Ukubwa wa madirisha ya nyumba

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,102
3,615
Wataalamu wa ujenzi, ni ukubwa gani wa dirisha unatosha kiafya achilia mbali suala la mwonekano wa nyumba.

Nimejaribu kuzitazama nyumba za Sudan Khartoum kutokana na hii vita, nimeona nyumba zao nyingi hadi maghorofa yana madirisha madogo madogo. Je, hii imesababishwa na nini kitaalamu wadau wa ujenzi?

Binafsi naunga mkono kwenye mikoa ambayo haina joto, kuweka dirisha dogo tu mfano upana futi nne, au inakuwaje wadau wa ujenzi?

Kwa maoni yangu, kuna faida za kuweka dirisha dogo kwani utasevu gharama za aluminium na grili! Huu ni mwaka wa tatu nimeshindwa kuweka aluminium kwa sababu madirisha ya nyumba yangu ni futi tano kwa tano, sebuleni ni futi sita.

Nilipotembelea kwa jamaa, nikakuta nyumba yake ina madirisha ya futi sita kaweka na aluminium ila hata hayafunguliwi yote, yaani yamefungwa tu anasema upepo na vumbi. Sasa kama hayafunguliwi, nini umuhimu wa madirisha makubwa?

Inabidi Watanzania tuache kufanya mambo kama utaratibu, bali tuwe tuna hoji sababu za kufanya hivyo.

Picha hapo chini ni nyumba za Khartoum Sudan na madirisha madogo na machache!

images%20(2).jpg
 
Ukubwa au udogo wa madirisha unategemea hali ya hewa, ukubwa wa nyumba na aina ya vioo/louvers au pannel unazotaka kuweka.

Kwa vile kazi ya madirisha ni kuleta hewa ya kutosha na mwanga wa kutosha, lakini pia madirisha huoendezesha nyumba, hasa yakiwa na uwiano mzuri na nyumba.

Hivyo basi, standard zinategemea na hivyo vitu. Ki-daslam 5x5ft, 5x6ft, 6x6ft, 4x6ft kutegemeana na ukubwa wa chumba.
 
Umepiga picha nyumba ya Khartoum ila ukashindwa kupiga nyumba yako wala ya huyo unayeita jamaa yako, umekusudia tujadili nini…. au tuchukue tu hilo hitimisho lako?
Hoja ni dirisha dogo au kubwa! Halafu nilikuwa nawauliza wale wenye exposure ya kusafiri hizo nchi au mainjinia ni kwa nini hapo Khartoum wanaweka madirisha madogo madogo!

Kupitia madirisha ya hapo Khartoum nimekumbuka nyumba za zamani huku bongo na pia nimejifunza hakuna haja ya kuhangaika na madirisha makubwa kama sehemu haina joto.


Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Hoja ni dirisha dogo au kubwa! Halafu nilikuwa nawauliza wale wenye exposure ya kusafiri hizo nchi au mainjinia ni kwa nini hapo Khartoum wanaweka madirisha madogo madogo!

Kupitia madirisha ya hapo Khartoum nimekumbuka nyumba za zamani huku bongo na pia nimejifunza hakuna haja ya kuhangaika na madirisha makubwa kama sehemu haina joto.


Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Basi usiweke dirisha kabisa. Mbona zile full suti zile za wachaga hazikuwa na dirisha na waliishi vizuri tu humo ndani pamoja na ngombe, mbuzi na kuku
 
Jamaa anataka mtazamo wake uwe wa wote, itakuwa ameshaweka madirisha aina fulani anatafuta faraja ya kuungwa mkono.
Madirisha yangu ni makubwa ila kwa sasa ndio najiuliza, mbona nimeingia gharama za grili bila sababu za msingi kwa sababu eneo naloishi hakuna joto. Pia, kila nikipiga hesabu za aluminium naona kabisa ningesevu pesa endapo madirisha yangekuwa ni madogo.

Yote kwa yote nilileta hii hoja ya udogo wa madirisha ya Khartoum Sudan ili kuchangamsha jukwaa lakini naona mambo yamekuwa mengi.

Sasa natoa majibu mwenyewe ambayo sijayafanyia utafiti, ni hisia tu.

1.Nchi hasa za jangwani hupendelea kujenga nyumba na kuweka madirisha madogo madogo kwa sababu ya kukwepa upepo mana eneo linakuwa ni plain. Rejea nyumba za Dodoma vijijini, madirisha madogo madogo.

2. Wanaweka madirisha madogo kwa ajili ya kuokoa gharama za matirial ya gril na vioo.



Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Matundu ya kufunga dirisha za aluminum huwa yanaweza fungwa nyavu kwa muda baada ya kuweka grills.

Sio lazima uweke aluminum papo hapo. Lile tundu gharamikia kuweka grills halafu weka sasa nyavu.
 
Toa neno wachaga hapo.
Wachaga nyumba zao zimejengwa kwa nyasi kuanzia juu mpaka chini, na ina kamlango kamoja tu. Huko ndani wanalala baba, mama, watoto, mbuzi, ngombe na kuku. Juu kuna dari ya kuivishia ndizi. Au nasema uongo mangi?
 
Wengi huwa hatutafiti mazingira na hali ya hewa kabla ya kujenga! Mfano: Kuna tiles ukijengea kwenye baridi hiyo nyumba utahama, zinaongeza baridi kweli kweli!!! Zinafaa kwenye joto tu!!

Kuna nyumba niliikuta mkoa X (mmiliki yumo humu asijefungua code akajisikia vibaya), kuna baridi akaijenga kama za DSM. Ndefu juu, madirisha makubwa na tiles zisizofaa kwenye baridi!!

Nyumba ilikuwa ukiingia asubuhi au jioni ni kama friji daaaah!! Mpaka tulipomshauri abadilishe tiles na aweke zulia! Alishaanza kuumwa visigino na watoto kila siku hospitali kwa nimonia!!

Madirisha nayo yalikuwa makubwa yanachochea baridi kweli kweli!! Utafiti ni muhimu sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom