Madawa ya Kulevya na aibu ya Tanzania - Yatosha sasa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madawa ya Kulevya na aibu ya Tanzania - Yatosha sasa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by n00b, Jul 11, 2013.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2013
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 958
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 60
  masogange-mbwembwe.png Hatuwezi kuendelea kukaa kimya. Taifa letu linaaibika vibaya sana.

  Wahusika wanajulikana. Wametajwa mara nyingi na mbinu wanazozifanya kwa kutumia wasanii wa kizazi kipya na waigizaji almaarufu kama 'Bongo Movie'.  Inaudhi, inakera na inatuongezea chuki sana kwa serikali iliyo madarakani. Kaeni kimya na endeleeni kulichafua taifa, kuna siku mtatueleza yote. Au kwakuwa wahusika ni wanenu? Au kwakuwa wakuu wa juu ni wale waliowawezesha kuingia madarakani kisiasa?

  Ndugu zangu, hii ni aibu kubwa kwa Taifa. Inasikitisha sana na inazidi kutuaibisha wengine tunaosafiri ng'ambo. Taifa kama halina rais, taifa kama halina Vyombo vya Dola. Ni upumbavu, ni ufedhuli na mtambue sasa tumechoka. Sasa, tunaanza kuziweka habari za kila anayekamatwa na madawa hadharani, tunaanza kuweka hadi wanaowatuma. Tutawafikia mapapa wote!

  Mambo haya mlimchomekea mtoto wa Mengi, mambo haya mnawachomekea wanyonge wenye njaa kali na hadi mmeua vijana wetu kwa kuwabebesha mizigo michafu hivi!

  Kwa ambao hamjasoma habari hii ya aibu, someni hapa:

  Someni zaidi hapa Watanzania Wawili wakamatwa South Africa na Madawa


  USHAURI KWA VIJANA WA KITANZANIA:
  *************************************

  Habari zaidi ndani ya JF:

  *************************************
  - CHADEMA yatoa tamko baada ya Mbowe kutajwa katika listi ya Makonda

  - Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...
  - News Alert: - Rais Magufuli apigilia msumari jeneza la wauza Dawa za Kulevya, asema si kazi ya Makonda pekee
  - Mbunge wa Kinondoni umefeli kupambana na Madawa ya kulevya!
  - Tuseme: Makonda, Haya hapa Majina ya Wauzaji Madawa ya Kulevya wakubwa
  - MADAWA YA KULEVYA: RC Makonda na Kamanda Sirro waongea na waandishi wa habari

  - Updates: Wasanii Waitikia wito wa Makonda Kufika Polisi
  - DAR: RC Makonda awataja Askari 9 watuhumiwa kushirikiana na mtandao wa Dawa za Kulevya. Wamo wasanii
  - Hii ndio hali ya Nando (Mshiriki wa BBA) baada ya kuathirika na matumizi ya madawa ya kulevya

  - Biashara ya Madawa ya Kulevya Tanzania: Who is Pulling the Strings? [September, 2010]
  - Madawa ya Kulevya Tanzania, Serikali Yetu Hamyaoni Yanatumaliza? [March, 2011]
  - Madawa ya kulevya: Rais Kikwete akutana na mawaziri, wakuu wa mahakama na polisi [2013]
  - Kuficha watuhumiwa wa madawa ya kulevya... Wananchi, tufanye nini? [July, 2011]
  - Madawa ya Kulevya - Aina na Athari zake kwa Mtumiaji [February, 2012]

  - Dawa za kulevya: Watanzania watatu wakamatwa India, mmoja afariki
  - Mafia wa Italia na mihadarati Tanzania [December, 2012]
  - Mihadarati (Madawa ya Kulevya) yaivuruga CCM! [November, 2006]
  - Wajumbe Baraza la Wawakilishi Zanzibar watuhumiana kuhusika na Mihadarati (Madawa ya Kulevya) [June, 2011]

  - Serikali kuanika vigogo wa Madawa ya Kulevya bungeni [July, 2011]
  - Madawa ya Kulevya: Alivyotoroshwa Nurdin Akasha...
  - Mtanzania akamatwa na madawa ya kulevya Chicago, U.S.A.

