jogi
JF-Expert Member
- Sep 25, 2010
- 25,558
- 25,323
Pointi unayotaka tumalizie ni kuwa wa kwetu ni wa aina ipi?Gaddafi na Mobutu hawafanani.
Mobutu alikuwa aliwezeshwa kuingia madarakani na wazungu lakini Gaddafi hakusaidiwa na wazungu
Mobutu alilindwa na wazungu mwanzo mwisho lakini Gaddafi alipingwa na wazungu mwanzo mwisho
Mobutu aliihujumu Zaire mwanzo mwisho akisaidiwa Na wazungu wakati Gaddafi aliijenga Libya akisaidiana na walibya wenzie
Mobutu alikuwa mbinafsi lakini Gaddafi alikuwa si mbinafsi
Mobutu aliiacha nchi ikiwa hohehahe katika kila kitu lakini Gaddafi aliiacha nchi ikiwa nzur ingawa miezi ya mwisho iliharibiwa Na wazungu na vibaraka wao
Mobutu hakuwa na nia ya kuwasaidia wa Zaire lakini Gaddafi alikuwa na nia thabiti ya kuwasaidia walibya
Mobutu alikuwa kibaraka wa wazungu wakati Gaddafi alikuwa kibaraka wa walibya
Mobutu alikuwa anautukuza uzungu lakin Gaddafi alikuwa anautukuza uafrika
Wapinzani wakubwa na wa maana wa Mobutu walikuwa wana fadhiliwa au kuwezeshwa na wanazaire wenyewe lakini wapinzani wakubwa wa Gaddafi walikuwa wanawezeshwa na kufadhiliwa na wazungu
Orodha inaweza endelea mpaka kesho. Niishie hapa kwa leo
Lakini wote Mobutu na Gaddafi walikuwa madikteta, inasemwa