Madawa ya Kulevya na aibu ya Tanzania - Yatosha sasa!

Alipoanzia ni pazuri wala sio pa kumbeza na kumkatisha tamaa hiyo chain itatupeleka mpaka kwa manyangumi i believe...japo najua wengi mnamkatisha tamaa God is with him...
 
Hao wasanii uliowataja mtoa mada ni wanasadikika kuwa ni watumiaji wa madawa tena wametajwa na wasanii wengne ambao tayar wameshakamtwa kama wakina petitman,so wanatakiwa wakafanyiwe mahojiano ili watoe info za wanaowauziga..mi nadhani ni mwanzo tu mzuri kwa vita hii.Makonda augwe mkono
 
Drug lords ....wapo wengi sema hatari hao wanaloga hata kuloga ..bila Mungu atakwisha
 
nipo tofauti na maoni ya wengi, uwezi kausha mti kwa kupukutisha jani mojamoja. kila unapofanya hivyo yanaota mengine. ondoa mizizi mikubwa majani yatapukutika yenyewe. kucheza na viposi dagaa unaacha papa na nyangumi, Makonda umechagua njia pita katikati tena nenda kasi sivyo kutembea pembeni ya barabara angalia usije angusha gari bila kufika mwisho wa safari.
 
Mkuu sio hatua mbaya. leo amekamatwa kijana anaitwa Said alteza huyu ni mtu wa drugs kitambo ila sijawai kusikia amekamatwa ila leo makonda na polis wamefika mpka kwake maeneo ya kigambon kibugumo hospital wameondoka nae...kuna kijana mwanyamala makaburin anaitwa Mack ni wa kitambo ktk unga alianza kuwauzia wanafunzi wenzie CBE miaka 1999- 2000 mpka leo amekuwa Don wa unga mwanyamala pia ajawai kushikwa ila leo makonda amemtaja so ni hatua nzur maana huu mtandao ni mkubwa...na madon wa drugs wapo wengi yupo unayemjua wew ila mimi simjui ila hatua nzur coz untouchable wa mtaa wetu pia wameanza kushikwa
Tumuombee kila la kheri atokomeze hili janga huyo alteza inaonekana alikua tishio
 
Huyu "mungu" wa Dar kwa nini asipeleke ushahidi wake polisi? Au anautangazia umma sababu hana imani na polisi?

Mimi nina uhakika ana nia njema lakini approach yake ya ku-undermine the police force and putting himself on the limelight will backfire, soon or later but it certainly will!
Critical thinker aiseeee ni kosa kubwa, na bado anawatumia hao hao polisi ktk vita hiii
 
nipo tofauti na maoni ya wengi, uwezi kausha mti kwa kupukutisha jani mojamoja. kila unapofanya hivyo yanaota mengine. ondoa mizizi mikubwa majani yatapukutika yenyewe. kucheza na viposi dagaa unaacha papa na nyangumi, Makonda umechagua njia pita katikati tena nenda kasi sivyo kutembea pembeni ya barabara angalia usije angusha gari bila kufika mwisho wa safari.
Yea mkuu ukweli ndio huo.
Majina yalikuwepo na yanajulikana na Mkapa anayajua kikwete anayajua aliejitolea kuyataja wakati ule AMINA CHIFUPA wakamuondoa.
Hata Magufuri na waziri mkuu wake wanayajua ila wanashindwa wataanzaje kuyataja..!!??
 
Tuache dola ifanye kazi yake.sidhan kama watafungwa au kufunguliwa mashtaka.tunataka tuwasaidie.
 
Mh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda anajitaidi kufanya kazi na kutafuta namna ya kukuza CV yake ya utawala ni jambo jema kabisa na anastahili kuungwa mkono katika ndoto zake za kuitengeneza Dar mpya.

Leo habari zimeenea katika mitandao kuwa ameamua kutangaza vita dhidi ya madawa ya kulevya DSM. Tena akasema anataka afanye kazi kiasi kwamba atakapokuwa kwa Mungu awe na majibu ya kumpa juu ya nini alichokifanya kuyatokomeza madawa ya kulevya ndani ya jiji la Dar.

Sasa kwenye battle graund Mh anapambana na watu kama Wema Sepetu, TID, Mr Blue, Chid Benzi n.k alafu na baazi ya askari polisi wenye vyeo kama sajent detective copro n.k

Hivi kwa picha hiii na watu alioanza nao nikweli ndio mzizi wa madawa ya kulevya?

Hivi hii vita alivyoianza ataifaulu? mbinu anayoitumia inafaa? Maana ni kama amewasha alarm vigogo wanao husika kama wapo si watachukua tahadhari? Mimi nilidhan angewakamata kimya kimya na angeanza na wauzaji wa kuu then kesi zikafika mahakamani alafu ndio akatangaza sasa

Kwanini katika majina yale hamna majina ya vigogo wanaosemwa semwa underground?

Kama kweli alidhamilia kwanini hakuomba ile orodha ya wauzaji wa Ngada aliyopewa mh Kikwete?

Aidha namuombea mapambano mema.
Mchango wako unajenga taswira gani? Mnataka nini hasa watz? Badala ya kusimama nyuma yake, mnaanzisha vijimaneno vya kumkatisha tamaa! Eti anatafuta namna ya kukuza cv yake, una matatizo wewe! Badilika
 
Kuna wasani hapo kama wakina blue na dogo hamidu wako karibu sana na wauzajji..wa powder...ndomana trip za south afrika zlikuwa haziishi....
Alafu hao wasani wakihojiwaga kwenye tv na rredio wanajiita kioo cha jamii

Ova
 
Back
Top Bottom