Madalali wa nyumba: Je, wanachofanya ni sahihi?

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MAISHA ni duni, lakini kati ya wale ambao wanachangia maisha ya walio wengi kuwa duni ni wenye nyumba. Ziko sababu nyingi, lakini suala zima na nyumba za kupanga hasa katika Jiji la Dar es Salaam, limekuwa ni tatizo.

Watu wengi hasa wale ambao wamepanga vyumba vya kuishi, wamejikuta wakitumia gharama kubwa za kuishi, kiasi cha kusababisha baadhi ya mikakati yao ya maendeleo kushindwa kufanyika.

Hujuma kwa wapangaji huanza tangu mwanzo, pale wanapotafuta vyumba au nyumba za kuishi, kwani wenye nyumba wengi huwatumia madalali, ambao kimsingi wanachangia gharama za nyumba.

Madalali hupandisha gharama kwa namna mbili; kwanza ni kwamba huwa wanahitaji kulipwa angalau kodi ya mwenzi mmoja zaidi ya miezi ambayo mwenye nyumba anahitaji kulipwa, lakini njia nyingine ambayo wanaitumia ni kupandisha kodi yenyewe, ili hata hiyo kodi ya mwezi mmoja ambayo ndio ujira wao, iwe kubwa.

Kwa mfano kama mwenye nyumba anapangisha nyumba yake kwa Sh15,000 kwa mwezi, madalali wanaweza kupandisha kodi hadi kufikia Sh25,000 au zaidi, ili tu waweze kupata fedha nyingi.

Aidha kumekuwa na tatizo kwamba miongoni mwa madalali, baadhi yao wako tayari kukushawishi upange kokote hata kama ni nyumba ambayo hujaa maji wakati wa masika.

Baada ya kupata chumba au nyumba husika, kwa baadhi ya wenye nyumba hutumia matatizo na huduma za kila siku hasa bili za umeme kwa ajili ya kuishi, kwa maana kuwa wanazipandisha na kuwa za juu kuliko kawaida.

"Nyumbani kwetu tuko wapangaji 9, kila mmoja analipa Sh10,000 kwa mwezi kama bili ya umeme, ndio kusema kwa mwezi tunalipa jumla ya Sh90,000, cha kusikitisha zaidi ni kuwa licha ya kulipa bili yote hiyo, mwenye nyumba huwa anakata umeme kila siku asubuhi na kuwasha kuanzia saa kumi na moja akisema kuwa gharama za umeme ni kubwa. Ukiangalia kwa makini ni wizi mkubwa tunaofanyiwa na mwenye nyumba, kwani karibu wengi wetu hatuna vifaa vingi vya kutumia umeme, kwa mfano mimi nina radio ndogo na pia huwa nawasha taa, sasa kwanini nilipe bili ya Sh10,000?" anahoji Mwajuma Haule, mkazi wa Tabata, Jijini Dar es Salaam.

Mwajuma ni kati ya maelfu ya wapangaji ambao wanatoa kilio cha aina hiyo, kwamba wanatozwa bili kubwa ya umeme, lakini hakuna uhuru wa kutumia kile ambacho wanalipia, huku baadhi ya nyumba kukiwa na masharti yenye kukera kuhusu vile ambavyo wapangaji wanatakiwa kuishi.

"Mimi mwenye nyumba wangu huwa hapendi wageni. Pia hapendi nirudi nimechelewa zaidi ya saa nne usiku. Kuna tangazo maalum kwamba kurudi mwisho saa nne na zaidi ya hapa geti halitafunguliwa, pia hataki watu ambao wameolewa au kuoa katika nyumba yake," anasema Mwajuma.

Wakati mwenye nyumba wa Mwajuma hataki waliooa wala kuolewa kuishi kwenye nyumba yake kwa maelezo kuwa wanaweza kuwa na watoto au wageni wengi ambao watasababisha uchafu kwenye nyumba hasa kujaza choo haraka, mpangaji mwingine katika nyumba moja huko Ubungo maziwa, anasema mwenye nyumba wake hataki kusikia wageni wa aina yoyote.

"Huwa anatuambia kwamba kama mnataka kuwa na wageni, jengeni kwenu, hapa kwangu sitaki mniletee wageni maana wengine ni wezi wanaweza kuniibia," anasema mkazi huyo wa Ubungo, Hamis Hamdan.

