shelumwa
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 516
- 190
Ni leo usiku huu nimeenda dukani nikaulizia chumvi sasa nikajibiwa hakuna nikauliza tena kama chumvi wanayo wakasisitiza kua hakuna, nikaamua kuondoka kwenda duka jingine lakini baada ya hatua kadhaa akaja binti huku anakimbia akiniita kugeuka akaniambia hivi "KAKA USIKU HATUUZAGI CHUMVI TUNAUZA DAWA YA JIKO/DAWA YA CHAKULA".
Nikarudi kusema naomba dawa ya jiko kama nilivyoambiwa nikapewa kuangalia nikakuta ni chumvi sasa nimeshangaa sana inakuaje bidhaa hii ya chumvi usiku inaitwa kwa jina jingine je ni kawaida au imani za gizani maana sijaelewa nini maana ya kunyimwa chumvi kisa jina nililotumia.
HII NI DESTURI YA WAPI? JE, IPO HAPA HAPA KINONDONI AU NA KWINGINE NIJUZE!!