Madikteta wote duniani hufanana

hii ni post njema na imetoka siku muafaka. Madikteta kweli wanafanana na wanatolewa pia kwa staili inayofanana. Ni kuwapa muda...watalijua jiji! Huu upepo wa kung'oa walioshindikana umeshaanza kuvuma! tusubiri muda tu, utaeneo bara hili lote
 
Madikteta wote wanafanana; wawe ni wale ambao ni mtu mmoja mmoja au wawe wa chama kimoja; kufanana kwao kunatabiri vitendo vyao. Hufanana katika mambo makubwa matano:

a. Huamini kuwa wao ndio pekee wenye uwezo wa kutawala (Katika fikra zao hawaamini kama kuna mtu au chama kingine kinachoweza kutawala vizuri kuliko wao). Baadhi yao (kama ni mtu mmoja au chama) hujiaminisha kabisa kuwa ni wateule wa Mungu kutawala nchi zao.
b. Huamini kuwa wanapendwa sana kupita kiasi (hili kuelezea kwanini picha, sanamu, n.k zao huenezwa kila kona ya nchi) Hupenda kuimbiwa nyimbo za kusifiwa na kupeperushiwa maua kila wapitapo kama ishara ya "upendo" huu.
c. Hawako tayari kuamini wanaweza kukataliwa; Mara zote inapotokea mtu anawapinga au kuwakataa hutafutiwa sababu ya kuoneshwa kuwa haiwezekani awakate wao kwani (b) wao wanapendwa sana!
d. Hata siku moja hawajawahi kutengeneza mifumo itakayowaondoa wao wenyewe madarakani. Hivyo, hutumia mbinu zote kufanya mabadiliko ya kimapambo tu ambayo kwa watu wasiofuatilia huweza kuvutiwa kuwa ni mabadiliko. HIvyo aidha hujikuta wanaondoka kwa kukimbia au kwa kukimbizwa na wananchi wao au mataifa ya nje!
e. Wako tayari kufanya jambo lolote kubakia madarakani - msisitizo hapa uko kwenye neno "LOLOTE".

Kutokana na hayo matatu tabia za madikteta wote huweza kutabirika (wawe ni mtu mmoja au chama kimoja). Na ili kuhakikisha hayo matatu madikteta wote duniani (wanaovaa nguo za kiraia na wale wanaovaa nguo za kijeshi)

1. Hutumia vitisho kulazimisha kupendwa na kukubalika - silaha ya dikteta ni vitisho (terror). Wakikukamata watakasumbua sana hadi uogope. Lengo ni kukushawishi uone ni kwanini wao wanastahli kupendwa! Hupenda kujiona kama wazazi wa wananchi - nani atamchukia mzazi wake?
2. Hutengeneza masimulizi ya sifa na kuyalazimisha yaaminiwe hata kama msingi wake ni uongo. Madikteta ni mabingwa wa kuunda (manufacture) uongo. Uwezo wao mkubwa wa kufanya hivi hutokana na ukweli kuwa wao humiliki vyombo vya habari vyenye kufikia watu wengi zaidi (radio, TVs n.k)
3. Inapofikia mahali kuwa upendo wa wananchi unapungua au wanaanza kuwa na mashaka nao madikteta huanza kupoteza watu. Yaani, pole pole watu huanza kukamatwa na kuwekwa "vizuizini" ili wasimpinge sana dikteta.
4. Kisingizio pekee cha madikteta wote (wawe wa mtu mmoja au chama kimoja) kuhalalisha kuwanyanyasa, kuwanyima wananchi uhuru na hata kuwatia watu nguvuni ni "kwa ajili ya nchi". Yaani, hutumia "taifa" kama kisingizio cha wao kuendelea kutawala.

Kwanini?

Kwa sababu madikteta wote wanataka kupendwa na kukubaliwa!

Ole wao wananchi wanaposema "hapana"!!!

Na. M. M. Mwanakijiji (BGM)

Bahati nzuri hapa kwetu tumeepuka udikteta ndio maana Mwalimu alishtuka na mapema kwa kuandika katiba inayoweka mipaka ya Rais asizidi miaka 10!
Tangu 1995 uchaguzi huru na wa haki umeendelea kufanyika nchini!
Vyama vya siasa kuendesha kampeni zao kwa huru ingawa kasoro za hapa na pale zinakuwepo!
Mahakama iliyohuru na inayoendesha kesi bila kuingiliwa na Serikali!
Uhuru wa Magazeti na haki ya kujieleza wa waandashi na Wananchi kwa ujumla!

Ushahidi ni nchi za Kidemokrasia za magharibi kama vile EU na Amerika kutambua utawala wa sheria TZ na hivyo kumimina misaada na kuwa na uhusiano mzuri kinyume na enzi za Utawala wa chama kimoja!

Nadhani TZ kwa kiasi fulani tumejitahidi ukilinganisha na nchi kama Uganda, Zimbabwe, Egypt, Libya, Tunisia, Burundi,nk
 
Tanzania hakuna udikteta? Ndiyo huwezi kulinganisha na hizo nchi lakini ukienda hospitali ukakuta wagonjwa wako serious kuliko wewe haina maana kuwa huumwi. Tanzania udikteta upo tele. CHAMA CHOCHOTE KINAPONGANGANIA MADARAKA KWA KUNYIMA FURSA ZOTE ZA UCHAGUZI HURU HUO NI UDIKTETA.

Kupewa misaada siyo kipimo cha kutokuwepo udikteta kwani hata hizo nchi ulizozitaja zinapata misaada kuliko Tanzania.
 
hujaza ndugu zao wa damu katika nafasi nyeti kama SHEMEJI kuwa IGP,watoto wao huogopwa sana na wakuu wa idara za serikali na chama mfano ni bora umpe mkulu neno live kuliko mtoto wake maana ataenda kuongeza chumvi na utaambiwa wewe sio raia,wake zao hutumia pesa za umma bila ukaguzi na hutoa ushauri wa kisayansi hata kama si Mwalimu wa sekondari.
Hutumia dini ili kuficha udhaifu wao kiutendaji, hawapendi vijana wawe na elimu sahihi, huteua mvivu atakayejifanya anashida kama za kwenu kuwa mkuu wa utendaji au waziri mkuu kuwazuga wanaichi.

Sahihi kabisa,

Hiki ndicho kinachoendelea hapa kwetu,sikuzote wanaogopa Changamoto ya wasomi hasa vijana wanaochipukia.
 
Ushahidi ni nchi za Kidemokrasia za magharibi kama vile EU na Amerika kutambua utawala wa sheria TZ na hivyo kumimina misaada na kuwa na uhusiano mzuri kinyume na enzi za Utawala wa chama kimoja!

Nadhani TZ kwa kiasi fulani tumejitahidi ukilinganisha na nchi kama Uganda, Zimbabwe, Egypt, Libya, Tunisia, Burundi,nk

Kama huo ndio ushahidi itabidi uwaombe radhi Misri!
 
Vyema, na Kweli kabisa. Sasa tuanze kuwaorodhesha madikteta wa dunia hii hapa. Mimi naanza na wachache ninaowafahamu. Wadau tusaidiane kutaja hadi wakamilike:

1) Gbagbo wa Ivory Coast ni Dikteta
2) Hosni Mubarak wa Egypt ni Dikteta
3) Yoweri Museveni wa Uganda ni Dikteta
4) Chama cha Mapinduzi cha Tanzania ni cha Kidikteta

5) ...
5... Robert Mugabe wa Zimbabwe
 
Duh!Kilichoandikwa kimeandikwa. Kalamu haimtupi mwandishi wake. Lakini, to be frank, Mzee Mkjj bado hajaenda mbali. Post yake ya kiingereza jana imeeleza juu ya udikteta japo alikuwa anauma na kupuliza. We need original Mwkjj back.
 
Asante ndugu yangu.. I'm still here. Bado nafanyia kazi ile kitu...
 
Vyema, na Kweli kabisa. Sasa tuanze kuwaorodhesha madikteta wa dunia hii hapa. Mimi naanza na wachache ninaowafahamu. Wadau tusaidiane kutaja hadi wakamilike:

1) Gbagbo wa Ivory Coast ni Dikteta
2) Hosni Mubarak wa Egypt ni Dikteta
3) Yoweri Museveni wa Uganda ni Dikteta
4) Chama cha Mapinduzi cha Tanzania ni cha Kidikteta

5) ...

6......... Watu wote Duniani Na bila ya kujisahau wewe ni Madikteta.
 
Jk hakuwahi kuwa dikteta hata siku moja alikuwa mvumilivu sana lkn pia alifanya kazi na kiukweli kazi zake zimeonekana.
 
Vyema, na Kweli kabisa. Sasa tuanze kuwaorodhesha madikteta wa dunia hii hapa. Mimi naanza na wachache ninaowafahamu. Wadau tusaidiane kutaja hadi wakamilike:

1) Gbagbo wa Ivory Coast ni Dikteta
2) Hosni Mubarak wa Egypt ni Dikteta
3) Yoweri Museveni wa Uganda ni Dikteta
4) Chama cha Mapinduzi cha Tanzania ni cha Kidikteta

5) ...
Mohamed Shein wa Znz
 
Bado kwa hoja hizi leo Mwanakijiji atakuja hapa kupinga! Hapo kila hoja inamlenga Magufuli kwa ukamilifu.... Mwanakijiji&Lipumba mnaonyesha unafiki na uzandiki wa kitoto kuliko kawaida lakini niwahakikishieni kuwa Mwanakijiji utakuja hapa mwenyewe kujikana kabla Jogoo hajawika na Lipumba utafutika kisiasa na kubaki hohehahe! Mumeonyesha namna mlivyo wahuni kisiasa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom