Madini adimu duniani tunawapa wageni na kuishia kupata 16%

Michael Uledi

Senior Member
Mar 29, 2023
132
322
Unaambiwa yale madini ya pale Ngwala-Songwe ni moja ya madini adhimu sana duniani na matumizi yake ndio yanaenda kutawala kwenye miaka 50 ijayo duniani (Rare Earth Minerals au Strategic & Critical Minerals).

Ukitaka kupima vision ya Taifa letu unaweza ukaona jinsi gani hata madini ya namna hiyo tunawapa wawekezaji kwa mchanganuo wa 16% kama dhahabu ambayo tunayo almost kila kona ya Nchi!

Madini haya yangegundulika nchi serious kama China then Mmarekani au Mjapani aende na uwekezaji wake hata wa dola zote duniani hawezi kupewa! Common!

Hii ngoma tunataka tuupeleke wapi (hii NCHI tunataka iweje by mwaka let say 2050)? Do we have that vision?

Hivi tunataka tutengeneze Taifa la namna gani na lini?Je, tunajihoji maswali haya tukiwa kitandani, ofisini au nyumbani?

Mbombo ngafu!

"Wiki hii serikali ya Tanzania ilisaini mkataba na makampuni matatu ya Australia kwa thamani ya dola milioni 667. Kwahiyo makampuni ya Australia yana haki za uchimbaji wa madini kwenye migodi matatu nchini Tanzania kwa lengo la kuchimba madini adimu ya ardhi na grafiti.

"Madini haya ni muhimu sana katika maendeleo ya teknolojia, mfano teknolojia za umeme, betri, magari, simu za mkononi, kompyuta mpakato (laptops) na grafiti inajulikana kutumika katika upakaji hasi wa betri ya lithiamu ion.

"Hii inaonyesha jinsi kampuni za kigeni zinavyowekeza Afrika na kutajirika maradufu kutoka kwenye rasilimali na madini ya Afrika. Dola milioni 667 kwa ajili ya migodi mitatu ni upuuzi. Wakati mgodi mmojawapo utatengeneza mabilioni na mabilioni ya dola."
=====

Nakili kiunganishi

Madini hayo ya kipekee yamepatikana katika maeneo ya Chilalo Wilayani Lindi, Epanko Wilayani Ulanga, na Nguala Wilayani Songwe. Makubaliano hayo ni sehemu ya mkakati wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wa kuimarisha mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa taifa hilo kwa angalau asilimia 10 kufikia mwaka 2025.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa timu ya majadiliano ya Tanzania Palamagamba Kabudi, nchi hiyo itanufaika na asilimia 16 katika kila mradi. Mataifa ya Magharibi yanajaribu kupunguza utegemezi wao kwa China katika madini ya Kinywe na adimu.

Madini hayo ni muhimu katika vifaa vya elektroniki kama vile simu za kisasa, kompyuta na betri pamoja na teknolojia ya kisasa ambayo inaweza kupunguza utegemezi wa nishati ya mafuta.

DW
 
hahahahaha bado vichwa maji tu.

wakati tulipaswa kufanya survey wenyewe kujua deposit ikoje for 100yrs then tutafute watalaam kadhaa wadesign michoro rahisi, tuanze kuchimba in small scale na small plant yakurefine na tujenge kiwanda cha kutengeneza final product hapo hapo mbeya hata kwa matumizi ya ndani na nchi jirani kama Mbeya.

Huku tukichimba in small scale huku tunajipa say 20yrs yakutafuta large capital na kuingia sasa kwenye large scale production with big refine plant na viwanda kadha wa kadha vijengwe hapo depending hiyo raw materials kutoka hapo.. means in 100yrs next generation will enjoy the life na kushukuru babu zao..
 
Yaani hii akili waitoe wapi kwa mfano
 
Tuwe tu wakweli madini sisi tutayafanyia nini? Yakae tu chini ya ardhi au tuyauze tupate fedha za kigeni? Maana hata kuchimba wenyewe hatuwezi
 
hahahahaha bado vichwa maji tu.

wakati tulipaswa kufanya survey wenyewe kujua deposit ikoje for 100yrs then tutafute watalaam kadhaa wadesign michoro rahisi, tuanze kuchimba in small scale na small plant yakurefine na tujenge kiwanda cha kutengeneza final product hapo hapo mbeya hata kwa matumizi ya ndani na nchi jirani kama Mbeya.

Huku tukichimba in small scale huku tunajipa say 20yrs yakutafuta large capital na kuingia sasa kwenye large scale production with big refine plant na viwanda kadha wa kadha vijengwe hapo depending hiyo raw materials kutoka hapo.. means in 100yrs next generation will enjoy the life na kushukuru babu zao..
Hata mipango kama hii inashindikana watu kufikiria zaidi ya kuwaza asilimia 10 na matumbo yao na familia zao hatujifunzi kwenye madini mengine tunaendeleza makosa yaleyale yaliyofanyika huko nyuma
 
Unaweza kuwa una maoni mazuri Mkuu, lakini umewahi kufikiri hizo gharama za Uchimbaji Serikali itapata wapi iwapo ikiamua yenyewe kuchimba?

Serikali hii hii ambayo nusu ya Bajeti yake inategemea Wafadhiri.

Serikali hii hii ambayo bado nusu ya Wilaya zake hazina Huduma ya maji safi na salama.

Serikali hii hii ambayo zaidi ya nusu ya wilaya zake hazina barabara za Lami

Serikali hii hii ambayo bado inatafuta rasilimali fedha ili kuweza kufikisha Umeme kwenye Kila Kijiji kabla ya 2025.

Kwa kifupi Serikali yetu bado ina kazi kubwa zinazohitaji Rasilimali fedha kuweza kufikisha huduma za Maji, Barabara, Afya, Elimu n.k

Hivyo ni muhimu Wapatikane Wawekezaji wenye Mitaji waje wachimbe alafu Sisi kama Nchi tukusanye Kodi, Ajira kwa Watanzania wenzetu pamoja na kupata Mirahaba kupitia Win-Win Contracts.

Kwahiyo nadhani sisi kama Nchi tuhakikishe Mikataba tunayosaini dhidi ya Wawekezaji hawa inainufaisha Nchi badala ya kugeuka Mikataba ya Kinyonyaji dhidi yetu.
 
Unaambiwa yale madini ya pale Ngwala-Songwe ni moja ya madini adhimu sana duniani na matumizi yake ndio yanaenda kutawala kwenye miaka 50 ijayo duniani (Rare Earth Minerals au Strategic & Critical Minerals).

Ukitaka kupima vision ya Taifa letu unaweza ukaona jinsi gani hata madini ya namna hiyo tunawapa wawekezaji kwa mchanganuo wa 16% kama dhahabu ambayo tunayo almost kila kona ya Nchi!

Madini haya yangegundulika nchi serious kama China then Mmarekani au Mjapani aende na uwekezaji wake hata wa dola zote duniani hawezi kupewa! Common!

Hii ngoma tunataka tuupeleke wapi (hii NCHI tunataka iweje by mwaka let say 2050)? Do we have that vision?

Hivi tunataka tutengeneze Taifa la namna gani na lini?Je, tunajihoji maswali haya tukiwa kitandani, ofisini au nyumbani?

Mbombo ngafu!

View attachment 2599243

"Wiki hii serikali ya Tanzania ilisaini mkataba na makampuni matatu ya Australia kwa thamani ya dola milioni 667. Kwahiyo makampuni ya Australia yana haki za uchimbaji wa madini kwenye migodi matatu nchini Tanzania kwa lengo la kuchimba madini adimu ya ardhi na grafiti.

"Madini haya ni muhimu sana katika maendeleo ya teknolojia, mfano teknolojia za umeme, betri, magari, simu za mkononi, kompyuta mpakato (laptops) na grafiti inajulikana kutumika katika upakaji hasi wa betri ya lithiamu ion.

"Hii inaonyesha jinsi kampuni za kigeni zinavyowekeza Afrika na kutajirika maradufu kutoka kwenye rasilimali na madini ya Afrika. Dola milioni 667 kwa ajili ya migodi mitatu ni upuuzi. Wakati mgodi mmojawapo utatengeneza mabilioni na mabilioni ya dola."

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
Ahh! Tufanyeje sasa!??
 
Mkoloni CCM kajimilikisha nchi usitegemee kutakuwa na right thinking kwenye rasilimali za taifa.

Aliyeshika remote ndiye anayeamua channel ipi muangalie
 
Utawala wa CCM ni alama halisi ya ule wa mfalme Mangungo wa Msovero. Tumeshuhudia vituko vingi katika uingiaji mikataba tofauti ya nishati na madini kama vile gesi na dhahabu, huku viongozi wakizidiwa akili na maarifa kwa mbali sana na wakina Karl Peters wa nyakati zetu.
Unaambiwa yale madini ya pale Ngwala-Songwe ni moja ya madini adhimu sana duniani na matumizi yake ndio yanaenda kutawala kwenye miaka 50 ijayo duniani (Rare Earth Minerals au Strategic & Critical Minerals).

