Madeni ya Serikali yaiweka PSPF njia panda

Madeni ya Serikali yaiweka PSPF njia panda

Nimebaki kulia tu, maana mzee wangu katumikia nchi hii kwa miaka 33 akiwa kma daktari na sasa ana miaka 7 hajalipwa mafao yake, kila siku nai danadana tu. CCM Tutaonana 2015.
 
hapa kuna mchezo mbaya unaendelea na sijafuatilia zaidi kujua deni la taifa ambalo sasa limepita trillion 20 wanaodai serikali wengi huenda wakawa ni mafisadi.
Angalia sasa hivi hawa PSPF wanajenga jengo jirani na TRA makao makuu ambapo mkandarasi wake ni mtuhumiwa wa ufisadi na mbele ya hilo jengo kapewa tena jengo la TPA.
Sio kuwa naleta wivu wa kike bali ukiangalia milolongo kama hii inayoonekana kwa macho na ukaunganisha na isiyoonekana unajua ni mkondo wa ulaji pesa tu na ndio maana SSRA wakawahi na kuzuia watu wasijitoe kuepuka aibu
 
sasa nimeanza kuelewa sababu za watumishi waliostaafu tangu mwakajana kutolipwa mafao yao.
 
Fuatilia wamewekeza katika vitega uchumi gani? Vinaingiza mapato kiasi gani? Vitarejesha mitaji baada ya miaka mingapi? Wana Fungu kiasi gani kwa ajili ya mafao ya wastaafu? Wastaafu wanaongezeka katika kasi ipi nk utagundua kitu
 
Te te teh..! Shamba la bibi tamu..!

Ukistaafu utakapo anza kufatilia kiinua mgongo chako ndipo utakapo litambua hili, jamaa kung'ang'ani fao la kuto jitoa walikuwa wanawaza hizo Trilioni walizo gawana
 
Kukiwa na provision ya consensual subscription, ndio itakua mwisho ya hii mifuko ambayo obviously ni miradi ya wajanja wachache kupiga bingo without consequences/
Nani wa kuruhusu hiyo kitu kutokea? Mijitu na mindevu yao bado inachumia tumbo, the only solution ni kiing'oa meno ccm! Ccm ni zaidi ya jiwe.! Wote ni wazee wa kazi, I mean wazee wa deal, shamba la bibi ni tamu so wanalila haswa..!
 
Wajanja wamekula Trilioni kazi kwenu waajiriwa
nakumbuka miaka ya 80s mtu aliwahi kufungwa jela kwa kuharibu pesa iliyokuwa chini ya sh. 10,000 ya umma. Baadae miaka ya 90 ndio tulianza kusikia ukwapuaji wa kitu kama 30 million kabla ya kesi za wakati Mzee Mkapa anaingia ambazo tulipigwa butwaa pia kusikia mtu kaiba 120 million. Mwendo ulienda hivyo hadi ujio wa JK pale EPA ilipounguruma kwa 300 billion ambapo hakuna mtu aliyedhania kama kuna Mtanzania jasiri wa kuiba kiasi kama hicho cha pesa!
Sasa 2013 tunasikia watu wanaanza kukwapua TRILLION!!!!!!! na hakuna hata anayehojiwa bado, nini kitafuata labda mtu aibe benki kuu na hazina kuzimiliki ziwe zake binafsi!

 
Dah... Sijui mifuko mingine ina hali gani? Hii nchi imeliwa sana!
 
