Madawa ya Kulevya na aibu ya Tanzania - Yatosha sasa!

Ninavyofahamu kuna aina kuu mbili za vita za madawa ya kulevya
  1. Vita ya serikali dhidi ya watumiaji na wauzaji wa madawa ya kulevya
  2. Vita baina ya magenge
Katika aina hii ya vita Serikali ,kwa mikakati maalum na kutumia vyombo vyake maalum
hupambana na watumiaji na wauzaji/wasambazaji wa madawa ya kulevya .Vita hufanywa
bila ya ubaguzi wa aina yoyote ,uwe wa dini , kabila, rangi, jinsia, vyama vya kisiasa au kijamii nk

Aidha katika aina hii magenge (kundi moja dhidi ya kundi/makundi)
hupambana yenyewe kwa yenyewe kutafuta ukuu/ukiritimba (supremacy/monopoly) katika biashara hiyo. Hapa mbinu zote hutumika ikiwemo ''kuchomekeana'' kwa polisi.

Kwa mtazamo mh.Makonda anapambana vita aina ya pili, iwe kwa hiari yake au kwa kushinikizwa.

Ninawaomba wanaJF tunapojadili humu tutilie maanani hayo hapo juu.
Tuweke mbele maslahi ya taifa letu la Tanzania tuache ushabiki wa vyama kwenye hili.
Nina imani Rais wetu JPM anayo nia ya kupigana vita aina ya kwanza.
Tumsaidie, tumuunge mkono,asipotoshwe kama ilivyo tukaingia gharama za kupigana vita binafsi

Ninawasilisha.
 
Katika vyombo vya habari tofauti leo vimeripoti kuwa baadhi ya wakuu wa mikoa wakizungumzia hili sakata la madawa ya kulevya wamewataka wananchi kuwasilisha majina ya washukiwa Polisi ili yafanyiwe uchunguzi na kama wanahusika wachukuliwa hatua stahiki.

Hapa ndipo najiuliza je huyu mkuu wetu wa Dar alikosa hii busara au hana uelewa huu !?

Pia kwa tetesi nilizo zisikia kuwa wale wafanya biashara wakubwa waliotajwa na Mh. huyu , tayari watakuwa. Wameingia kwenye hasara kubwa kibiashara na pia kwa sheria za nchi za ughaibuni kama unatuhumiwa kuhusika na madawa ya kulevya huruhusiwi kuingia katika nchi hizo hadi pale utakapo safishwa na nchi iliyo kuchafua.

Je, Mh huyu kesha jianda na sabuni na jik za kutosha kuwasafisha hawa alio wachafua?

Kwa tetesi nyepesi nyepesi nasikia tayari mfanyabiashara mmoja mkubwa ambaye ametajwa kwenye sakata hili amepokea simu toka kwa washirika zake wa ughaibuni kumlaumu mshirika mwenzao kwa kujihusisha na biashara hii haramu na hadi hivi sasa biashara zake ziko matatani kwani washirika zake wamepatwa na taharuki kubwa na wanashindwa kuamini maelezo yake hivi sasa!!

Hili jambo kwa hisia zangu naona laweza kuliingiza taifa letu kwenye hasara kubwa !!

Niwakati wa Kuliombea Taifa letu ..... !! Ewe Mola tunaomba uwafanyie wepesi wale waliotajwa kimakosa katika sakata hili na uwasafishe na Uchafu huu.

Pia tunaomba Uwape Busara Viongozi wetu walio kosea katika utendaji wao ili wajirekebishe na kuweza kuisimamia haki katika Taifa letu..!! Ameen.
 
Siku zote ku copy ni karama na usije ukacooy kitu kwa mtu ukawa sahihi kwa 100% na hasa kwenye utawala na uongozi kwani mazingira yanatofautiana kati ya nchi na nchi na jingine kwa nchi kubwa lazima itofautiane na nchi ndogo ambao kwa ujumla ina makabila machache na mila na desturi hazitofautiani sana tofauti na nchi kubwa ambayo inamakabila mangi ya mila zao zinatofautiana kutokana na maeneo walikotoka! Mfano mzuri ni vipi kabila kubwa au nchi kubwa kama congo ya DRC kwenda kukopi uongozi wa gambia ,Benin, Burundi na hata Rwanda uwashawishi WA congomani wafuate mila na desturi za kihutu hapo lazima patakuwa na sintofahamu! Je kwetu itafikia hayo itakuwaje?
 