  - Mtanzania akutwa na madawa ya kulevya uwanja wa ndege wa Marekani-Texas tumboni kwake
  - Rais Obama amtaja mfanyabiashara wa madawa ya kulevya mwanamke wa kitanzania aishie Mbezi
  - Polisi wamnasa muuza dawa za kulevya wa kimataifa aitwaye Leila...
  - Kikwete 'awapakazia' viongozi wa dini biashara ya madawa ya kulevya

  - Pengo: Wananipakazia madawa ya kulevya!
  - Dadake mbunge Munde Tambwe (CCM) akamatwa na dawa za kulevya!
  - Kangi Lugola, mbunge CCM atuhumu Mawaziri ni wauza mihadarati! Serikali yawatetea, awekwa kitanzini!
  - Mtandao wa uhalifu Polisi... Wahusishwa na mauaji, biashara ya mihadarati na ulaji rushwa!

  - Mfanyabiashara jamaa ya Mbunge akamatwa na Shehena ya Madawa ya Kulevya
  - Mtangazaji wa redio kutoka Tanzania amekamatwa na dawa za kulevya Kenya!
  - Mtoto wa Liyumba akamatwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya Bil 9 Tsh

  - Wapakistan waliokamatwa na madawa ya kulevya ya billion 6 waachiwa kwa dhamana!
  - Picha: Msichana wa KITANZANIA aliyekamatwa na Unga EGYPT kunyongwa...
  - Madawa ya Kulevya: Mabondia wa Tanzania wafungwa miaka 15 nchini Mauritius!

  - Watanzania Wawili wakamatwa South Africa na Madawa
  - Watanzania wawili wakamatwa na madawa ya kulevya Hong Kong
  - Binti ashikwa na Madawa ya Kulevya JNIA; Polisi wa usalama waomba Rushwa wakataliwa...
  - Mtanzania afungwa jela miaka 15 Zimbabwe kwa kukutwa na madawa ya kulevya

  - Wafungwa wa Kitanzania waliokamatwa na madawa ya kulevya Hong Kong wafunguka!
  - Kilumbe Ng'enda: Mbunge Azzan Anahusika na Biashara ya Dawa za Kulevya

  - Mtanzania akamatwa na madawa ya kulevya US
  - Mapapa wa madawa ya kulevya watajwa, wamo Morine Amatus Liyumba na mdogo wa Rostam Aziz
  - Kumekucha Madawa ya Kulevya: Kina 'Masogange' wawataja waliowatuma!

  - Mtambo wa Dawa za kulevya waingizwa nchini, upo Mbezi Beach!
  - Serikali sasa kuanzisha mahakama ya madawa ya kulevya...!!
  - Madawa ya Kulevya: Mashine mpya zafungwa JKIA
  - Bungeni Live: Hoja juu ya Madawa ya Kulevya
  - CHADEMA watoa tamko kuhusu madawa ya kulevya
  - Vita dhidi ya madawa ya kulevya: Waziri akiri wauza unga kuifadhili CCM, Nzowa aizamisha Jambo leo
  - Sakata la madawa ya kulevya: Kamanda wa polisi viwanja vya ndege ahamishwa
  - Sakata la madawa ya kulevya: Viongozi wachunguzwa na kuhojiwa
  - Majina ya Majaji wanaolinda wauza madawa ya kulevya yatajwa! Wamo Pendo Msuya na Dr Fauz Twalib
  - Mtanzania adakwa na mihadarati China
  - Mtanzania akamatwa akiwa na Madawa ya Kulevya United Arab Emirates (UAE)

  - Mshambuliaji wa zamani wa Simba akamatwa na madawa ya kulevya...
  - Mbwana Matumla akamatwa na madawa ya kulevya Spain
  - Madawa ya Kulevya: Matumla na Kaniki wakamatwa!

  - Mtanzania aliyekamatwa na madawa ya kulevya Dubai amlaumu mumewe
  - Madawa ya Kulevya: Meli ya Tanzania iliyobeba unga wa Sh. Bilioni 123 yazua kizaazaa nchini Italia!
  - Ripoti UN: Tanzania kinara dawa za kulevya
  - Uchochoro wa kuvusha dawa za kulevya Dar huu hapa
  - Baadhi ya njia zinazotumika kupitisha madawa ya kulevya uwanja wa ndege JKNIA
  - Madawa ya kulevya: Mtanzania afia Dubai, wengine wadaiwa kukamatwa China na Brazil
  - Madawa ya Kulevya: Aisha Bui (mke mwenza na Amina chifupa) naye akamatwa Brazil
  - Mwanajeshi Rashid Mohamed akamatwa na mirungi kilo 20 huko Tanga
   
 2. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2013
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mkuu umesema wanafahamika lakini hukutaja hata mmoja. Labda na Rais anaogopa kuwataja kama wewe kwani wana nguvu nyingi.
   
 3. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2013
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 958
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 60
  Mkuu,

  Kauli yangu umeielewa vema? Unadhani ni siri tena? Ni wakati wa wao kuisoma na kuelewa kuwa wengine tumechoka sana. Upumbavu huu hauvumiliki.

  Nilisema:
   
 4. Super H

  Super H JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2013
  Joined: Oct 6, 2012
  Messages: 1,005
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Rais KIKWETE ana orodha ya wauza dawa za kulevya Muda ukifika atawakamata, CCM ni wasikivu sana! Tulia....
   
 5. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2013
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,598
  Likes Received: 978
  Trophy Points: 280
  Mkuu wote tuna uchungu sana na yanayotokea lakini viongozi wetu wa juu wameshindwa mmoja alisema anawajua na waache kufanya hiyo biashara mwingine akasema kwa sababu hawa ni wafanyabiashara wakubwa wakikamatwa nchi ITAYUMBA kwani hawa ndo wanaochangia kwa nguvu zote chama cha CCM pamoja na .baadhi ya shughuli za kijamii
   
 6. C

  CT SCan Mchina JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2013
  Joined: Mar 13, 2013
  Messages: 1,244
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  CCM Ni Janga kwa VIJANA.
   
 7. o

  option JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2013
  Joined: Jan 15, 2013
  Messages: 1,724
  Likes Received: 829
  Trophy Points: 280
  Mkuu, they will have to spend 20 years behind bars then wakitoka wanadungwa sindano za sumu wakafie mbele
   
 8. fyddell

  fyddell JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2013
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 2,252
  Likes Received: 938
  Trophy Points: 280
  Kweli aibu alafu mbaya zaidi sasa. Sifa ya iliyokuwepo nje ni kwamba biashara hii inafanywa na watu wenye nafasi zao serikalini na wafanyabiashara wakubwa nchini wanaochangia fedha nyingi kwaajili ya kuendesha serikali[ tukitoa kodi] that's why wanashindwa kukamatika ingawa wanajulikana. Aibu kubwa hii
   
 9. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #9
  Jul 11, 2013
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 145
  Agnes Gerald (sio Jerald) alijipatia umaarufu baada ya kushiriki shindano la Miss Tanzania, na kupata mafanikio ya wastani. Sikumbuki kama alishinda nafasi yoyote ile, lakini huko ndiko alikoanzia. Alijipatia jina la "Masogange" baada ya kushiriki kwenye video ya msanii Belle 9, ya wimbo wake wa "Masogange". Melissa Edward anadaiwa kuwa mdogo wake.

  Wasanii wengi wamekuwa, kutokana na dhiki zao, wakitumiwa na vigogo wanaofanya na kuratibu biashara ya madawa ya kulevya. Nasema "wanaofanya na kuratibu" kwa kuwa hili ni genge la wafanyabiashara na viongozi wa ngazi za juu serikalini. Ukidadisi mtaani utayapata mengi. Watu wanajua, ila hawaongei.

  Haiyumkini Agnes na Melissa wakajikuta wameingizwa kwenye "mkenge" huo wa kuwa "punda" wa kubeba madawa hayo na kuyasafirisha, wakichukua "risk" kubwa sana. Kwa kutaka utajiri wa mkato, kuendesha magari ya kifahari, kuishi katika nyumba za kifahari pasi na kuzifanyia kazi halali, haya ndiyo matokeo yake.

  Kubeba kilo 150 za madawa aina ya Crystal Meth, kwenye mabegi 6, inaonesha, mosi, jinsi mabinti hawa walivyo na tamaa, na pili, jinsi ambavyo wana elimu ndogo ya kukubali kuamini kwamba wangeweza kufanikiwa kupita uwanja wa ndege wa kisasa kama huo wa nchini Afrika Kusini, pasi na kukamatwa.

  Maofisa wa Afrika Kusini wanaohusika na udhibiti wa madawa ya kulevya walisema "Hiki ni kiwango kikubwa kuliko vyote katika historia yetu hapa nchini cha madawa ya kulevya kilichowahi kukamatwa."

