• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Madawa ya Kulevya na aibu ya Tanzania - Yatosha sasa!

n00b

n00b

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2008
Messages
981
Points
500
n00b

n00b

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2008
981 500
1198746_masogange-mbwembwe.png
Hatuwezi kuendelea kukaa kimya. Taifa letu linaaibika vibaya sana.

Wahusika wanajulikana. Wametajwa mara nyingi na mbinu wanazozifanya kwa kutumia wasanii wa kizazi kipya na waigizaji almaarufu kama 'Bongo Movie'.Inaudhi, inakera na inatuongezea chuki sana kwa serikali iliyo madarakani. Kaeni kimya na endeleeni kulichafua taifa, kuna siku mtatueleza yote. Au kwakuwa wahusika ni wanenu? Au kwakuwa wakuu wa juu ni wale waliowawezesha kuingia madarakani kisiasa?

Ndugu zangu, hii ni aibu kubwa kwa Taifa. Inasikitisha sana na inazidi kutuaibisha wengine tunaosafiri ng'ambo. Taifa kama halina rais, taifa kama halina Vyombo vya Dola. Ni upumbavu, ni ufedhuli na mtambue sasa tumechoka. Sasa, tunaanza kuziweka habari za kila anayekamatwa na madawa hadharani, tunaanza kuweka hadi wanaowatuma. Tutawafikia mapapa wote!

Mambo haya mlimchomekea mtoto wa Mengi, mambo haya mnawachomekea wanyonge wenye njaa kali na hadi mmeua vijana wetu kwa kuwabebesha mizigo michafu hivi!

Kwa ambao hamjasoma habari hii ya aibu, someni hapa:

Wanawake wawili raia wa Tanzania wametambuliwa kuwa ndiyo wanaodaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

Akizungumza na NIPASHE jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.

Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.

Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.
Someni zaidi hapa Watanzania Wawili wakamatwa South Africa na Madawa


USHAURI KWA VIJANA WA KITANZANIA:
Hakuna mtu asiyependa utajiri lakini utajiri unaweza kupatikana bila kufanya biashara haramu au kujihusisha na mambo ya kuhatarisha maisha yako. Kwa miaka ya karibuni kumekuwa na Watanzania wengi wanajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya na wanaofaidika ni wachache tu wengi wao wanaishia kupata pesa ndogo na wanahatarisha maisha yao kwa kufugwa, kifungo cha kifo na hata madawa kupasuka tumboni na kuwaua. Kabla hujapata utajiri wa kudumu unatakiwa kupenda maendeleo kwanza na sio sifa pekee kwenye jamii. Fanya yafuatayo na polepole utafanikiwa.

1. Tafuta mtu ambaye unataka kuwa kama yeye: Usiangalie ukabila udini wala rangi ya mtu. Kama unataka kuwa kama Mengi, Mkono, Manji, Wanasiasa, wasomi au hata wasomi wa kimataifa wanaofanya kazi kwenye UN, World bank, diasporas. Tafuta mtu mmoja au wawili na waombe wawe kama walimu wako. Usiogope kutafuta utapata mtu na fuata wanayo kuambia hata kama wewe huoni umuhimu kwa sasa.

2. Jiendeleze kielimu: Hakuna mtu ambaye hawezi kufanya hili hata kama ni polepole. Elimu sio lazima iwe ya degree kwani duniani sasa kazi zinazolipa hazifundishwi kwenye degree bali certification mfano sasa tuna gas jifunze ufundi wa machine za kuchimba mafuta, project management, computer language, database kama SAP,Oracle, dot.net. Vilevile kuna Veta tafuta kitu ambacho kinauhusiano na Gas na Oil. Kwa ujumla jiwekee utamaduni wa kujiendeleza.

3. Marafiki: Tafuta marafiki ambao wanakusaidia kujiendeleza na wanakupenda badala ya wale wanaotaka kukutumia na wanao ku support kinafiki. Kama huna marafiki wazuri tafuta uhusiano wa kuomba kama mtanzania mwenzako omba urafiki kama Watanzania walivyokuwa wanafanya miaka ya zamani. Marafiki wabaya watakupeleka jela na kukuingiza kwenye ushabiki wa kimaisha na kukutumia.

4. Acha kulalamika: Kama unataka kuendelea uache utamaduni wa kulalamika badala yake jiulize je ni kitu gani naweza kufanya kufanikiwa bila kuiba. Tabia nzuri inaweza kukupeleka mbali kuliko unavyofikiri pesa pekee sio sababu ya kushidwa kuanza bali mara nyingi ni tabia. Ukiwa na tabia nzuri na kujihusisha na watu wazuri pesa haitakuwa kigezo.