Katika vyombo vya habari tofauti leo vimeripoti kuwa baadhi ya wakuu wa mikoa wakizungumzia hili sakata la madawa ya kulevya wamewataka wananchi kuwasilisha majina ya washukiwa Polisi ili yafanyiwe uchunguzi na kama wanahusika wachukuliwa hatua stahiki.

Hapa ndipo najiuliza je huyu mkuu wetu wa Dar alikosa hii busara au hana uelewa huu !?

Pia kwa tetesi nilizo zisikia kuwa wale wafanya biashara wakubwa waliotajwa na Mh. huyu , tayari watakuwa. Wameingia kwenye hasara kubwa kibiashara na pia kwa sheria za nchi za ughaibuni kama unatuhumiwa kuhusika na madawa ya kulevya huruhusiwi kuingia katika nchi hizo hadi pale utakapo safishwa na nchi iliyo kuchafua.

Je, Mh huyu kesha jianda na sabuni na jik za kutosha kuwasafisha hawa alio wachafua?

Kwa tetesi nyepesi nyepesi nasikia tayari mfanyabiashara mmoja mkubwa ambaye ametajwa kwenye sakata hili amepokea simu toka kwa washirika zake wa ughaibuni kumlaumu mshirika mwenzao kwa kujihusisha na biashara hii haramu na hadi hivi sasa biashara zake ziko matatani kwani washirika zake wamepatwa na taharuki kubwa na wanashindwa kuamini maelezo yake hivi sasa!!

Hili jambo kwa hisia zangu naona laweza kuliingiza taifa letu kwenye hasara kubwa !!

Niwakati wa Kuliombea Taifa letu ..... !! Ewe Mola tunaomba uwafanyie wepesi wale waliotajwa kimakosa katika sakata hili na uwasafishe na Uchafu huu.

Pia tunaomba Uwape Busara Viongozi wetu walio kosea katika utendaji wao ili wajirekebishe na kuweza kuisimamia haki katika Taifa letu..!! Ameen.
Hahahhahaaaa! Wananchi wapeleke majina kwa siri. Kisha polisi wachunguze kwa siri halafu majina yawe siri halafu na kesi ziendeshwe sirini so interesting ili wananchi wasiwatambue na wasije wakaumbuka. Coz wengi wao ni watu maarufu, wanasiasa, wafanyabiashara, wafadhiri na wadhamini, wengine ni viongozi wa NGO mbalimbali. Stupid.
Nimeipenda ya makonda kuwa tutawangaza waziwazi ili hata watoto wadogo wawajue kuwa hawa ndio ama watumiaji au wasambazaji au watuhumiwa,! Ili watoto wetu wapone wakiwaona tu wajue kuwa karibu nao sio salama kwao.!!
Kwa kufanya hivyo jamii yetu itapona. Endeleeni kumponda endeleeni kufanya siasa lakini ukweli umejulikana kuwa wengi wenu mpo kwa fadhira za mabwana zenu wanaofanya hii biashara jipu limeshatumbuka.
 
vyote vinawezekana tu ila watu wanapiga pesa nakusepa katika miradi na harakati mbalimbali kwani ukuonaga au kusikia kuhusu mapambano dhidi ya malaria semina kibao shoo kibao wapambanaji kibao mpaka vyandarua kibao ila dah tukiamua tunaweza ...!?
 
Time will tell !! Vita kama hii haipiganwi kijinga hivi !! Ushamba unawasumbua....!!
 
Time will tell !! Vita kama hii haipiganwi kijinga hivi !! Ushamba unawasumbua....!!
Bila shaka na watu wa mjini wanafanana na wewe huishi kwa kutegemea hisani za watu, hongera sana mkuu, na wewe ulienda kufuta gari ya manji pale polisi? Au ulikuwa kwenye kwaya.!
 
vyote vinawezekana tu ila watu wanapiga pesa nakusepa katika miradi na harakati mbalimbali kwani ukuonaga au kusikia kuhusu mapambano dhidi ya malaria semina kibao shoo kibao wapambanaji kibao mpaka vyandarua kibao ila dah tukiamua tunaweza ...!?
Makampuni ya madawa ni biashara kubwa sana na wanapesa na ndio wahujumu wakubwa wa kampeni hizi za malaria.
 
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ametaja kasoro kadhaa katika zoezi la vita ya dawa za kulevya lililoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.

Amesema, Kwanza, Mkuu wa Mkoa hana mamlaka yoyote ya kuelekeza watu kwenda kuripoti polisi. Hii ni licha ya mamlaka yake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na mamlaka yake ya kipolisi yapo chini ya Sheria ya Tawala za Mikoa.

Pili, kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Jinai, kila mtu ana wajibu wa kutoa taarifa ya kosa la jinai analoona limetendeka kwa polisi. Hii ni ile inayoitwa kufungua RB. Mkuu wa Mkoa Makonda alitakiwa afungue RB kwa wote anaowatuhumu kufanya biashara ya madawa. Hajafanya hivyo na ni kosa la jinai kutokufanya hivyo.

Tatu, kwa kutumia mamlaka yake ya kipolisi, Mkuu wa Mkoa Makonda alikuwa na uwezo wa kuamuru wale wote anaowatuhumu kufanya biashara ya madawa kukamatwa na kuwekwa kizuizini kwa masaa 48 na baadae kufikishwa mahakamani. Badala ya kuamuru 'wahalifu' hawa wakamatwe, Mkuu wa Mkoa Makonda aliwaelekeza wajipeleke polisi kwa mahojiano.

Nne, kwa kuzingatia hatari kubwa ya madawa ya kulevya kwa jamii yetu, sheria husika za nchi zimeweka adhabu ya chini kabisa ya kifungo cha miaka 20 kwa wanaothibitika na mahakama kuhusika na biashara hiyo. Aidha, makosa ya madawa ya kulevya hayana dhamana kisheria. Iweje wale wote waliotuhumiwa na Mkuu wa Mkoa Makonda wamepelekwa mahakamani lakini wote wamepewa onyo tu au wamepewa dhamana Mahakamani.

Kati ya mapolisi 11 waliotuhumiwa, hakuna hata mmoja aliyepelekwa mahakamani na kushtakiwa kwa tuhuma hizi. Badala yake, tunaambiwa wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa polisi dhidi yao. Kwa mujibu wa Sheria zetu za ajira, mtumishi anayesimamishwa kazi analipwa mshahara kamili kwa muda aliosimamishwa

Tano, kitendo cha kuwatangaza watuhumiwa kwa namna alivyofanya Mkuu wa Mkoa Makonda, kesi yoyote itakayofunguliwa dhidi yao itaharibika. Kila mtuhumiwa atajitetea kwamba amekamatwa na kushtakiwa kwa sababu za kisiasa na kwa amri haramu za Mkuu wa Mkoa. Kila mtuhumiwa atajitetea kwamba hakuna RB yoyote iliyofunguliwa dhidi yake na kila wakili wa utetezi atataka Mkuu wa Mkoa Makonda aitwe mahakamani kwa ajili ya kuhojiwa. Makonda ataliwa nyama na mawakili kwenye cross-examination. Kwa kifupi, hii sio vita dhidi ya wauza 'unga', hii ni political charade na character assassination inayofanywa kwa mbinu za ovyo kabisa bila kufuata sheria Haitafika popote.
 
Nafikiri pale bungeni wako wanahusika pia na hii mambo, wakamatwe na wao na asiachwe hata mmoja. Hawa ni wasaliti kwetu na ni lazima tuwageuzie mitutu yetu, ama wao ama sie. We must squeeze them
 
Back
Top Bottom