  Maofisa wa kitengo cha madawa ya kulevya wa taasisi ya SARS (South African Revenue Service) wamesema madawa hayo yanakisiwa kuwa na thamani ya Rand milioni 42.3, kiwango ambacho ni kikubwa kuliko vyote ambavyo vimewahi kukamatwa nchini humo cha madawa ya kulevya.

  TATHMINI YANGU:

  1. Agnes amekuwa akipiga picha kwenye mitandao ya jamii, akijinadi kuwa mrembo mwenye pesa asiyehitaji chochote kwa mtu yeyote, huku akipiga picha pesa nyingi alizokuwa akizisambaza kwenye kitanda. Nyuma ya pazia, pesa hizo zilikuwa chafu, haramu, kwa kuwa zilipatikana kwa njia ya uhalifu.

  2. Agnes na mdogo wake Melissa, ambaye kwenye mtandao wa jamii wa Facebook anatumia jina la "Meliss Edward", wameliaibisha taifa letu la Tanzania. Sasa Tanzania imewekwa doa rasmi.

  3. Usishangae mara nyingine utakapokuwa ukisafiri kuingia nchini Afrika kusini ukajikuta ukapekuliwa na kuulizwa maswali lukuki, na kuhojiwa kwa saa kadhaa. Jipange. Hakikisha una nyaraka zote zitakazokutambulisha na kuelezea sababu yako ya kwenda nchini humo, hata kama unaenda kusoma. Usishangae kuulizwa: "Kwani Tanzania hakuna vyuo vikuu?" Ukishindwa kujibu kwa ufasaha, unapakiwa kwenye "pipa" na unakwea anga kurudi kwenu, tena kwa gharama zao!

  4. Sio siri, inajulikana kwamba Watanzania wengi waliolowea nchini Afrika Kusini wamekuwa wakijihusisha na biashara au shughuli za madawa ya kulevya. Sasa watakaojulikana watakusanywa wote na kulundikwa mahala, kisha, baada ya kuhojiwa, watakaothibitika kujihusisha na biashara huyo haramu watafunguliwa mashtaka na watakaopatikana hatia watakula mvua nyingi jela au kuhukumiwa adhabu ya kifo.

  5. Tukio moja, athari lukuki.

  Ndugu zangu, biashara hii haramu ni ya hatari. Ndio, inalipa haraka tena kwa kiasi kikubwa, lakini kwa nini uhatarishe uhai wako kwa kutaka utajiri wa mkato, tena kwa njia ambayo ni UASI mkubwa kwa Mwenyezi Mungu? Pesa utakazozipata ni za Shetani, ambazo hutazifanyia jambo lolote la maana, zaidi ya anasa na starehe.

  Kwa wale wasioelewa, hakuna "mzigo" wowote ule wa madawa ya kulevya ambao unaweza kuvuka mipaka kutoka nchi moja hadi nyinyine pasi na kuwa "taratibu" zote zimekamilika. Wahusika wa "mzigo" huo huhakikisha kwamba wadau wote wanaopaswa kuhakikisha usalama wa "mzigo" huo wanapata mgao wao mapema kabla hata siku ya kuusafirisha, na taarifa za kusafirishwa kwa "mzigo" huo hutolewa dakika za majeruhi ili kuzuia kutovuja kwa siri. Wanaohusika kwenye viwanja vya ndege ni maofisa wa polisi na wa kudhibiti madawa ya kulevya, maofisa wa ukaguzi na usalama, maofisa wa forodha na maofisa wa uhamiaji. Miongoni mwao kuna timu kabambe ya kuratibu uvushwaji wa "mzigo" huo, kuanzia unapowasili uwanjani. Viwanja vya ndege vimejengwa vikiwa na njia nyingi za siri; nimeshashuhudia. Njia hizi hutumika wakati wa kuwapeleka wahalifu hatari au watu ambao hawataki usumbufu "VIP" kutoka sehemu moja ya uwanja hadi nyingine, au moja kwa moja hadi ndani ya ndege. Pia zimo njia za kuhamisha mizigo kutoka pale inapoingia, pasi na kukaguliwa, moja kwa moja hadi ndani ya sehemu ya mizigo ya ndege, mingine ikiwa na lakiri bandia za "diplomatic pouch", yaani, "mfuko wa kidiplomasia". Mizigo ya aina hii kwa mujibu wa Mkataba wa Geneva haipaswi kukaguliwa, kwani ni ya Kibalozi.

  Kumbukeni daima, mwonja asali haonji mara moja. Agnes alianza taratibu kuvusha madawa, akiwekewa wingu la kumlinda. Hakuzijua siri za biashara hii. Akajijengea uaminifu kwa waajiri wake. Akawashawishi amwingize na mdogo wake ili mzigo uwe mwingi; wakakubali. Si jambo rahisi? Tamaa ikamwingia. Baada ya kuona anafanikiwa akasema ngoja nitafute mzigo wa "kustaafia" nikiwa uhamishoni Afrika Kusini. Ng'ombe wa maskini hazai. Waajiri wake walivyojua kwamba "wamezikwa", wakasema: Tuwashikishe adabu madogo hawa, potelea mbali mzigo ufe, lakini fundisho wapate.

  Taarifa zikapelekwa. Wale ambao, kwa upande wa Afrika Kusini walikuwa wanategemea mgao wao baada ya kuupokea na kuuvusha salama mzigo wakapokea taarifa kwa wakubwa wao wa kazi kwamba "dili" imekufa, sasa ni kukamata tu. Ndivyo ilivyotokea, kama sinema. Agnes na Melissa wakajikuta kifungoni; mbio za sakafuni zikaishia ukingoni.

  Je, mmeiona hatari ya mchezo huu mchafu?

  Na huku Bongo nako kimenuka. Wale ambao walikuwa zamu JNIA ambao walipaswa kukagua mizigo siku Agnes na Melissa walipoondoka sasa wanahojiwa; Kulikoni mkatuaibisha namna hii?

  Lakini ukweli unajulikana.

  Pesa ni Shetani. Ukiiendekeza inakupiga chini. Tamaa mbaya, na ndicho kilichotokea kwa Agnes na Melissa.

  Sasa hebu ona aibu iliyowafika wazazi wao na familia yao yote, hadi kijijini. Macho na masikio ya Watanzania ni kujua hatma ya mabinti hawa; nyumbani kwa wazazi ni vilio, wakimlaani Shetani na kufanya maombi lukuki. Lakini walipokuwa wakipokea mabulungutu kutoka kwa mabinti hawakuuliza zimetoka wapi. Eeeeeh?

  Mwenye macho aone, mwenye masikio asikie. Pesa ni Shetani, kama hukuipata kwa njia halali.

  Jiepushe na madawa ya kulevya, usiwe mtumwa wa Shetani! Mwogope sana Mungu!
   
 10. sokwe

  sokwe JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2013
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 2,028
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Waache wakanyee debe, unavuna unachopanda, watanzania wachache wapuuzi wanatafuta utajiri kwa nguvu zote, watanzania kibao wamekuwa wakikamatwa hapa Japan na madawa ya kulevya, wajapan Mao wanafanya Kama south Kama ukipigwa maswali airport na ueleweki wanakupandisha ndege hiyo hiyo uliokuja nao, yaani sisi tunaoishi hapa ukitoka nje ya Japan ukirudi unachunguzwa mpaka mauzi lakini siwalaumu wajapan, aaagrrr
   
 11. k

  kibolibo JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2013
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 335
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 45
  Duuuuuuh...ebwanaeee!!!kama kwenye movie hivi..
  ebu subiri ninywe kahawa ya bure ofisini..ati!!
   
 12. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2013
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Kuna siku Police Patrol walikamata gari lililokuwa likitoka Airport kwa mwendo mkali sana usiku wa manane. Walipofika maeneo ya Salender Bridge wakafanikiwa kulisimamisha gari lile. Lilipopekuliwa lilikutwa na viroba vya "Sembe" wakambana dereva na wengine waliokuwemo humo kwenye gari. Alipopigiwa Rostam Aziz walikubaliana atawalipa mshiko ili kesi iishe, Askari watano waligawana kila mmoja 80M. Kulipokucha kila askari alikuwa tayari ana maisha bora na familia yake.

  Siri hazifi walibana lakini mwisho walipanua na kusema. Sasa nilikuwa nauliza hivi sasa hivi ameacha kuuza sembe??? Nauliza hivi kwasababu viongozi wengi wengine wamediriki kujifanya kusoma taarifa bungeni kuhusu hali ya madawa ya kulevya wakati ndiyo wenyewe wauzaji wakubwa. Kama hawaondoki madarakani hawa nyangumi wa madawa ya kulevya Tanzania bila madawa ya kulevya haiwezekani. Tunasubiri majibu ya nani amewatuma hawa mabinti wawili huko Afrika Kusini na gunia la kilo 150 la sembe hiyo.

  Hakika ukipita mitaani ukaona vijana wanavyoharibika kwa madawa ya kulevya, utakuja na jibu kwamba wahusika wakikamatwa adhabu yao iwe ni kunyongwa, maana vijana wana hali mbaya sana.
   
 13. sokwe

  sokwe JF-Expert Member

  #13
  Jul 11, 2013
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 2,028
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Watu wengine wanapita airport, wanakuweka muda mrefu mpaka mizigo ichunguzwe sana, nilikwenda Singapore wiki 2 zilizopita ni tabu tupu, nawauliza customs officer, Mimi naishi Japan madawa ya kulevya nayatoa wapi? Wakanijibu kuna watu wanafanya connection route, let's say mtu anatoka Tanzania anakuja Japan, akifika hapa anashusha mzigo, mwenyeji anapokea anapeleka destination nyingine!

  Nilichoka kabisa.
   
 14. ligendayika

  ligendayika JF-Expert Member

  #14
  Jul 11, 2013
  Joined: Aug 31, 2012
  Messages: 1,175
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  Wasanii wabongo mtaisha mojabaada ya mwingine kwa tamaa zenu sijui kama mtafikia hata umri wa kina Gurumo. Alafu huu si mtandao wa wachovu, hivi ile kauri ya mh ana majina imeishia wapi?

  Naona askari wetu kazi yao ni kuwadunda raia tu kama agizo la aliepinda linavyosema. Viongozi wote ni kuimaliza cdm tu mambo ya msingi hawayajui. Wasanii mafanikio hayaji kama mvua, mnatakiwa kuyatafuta si kupewa kwa kubeba mihadarati
   
 15. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #15
  Jul 11, 2013
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  Kuwafunga hao ndama na kuwaacha wanaowazaa haitasaidia chochote. Hao wametumiwa tuu kama gari ya kusafirisha mzigo. Wamiliki wa mzigo wapo na bado wanapeta. Watakachofanya ni kutafuta usafiri mwingine na kuendelea na biashara yao kama kawaida.

  Madawa ya kulevya ni tatizo sugu sana nchini, but no body seems to care. Yanaingizwa nchini kiulaini kama dhahabu inavyopelekwa nje ya nchi. Madawa ya kulevya yanaadhiri sana vijana. Kutokana na hali ngumu ya maisha, na pia kutokana na biashara hiyo kuendeshwa na watu ambao wana status kubwa sana kwenye jamii, vijana wanashawishika kirahisi sana kujiingiza kwenye hiyo biashara.

  Inawezekana kabisa kuwa vinara wa hiyo biashara wanajulikana na vyombo husika lakini hawachukuliwi hatua zozote either kwa sababu ni "watu wakubwa sana" in whatever sense or wanaotakiwa kuwachukulia hatua ni sehemu ya hiyo biashara. Nasema hivyo kwa sababu siyo kawaida kwa hao wanawake waliotajwa kuweza kumiliki takribani kilo 150 za madawa ya kulevya. Walikuwa ni wasafirishaji tuu.

  Mbaya zaidi wamiliki wa hii biashara wanawatumia sana vijana na wakikamatwa wanaachwa kwenye mataa. Mwezi uliopita kuna mambondia wa Kitanzania wamefungwa huko Mauritius miaka 15 baada ya kupatikana na kosa la kuingiza madawa ya kulenywa nchini humo: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-sheria-the-law-forum/473554-watanzania-wanne-wafungwa-miaka-15-mauritius.html. Hawa walienda kama wanamichezo lakini kumbe walikuwa na agenda nyingine kubwa zaidi.

  Kuna yule mwanamuzi aliyefariki huko Afrika Kusini ambaye naye inasemekana sababu ni madawa ya kulevya. Kuna Mtanzania mwingine mwanamke alikutwa amefariki kwenye hoteli aliyofikia huko Italia mwezi uliopita baada ya madawa aliyokuwa amebeba kupasukia tumboni.

