rosemarie
JF-Expert Member
- Mar 22, 2011
- 6,887
- 3,412
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) mkoa wa Kilimanjaro imeingia katika malumbano na Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini, Philemon Ndesamburo.
Malumbano hayo yanatokana na taarifa zilizozagaa kuwa Takukuru wamepelekewa majina ya madiwani watano wa Chadema wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Habari hizo zinadai kuwa madiwani hao wamekuwa wakishinikiza kutolewa kwa vibali vya ujenzi na kuruhusu ujenzi holela na ukarabati wa majengo chakavu ndani ya mji huo.
Hata hivyo Katibu wa mbunge huyo, Basil Lema alipoulizwa jana, alikiri kupewa taarifa ya Takukuru kupelekewa majina lakini anashangaa taasisi hiyo kutochukua hatua.
"Mimi na mheshimiwa Ndesamburo tulikwenda kuonana na kamanda wa Takukuru juu ya jambo hilo ambalo kimsingi linakipaka matope chama bila sababu," alisema Lema.
Lema alisema katika mazungumzo yao, Lema alimkariri Kamanda huyo akikiri kuwa na majina ya madiwani hao na kwamba wanatuhumiwa kushinikiza utoaji wa vibali vya ujenzi.
"Hoja ya Ndesamburo ni kuwa mwenye mamlaka kisheria kutoa vibali ni mkurugenzi kwa hiyo mwisho wa siku kama vipo vibali jambo hilo linarudi kwa mkurugenzi," alisema.
Lema alisema anaongea kwa niaba ya mbunge huyo, alisema kama wapo madiwani wanaotuhumiwa katika kashfa hiyo washtakiwe kama watu binafsi bila kuhusisha chama.
Hata hivyo kamanda wa Takukuru, Lawrence Swema alipohojiwa jana alisema hajawahi kupokea majina ya madiwani hao licha ya kumtaka Ndesamburo ampelekee majina hayo.
Swema alisema tangu Ndesamburo na Lema wafike ofisini kwake na kuwataka walete ushahidi wa majengo yaliyotolewa vibali, hadi jana walikuwa hawajarudi ofisini kwake.
Lema alipoulizwa kwa mara ya pili kuhusu msimamo huo wa Takukuru, alisema wao hawakwenda kupeleka majina bali kupata ufafanuzi wa kuwapo kwa majina hayo.
CHANZO: Mwananchi