Madereva wa magari ya shule ni hatari kwa maisha ya watoto wetu

Makamura

JF-Expert Member
May 19, 2022
356
550
Siku Hizi kumekuwa na trend ya matukio kadhaa ya madereva wa gari za shule 'School Bus' kuwa rough njiani, na hawako makini kabisa, hawajali kabisa kama wamebeba watoto ndani ya gari hizo.

Hii video ni moja ya matukio ambayo yamekamatwa kwenye camera Gari ya shule yenye jina la MARTHA MONTESSORI iliyopo Kimara Temboni yenye nambari za usajili T430 EAW ikiwa inatembea speed ya 120+ km/h ikiwa na wanafunzi ndani yake

Anahama Barabara bila Indicator wala kuchukua taadhari, kwa speed hii ikatokea adha katika barabara ni ngumu kuzuia gari kwa haraka


 
Usalama wa raia na watoto bado sana nchini mwetu. Madereva hawathamini kazi zao. Waajiri na serikali hawathamini maisha ya wananchi. Maisha ya watoro yanakabidhiwa madereva ambao hawana akili timamu. Hakuna anaejali suala la usalama.
 
Nimefanya kazi kama school bus driver shule ilikuwa mbezi chini,
Route yangu ni Tegeta, mashamba ya jeshi, madale, Mivumoni
Kipindi hicho hamna barabara ya lami na kila mtu sheria ya shule ni umchukulie nyumbani kwao, na humrudishe kwao plus usumbufu wa wazazi mbona umechelewa kumleta mtoto au umechelewa kumrudisha mtoto!
Matokeo yake kulinda ajira zao hao madereva wanatembea hivyo!

Suluhisho madereva wa mabasi ya shule wawe na
Mikataba ya ajira atleast hata kwa miaka 3 renewable.
Kuwa na mda wa kutosha kutoa huduma atleast masaa 3-4 kwa asubuhi na jioni. Yaani kama kuanzia saa 11- 2 asubh na kwa jioni 9-12:30.
Kuwa na mda maarumu wa kupitiwa kwa mtoto gari ikifika hujamuaandaa heri wa waondoke, utampeleka mtoto mwenyewe.
At least tutapunguza hizi changamoto kwa kiasi kikubwa.
 
Back
Top Bottom