Ukitaka kupima vision ya Taifa letu unaweza ukaona jinsi gani hata madini ya namna hiyo tunawapa wawekezaji kwa mchanganuo wa 16% kama dhahabu ambayo tunayo almost kila kona ya Nchi!

Madini haya yangegundulika nchi serious kama China then Mmarekani au Mjapani aende na uwekezaji wake hata wa dola zote duniani hawezi kupewa! Common!

Hii ngoma tunataka tuupeleke wapi (hii NCHI tunataka iweje by mwaka let say 2050)? Do we have that vision?

Hivi tunataka tutengeneze Taifa la namna gani na lini?Je, tunajihoji maswali haya tukiwa kitandani, ofisini au nyumbani?

Mbombo ngafu!

View attachment 2599261

"Wiki hii serikali ya Tanzania ilisaini mkataba na makampuni matatu ya Australia kwa thamani ya dola milioni 667. Kwahiyo makampuni ya Australia yana haki za uchimbaji wa madini kwenye migodi matatu nchini Tanzania kwa lengo la kuchimba madini adimu ya ardhi na grafiti.

"Madini haya ni muhimu sana katika maendeleo ya teknolojia, mfano teknolojia za umeme, betri, magari, simu za mkononi, kompyuta mpakato (laptops) na grafiti inajulikana kutumika katika upakaji hasi wa betri ya lithiamu ion.

"Hii inaonyesha jinsi kampuni za kigeni zinavyowekeza Afrika na kutajirika maradufu kutoka kwenye rasilimali na madini ya Afrika. Dola milioni 667 kwa ajili ya migodi mitatu ni upuuzi. Wakati mgodi mmojawapo utatengeneza mabilioni na mabilioni ya dola."
Viongozi wa CCM bado wanafanya usiri mkubwa katika mikataba inayoingiwa ndani ya karne hii ya 21! Angalau hata wangaipeleka bungeni ili ikajadilwe kwanza hata na wabunge wengi waliokuwa vilaza, angalau wale wachache walio makini wangaliweza kufumbua wengine macho.

Viongozi kwa kujua ama kutokujua thamani halisi ya vitu, wanajifunga katika mikataba ya hovyo kabisa, na ya muda mrefu na makampuni ya kibwanyenye yenye ukwasi mkubwa. Ambao yana uzoefu mkubwa kuingia yenye kuzinyonya nchi changa.

Kibaya zaidi kwa sasa hakuna pa kukimbilia ama kushitaki, katika "bilateral trade" ni mkataba kati serikali na makampuni hayo, hakuna uwekaji wa hati fungani katika ya serikali moja na nyingine, isipokuwa ni serikali yetu na makampuni hayo. Lissu alilieleza kwa kina jambo kama hili jinsi lilivyo, na hata athari zake katika MIGA, lakini vilaza wengi wakaishia kumkejeli na kumdhihaki.

Ni lazima ifike wakati viongozi waanze kujithamini wao wenyewe kama wanatosha kufanya maamuzi katika uingiaji wa mikataba ya rasilimali za nchi yetu. Haya mambo yakuwekeana kinga ya kutokushtakiwa kwa viongozi ndio uchochoro mkubwa kwao kuzidi kushupaza shingo zao. Itafika kipindi nchi itafilisika kutokana mzigo mkubwa wa madeni, pamoja na masharti ya hovyo ya mikataba tuliyokwisha kujifunga nayo kama nchi.

Ama kwa hakika utawala wa CCM ni "replica" ya ule utawala wa mfalme Mangungo. Tofauti ni mavazi, wakati yeye alivaa mavazi ya kizamani, ila hawa wa sasa wanapiga suti za gharama, na ndani ya ofisi zenye viyoyozi, lakini akili ni ileile tu!
 
Sleeping giant mwenyewe anaongozwa na kichwa cha kukodi toka visiwa viduunchu kama sisimizi unategemea hao waliojaliwa na mola hilo ligiant wako serious kweli. Hivi itakuja tokea kiumbe toka huku ugiantini akatawale vile visiwani kweli. AMKENI.
 
Hebu twendeni polepole kwanza, je mnaposema 51% kwa 49% ratio nyie pia mtaweka initial capital au mnasomba faida tuu? Pili hizo 16% mnachukua na pia raia wenu wanaajiriwa na pia mtapata kodi zote PAYE,CORPORATE TAX,WITHHOLDING TAX etc, bado NSSF na WCF zote hizi kuna uhakika kila mwezi ama quarter mbona mnakuwa hivyo.

Ni fair share kabisa acheni ujuaji kwani ile kampuni ya Twiga corp ina hisa ngapi si 16% so kusema walioshiriki kipindi kile cha awamu yenu pendwa ni wajinga.
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom