Mala nyingi watu wanao miliki maduka wanatumia uchawi so kwa kununua kwako chumv kwa Iman za kichaw na kuitaja jina usiku unakua umekiuka mashart so unakua umetegua uvhaw
Yaabda tupate ufafanuzi kwenye hoja ua msingi ambapo ni kwann hii kitu inachange jina kutokana na wakati! Ukiita chumvi usiku inamadhara gani?
Ushirikina tu mkuu, ni imani za kishirikina zinawasumbua watanzania. Zaidi ya 80% ya watanzania wanaamini uchawi na ushirikina, ndip maana kesi za mauaji ya albino,vikongwe hayaishi hata siku moja, tunahitaji karne nyingine kwa watanzania kubadilika.
Nadhani kwa upande wa afrika mashariki na kati na kusini mwa jangwa la sahara Tanzania ndio ina raia wengi wanaoamini uchawi na uganga karne hii ya 21.
Mimi nikajua hio mambo ya chumvi imeisha kumbe bado ipo? Maana miaka ya 90 ndio ilikua maarufu,ukosema chumvi hupewi, ukisema dawa ya mboga unapewa. Ukiomba wembe au sindano usiku hupewi..watanzania hawqjiamini, hawawezi kusimama wenyewe bila uchawi, hawawezi kuanzisha biashara bila uchawi, bila kujali wamesoma au hawajasoma, ni hatari.
Mila ikivunjwa huua ila Dini ikikiukwa haiuwi!!!!!!!!ni leo usiku huu nimeenda dukani nikaulizia chumvi sasa nikajibiwa hakuna nikauliza tena kama chumvi wanayo wakasisitiza kua hakuna , nikaamua kuondoka kwenda duka jingine lakini baada ya hatua kadhaa akaja binti huku anakimbia akiniita kugeuka akaniambia hivi
KAKA USIKU HATUUZAGI CHUMVI TUNAUZA DAWA YA JIKO/DAWA YA CHAKULA
nikarudi kusema naomba dawa ya jiko kama nilivyoambiwa nikapewa kuangalia nikakuta ni chumvi sasa nimeshangaa sana inakuaje bidhaa hii ya chumvi usiku inaitwa kwa jina jingine je ni kawaida au imani za gizani maana sijaelewa nini maana ya kunyimwa chumvi kisa jina nililotumia .
HII NI DESTURI YA WAPI JE IPO HAPA HAPA KINONDONI AU NA KWINGINE NIJUZE! !!!!!
Khaa!!! Siku nyingine jaribu kuulizia ''unga'':glasses-nerdy:ni leo usiku huu nimeenda dukani nikaulizia chumvi sasa nikajibiwa hakuna nikauliza tena kama chumvi wanayo wakasisitiza kua hakuna , nikaamua kuondoka kwenda duka jingine lakini baada ya hatua kadhaa akaja binti huku anakimbia akiniita kugeuka akaniambia hivi
KAKA USIKU HATUUZAGI CHUMVI TUNAUZA DAWA YA JIKO/DAWA YA CHAKULA
nikarudi kusema naomba dawa ya jiko kama nilivyoambiwa nikapewa kuangalia nikakuta ni chumvi sasa nimeshangaa sana inakuaje bidhaa hii ya chumvi usiku inaitwa kwa jina jingine je ni kawaida au imani za gizani maana sijaelewa nini maana ya kunyimwa chumvi kisa jina nililotumia .
HII NI DESTURI YA WAPI JE IPO HAPA HAPA KINONDONI AU NA KWINGINE NIJUZE! !!!!!
Labda hiyo ipo kwenu Tandahimbakinondini dar es salaam
Ataambiwa we TEJA?Khaa!!! Siku nyingine jaribu kuulizia ''unga'':glasses-nerdy:
Binafsi naamini haya ni mambo ya imani za enzi za wazee wetu. Lakini ninaamini hakuna madhara yoyote endapo utatamka Chumvi usiku ukienda kununua kwani mimi nishanunua sana chumvi usiku kwa kutamka hivyo "chumvi".
Hizi ni imani kama zile nyingine, mfano:-
1. Usikae juu ya kinu
2. Mwanaume usile kwenye sufuria - Eti siku ya harusi yako itanyesha mvua
3. Usisimame kizingitini (Mlangoni)
4. Mtoto akivimbiwa eti wanachukua mwiko na kufanya kama vile wanampakua ili kumwondoa katika shida ya kuvimbiwa
Hizi ni imani tu ambazo mimi naziita za ajabu ajabu.