5. Nenda ugaibuni kama umeshidwa yote: Kama yote umeshidwa na mazingira uliyo nayo si mazuri labda kabla ya kujihusisha na biashara haramu jitoe kwenye mazingira uliyopo. Kama bado ni kijana na mambo hayaendi yote hapo juu tafuta njia za kwenda nje lakini hayo mambo hapo juu inabidi uyafuate hata kama uko ugaibuni.

6. Uvumilivu: Hii nitakupa mfano wa ukweli kabisa. Watanzania wengi tulikuwa USA miaka ya 1996-2000 kutafuta maisha kwenda shule n.k. Watanzania wote tuliishi pamoja na mimi nilikuwa mojawapo pale Houston, TX tulifanya kazi pamoja umri ulikwa kama sawa tu kwa ufupi tulianza wote kwenye zero. Baaada ya miaka michache Watanzania wengine walihusisha na biashara, wengine shule, wengine mission town deals. Waliopiga deal walichukua pesa na kukimbia Tanzania na hawa walienda na magari, pesa na walipata wanawake, wanaume wanaowataka nyumbani. Wengi wao walienda bila kumaliza shule au kujifunza biashara.

Waliobaki makundi mawili wanaofanya kazi na kwenda shule na wanaofanya kazi lakini hawaendi shule. Wale walioenda Tanzania wengi wao wameishiwa na hawawezi kuja kwani ni wezi. Wengine walifungwa kabla hata ya kwenda Tanzania na walirudishwa bila kitu. Waliobaki ambao hawakwenda shule ndiyo sasa wanaanzan kwenda shule wakiwa na miaka 35 au zaidi. Walioenda shule hata kama kwa shida wanafanya vizuri sana na community imekuwa na watu wenye mafanikio kiuchumi kuliko community nyingi za Kitanzania duniani. Kuna Watanzania ambao ni VP wa kampuni kuna Watanzania wengi sasa wanatengeneza $50,000 mpaka $120,000 kwa mwaka kwenye mishahara. Hivyo maisha si kuiba tu unaweza kufanikiwa bila kuiba.

Alex Masawe ni tajiri mkubwa sana wa Kitanzania laikini kwasababu kapata utajiri wake kwa kuiba na hata kuua sasa kwenye miaka karibu sabini ndiyo anaenda jela badala ya kutumia pesa alizopata anaenda jela. Serikali inaweza kutaifisha mali zake hivyo uwizi wote huo aliofanya miaka yote ameishia wapi!!. Usisikilize watu wanaokuambia huwezi kufanya kwani si ukweli
*************************************

Habari zaidi ndani ya JF:

*************************************
- CHADEMA yatoa tamko baada ya Mbowe kutajwa katika listi ya Makonda

- Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...
- News Alert: - Rais Magufuli apigilia msumari jeneza la wauza Dawa za Kulevya, asema si kazi ya Makonda pekee
- Mbunge wa Kinondoni umefeli kupambana na Madawa ya kulevya!
- Tuseme: Makonda, Haya hapa Majina ya Wauzaji Madawa ya Kulevya wakubwa
- MADAWA YA KULEVYA: RC Makonda na Kamanda Sirro waongea na waandishi wa habari

- Updates: Wasanii Waitikia wito wa Makonda Kufika Polisi
- DAR: RC Makonda awataja Askari 9 watuhumiwa kushirikiana na mtandao wa Dawa za Kulevya. Wamo wasanii
- Hii ndio hali ya Nando (Mshiriki wa BBA) baada ya kuathirika na matumizi ya madawa ya kulevya

- Biashara ya Madawa ya Kulevya Tanzania: Who is Pulling the Strings? [September, 2010]
- Madawa ya Kulevya Tanzania, Serikali Yetu Hamyaoni Yanatumaliza? [March, 2011]
- Madawa ya kulevya: Rais Kikwete akutana na mawaziri, wakuu wa mahakama na polisi [2013]
- Kuficha watuhumiwa wa madawa ya kulevya... Wananchi, tufanye nini? [July, 2011]
- Madawa ya Kulevya - Aina na Athari zake kwa Mtumiaji [February, 2012]

- Dawa za kulevya: Watanzania watatu wakamatwa India, mmoja afariki
- Mafia wa Italia na mihadarati Tanzania [December, 2012]
- Mihadarati (Madawa ya Kulevya) yaivuruga CCM! [November, 2006]
- Wajumbe Baraza la Wawakilishi Zanzibar watuhumiana kuhusika na Mihadarati (Madawa ya Kulevya) [June, 2011]

- Serikali kuanika vigogo wa Madawa ya Kulevya bungeni [July, 2011]
- Madawa ya Kulevya: Alivyotoroshwa Nurdin Akasha...
- Mtanzania akamatwa na madawa ya kulevya Chicago, U.S.A.

- Mtanzania akutwa na madawa ya kulevya uwanja wa ndege wa Marekani-Texas tumboni kwake
- Rais Obama amtaja mfanyabiashara wa madawa ya kulevya mwanamke wa kitanzania aishie Mbezi
- Polisi wamnasa muuza dawa za kulevya wa kimataifa aitwaye Leila...
- Kikwete 'awapakazia' viongozi wa dini biashara ya madawa ya kulevya

- Pengo: Wananipakazia madawa ya kulevya!
- Dadake mbunge Munde Tambwe (CCM) akamatwa na dawa za kulevya!
- Kangi Lugola, mbunge CCM atuhumu Mawaziri ni wauza mihadarati! Serikali yawatetea, awekwa kitanzini!
- Mtandao wa uhalifu Polisi... Wahusishwa na mauaji, biashara ya mihadarati na ulaji rushwa!

- Mfanyabiashara jamaa ya Mbunge akamatwa na Shehena ya Madawa ya Kulevya
- Mtangazaji wa redio kutoka Tanzania amekamatwa na dawa za kulevya Kenya!
- Mtoto wa Liyumba akamatwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya Bil 9 Tsh

- Wapakistan waliokamatwa na madawa ya kulevya ya billion 6 waachiwa kwa dhamana!
- Picha: Msichana wa KITANZANIA aliyekamatwa na Unga EGYPT kunyongwa...
- Madawa ya Kulevya: Mabondia wa Tanzania wafungwa miaka 15 nchini Mauritius!

- Watanzania Wawili wakamatwa South Africa na Madawa
- Watanzania wawili wakamatwa na madawa ya kulevya Hong Kong
- Binti ashikwa na Madawa ya Kulevya JNIA; Polisi wa usalama waomba Rushwa wakataliwa...
- Mtanzania afungwa jela miaka 15 Zimbabwe kwa kukutwa na madawa ya kulevya

- Wafungwa wa Kitanzania waliokamatwa na madawa ya kulevya Hong Kong wafunguka!
- Kilumbe Ng'enda: Mbunge Azzan Anahusika na Biashara ya Dawa za Kulevya

- Mtanzania akamatwa na madawa ya kulevya US
- Mapapa wa madawa ya kulevya watajwa, wamo Morine Amatus Liyumba na mdogo wa Rostam Aziz
- Kumekucha Madawa ya Kulevya: Kina 'Masogange' wawataja waliowatuma!

- Mtambo wa Dawa za kulevya waingizwa nchini, upo Mbezi Beach!
- Serikali sasa kuanzisha mahakama ya madawa ya kulevya...!!
- Madawa ya Kulevya: Mashine mpya zafungwa JKIA
- Bungeni Live: Hoja juu ya Madawa ya Kulevya
- CHADEMA watoa tamko kuhusu madawa ya kulevya
- Vita dhidi ya madawa ya kulevya: Waziri akiri wauza unga kuifadhili CCM, Nzowa aizamisha Jambo leo
- Sakata la madawa ya kulevya: Kamanda wa polisi viwanja vya ndege ahamishwa
- Sakata la madawa ya kulevya: Viongozi wachunguzwa na kuhojiwa
- Majina ya Majaji wanaolinda wauza madawa ya kulevya yatajwa! Wamo Pendo Msuya na Dr Fauz Twalib
- Mtanzania adakwa na mihadarati China
- Mtanzania akamatwa akiwa na Madawa ya Kulevya United Arab Emirates (UAE)

- Mshambuliaji wa zamani wa Simba akamatwa na madawa ya kulevya...
- Mbwana Matumla akamatwa na madawa ya kulevya Spain
- Madawa ya Kulevya: Matumla na Kaniki wakamatwa!

- Mtanzania aliyekamatwa na madawa ya kulevya Dubai amlaumu mumewe
- Madawa ya Kulevya: Meli ya Tanzania iliyobeba unga wa Sh. Bilioni 123 yazua kizaazaa nchini Italia!
- Ripoti UN: Tanzania kinara dawa za kulevya
- Uchochoro wa kuvusha dawa za kulevya Dar huu hapa
- Baadhi ya njia zinazotumika kupitisha madawa ya kulevya uwanja wa ndege JKNIA
- Madawa ya kulevya: Mtanzania afia Dubai, wengine wadaiwa kukamatwa China na Brazil
- Madawa ya Kulevya: Aisha Bui (mke mwenza na Amina chifupa) naye akamatwa Brazil
- Mwanajeshi Rashid Mohamed akamatwa na mirungi kilo 20 huko Tanga
 
Jackline Aloyce

Jackline Aloyce

Senior Member
Joined
Aug 31, 2016
Messages
112
Points
225
Jackline Aloyce

Jackline Aloyce

Senior Member
Joined Aug 31, 2016
112 225
nawe unaeamini serikali inapambana na wauza dawa za kulevya ni jinga la majinga.!
hata yule mange nae hawajui..anapewa info na zote zinahusu kambale..nyangumi hawajui.na ili uwaumbue tu hawa watu must uwe mtu wa karibu na system na pia upate ushahidi.
refer to amina chifupa..alipata ubunge na kuwa nao close...akatangaza vita walampoteza kwa kifo cha ghafla!
kuna alietangaza nia ya dhati kupamnana na dawa za kulevya baada ya amina?

leo mkawa mnamshangilia makonda
bila kujua huyu kijana no kibaraka wa walewale
makonda alipewa go on na mzee juma iwe kama kiki..manyangumi wakakutana mkuu wa kaya akatoa wasiwasi mpo salama..msihofu!
wakaanda list ndeefu ya kambale na dagaa ikiwemo hawa mapunda na mateja wanaomwaga udenda mitaani..mnashangilia wee!!
eti vita ya kupambana na madawa unakamata mateja...eti kila mzaz ataekutwa na kijana mtumiaji sheria i juu yake
hata lissu aliongea wee nyangumi mbona wanaachwa..
hivi leo ukishamiri ushirikina watu wanalogwa wanakufa wengine wako hoi kitandani..utawakamata hao waliologwa ili kukomesha uchawi eenh? halafu mnashangilia wee

sasa sikilizeni:
biashara ya dawa za kulevya ilianza tangu enzi za nyerere...na alieianzisha ni kiongozi mkubwa tu ndani ya serikali baada ya kuona inalipa
baadae wengine wakafuatia.
vigogo na watoto wao wanahusika mpaka sasa hivi biashara inaenda.
wana njia mpya..
ukimuona mzee juma shujaa kwa kuweza kuthibiti mitambo pale airport yote hii ni kwa kutafuta sifa kwa wananchi..na wanaonasa pale ni kambale na dagaa..nyangumi wana njia yao mpya na wote wanajua
wanatumia meli za mizigo kubwaa..
meli zikikaribia kutia nanga mzigo unashushwa...mtu mzito akipiiga simu na kutoa oda wote wanaufyata
mzigo unaingizwa kwenye nitumbwi ya uvuvi mpaka ferry
kuna sehemu haifikiw sana na watu imepaki na kuhifadhi mitumbwi chakavu..huko wanashusha mzigo safar inaendelea..
biashara ipo kama kawaida na unga unapatikana kama kawaida..
mnachezewa akili..

roma aliropoka ukweli kupitia post yake mtandaoni yule bwana mwenye makalio makubwa ka anachambia hamira akaamua kumnyamazisha kwa ubaya..
alikua namharibia sinema lake..

wasanii kibao wanawajua hawa nyangumi.
wametumika sana sabb ya tamaa zao
but sharti lao kuu ni moja..
ukimtaja anakupoteza mazima.


USIKUBALI KUCHEZEWA AKILI..

mi naenda kulala..
Kinachoo shangaza zaid hii vitaa ya madawa ya kulevya haionekanagii mwisho wakee inazungukaa tyuu watuu wanakamatwa mwisho wa Siku holaa kweli wanacheza na akilii zetu
 
Desire Dizaya

Desire Dizaya

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2015
Messages
6,512
Points
2,000
Desire Dizaya

Desire Dizaya

JF-Expert Member
Joined Feb 16, 2015
6,512 2,000
Hata America hawajaweza kumaliza kabisa ila umepungua sana, Ndio maana hata mapapaa wa kurusha dola kwenye benzi na birthday wamepotea
waliotishwa kwa idadi kubwa ni wauzaji wa kati..hao ndo walikuqa wanafanya anasa za kurusha pesa..ila ma don wapo
tatizo mzunguko wa pesa hauko vizuri kana enzi za jk..maelfu hawana kazi..wanunuzi wamepungua na biashara imepoa.
 
eden kimario

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Messages
10,187
Points
2,000
eden kimario

eden kimario

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2015
10,187 2,000
Kama kichwa kinavyosema,

Au waliokutwa na hatia kama wapo maana vita ilikuwa kubwa sana halafu sasa naona kimya waliokwenda gerezani wapo jamani au waliokutwa na hatia?

Yule kamishna wa kupambana na madawa ya kulevya sijui yuko wapi.

Mbona kimya!
 
K

kiloriti

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2016
Messages
488
Points
1,000
K

kiloriti

JF-Expert Member
Joined May 12, 2016
488 1,000
zile zilikuwa mbwembwe.walitaka tu kupima watu mikojo hawana lolote hao
 
Lukwafya bhagasi

Lukwafya bhagasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2017
Messages
1,241
Points
2,000
Lukwafya bhagasi

Lukwafya bhagasi

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2017
1,241 2,000
Bashite anasema alifanikiwa kuishinda matokeo yake akaambulia kulia kanisani
 
eliakeem

eliakeem

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2009
Messages
9,402
Points
2,000
eliakeem

eliakeem

JF-Expert Member
Joined May 29, 2009
9,402 2,000
JPM kawachakaza hawa wauza unga. hata ukiangalia takwimu za vijana wanaokamatwa nje ya nchi imepungua sana.
bravo JPM.
 
mgaya chacha

mgaya chacha

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2015
Messages
504
Points
1,000
mgaya chacha

mgaya chacha

JF-Expert Member
Joined Aug 22, 2015
504 1,000
Huwa najiuliza mbona Makonda alijitananmbaisha kuwa Amethibiti Madawa ya Kulevya Mimi niko Morogoro Mjini Njoo maeneo ya Msamvu Stand/ITIGI jina Maarufu Kuna mateja wa kumwaga wanayatoa wapi? Nenda MANZESE ya Morogoro wapo Mateja Kibao Tena ni wakabaji Balaaa! Njoo tumbaku Kwenye Mataa Pia nikituo Cha Maroli ya Michanga Tuna mateja kibao Tena wapo Live Na Polisi wanawajua Wananunua Wapi? Hizo ni Sehemu ninazozijua Au ilikuwa ni Mbinu za kuwazalilisha watu huku wahusika wakiachwa Pembeni.
 
mchillo

mchillo

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2010
Messages
485
Points
225
mchillo

mchillo

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2010
485 225
JPM kawachakaza hawa wauza unga. hata ukiangalia takwimu za vijana wanaokamatwa nje ya nchi imepungua sana.
bravo JPM.
Imepungua vipi na juzi imekamatwa meli nzima ya Tanzania huko ughaibuni?
 
mbotoki

mbotoki

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2015
Messages
260
Points
225
mbotoki

mbotoki

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2015
260 225
Huwa najiuliza mbona Makonda alijitananmbaisha kuwa Amethibiti Madawa ya Kulevya Mimi niko Morogoro Mjini Njoo maeneo ya Msamvu Stand/ITIGI jina Maarufu Kuna mateja wa kumwaga wanayatoa wapi? Nenda MANZESE ya Morogoro wapo Mateja Kibao Tena ni wakabaji Balaaa! Njoo tumbaku Kwenye Mataa Pia nikituo Cha Maroli ya Michanga Tuna mateja kibao Tena wapo Live Na Polisi wanawajua Wananunua Wapi? Hizo ni Sehemu ninazozijua Au ilikuwa ni Mbinu za kuwazalilisha watu huku wahusika wakiachwa Pembeni.
Makonda alishughulikia Zaidi Dar, huko Moro hana mamlaka napo ki vile.
Ni jukumu lenu sasa, kwenda kureport hivyo vijiwe unavyovitaja ili wadhibitiwe.
 
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
15,119
Points
2,000
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
15,119 2,000
Kama hili linatokea kwenye jeshi la marekani...basi inabidi tuwa makini na nini wamarekani wanatushauri...!!
Na sisi tuchunguze kwa umakini vyombo vyetu vya usalama kama viko salama.
=====
US Navy investigators are looking into claims of a drug ring that was selling illegal substances over the dark web, including cocaine, LSD, and ketamine – a powerful sedative, local media reports.
As many as dozens of midshipmen are being investigated for an alleged drug abuse, Fox News reported. The investigation revolves around allegations of a drug ring at the US Naval Academy, the leading institution in charge of commissioning officers for the Navy and the Marine Corps

As of Sunday, three Navy cadets were accused of selling cocaine, ketamine, which is a powerful sedative substance, and LSD to their classmates who purchased the drugs via the dark web using bitcoin, Fox said, citing several midshipmen currently enrolled at the academy.

Claims of drug ring at US Naval Academy selling cocaine, LSD on dark web trigger probe
 
Nguvu moja

Nguvu moja

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2017
Messages
3,399
Points
2,000
Nguvu moja

Nguvu moja

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2017
3,399 2,000
Piga vita madawa ya kulevya "Tanzania bila madawa ya kulevya inawezekana"
 
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
15,119
Points
2,000
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
15,119 2,000
Trump (rais wa Marekani) amuunga 'mkono Durtete'. Ni katika masuala ya kudhibiti madawa ya kulevya. Akiri wauza madawa ya kulevya ni wauaji wa vizazi kwa kusema mtu mmoja anaweza kuua watu 5,000 kwa madawa ya kulevya.
Hongera Trump kwa kuliona hilo.
Tanzania tunaweza kuliangalia suala hili la adhabu kwa wanaothibitika kujishughulisha na madawa ya kulevya kwa mapana zaidi.
========
Death penalty for drug dealers

Trump praised other countries for imposing the death penalty or life in prison for drug dealers, saying the United States should consider similar penalties.
"I think it's a discussion we have to start thinking about. I don't know if we're ready -- I don't know if this country's ready for it," Trump said.
He said those convicted of killing just one person in shootings and stabbings at times face the death penalty or life in prison without parole. But, he said, someone can "kill 5,000 people with drugs because you're smuggling them in and you're making a lot of money and people are dying," and go without serious punishment.

Trump stumps for struggling GOP candidate, talks up death penalty for drug dealers in whirlwind rally - CNNPolitics
 
castor magnus

castor magnus

Member
Joined
Sep 25, 2017
Messages
57
Points
95
castor magnus

castor magnus

Member
Joined Sep 25, 2017
57 95
Makonda alishughulikia Zaidi Dar, huko Moro hana mamlaka napo ki vile.
Ni jukumu lenu sasa, kwenda kureport hivyo vijiwe unavyovitaja ili wadhibitiwe.
Halafu nchi haijengwi na serikali pekee Bali hata wewe unaweza kusaidia
 
Jehujehu

Jehujehu

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2018
Messages
224
Points
250
Jehujehu

Jehujehu

JF-Expert Member
Joined May 4, 2018
224 250
Mtandao wa KenyanTalk umetaja orodha ya wafanyabiashara wakubwa wa madawa ya kulevya aina ya heroine kwa Afrika Mashariki. Orodha hiyo inajumuisha viongozi wakubwa wa kisiasa kutoka Kenya na Tanzania ambao wanatajwa kuingiza na kusambaza "heroine" katika nchi nyingine za EAC. Watu hao wanaodaiwa kuwa ni magwiji wa mihadarati aina ya heroine ni:
1.Rais Uhuru Kenyata (KE)
2.Gavana wa Mombassa Ali Hassan Joho (KE)
3.Mfanyabiashara na mbunge wa zamani Harun Mwau (KE)
4.Seneta wa Nairobi Mike Sonko (KE)
5.Gavana wa Kiambuu Wilium Kabongo Gitau (KE)
6. Mtoto wa Rais Mstaafu Ridhiwani Kikwete (TZ)
7.Waziri Mwigulu Nchemba (TZ)
8.Waziri mstaafu Juma Kapuya (TZ)
9.Balozi Emanuel Nchimbi (TZ)

Kwa taarifa zaidi ingia Whose Heroin? Exposing The Six Most Powerful Drug Dealers Of The East African Coast.
Hili ni kaburi la kufukua maana kama ni kweli ukishakula nyama ya mtu huachi kwani hata ukitaka kuacha waliokualika watakutishia usiache ni kama kujiunga free mason.
 
O

Onjwaria

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Messages
928
Points
1,000
O

Onjwaria

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2016
928 1,000
Kuna watu walitajwa na Makonda kwa kuandikwa majina kwenye karatasi ya kuokota , vipi ile nilikuwa swaga za kupotezea ishu ya nini vile
 

Forum statistics

Threads 1,403,290
Members 531,177
Posts 34,419,822
Top