  Kuna Mtanzania alikamatwa na madawa ya kulevywa Marekani mwaka jana. Mwezi Februari mwaka huu kulikuwa na habari za mwanamuziki wa Bongo Fleva kukamatwa na madawa ya kulenywa nchini Burundi: https://www.jamiiforums.com/celebrities-forum/407776-timbulo-akamatwa-na-madawa-ya-kulevya-burundi-cheki-picha-za-tukio-hapa.html

  Tumesikia pia kuhusu Mtanzania aliyekamatwa na madawa ya kulevya huko Misri japokuwa yeye amekana kuwa Mtanzania. Sasa tunaambiwa kuwa wanawake wawili raia wa Tanzania wametambuliwa kuwa ndiyo wanaodaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

  Kuna Mtanzania mwingine aliyefungwa miaka nane huko Angola baada ya kupatikana na madawa ya kulevya aliyokuwa akisafirisha kwenda Afrika Kusini. Inadaiwa huyu Mtanzania aliondoka Afrika Kusini na kwenda kufuata dawa za kulevya Brazil na akafanikiwa kuchukuwa ila wakati anarudi Afrika Kusini kwenye kubadilisha ndege Angola alikamatwa na kukutwa na dawa za kulevya miaka mitatu iliyopita.

  Kwa kipindi chote hicho huyu jamaa alikuwa ameshikiliwa Angola bila kujua hatma yake na hata kushindwa kukutana na Balozi wa Tanzania Angola lakini mwezi uliopita ndiyo amehukumiwa kifungo cha miaka nane. Ombi lililoambatana na ndugu hawa kupaza sauti, ni kuiomba serikali kusaidia mtu huyu kukutana na balozi wa huko ili utaratibu wa kuja kufungwa Tanzania ujulikane. Mara nyingi Mtanzania huyu amekuwa akituma SMS kwa kutumia simu za watu wengine aliokutana nao gerezani.

  Moja ya SMS zake.


  [​IMG]
   
 16. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #16
  Jul 11, 2013
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  Kumbe ndiye huyo?
   
 17. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #17
  Jul 11, 2013
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,185
  Likes Received: 877
  Trophy Points: 280
  mkuu Invisible hii post ina thamani kubwa kwa ustawi wa jamii yetu na hasa kwa hawa vijana waliomaliza sekondari ambao tuko nao humu, na wengine waliomaliza vyuo ambao hawana ajira na wanataka utajiri wa haraka, hii post itengenezwe vizuri na iwe na thread yake inayojitegemea na ikibidi iwe stick katika majukwaa yote! ina mafundisho mazuri sana.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. m

  mavumbi JF-Expert Member

  #18
  Jul 11, 2013
  Joined: Feb 8, 2013
  Messages: 411
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Huyo Nzowa ni nani?

  Ni lini aliwahi kutoa taarifa ya namna ambavyo kesi za watuhumiwa wa madawa ya kulevya zilivyoendeshwa na hatma zake hapa nchini?

  Huyu sio mmoja wa hao hao wanaojua kuongea hewa na waandishi wa habari na hatimaye kuishia na ukimya wa kifisadi?

  Wewe wasema sasa yatosha......wenzio wanasema sasa twaanza, maana kila kukicha kesi za kukamatwa Watz zaongezeka!

  Kuna wapuuzi wengine wanadai ati suala la madawa ya kulevya halina uzito wa athari Tanzania kwa kuwa nchi hii ni "conduit" tu, yaani bomba la kupitishia madawa ambayo masoko yake makubwa yako ughaibuni!

  Mitaani Dar es Salaam wanaoshughulika na biashara hii wanajulikana vema tu, lakini Nzowa anasubiri kutoa taarifa kwenye magazeti ya waTz wanaokamatwa huko nje!

  LAANA TUPU!
   
 19. Kamanda Kazi

  Kamanda Kazi JF-Expert Member

  #19
  Jul 11, 2013
  Joined: Dec 15, 2012
  Messages: 2,622
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Ingekuwa China, huyo Agnes(Masogange) na uzuri wake wooote tungempoteza!
   
 20. M

  Makalanja Member

  #20
  Jul 11, 2013
  Joined: Jun 25, 2013
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Uchafu huu utokomezwe au baadhi ya viongozi wasio waaminifu wana ubia na hawa wauzaji na wasafirishaji wa madawa ya kulevya?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...