Madereva wa kampuni ya mabasi ya Sauli wamshambulia abiria aliyeripoti kuhusu mwendokasi

Endelea kushangalia siku utakapokatika kiwiliwili ndio utajua Mwendokasi sio mzaha
Siku ambayo wataokota kiwiliwili basi nawewe shangilia. Mnalalamika utafikiri mnalazimishwa kupanda! Kama mnakerwa na mwendo fanyeni kwa vitendo, kimbieni gari isipate wateja huenda watabadilika. Ajabu ndio gari inayojaza sana kwenye route ya Mbeya-Dar manafiki nyie.
 
Kuna mwingne alitekwa na kisbo ya kahama kutoka msamvu kisa kureport bus lao wakaenda kumshusha maporini uko akapambane na hali yake
 
Dereva wa basi la Kampuni ya Saul T 485 DXE wamemshambulia abiria kisa kureport gari ikiwa na speed meter 115-120.

Kutokana na story ya muhusika anasimulia kuwa alikua na App ya kusoma speed ya gari na kutuma kwenye group la wasafiri mojawapo.

Baada ya muhusika kurecord tukio hilo kwenye group alipokea DM za vitisho kutoka kwa namba tofauti.

Baadae kidogo alipigiwa simu na dereva wa gari hilo na kumtaka asogee mbele yani atoke siti hiyo akakae mbele kwa dereva, alipofika dereva alimpokonya simu na kumtishia.

Baada ya safari kwenda kwa saa kadhaa bila muhusika kupewa simu yake ilifika hatua abiria huyo alitaka kushuka sehem inayoitwa Uyole wakati anataka kushuka walimzuia na kumtaka asishuke kwamba wanampeleka polisi kwa kosa la kurec na kuwachomea maovu yao.

Abiria alijitahidi kuwaomba na kuwasisitiza lakini waligoma na kuondoka nae pasipo kumpeleka polisi (utekaji huu).

Baada ya kufika mwisho wa safari walishusha abiria wote na kubaki wao madereva na baadhi ya watu wachache na kuanza kumhoji na kumpiga kwa kumlazimisha kusema nani amemtuma kurecord maovu ya kampuni yao ya SAUL na ilifikia hatua ya kumlazimisha amtaje moja ya mtu wa kampuni shindani ya New force.

Baada ya kipigo na vitisho vya muda mrefu walikagua simu na kujaribu kuweka namba za baadhi za watu waliohisi wao ndio wamemtuma ila walikuta abiria huyo hana namba za wahusika hao kabisa, ndipo walipomlazimisha kuformat simu yote na vitisho juu.

Baada ya muda walimuachia abiria huyo akiwa na majeraha maeneo ya mgongoni kutokana na kipigo walichomshushia.

Kutokana na taarifa hiyo inaonesha ukanda huo Dar mpaka Tunduma kumekuwa na ajali nyingi sana sababu ya rushwa na madereva kujiona tayari wameshika system.
Tunaenda wapi? Ajali zitaisha kweli?
 
Mkuu, kuna ajali nyingi sana za mabasi huko mabarabarani zinatokea kila siku na huwezi kusikia polisi au vyomb vya habari wakiziongelea hata kidogo, mfano ajali ya Super feo, ambayo ilikuwa reported humu kwenye forum na mmoja wa abiria, pengine kuna uwezekano wa rushwa kwa sehemu fulani. Hizi sauli zinapata sana ajali na ni mara chache sana kusikia zikitangazwa- Mf. Ajali ya sauli kibaha
Ww haujasikiaa hiyo ya kibaha sauli anapata ajali mpaka millard anareport mpaka watu wakammind millard ni mnaz wa newforce
 
Dereva wa basi la Kampuni ya Saul T 485 DXE wamemshambulia abiria kisa kureport gari ikiwa na speed 115-120.

Kutokana na story ya muhusika anasimulia kuwa alikua na App ya kusoma speed ya gari na kutuma kwenye group la wasafiri mojawapo.

Baada ya muhusika kurecord tukio hilo kwenye group alipokea DM za vitisho kutoka kwa namba tofauti.

Baadae kidogo alipigiwa simu na dereva wa gari hilo na kumtaka asogee mbele yani atoke siti hiyo akakae mbele kwa dereva, alipofika dereva alimpokonya simu na kumtishia.

Baada ya safari kwenda kwa saa kadhaa bila muhusika kupewa simu yake ilifika hatua abiria huyo alitaka kushuka sehem inayoitwa Uyole wakati anataka kushuka walimzuia na kumtaka asishuke kwamba wanampeleka polisi kwa kosa la kurekodi na kuwachomea maovu yao.

Abiria alijitahidi kuwaomba na kuwasisitiza lakini waligoma na kuondoka nae pasipo kumpeleka polisi (utekaji huu).

Baada ya kufika mwisho wa safari walishusha abiria wote na kubaki wao madereva na baadhi ya watu wachache na kuanza kumhoji na kumpiga kwa kumlazimisha kusema nani amemtuma kurecord maovu ya kampuni yao ya SAUL na ilifikia hatua ya kumlazimisha amtaje moja ya mtu wa kampuni shindani ya New force.

Baada ya kipigo na vitisho vya muda mrefu walikagua simu na kujaribu kuweka namba za baadhi za watu waliohisi wao ndio wamemtuma ila walikuta abiria huyo hana namba za wahusika hao kabisa, ndipo walipomlazimisha kuformat simu yote na vitisho juu.

Baada ya muda walimuachia abiria huyo akiwa na majeraha maeneo ya mgongoni kutokana na kipigo walichomshushia.

Kutokana na taarifa hiyo inaonesha ukanda huo Dar mpaka Tunduma kumekuwa na ajali nyingi sana sababu ya rushwa na madereva kujiona tayari wameshika system.
Pole sana kaka. Na wewe ukakubali wakupige kabisa?
 
Wakati huyo abiria anafanyiwa hvyo ww ulkuwa bizy kupandisha nyuzi kumhusu huyo abiria badala ya kumnasua mwenzak na kipigo, So sad ,ila wakubwa tumeelewa kuwa mhusika huyo ni ww, ndo umeshushiwa kipigo, pole hapo jeraha la goti weka spirit, Next time panda ungo.
 
Mimi napenda basi linalokimbia sana
Huyo abiria siku ingine apande trekta litakaliendana na spidi yake atakavyo
Watu unataka kuwahi tuendako halafu mtu anataka dereva aendeshe basi mwendo wa konokono
Boss Kama unataka kuwah check na ATCL
 
Back
Top Bottom