Serikali yaumbuka:• PSPF YAELEZA ILIVYOFILISIWA KWA DENI LA TRILIONI 6/-na Martin Malera, DodomaSERIKALI imekiri kuhusika kuufilisi Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kutokana na kushindwa kulipa zaidi ya sh trilioni 6.4 inazodaiwa.Fedha hizo zinatokana na malimbikizo ya madeni sugu na ya muda mrefu ya fedha za PSPF zilizokopwa na baadhi ya taasisi, zikiwamo za umma kwa kudhaminiwa na serikali.Hatua hiyo ilibainika jana wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) ilipokutana na uongozi wa PSPF na uiagiza serikali kuhakikisha inaanza kulipa madeni hayo na taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo kupelekwa mara moja kwenye kamati hiyo ndani ya wiki hii.PAC chini ya mwenyekiti wake Zitto Kabwe ilikutana na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), uongozi wa PSPF, Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na Wizara ya Fedha, kutaka kupata picha halisi ya tatizo la mfuko huo.Kamati hiyo ambayo imetoa wiki moja kwa serikali kuja na majibu imelazimika kuingilia kati kunusuru mfuko huo ambao umeelezwa kwamba umefilisika kutokana na uwezo wake wa kuwalipa wastaafu mafao yao kushuka kwa kiwango cha kutisha.Uwezo wa PSPF wa kuwalipa wastaafu hao mafao yao umeelezwa kuwa umeshuka kufikia asilimia 10 badala ya asilimia 40, kutokana na upungufu wa thamani ya mfuko huo unaofikia sh trilioni 6.4 hadi sasa.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu alikieleza kikao hicho kuwa kama malimbikizo ya madeni hayo hayatalipwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu kuanzia sasa, mfuko huo utakabiliwa na hatari ya kufilisika kabisa. Mayingu alisema malimbikizo ya madeni hayo yalianza baada ya serikali kushindwa kulipa sh bilioni 250.Alisema fedha hizo zilitakiwa zilipwe na serikali baada ya kuwaingiza watumishi wake kwenye mfuko huo ulipoanzishwa mwaka 1999.Mayingu aliendelea kuianika serikali kuwa kabla ya PSPF kuanzishwa, watumishi wa umma wastaafu walikuwa wakilipwa fedha za mafao yao kupitia Hazina.Alisema kikosi kazi kilichoundwa na serikali mwaka 1997, kilifanya tathmini na kubaini kwamba kama serikali isingekuwa imelipa fedha hizo sh bilioni 250 kufikia mwaka 2006, upungufu wa thamani ya fedha za PSPF ungefikia sh bilioni 658.Mayingu alisema pia mwaka 2003 ilifanyika tathmini nyingine na kubaini upungufu wa thamani ya fedha za PSPF za kuwalipa wastaafu ni sh bilioni 933.4.Vilevile alisema tathmini nyingine ilifanyika mwaka 2007 na kubaini upungufu wa thamani ya fedha za mfuko huo za kuwalipa wastaafu sh trilioni 3.3.Alisema kutokana na upungufu huo, uwezo wa PSPF wa kuwalipa wastaafu kipindi hicho ulishuka kutoka asilimia 93 hadi asilimia 43 na sasa umefikia kumi.Mayingu alisema kutokana na malimbikizo ya madeni hayo, hivi sasa upungufu wa thamani ya fedha za mfuko huo za kuwalipa wastaafu umefikia sh trilioni 6.4.“Thamani ya sasa ya kuwalipa wastaafu ni sh trilioni 6.4. wanachama wanaongezeka, muda unaongezeka na nakisi (upungufu) inakwenda, inakua. Tunaweza kufikia mahali tukashindwa kulipa,” alisema.Alisema hali hiyo inatokana na uwezo wa PSPF wa kuwalipa wastaafu hivi sasa kushuka kutoka asilimia 93 hadi asilimia 10.Kutokana na hali hiyo, alionya kuwa kama malimbikizo ya madeni hayo hayatalipwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu kuanzia sasa, mfuko huo utakabiliwa na hatari ya kufilisika kabisa. Alisema kuanzia mwaka 2010, serikali ilichukua dhima ya kulipa sh bilioni 71, lakini hadi sasa haijalipa sh bilioni 716.“Ukishaonesha kushindwa kuwalipa watumishi imani itawavunjika,” alionya Mayingu.Alishauri kwamba pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni hayo, serikali pia inapaswa kuongeza michango kutoka asilimia 15 za sasa hadi asilimia 25 ili kufidia upungufu uliopo.Katika maagizo ya PAC, waliitaka serikali kulipa fedha hizo kwa kuanza kutoa sh bilioni 50 kwa mfuko huo.Pili kamati hiyo imetoa siku saba kwa serikali kuja na majibu kamili baada ya jana kudai kuwa hawakujiandaa.Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka alisema kulingana na tathmini waliyoifanya, wamebaini kuwa PSPF ina hali mbaya.Alisema kutokana na hali hiyo, Machi mwaka huu, walitoa mwongozo, ikiwamo kutaka wanachama wa mfuko huo kutolipwa kiasi chote, bali kile tu walichochangia.Irene alisema mbali na mwongozo huo, pia wanashauri pamoja na mambo mengine, serikali kulipa sh trilioni 1.2 ambazo ni sawa na asilimia 70 ya malimbikizo ya madeni kufidia upungufu wa thamani ya fedha za PSPF za kuwalipa wastaafu mafao yao.Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene alisema wanakubali kwa asilimia 100 kwamba PSPF inaidai serikali.Hata hivyo, alisema kwa sasa serikali haiwezi kutoa kiasi hicho cha fedha kwani kinaweza kuathiri mipango mingine ya maendeleo.“Itabidi tujipange upya na kuanzia sasa kipaumbele cha serikali itakuwa ni kurejesha fedha hizo. Kwa mwaka huu tutatoa sh bilioni 50,” alisema.WATUMISHI WAMEGAWANYIKA KIMASILAHI, VYAMA VYA WAFANYAKAZI (CWT, TUGHE, RAAWU, TAWLGU, nk)! Political investment/inetrest!WATUMISHI WAKUMBUKE WENZAO WA EAC ( until 1977): Wanavyoandamana/lala barabarani kufuatia mafao yao! HILI NALO LITAWAPATA WAFANYAKAZI. UGIRIKI - Mafao yamepunguzwa na serikali kwa kuwa serikali imefilisika!
 
