#COVID19 Madereva watano wa Tanzania wakatiliwa kuingia Uganda

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,877
Madereva 5 wa magari ya mizigo wamekataliwa kuingia Uganda baada ya kukutwa na maambukizi ya #CoronaVirus. Sampuli za watu 655 zilipimwa mpakani na madereva hao wakakutwa, na kukabidhiwa kwa mamlaka za Tanzania

Awali, madereva walikuwa wanaruhusiwa kuingi nchini humo kabla ya kupatiwa majibu na walikuwa wakifuatiliwa ikiwa dereva husika akikutwa na maambukizi. Halii hii ilihatarisha watu wengine na utaratibu ukabadilika na madereva hulazimika kusubiri majibu

Wizara ya Afya nchini Uganda imetangaza kuwa na jumla ya maambukizi 294 za #CoronaVirus baada ya maambukizi mapya kupatikana katika sampuli 1,739 zilizopimwa Jumapili, Mei 24. Hadi hivi sasa Uganda haijaripoti kifo cha #COVID19
 
Back
Top Bottom