Madini adimu duniani tunawapa wageni na kuishia kupata 16%

Kama hatuna Teknolojia, Kuna uharaka gani wa kuyachimba?
Kama wazee wetu wangekuwa na haraka hiyo, sisi tungeyakuta?
Acheni ubinafsi.
Wafikirieni watoto wenu na wajukuu zenu pia.
Acheni kufikiri kwa kutumia matumbo yenu.
Yaani tukose 16% ya pesa yote itakayopatikana hapo Leo kugonja sijui lini!?..wa Leo hatustahiki maisha mazuri!?.. unadhani shida ya kuchimba ni teknolojia tu!?..mtaji babu!!,ikipatikana Dola $100b sisi tunapata $16b,tunakuwa wapi kwenye kujitegemea kibajeti!?
 
Ujasiri wa kuilinganisha China na Tanzania unautoa wapi?
Kwahiyo kwa akili yako ilitakiwa Tanzania kusiwepo wawekezaji kabisa?? Eti tusubirie until when maisha hayakai hapo kukusubiri.

China ana siasa za kijamaa ambazo ndo siasa ambazo Tanzania ana mizizi nazo sasa kama mjamaa China amemkaribisha beberu US wewe ni nani hata uzuie uwekezaji Tanzania?
 
Nchi inatawaliwa na Wazanzibar unategemea nini? Hata mimi ningekuwa Mzanzibar natawala Tananganyika ningeuza tu kwa kubadilishana na matundu ya vyoo.........................Who cares?
Hizi ni kauli za kibaguzi sana lini waliwavamia hao wa zanzibar?
 
hahahahaha bado vichwa maji tu.

wakati tulipaswa kufanya survey wenyewe kujua deposit ikoje for 100yrs then tutafute watalaam kadhaa wadesign michoro rahisi, tuanze kuchimba in small scale na small plant yakurefine na tujenge kiwanda cha kutengeneza final product hapo hapo mbeya hata kwa matumizi ya ndani na nchi jirani kama Mbeya.

Huku tukichimba in small scale huku tunajipa say 20yrs yakutafuta large capital na kuingia sasa kwenye large scale production with big refine plant na viwanda kadha wa kadha vijengwe hapo depending hiyo raw materials kutoka hapo.. means in 100yrs next generation will enjoy the life na kushukuru babu zao..
CCM wafikirie miaka 20 ijayo? Haaahaaaa Hilo haliwezekani. Wao wanajali kinachopatikana sahivi wale wakimalize hayo ya kufikiria future alikufa nayo Nyerere.
 
Kuna wapuuzi wana walaumu waking lisu ati hawalipiganii taifa wanaacha kuwalaaumu wezi wenzao. Hawa ndiyo ccm bhana wao nyeupe ni nyeusi
Ache tupigwe tu kwasababu tumeweka akili zetu mifukoni.
 
Ndgu kuchimba madini si mchezo mdogo kuna mambo mengi mno:-
  • Technology
  • Mtaji
  • Manpower
  • Resorces
Kama nchi mnaweza kuwekeza Tshs Trilion 4 na madini yasitoke hata kilo moja. Cha msingi wacha tupate hiyo 16% inatosha.
 
Umiliki 16%
Mapato 20%
JUMLA 36%
KATIKA 100% Muwekezaji anabaki na 64%
Kuna malipo mengine atayafanya kama - Service levy %
- CSR %
MIMI NINACHOONA NI KAMA MUWEKEZAJI ATABAKIWA NA 50%
Lkn kuna faida zingine tutakazopata zaidi ya izo kama
  • Ajira
  • Malipo ya kutumia bandari ili kuutoa mzigo Nchini
  • Kuchangamka kwa Uchumi na mengineyo kama nimeyasahau.

Upande wangu nadhani ambae anahisi tumepigwa basi awe na hoja iliyoshiba ... kama alete mkataba wa aina hiyo ambao Nchi ingine imeingia na kupata zaidi ya sisi... sio kama mleta mada aliyewasilisha Malalamiko pasipo kua na Msingi wa kunyonywa huko kupitia uzoefu wake..... Kufananisha Tanzania na China sio sawa maana wao wanakazi nayo hayo madini na uwezo wa kuchimba wanao kwao ni heri wauze final product.... vipi kuhusu akina sie

Kwangu naona ni fea tu kupitia mgawanyo ninaouna kihesabu.... anayeona sio sawa aseme alitaka iweje sio kubeza tu na kumbe Tiba za kulikomboa taifa mnazo
 
Mkapa mtanganyika aliweka 3% kwenye madini
Ujinga ni ujinga tu haijalishi umefanywa na nani.
Binafsi kwenye suala la ukanda, udini, ukabila, jinsia n.k, huwa siviungi mkono kabisa.
Kama mtu kafanya vizuri anastahili pongezi.
Kama kazingua, lazima tumkosoe iwe kwa busara au kwa vyovyote, ilmradi ajue kazingua!
 
