Madereva wa mabasi ya Rungwe na Happy Nation mbaroni kwa ku-bet na kufanya ligi barabarani

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,388
2,000
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Fortunatus Muslimu amesema kwamba madereva wawili wa mabasi ya Rungwe na Happy Nation wamekamatwa baada ya video kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha madereva wakishindana 'LIGI'

Pia soma > Hii kamari ya kubetia mabasi ipoje?

Amesema

Hili suala la madereva ambao mmeona clip inatembea ikionesha Mabasi ya Rungwe na Happy Nation wanakimbizana ili kuona nani wa kwanza kufika kwenye stendi fulani, tumekuja kubaini hawa madereva wali-bet hiki kitendo tunakikemea kwa nguvu

Nimechukua hatua kali sana, tumewakamata wote na wako ndani na tumeandaa utaratibu wa kisheria ikiwemo kuwafikisha Mahakamani, Sheria inanipa uwezo wa kuwaondolea sifa wa kuendesha haya magari ya mizigo na biashara na kwa miezi 6 hawa hawatokuwa barabarani wakiendesha Mabasi wala Malori labda hivi vigari vidogo.
 
guwe_la_manga

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
1,960
2,000
Afande ungewafungia milele kabisa
Matako yao hawa jamaa
Hawajui kuwa wanabeba roho za watu ila na huyo aliyerecodi huu ufirauni ajiandae kisaikolojia
 
Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,134
2,000
Game tamu sana hizo, acheni kabisa. kwanza hapo bado kabisa mbona? Hizo gemu tamu balaaa, kuna mtu juzi nimesema hapa ving'amujzi havifanyi kazi, akanibishia, haya nambie sasa hapo kuna speedometer gani inafanya kazi? Hao wamekamatwa baada ya video kwenda viral not tracking system ya hao siju wapi huko
 
Lyamber

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
10,216

Hivyo ving'amuzi vinafanyaje kazi? Vinawekwa wapi? Na nani anakua anaviangalia mkuu?
 
king kan

JF-Expert Member
May 6, 2011
1,504
2,000
Game tamu sana hizo, acheni kabisa. kwanza hapo bado kabisa mbona? Hizo gemu tamu balaaa, kuna mtu juzi nimesema hapa ving'amujzi havifanyi kazi, akanibishia, haya nambie sasa hapo kuna speedometer gani inafanya kazi? Hao wamekamatwa baada ya video kwenda viral not tracking system ya hao siju wapi huko

Una hakika gani kwamba pale walizidisha speedometer?

Hapo hawana kosa la spidi labda lile la reckless driving ambalo nalo ni gumu kulithibitisha jamaa iwapo aliovertake mahali panaporuhusiwa.

Jamaa wa Happy Nation ana kosa la hisia. Itakuwa gumu kulithibisha.
 
Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,134
2,000
Una hakika gani kwamba pale walizidisha speedometer?

Hapo hawana kosa la spidi labda lile la reckless driving ambalo nalo ni gumu kulithibitisha jamaa aliovertake mahali panaporuhusiwa.

Jamaa wa Happy Nation ana kosa la hisia. Itakuwa gumu kulithibisha.
Duh basi sawa
 
Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
29,378
2,000
Game tamu sana hizo, acheni kabisa. kwanza hapo bado kabisa mbona? Hizo gemu tamu balaaa, kuna mtu juzi nimesema hapa ving'amujzi havifanyi kazi, akanibishia, haya nambie sasa hapo kuna speedometer gani inafanya kazi? Hao wamekamatwa baada ya video kwenda viral not tracking system ya hao siju wapi huko

Ila wewe!!!!Kwahiyo wewe unafurahi eh??...kuwa makini kijana! Barabara hizi sio kabisa!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom