Chachasteven
JF-Expert Member
- Jul 4, 2014
- 1,878
- 1,849
Mchakato wa kusajili laini za simu kwa alama za vidole bado ni mgumu sana kwa sababu kadhaa. Moja na kubwa ikiwa ni ya NIDA kushindwa kutoa vitambulisho kwa wakati kulingana na idadi ya watu pamoja na mahitaji na muda uliopangwa. Pamoja na kuwa siku za kukamilisha usajili ziliongezwa, bado kuna changamoto kubwa ya watu ambao bado hawajasajiliwa.
Ukiacha taarifa ya usalama wa pesa za watu watakaofungiwa laini zao - yaani pesa zitakuwa salama kwa miezi mitatu tu na baada ya hapo mmiliki wa laini atatakiwa kufuatilia kwenye kampuni husika - Vodacom pia imekuja na mbinu itakayowezesha mchakato wa kusajili laini kwa alama za vidole uwe wa haraka. Baadala ya kufunga masaa ya kawaida ya kazi, wao watakuwa wazi kuwahudumia wateja kwenye maduka yao kwa masaa 24 hadi tarehe mbili (2) mwezi wa pili. Kazi kwenu.
Yajayo yanafurahisha. Upo tayari!