Madereva wa Mabasi ya Mwendo kasi Kugomea Mikataba

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Madereva wa Mabasi yaendayo Kasi jijini Dar watagoma kuendesha magari hayo kufuatia uongozi wa mabasi hayo kuwapa mkataba wa kazi usiokidhi mahitaji.

Kama hili likitokea, basi litakuwa pigo jingine kwa Serikali kwani ilitaka Usafiri wa Mabasi yaendayo kasi Uanze mara moja.

Kuanza kwa Safari kwa Mabasi Yaendayo kasi bado kunakubwa na changamoto nyingi kwani wananchi walilalamikia nauli ya Mabasi hayo na Serikali kupitia Waziri Mkuu kugomea nauli ya 1,200 hadi 1,400 kwa Safari moja kama walivyopendekeza na wasafirishaji.

Serikali iliwataka wapunguze bei vinginevyo Serikali itasimamia mradi yenyewe.
 
MWENDO KASI: Madereva wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar watagoma kuendesha magari hayo kufuatia uongozi wa mabasi hayo kuwapa mkataba wa kazi usiokidhi mahitaji.

Kama hili likitokea, basi litakua pigo lingine kwa Serikali kwani Serikali inataka Usafiri wa Mabasi yaendayo kasi Uanze mara moja.

Kuanza kwa Safari kwa Mabasi Yaendayo kasi bado unakubwa na changamoto nyingi kwani wananchi walilalamikia nauli ya Mabasi hayo na Serikali kupitia Waziri mkuu kugomea nauli ya 1200 hadi 1400 kwa Safari moja kama walivyopendekezwa na wasafirisgaji.

Serikali iliwataka wapunguze bei vinginevyo Serikali itasimamia yenyewe.
Huu mradi umekuwa kizungumkuti kutokana na figisufigisu zisizoisha, sijui ni lini tutafanya jambo likanyooka bila sarakasi nyingi labda kupiga dili za rushwa
 
Huu Mradi Umekufa Kabla Haujaanza..... Anasubiriwa Nani Wa Kuuzika Tu!


Tanzania ni nchi ya Maajabu.
 
yaani umlipe mtu laki nne anashinda road kutwa nzima, wanakumbana na masaibu kibao wakati wao wanashinda ofisini wanalipwa mamilioni, is not fair!
 
Tatizo wasemaji wamekuwa wengi sana, ila uangalizi na ufuatiliaji ni sifuri. Changamoto kama hizi zinapaswa kuangaliwa tokea mwanzo wa mradi, siyo kwa njia ya zima mtoto na kuharakisha mambo.
 
Haaaaa mkuu mbona kakaa kimya hv kuna jambo mradi ule una siri nyingi sana ulifel kabisaaaaaaaaaa
 
HIVI kwa wale mliosafiri huko nje ya nchi ya Tanzania hukoo maulaya kuna mambo kama haya kweli? Yaani kitu kinaanzishwa utadhani ni Watoto wa nursery ndo wanasimamia mradi
Wenzetu wanafanya vitu vilivyonyooka mno na anayefanya ujinga anawajibishwa on the spot
 
Dr.dhaifu na vibaraka wake ndio wakulaumiwa,huu mradi ulifanywa ki ghetogheto..

Sasa mnategemea miujiza wakati mradi ulishakufa na utazikwa soon makaburi ya msoga..
 
Kwanza original plan ni tofauti na kilichojengwa, gharama za mradi inasemwa zimechakachuliwa, kuna baadhi ya maeneo barabara imefinywa na hakuna njia ya Wenda kwa no 11 nknk
and on top of All that wanataka kutuibia wa wananchi nauli mara 3,khaaaaaaa
 
Tarehe 10 si ndo leo, mliopo dsm tuambien, magari yameanza kufanya kazi???
 
Mkumbuke mradi upo chini ya TAMISEMI kwa kiasi kikubwa na masimamizi wa mradi ndo alikuwa mama Hawa Chaos,wapi alipowahi kufanikiwa kwa jambo lolote pale alikopita
 
Back
Top Bottom