kusajili laini kwa alama za vidole uwe wa haraka. Baadala ya kufunga masaa ya kawaida ya kazi, wao watakuwa wazi kuwahudumia wateja kwenye maduka yao kwa masaa 24 hadi tarehe mbili (2) mwezi wa pili. Kazi kwenu.

Yajayo yanafurahisha. Upo tayari!
Tunamsikiliza rais wa wanyonge atakujaje leo.
Ishu ni NIDA ID pia na mtandao wao uko down toka Ijumaa mchana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee seva za nida ni shida.
Lain hazisajiliki.
Pita kwa kijana anayesajili hapo ndo utaelewa


NIDA wameyataka wenyewe, Serikali ichunguze mfumo mzima wa NIDA, kuna mahali walipiga 10% nene inashindwa kufidia gap
 
Ishu ya kusajili laini zenye majina tofauti, ati hadi upate kiapo toka mahakamani!
That's totally awkward!
Na kwanini mitandao mingine hawaku stress huo upuuzi!
Voda tu ndo wamekomalia ile mbaya,
Kusema kweli yawezekana hiyo kitu imefanya walio wengi wakazitupa kando laini tata kama hizo na kusajili laini tofauti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukijiuliza Kwanini Foleni Zimejaa Nida Badala Ya Kwenye Makampuni Ya Simu, Ndipo Utajua Aliyetoa Hili Wazo.................... (jaza nafasi iliyoachwa wazi)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom