Madhara ya kunywa maji ya baridi haya hapa

Vipi vinywaji vingine kama bia baridi na soda baridi ? ruksa!!
Mkuu leipzig Vinywaji vya Bia iwe moto au baridi na Soda iwe moto au baridi vina madhara kwa binadamu mkuu havina faida kabisa.

water1.jpg


KUNA mjadala mkali unaendelea kuhusu vinywaji baridi hususani soda, baada ya utafiti wa hivi karibuni kuonyesha kuwa soda inaweza kuwa na madhara zaidi kiafya kuliko hata sigara!

Hii inaweza kuwa changamoto nyingine kubwa kumkabili binadamu katika masuala ya afya, kwani makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake bila kutaja madhara ya vinywaji vyao.

Soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi (obesity), ugonjwa wa ini (liver disease) na hata tabia za vurugu (violent behavior). Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, unywaji wa vinywaji baridi mara kwa mara unachangia tabia ya ugomvi kwa asilimia kati 9-15!

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa nchini Marekani, soda huwekwa ‘fructose’ (sukari) nyingi ikiwa katika mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla.

Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya lishe asilia na tiba mbadala anasema: ” Ninaposema kunywa soda ni hatari sawa na mtu anayevuta sigara au pengine zaidi, siyo jambo la kutia chumvi, bali ndiyo ukweli halisi”.

Dk. anaendelea kusema kuwa unywaji wa soda kwa njia nyingi ni mbaya kuliko uvutaji wa sigara, ila kutokana na kampeni kubwa ya matangazo inayofanywa na makampuni haya, inafanya vinywaji hivi vyenye sukari kuonekana havina madhara kwa watu wasio na hatia, hasa watoto wetu!

SABABU KUBWA YA KUDHARAU SODA
Unayesoma makala haya kuhusu madhara ya soda kwa mara ya kwanza bila shaka utakuwa unashangaa na kujiuliza; soda ina ubaya gani? Kwa mujibu wa Dk. Mercola, hakuna sababu yoyote ya kuendelea kunywa soda, labda ujikute uko katikati ya jangwa na hakuna kinywaji kingine isipokua soda!


Kiafya, unywaji wa soda au vinywaji vingine baridi vyenye ‘fructose’ una madhara. Unywaji wa kiasi cha kopo moja tu la soda kila siku, utakuongezea uzito wa mwili wa kilo 10 kila mwaka na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari (diabetes) kwa asilimia 85!

‘FRUCTOSE’
‘Fructose’ ni kirutubisho kilichomo ndani ya sukari na kiwango kinachowekwa wakati wa utengenezaji wa soda ni kingi kuliko kawaida. Inaelezwa kuwa miaka 100 iliyopita, Mmarekani mmoja alikuwa akitumia kiasi cha gramu 15 ya sukari (fructose) kwa siku, tena kwa kula matunda. Miaka 100 baadaye, (yaani hivi sasa), robo ya Wamarekani wote wanatumia kiasi cha gramu 135 (kutoka 15) kwa siku, tena kwa kunywa soda!

Ulaji wa sukari (fructose) kiasi cha gramu 15 kwa siku hauna madhara kiafya, labda uwe na ugonjwa wa kisukari (high uric acid levels). Hata hivyo, kwa kula sukari mara kumi zaidi ya kiwango cha gramu 15 kinachokubalika kiafya, inakuwa ndiyo chanzo cha unene wa kupindukia na magonjwa mengine hatari yanayoibuka mwilini (degenerative diseases).

Utafiti unaonesha kuwa vinywaji vingi baridi vina sukari nyingi kuliko wastani unaotakiwa. Badala ya kuwa na asilimia 55 ya ‘fructose’ na asilimia 45 ya ‘glucose’, vingi vina asilimia 65 ya ‘fructose’, ikiwa ni karibu asilimia 20 zaidi na inavyotakiwa.

Utafiti zaidi umeonesha kuwa ‘fructose’ ndiyo chanzo kikubwa cha tatizo la ugonjwa wa ini kwa watoto wengi nchini Marekani, ingawa hawatumii kilevi chochote (alcohol). Inaelezwa kuwa ‘fructose’ huleta madhara kwenye ini kama inavyofanya pombe. chanzo
https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/210672-madhara-ya-kunywa-soda.html
 
Last edited by a moderator:
Pombe ina magonjwa 60 kwa binadamu:

images




MOJA ya vyanzo vinavyolipatia taifa mapato kupitia makusanyo ya kodi ni pombe.

Lakini pamoja na faida zote tunazozipata, ukweli unabaki palepale kwamba pombe ina athari katika maisha ya binadamu.

Mwanzoni mwa mwaka huu wataalamu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na madaktari wastaafu walikutana na wanahabari jijini Dar es Salaam na kuzungumzia juu ya mkutano utakaozungumzia athari za pombe katika jamii.

Mkutano huo unaotarajia kufanyika Jan 13 hadi 14 mwaka huu mkoani Arusha, utashirikisha nchi za Afrika Mashariki.

Watunga sheria na wataalamu wengine kutoka serikalini watahudhuria huku ujumbe wa mkutano huo ni: ‘Kilevi si bidhaa ya kawaida na ni kikwazo katika maendeleo.’


Mkurugenzi Msaidizi na Katibu wa Magonjwa yasiyoambukiza, Dk. Joseph Mbatia, kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anasema serikali ipo mbioni kutengeneza sera itakayohusu utumiaji wa pombe ili kupunguza athari zake katika jamii.


Dk. Mbatia anasema wamelazimika kutunga sera hizo baada ya kuona matatizo yanayotokana na pombe yanaongezeka kila kukicha.

Anasema kabla ya sera hizo kupitishwa watafanya utafiti katika maeneo mbalimbali ili kujua ni jinsi gani jamii inavyolichukulia suala la pombe na madhara yake.

“Mfano, katika vijiji vichache tulivyofanya utafiti, wananchi walikuwa wakijitetea kwamba pombe imewasaidia kuendesha maisha yao…lakini ukweli ni kwamba pamoja na faida ambazo zimekuwa zikiorodheshwa, hasara ni nyingi kuliko faida.


“Kwa mfano, bima zimekuwa zikilipwa kutokana na ajali zinazosababishwa na kulewa kupita kiasi,” anasema Dk. Mbatia.

Anabainisha kwamba sera zitakazowekwa si katika kupiga vita biashara ya pombe na badala yake zitakuwa zikiangalia njia bora za

matumizi yake na kwa wale wataoonekana wameshaathirika watawekewa utaratibu wa kupatiwa tiba.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Kanda ya Afrika Mashariki ya ‘IOGT-NTO Movement’, ambao ni waandaaji wa mkutano huo, Gunnar

Lundstrom, anasema bado kuna changamoto zinazolikabili taifa katika kupunguza athari za pombe.

Anasema changamoto hizo ni pamoja na pombe kupatikana kwa gharama nafuu na hivyo kusababisha watu kunywa kupindukia.

Tatizo lingine anasema ni pombe kuwa moja ya chanzo cha mapato nchini, jambo linalofanya serikali kushindwa kupiga marufuku.

Naye Daktari mstaafu, Maletnlema Tumsifu, anasema kuna jumla ya magonjwa 60 yanayosababishwa na unywaji wa pombe.
Anataja baadhi ya magonjwa hayo kuwa ni mfarakano katika familia, maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi, unene kupita kiasi, utapiamlo hasi, mimba kuharibika na kisukari.

Dk. Maletnlema anasema kuna madhara ya pombe ya aina mbili. Kwanza ni kuathirika kwaa mishipa ya fahamu mwilini kote kwa kupunguzwa uwezo na pili ni kuungua baadhi ya ogani za mwili hasa tumbo pindi mtu anapokunywa.


Anaeleza kwamba katika kuathirika mishipa ya fahamu kumetizamwa kwa hatua nne za wanywaji, hatua ya kwanza ni ile ya kuchangamka.


Hapa mtu hujisikia mzima zaidi ya kawaida, moyo unapiga haraka, tumbo linameng’enya chakula haraka na hamu ya chakula kuongezeka.


Hatua ya pili, mtu akiendelea kunywa anachanganyikiwa na kuzungumza sana, kukosa aibu, utu kubadilika, kutawala tabia za kimwili, hamu ya chakula kuongezeka na hapa ndipo watu wanaagiza nyama choma kwa wingi.

Mnywaji akiendelea kunywa pombe hucharuka kutokana na neva zake za ubongo kushindwa kumiliki mwili.
Mambo yote anayoyafanya hayana utaratibu kwani mnywaji huwa mkorofi.

Dk. huyo anasema mnywaji huwa mkorofi na anaongea maneno yasiyo na maana, baadhi ya wanywaji huchukulia hatua hii kama raha yao. Hapa kitu kinachojitokeza ni kupoteza hamu ya kula.


Hatua ya nne mtu akilewa kupita kiasi huwa hajijui na analala fofofo kutokana na kupoteza fahamu. Huenda akajikojolea au kutapika, inategemea na kiasi cha pombe alichokunywa.


Wakati kwa upande wa ogani, pombe huathiri zaidi viungo vinavyopata pombe nyingi kila wakati mtu akiwa anakunywa.

Mfano wa viungo hivyo ni mdomo, koo na tumbo, ambavyo vyenyewe hufikiwa na pombe nyingi mara mtu anapomeza.

Tumbo likiumia inaonekana kama maumivu ya tumbo, pengine kutapika na kuharisha. Lakini kutokana na utaratibu wa tumboni, lazima chakula chote pamoja na sumu au madawa vinavyonyonywa tumboni vipitie katika ini kuondoa sumu na vyakula visivyohitajika.

Na kwa sababu hii, pombe yote mtu anayokunywa hupita katika seli za ini na zinajaribu kuiondoa lakini nazo zinalewa chakari na baadhi zina kufa.

Ieleweke kwamba tukinywa kidogo seli chache zinakufa na tukinywa sana zinakufa seli nyingi na nafasi yake inajazwa nyuzi nyuzi za kovu.


Ini huwa na mabilioni ya seli ambazo ni imara, hata mtu akinywa pombe nusu, seli zake bado zitaendelea na maisha kama inafikia kikomo ini linashindwa kufanya kazi na kujikuta njia za nyongo na mishipa ya damu inaziba.

Kila ogani ya mwili inaumia kivyake, lakini tumbo na ini ni mifano wazi.http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=1500


 
Mimi sinywi chai -Asubuhi uji wa ulezi au juice mara nyingi mango au passion,mchana na usiku msosi lazima niusindikize na juice baridi na si glasi moja, vp hapo nitasalimika?
Juice utengeneze wewe mwenyewe sio juice ya kununuwa dukani sio nzuri pendelea kunywa maji ya Uvuguvugu glasi 2 au 3 unapoamka Asubuhi kabla ya kla kitu itakusaidia kiafya yako kuwa ni nzuri 124 Ali
 
Last edited by a moderator:
kwa hiyo naweza kunywa maji baridi af baadae nikinywa maji moto na asali itakuwa poa? au siruhusiwi kabisa kunywa maji ya baridi
 
Effects of Cold Water

If you like to drink cold water then you should read this article. It feels good to have a cup of cold drink after eating but cold water will

solidify the oily stuff that you've just consumed. It slows down your digestion and once this sludge

reacts with acid, it will then break down

and the intestine will absorb it faster than the solid food. It will then line the intestin
e and very soon it will turn into fats and lead to cancer.

The best thing to do after a meal is to drink warm water or hot soup.


 
Hivi kuna kitu ambacho ni salama kula au kunywa?
Kila sehemu naona wataalamu wakionya kuhusu kitu hiki au kile. Nadhani sasa niamue tu kula na kunywa chochote maana karibu vyote ni hatari kwa afya yangu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Eleweni!
Ni mbaya kunywa baridi baada ya kula, lakini kabla ya kula, au wakati mwingine wowote ni ruksa!
 
Hivi kuna kitu ambacho ni salama kula au kunywa?
Kila sehemu naona wataalamu wakionya kuhusu kitu hiki au kile. Nadhani sasa niamue tu kula na kunywa chochote maana karibu vyote ni hatari kwa afya yangu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Mkuu Mpita Njia Kitu cha salama ni Maji ya Kunywa lakini Maji ya kunywa yawe ya Uvuguvugu sio Maji ya baridi Mkuu hayo maji ya po salama kwa Asilimia 1000&1000 hakuna kitu chengine kilicho kuwa salama zaidi ya Maji ya kunywa haswa hayo ya Uvuguvugu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom