Hivi madaraka yana nini hasa cha kumfanya kufanya mauaji ya kinyama kiasi hiko..soooo sad
watu wanaogopesha sana siku hizi,,ubinadamu hakuna.
Kupata utajiri bila jasho.
Kuheshimika na jamii.
Kujihakikishia pensheni bora.
Kulinda hadhi ya cheo.
Kuishi kifalme.
Mambo hayo kwa baadhi ya watu yanathamani kuliko maisha na utu wa mamilioni ya watu.
Mtu yuko radhi kufanya mauaji ya halaiki ili ayapate hayo maisha.
Kwa yeye maisha ya duniani ndiyo ridhiko lake la moyo, huko Mbinguni hana shida nako.
Inamfaa apate utajiri wa dunia hii na aikose (aichome) roho yake.
Si mnawaona wanaouza roho zao kwa Ibilisi ilimuradi wapate tonge nono hapa duniani.
Binadamu tunatofautiana sana katika levo ya ufahamu na fikra kwa ujumla.
Wako wanaoitumainia dunia hii tu, hao ni watu dhaifu. week person, very material. hufanya chochote kibaya ili waishi maisha ya anasa.
Ninyi mnao ona kuna maisha bora zaidi Mbinguni na mlio na hofu ya Mungu ninyi ni watu bora kabisa, haijalishi mna elimu gani, you are very Great Person, Supper human being.
hamuwezi kukubali kuuwa mtu eti kwa sababu ya kutembelea VOGO, BENZI, au eti kuchovya tonge la ugali kwenye mchuzi wa Samaki, wakati maharage yapo.
Binadamu tunatofautiana sana ki hadhi.
Jitambue ndugu.