Ndgu kuchimba madini si mchezo mdogo kuna mambo mengi mno:-
  • Technology
  • Mtaji
  • Manpower
  • Resorces
Kama nchi mnaweza kuwekeza Tshs Trilion 4 na madini yasitoke hata kilo moja. Cha msingi wacha tupate hiyo 16% inatosha.
Botswana waliwezaje?
Maana tukienda South Africa, utasema ooh, huko kuna Makabulu!
 
Kwahiyo kwa akili yako ilitakiwa Tanzania kusiwepo wawekezaji kabisa?? Eti tusubirie until when maisha hayakai hapo kukusubiri.

China ana siasa za kijamaa ambazo ndo siasa ambazo Tanzania ana mizizi nazo sasa kama mjamaa China amemkaribisha beberu US wewe ni nani hata uzuie uwekezaji Tanzania?
Nafikiri shida siyo wawekezaji, shida ni aina ya viongozi tulio nao. Wengi wako pale kwa maslahi yao binafsi na wala siyo kwa maslahi ya nchi.
 
Unaweza kuwa una maoni mazuri Mkuu, lakini umewahi kufikiri hizo gharama za Uchimbaji Serikali itapata wapi iwapo ikiamua yenyewe kuchimba?

Serikali hii hii ambayo nusu ya Bajeti yake inategemea Wafadhiri.

Serikali hii hii ambayo bado nusu ya Wilaya zake hazina Huduma ya maji safi na salama.

Serikali hii hii ambayo zaidi ya nusu ya wilaya zake hazina barabara za Lami

Serikali hii hii ambayo bado inatafuta rasilimali fedha ili kuweza kufikisha Umeme kwenye Kila Kijiji kabla ya 2025.

Kwa kifupi Serikali yetu bado ina kazi kubwa zinazohitaji Rasilimali fedha kuweza kufikisha huduma za Maji, Barabara, Afya, Elimu n.k

Hivyo ni muhimu Wapatikane Wawekezaji wenye Mitaji waje wachimbe alafu Sisi kama Nchi tukusanye Kodi, Ajira kwa Watanzania wenzetu pamoja na kupata Mirahaba kupitia Win-Win Contracts.

Kwahiyo nadhani sisi kama Nchi tuhakikishe Mikataba tunayosaini dhidi ya Wawekezaji hawa inainufaisha Nchi badala ya kugeuka Mikataba ya Kinyonyaji dhidi yetu.
Umesikiliza huyo dada kwenye clip anavyosema?
Kimsingi yeye anaona kama tunaendeleza yale yale ya chifu Mangungo.. tunatoa vitu vya thamani kubwa almost bure!
".....us$667 million for three mines is a joke when one of these mines will make billions and billions of dollars per year...!"
 
Nafikiri shida siyo wawekezaji, shida ni aina ya viongozi tulio nao. Wengi wako pale kwa maslahi yao binafsi na wala siyo kwa maslahi ya nchi.
Unafikiri au sio? Ni vipi unaweza kutuhakikishia mafikirio yako?
 
Unafikiri au sio? Ni vipi unaweza kutuhakikishia mafikirio yako?
Kwani huoni mambo yanavyoendelea?
Au na wewe ni mojawapo ya walamba asali?
Hivi kwa wingi wa madini ya almasi dhahabu, chuma, makaa ya mawe, ulanga, Tanzanite, chumvi, n.k, tulipaswa kuwa bado tunategemea fedha za kukopa kujenga madarasa?
Tungekuwa bado tunatembeza bakuli ili tupate fedha za kuchimba matundu ya vyoo?
N.k
 
Kwani huoni mambo yanavyoendelea?
Au na wewe ni mojawapo ya walamba asali?
Hivi kwa wingi wa madini ya almasi dhahabu, chuma, makaa ya mawe, ulanga, Tanzanite, chumvi, n.k, tulipaswa kuwa bado tunategemea fedha za kukopa kujenga madarasa?
Tungekuwa bado tunatembeza bakuli ili tupate fedha za kuchimba matundu ya vyoo?
N.k
Marekani anakopa pia, unalijua hilo?
 
Back
Top Bottom