By The guardian reporter
25th April 2013

PSPF acting Director General, Adam Mayingu
The Public Service Pension Fund (PSPF) will collapse in three years’ time if urgent steps are not taken to rescue it by injecting more funds, Parliament was told here yesterday.
Briefing the Parliamentary Standing Committee on Public Accounts, PSPF acting Director General Adam Mayingu said his organization is “currently in a serious financial crisis.”

He said the Fund’s financial liabilities were growing more than the increase of contributions and investment income, making payment unsustainable.
He said the best practice required a Fund to have a funding of around 80 percent of its liabilities but PSPF is currently 10.1 percent funded.
“If this trend is not checked immediately, PSPF will in the near future resort to government to meet the liabilities of its members,” he said.

The Public Accounts Committee (PAC) summoned the PSPF management and the Social Security Regulatory Authority (SSRA) to Dodoma yesterday to try to get a clear picture of the Fund, including looking for means to address its precarious financial position.
Deputy finance minister Janeth Mbene and the Deputy Permanent Secretary Elizabeth Nyambibo attended the meeting.

Explaining, Mayingu said the financial crisis was initially triggered by failure by the government to inject 250bn/- as a response to address the pre-July 1999 actuarial deficit.
He said the same report that came up with the actuarial deficit of 250bn/- also projected that the liabilities would jump to 658.23bn/- in year 2006 of which it would need raising the contributions to meet the liabilities.
In explaining how things went from bad to worse for PSPF, Mayingu said in 2003 before the Fund started paying benefits, the first official actuarial valuation was conducted showing a deficit of 933.4bn/-.

The shortfall was to be paid by the government as the liability related to the period when the scheme was non-contributory (before 1999). The funding level at the time of valuation was 93.3 percent, he said.
“However, the government did not pay despite the Fund’s effort to make a follow-up,” he noted.

He explained that the second actuarial valuation was conducted in 2007 after the Fund started paying benefits. In that valuation it was noted that the financial position of the scheme had deteriorated further mainly due to non-repayment of liabilities in respect of the pre-July 1999 actuarial deficit, this time reaching 3.3trn/-.
Mayingu said PSPF’s board of trustees tabled the report of the second actuarial valuation to the government, the defunct Public Corporations Accounting Committee (POAC), for action after which the Controller and Auditor General and the Social Security Regulatory Authority (SSRA) to verify authenticity of the liability.

According to Mayingu, the third actuarial valuation was conducted in 2010. In this valuation SSRA and the Bank of Tanzania (BoT) undertook the task to establish an independence of the results after which it was established that the Fund’s financial situation had further deteriorated with the liability reaching 6.4trn/-.
The third actuarial valuation observed that the Fund was 10.1 percent funded compared to 43.9 percent in 2007.
Mayingu said that the non-repayment of the liabilities has been a challenge to the scheme as it increases its financial burden.

He said several government entities borrowed from the Fund under government guarantee but such entities have failed to honour their commitments.
Minister Mbene responding acknowledged the debt the government owed PSPF, stating that in the 2013/2014 financial year a total of 50bn/- would be paid to the Fund.
PAC ordered the government, SSRA and PSPF to ensure the allocated 50bn/- is paid to PSPF and report back to it in a week’s time.
SOURCE: THE GUARDIAN
 
Je mnajua kuwa kulikuwa na versions 3 za CAG reports ambazo zote zimefichwa from the public?

Yes Ludovick Utouh either kwa kuambiwa au kwa kusudi ameamua kuwa wasiweke ile ripoti ya mahesabu ya PSPF wazi japo ni pesa za pensheni zinazolipwa na idara zote za serikali.

