Madirisha ya aluminium yanaruhusu mbu

Habari ndugu zangu.

Mimi nina jambo dogo, madirisha ya alminium, yanayo-slide yana upenyo naona kwenye nyumba yangu yenye wavu wa mbu kwenye madirisha mbu wanapita! Hizi reli zinaacha nafasi.

Hivi tatizo hili wengine mnalo? Au mmelizuiaje? Au mnalikabilije? Nisaidieni jamani.
Fundi wako mbovu. Kama fundi mzuri hayapitishi mbu. Tatizo siku hizi kila mtu ni fundi wa madirisha ya aluminium.
 
Hilo tatizo hata mie linanikumba sana inabidi at least kila baada ya siku mbili kupuliza dawa. Kudhibiti hiyo hali lazima usifungue kabisa vioo jambo ambalo haliwezekani kwakweli. Hapo dawa mjitahidi ikifika saa 12 madirisha yafungwe then washa AC pakipoa unaizima ikikaribia muda wa kulala unawasha tena unaizima baada ya muda then mnakula fan tu.
Tatizo mafundi wenu. Mimi dirisha la chumbani kwangu linakaa wazi muda wote na hakuna mbu anaingia.
 
Habari ndugu zangu.

Mimi nina jambo dogo, madirisha ya alminium, yanayo-slide yana upenyo naona kwenye nyumba yangu yenye wavu wa mbu kwenye madirisha mbu wanapita! Hizi reli zinaacha nafasi.

Hivi tatizo hili wengine mnalo? Au mmelizuiaje? Au mnalikabilije? Nisaidieni jamani.
Ni kweli lakini si aluminum zote.. King furnishing alluminium ndio zina hili tatizo kutokana na wembamba wake
 
Nenda kwenye maduka yanayuoza vifaa vya madirisha hayo ununue mipira maalum ambayo hubandikwa pembeni ya fremu ya wavu, mimi bibafsi nimefanya hivyo japo si maduka yote wanauza mipira hiyo, nakushauri uende Gerezani Dar es Salaam.

Kwa hiyo unatuagiza kwenda Gerezani as if wote tunaishi Dar! Kwani mbu wapo Dar peke yake? Na Je, aliyeleta huu uzi amekuambia anaishi Dar? Hili ni jibu fake kabisa!
 
Balaa mzee, hapo funga neti za kuzuia mbu tu then wakati wa kulala unajitandazia unapiga mbonji kama feni ni kitu unatumia then unawasha kwa burudani

Unaweza kuwasha feni Njombe? Mbu wapo hapa Njombe lakini njoo uwashe feni au ac huku ukione cha mtemakuni!
 
Fundi wako mbovu. Kama fundi mzuri hayapitishi mbu. Tatizo siku hizi kila mtu ni fundi wa madirisha ya aluminium.

Weka madirisha ya mbao, kwa nini upate shida yote hiyo wakati madirisha ya mbao ndiyo urithi wetu!
 
Weka madirisha ya mbao, kwa nini upate shida yote hiyo wakati madirisha ya mbao ndiyo urithi wetu
Madirisha ya mbao kwa sasa yana gharama zaidi nadhani, watu wanatumia alminium kupunguza gharama ya ujenzi.
 
Kwangu niliweka ducktape ndio angalau ila sasa siwez kufunga dirisha hasa ikija mvua
 
Kwani mbu wanazuiwa na aina ya madrisha kwamba ukiweka hayo ya kisasa ndo mbu hawaingii ndani ya jengo lako! Suluhuya adha hiyo ni hakikisha chamber za Maji taka zote hazina upenyo wa mbu kufanya mazalia karibu na mji wako, pia uwe na utaratibu wa kuspray kuta madawa ya kuzuia wadudu kama mbu, nzi, mende, kunguni, utaishi kwa amani sana ukiwa na fumigation ya Mara kwa Mara kwenye kuta za nje zote yaani wadudu hutowasikia kwamwe.
Aisee ni dawa ipi hiyo yakupulizia nje kwenye ukuta
 
Habari ndugu zangu.

Mimi nina jambo dogo, madirisha ya alminium, yanayo-slide yana upenyo naona kwenye nyumba yangu yenye wavu wa mbu kwenye madirisha mbu wanapita! Hizi reli zinaacha nafasi.

Hivi tatizo hili wengine mnalo? Au mmelizuiaje? Au mnalikabilije? Nisaidieni jamani.
Mkuu hilo dirisha lako lipo safi tu.

Hayo madirisha hayazuii mbu btw.

Mbu ni kiumbe wa ajabu sana, anaruka na kutambaa pia.

Chunguza kwenye taa zilizo sealed, mfano wa security lights ama tube lights, mbu anapenya ndani, hadi unakuta wamekaukiana na kuwa kama pumba nyepesi kwa maelfu!

Ukibaki kujiuliza mfuniko wa taa umegandamizwa kwenye gipsum na kukandikwa, lakini yumo ndani kapenya!
Cha msingi ni kutumia Mosquito net kitandani ama kuwapulizia.
 
Back
Top Bottom