Madiwani waliofukuzwa kwa nini watetewe na serikali?

Wanatetewa na serikali kwa sababu haipendi kuona mtu anaonewa kwa sababu ya unyonge wake, udhaifu nk. Kitendo cha madiwani hao kufukuzwa uanachama ni kitendo cha udikteta, uonevu na udhalilishaji mkubwa sana.

mkuu ndio sababu ilyowafanya nanyi msiwafukuze mafisadi kama mlivoaanza kutaka kuaminisha umma? Ndio sababu ya kulindana kwingi kunakoonekana ndani ya ccm kwa watendaji wabovu wanaojibainisha kila uchao?
 
Hivi mnategemea mahakama iwatalazimishe Chadema kurudisha uanachama wao never hata wao madiwani wanalijua hilo sijui kwa nini walikata rufaa kwenye Baraza la chama huku wamefungua kesi mahakamani.


wanataka udiwani wao hawataki kusikia kitu inaitwa Chadema!
 
Hizo ni siasa za mabavu na uoga wa serikali inayoongozwa na CCM, amna uhalali wa madiwani hao kuendelea kuwakilisha katika vikao
bila ya kuwa na udhamini wa chama, sheria ya kipengele hicho kinaeleweka wazi.

Kama wanataka kuendelea na udiwani kwa nini wasijiunge na CCM halafu waingie katika kinyang'anyiro? Hii inatia hofu na haiingii akilini kwa nini wawe wanang'ang'ania, hapo kuna ubadhilifu wa mali za wananchi wa Arusha.

Na hao madiwani inaonyesha wazi kama walikula rushwa kutoka ccm. Na hao si viongozi makini ni wenye tamaa ya utajiri wa haraka haraka na kuwakandamiza wananchi wa Arusha. Je sasa hivi wanamuwakilisha nani katika halmashauri ya Arusha.
 
Katika hili.......CDM imeshikwa pabaya.....Hadi rahaaa!!!..Hali hii inadhihirisha wazi ukomo wa uwezo wa kufikiri wa viongozi wake katika kushughulikia mambo ya kawaida kama issue hii ya madiwani. Sasa inabidi kuvutana mahakamani na madiwani wenu wenyewe kabla hamjafikiria upuuzi mlioanzisha wa kumpinga Meya.

Ushauri wa bure: jipangeni upya kwa uchaguzi wa Meya wa 2016. Kwa sasa inaonekana mmeingia cha kike.

Angalizo: mkijifanya kuleta ya kuleta baada ya kile mnachokiita siku 30.....kuweni tayari kwa matokeao ya mtakachokianzisha......100% itakula kwenu.
 
Leo nimesikia kwenye mapitio ya magazeti asbhi kuwa serikali inatambua madiwani waliofukuzwa na CHADEMA kuendelea na vikao mpaka mahakama itakapoamua.

Wadau hii imekaaje.
Wacha waendelee kukumbatia ujinga wananchi wa Tanzania ya sasa si wajinga, utafika muda watawahukumu na wao kama CDM ILIVYO WATOSA MADIWANI hao!!!!!!!!!!!!!!
 
Mimi nimemuelewa Dr. Slaa kwa maelezo alotoa. Kama mwanachama wa chadema, naamini kilichofanyika ni sahihi ndani ya chama. Nawaona wazee wa kutapatapa humu. Huwezi kujifannya mjuaji wa mambo ya CCM wakati ww ni CHADEMA, and vise versa is true.

So, CHADEMA haters, nyamazeni tu, mnajitia aibu.
Kamfundisheni wasira jinsi ya kujadili hoja, naona akili yake ipo kwenye masaburi, kichwani kuna mchanga wa baharini.
 
Wanatetewa na serikali kwa sababu haipendi kuona mtu anaonewa kwa sababu ya unyonge wake, udhaifu nk. Kitendo cha madiwani hao kufukuzwa uanachama ni kitendo cha udikteta, uonevu na udhalilishaji mkubwa sana.
Kuna watu mna maneno ya kuudhi sana. CCM ndio mwamuzi kuwa watu wanaonewa? Mbona CCM wanajivua magamba na hata wameshindwa kuwafukuza watu kuna watu wanawaingilia? Mbona CCM il;ishawafukuza watu wengi akina maalim Seif, Ndobo nk kuna mtu aliwaingilia? Kama walivyosema wengine hii ni kuingilia uhuru wa mahakama. Ni mahakama pekee ingeweza kutoa order kama hiyo si CCM. Kwa kweli nimeamini hao madiwani walihongwa.
 
Kwa maana nyingine baada ya CCM kushindwa kujivua gamba wameona Chadema wamepata credit kwa kuchukua maamuzi magumu sasa wanataka kuwakwamisha.
 
And this is the point. Kwa kifupi ni kuwa uamuzi wa kamati kuu ya CDM umepingwa mahakamani, na mahakama ikausitisha. Kama wangekata rufaa kwa kufuata ngazi za chama basi uamuzi huo ungeendelea.

Shida ni kuwa pale ambapo chombo cha juu cha chama kingeamua kubatilisha maamuzi wa kamati kuu, walalamikaji wangekuwa wameathirika tayari.