Sasa policy makers na REAL decision makers washa maliza mchakato wa kuifunga PSPF kwa sababu apart from mambo mengine ni kuwa hakuna justification ya serikali kuendelea kufanya baby sitting ya mfuko huu.

Cha ajabu ni kuwa mpaka actuarial valuation ya huu mfuko ulishawapa picha kamiili kuwa hauna muda and its just a matter of time.

Maswali kwa wana JF:

1. Mnajua kuwa iliundwa taskforce kama iliyoundwa NIC na ilipeka ripoti kwa wahusika? Mnajua kwa nini ile ripoti ilifichwa?

2. Mnajua Actuarial Valuation ya PSPF ilifanywa na nani na alilipwa kiasi gani kwa fedha za madafu? na kigogo gani ali recommend alipwe kiasi hicho?

3. Mnajua kwa nini hiyo valuation report ilifichwa?

4. Mnajua SIRI ya Ludovick Utouh (CAG) kutoa ripoti 3 tofauti?

5. Mnajua kwa nini ile ripoti nyingine imefichwa?


So much so for OPEN GOVERNMENT INITIATIVE...ukweli ni kuwa wale wenye akili zao kule mitaa ya Lithuli na Magogoni washaliona hili dude ni NOT VALUE FOR MONEY & PURPOSE and its just a matter of time habari ya kulivunjwa itatolewa lakini kama kawaida mtapewa majibu ya mkato mkato na yote kwa sababu hao wanaotegemewa kuuliza maswali magumu naya ndani wako bize wakipeana mipasho ya CHADEMA vs CCM ili mpotezwe lengo

Usiku mwema.
 
SSRA kupitia mkurugenzi mkuu wake wamewahakikisha wanachama wote kuwa, mafao yao hayataathirika, kwahiyo hakuna cha kuofia hapa.
 
Kwa sisi watumishi, hakika patachimbika aisee
 
mkuu unatuuliza sisi maswali tena?, wewe ndio unajua, thread imekaa kimbea mbea sana
 
Je mnajua kuwa kulikuwa na versions 3 za CAG reports ambazo zote zimefichwa from the public?

Yes Ludovick Utouh either kwa kuambiwa au kwa kusudi ameamua kuwa wasiweke ile ripoti ya mahesabu ya PSPF wazi japo ni pesa za pensheni zinazolipwa na idara zote za serikali.

Sasa policy makers na REAL decision makers washa maliza mchakato wa kuifunga PSPF kwa sababu apart from mambo mengine ni kuwa hakuna justification ya serikali kuendelea kufanya baby sitting ya mfuko huu.

Cha ajabu ni kuwa mpaka actuarial valuation ya huu mfuko ulishawapa picha kamiili kuwa hauna muda and its just a matter of time.

Maswali kwa wana JF:

1. Mnajua kuwa iliundwa taskforce kama iliyoundwa NIC na ilipeka ripoti kwa wahusika? Mnajua kwa nini ile ripoti ilifichwa?

2. Mnajua Actuarial Valuation ya PSPF ilifanywa na nani na alilipwa kiasi gani kwa fedha za madafu? na kigogo gani ali recommend alipwe kiasi hicho?

3. Mnajua kwa nini hiyo valuation report ilifichwa?

4. Mnajua SIRI ya Ludovick Utouh (CAG) kutoa ripoti 3 tofauti?

5. Mnajua kwa nini ile ripoti nyingine imefichwa?


So much so for OPEN GOVERNMENT INITIATIVE...ukweli ni kuwa wale wenye akili zao kule mitaa ya Lithuli na Magogoni washaliona hili dude ni NOT VALUE FOR MONEY & PURPOSE and its just a matter of time habari ya kulivunjwa itatolewa lakini kama kawaida mtapewa majibu ya mkato mkato na yote kwa sababu hao wanaotegemewa kuuliza maswali magumu naya ndani wako bize wakipeana mipasho ya CHADEMA vs CCM ili mpotezwe lengo

Usiku mwema.
Tarehe 23/03/2013 jioni mnamo saa kumi na mbili jioni kuelekea na nusu hivi niliwahi kuona document ya siri ya PSPF.na muda kidogo juzi baada ya kuanza bunge mambo yakafumuka zaidi.lakini document niliyoina ilikuwa na maelezo ya kufilisika kwa mfuko huu na matatizo mengine.hata wewe mleta uzi huu ninakusoma vema.nini kifanyike?
 
Back
Top Bottom