Wanakuwa hawana udiwani. Ndo maana wakakimbilia mahakamani.
Naomba nieleweke kuwa siwatetei madiwani hao, ila naelezea hali yenyewe.
Nafikiri huelewi mambo yanavyokwenda. Kama ni kuendelea na kazi hiyo order ilpaswa kufanywa na mahakama si serikali. Je, kwa mfano Lowassa akifukuzwa akiamua kwenda mahakamani, serikali itasema aendelee na ubunge? Mahakama pekee ndio ina uwezo na hapa waziri ameingilia uhuru wa mahakama
 
Kwa kuwa suala liko mahakamani, mi naona tusubirie tu maana suala la serikali wala la cdm tena
 
Kwa kuwa suala liko mahakamani, mi naona tusubirie tu maana suala la serikali wala la cdm tena
Kama hiyo ndio kauli yako, huoni waziri ametoa amri baada ya swala kwenda mahakamani? CCM wanapenda kusema swala likiwa mahakamani lisifanyiwe kazi. Mbona waziri ametoa amri wakati anajua swala lipo mahakamani?
 
Hivi serikali ya ccm inafaidika na nini kuhusu muafaka wa madiwani? Kwanini wakomae hivyo wakati madiwani wamevuliwa uanachama?
 
Leo nimesikia kwenye mapitio ya magazeti asbhi kuwa serikali inatambua madiwani waliofukuzwa na CHADEMA kuendelea na vikao mpaka mahakama itakapoamua.

Wadau hii imekaaje.
.

Hivi hii serikali ya Jakaya Kiwete inatupeleka wapi? Kwa hili MKUCHIKA AMECHEMSHA.Yale yale ya Jairo! Kesi ya msingi ya hawa madiwani waasi waliotimuliwa CHADEMA wanadai mahakama iwalazimishe CHADEMA WARUDISHIWE UANACHAMA ILI WAENDELEE NA NYADHIFA ZAO ZA UDIWANI.

Hapa MKUCHIKA ameingilia UHURU wa MAHAKAMA maana Mahakama bado HAIJATOA RULING!!! Hawa ndiyo Mawaziri wa Serikali ya Kiwete.
Hii ni serikali yenye kujichanganya kila siku, Kila Waziri akiibuka na lake. Ni mkanganyiko bin mseto!

Kama UDIWANI na UBUNGE mtu anachaguliwa kwa tiketi ya chama husika iweje leo mtu KAFUKUZWA UANACHAMA Waziri analazimisha diwani aendelee na kazi? Atakuwa anawakilisha SERA ZA CHAMA GANI WAKATI CHAMA KIMESHAMFUKUZA?

Serikali hii hii ya Chama Cha Magamba inasema HAITAKI kusikia WAGOMBEA BINAFSI IWEJE LEO IWATETEE WATU WASIO NA CHAMA???
Je, tukisema kuwa hawa madiwani waliofukuzwa CHADEMA ni mamluki wa CCM tutakuwa tumekosea?

Haiwezekani Serikali ya CHADEMA iwabebe hawa madiwani bure bure tu lazima kuna MKONO WA CCM hapa. Nawaomba viongozi wa CHADEMA watoe tamko kuhusu Mkuchika kuwarudisha madiwani kazini wakAti hawana CHAMA.
 
mimi ninaombi moja kwa walioko arusha kuwa tuendelee kuwazomea wote pamoja na meya fake wakati huu tukisubiri siku 30 ziishe..
 
Kwa hiyo kama haijatoa rulling hawa wanaendelea kuwa madiwani au sio madiwani? wanasheria wa Tumaini university na RUCO taabu kweli kweli.
Kama hulijui jambo kaa kimya. Mtu mjinga anayedhani anajua ni hatari sana. Kwa kukuelewesha tu kama unataka kuelewa, mtu ukifukuzwa uanachama unapoteza ubunge, urais au udiwani. Kwa hiyo wale si madiwani tena maana hawana chama. Sasa mahakama pekee ndio yenye uwezo wa kutoa zuio la muda. Sasa kama hutaki kuelewa ni sawa ila sasa kutukana watu haijengi. kwani Tumaini na RUCo kuna nini hadi unawadharau? Chuo ambacho kina vilaza ni UDOM tu ila pia si wote kuna baadhi ya wanafunzi wazuri sana UDOM.
 
...........................Katika mambo yanayonitia hasira ni hili pia,hii ni nini? Mwanachama anafukuzwa uanachama na vikao halali vya chama na matatizo yaliyowazi and then anakumbatiwa na watu wachache wanaotaka kulinda maslahi yao binafsi...msije shangaa hiyo kesi iliyopo mahakamani ikachukua miaka minne mpk uchaguzi ujao....watanzania ni wakt wa kuamuka,kuna dalili za wazi kuwatetea hawa majambazi.....CDM tunaomba maandamano mengine pale Arusha kupinga hawa madiwani kurudishwa kwa mgongo wa mahakama wakt ni njama za CHAMA CHA MAJAMBAZI/MAFISADI/MAFIRAHUNI/MAGAMBA(CCM)..............CDM tunaomba maandamano ya haraka na wananchi wa kata husika wapewe nafasi kusema yaliyo moyoni....huu ni ujambazi wa haki na maamuzi halali ya chama....kweli inatia hasira sana tena sana............
 
Back
Top Bottom