Hamdani pia anazungumzia adha nyingine ya nyumba za kupanga, kuwa wakati mwingine unalazimika kupika chakula zaidi ya kawaida, kwa sababu baadhi ya wapangaji hawana fedha za kununua chakula na huwaomba wapangaji wao.

"Wako wazazi wengine labda siku wanakuwa hawana fedha, wanawaambia watoto wao waende kwenye nyumba za wapangaji wengine kuomba chakula. Haya yote yanatokea kutokana na hali duni ya maisha, katika mazingira ya aina hii ni kama tunarudishana nyuma," anasema na kuongeza kuwa

"Unapojua kuzaa, ujue pia na kuwatafutia watoto wako matumizi, sio kuwafundisha watoto kwenda nyumba ya jirani kuomba chakula, kwani baadhi ya familia nazo zinakuwa na bajeti ndogo au bajeti maalum kwa ajili ya kuendesha maisha yao," anasema.

Catherine Kihombi mkazi wa Mwenge Dar es Salaam, analalamikia baadhi ya wanandoa wasio hofu wala maadili, kwamba baadhi yao wanaishi kwenye chumba ambacho hakina hata paa la ndani (silingi bodi), na bado wanafanya tendo la ndoa au kupiga makelele ya mahaba bila kujali kama nyumba ya pili watasikia au la.

"Utakuta mtu labda amelewa au mzima, wanafanya mambo ya ajabu, bila kujali kama wengine kwenye nyumba ya pili wanasikia au la. Aidha wapo wengine wanatukanana au hata kupigana huku watoto wengine wakisikia na kuona kinachoendelea, vitu ambavyo kimsingi vinaharibu mwelekeo wa watoto," anasema.

Denisia Mrema, mkazi wa Arusha anasema tatizo kubwa analoona kwa wenye nyumba wengi ni kujiangalia zaidi wao wenyewe, badala ya kuwaangalia pia wapangaji, huku wengi wao wakiwa mstari wa mbele kutumia matatizo ya wasio na nyumba kujinufaisha.

"Ukweli ni kwamba wenye nyumba wanapaswa kuwasaidia wapangaji wao na wapangaji nao wanapaswa kufanya hivyo, hapa namaanisha kuwa iko haja ya kuwa na ushirikiano mzuri miongoni mwao. Lakini pia ni jambo la msingi kwa kila mmoja wao kuona kwamba anayo haki ya kutenda haki," anasema.

Baadhi ya wenye nyumba hata hivyo wanakiri kutoza bili kubwa zaidi za umeme tofauti na ilivyo kawaida na kusema kuwa wanaofanya hivyo wanakosea na wanapaswa kuacha mara moja.

"Ni wizi mkubwa wapangaji kulipa bili ya umeme ya Sh90,000 kwa mwezi. Jambo hili ni lazima wenye nyumba waliache kwani linatia aibu na linaonyesha ni kwa kiasi gani hakuna usawa," anasema Mzee Jonathan Motto mkazi wa Kipunguni, Dar es Salaam.

"Ni lazima mwanadamu uwe na huruma," akaonya na kuongeza kuwa hali ngumu ya uchumi inamsumbua kila mtu na kwamba ikiwa hakutakuwa na huruma ya aina hiyo ni vigumu kwa taifa kuwa na maendeleo."

=============
27th January 2014
=============
For great thinkers only

Hivi sasa niko katika kijihatua cha awali kabisa kuinua kibanda changu cha kujihifadhi na mama watoto wangu pamoja na wanangu wawili J and E. Nimeishi katika nyumba ya kupanga kwa muda sasa. Leo nitazungumzia zaidi madalali wa nyumba zaidi ya wenye nyumba wenyewe.

1. Udalali wa nyumba siku hizi imekuwa ni kazi inayowaingizia kipato baadhi ya watu na hivyo kuwa sehemu ya kuendesha maisha yao ya kila siku. Mimi sipingani kabisa na kazi hii kwani wapo watu wengi tu wanaofanya kazi rasmi lakini wanavurunda zaidi ya kawaida. Kinachoniudhi ni huu utarartibu wa madalali wengi kuongeza pesa kiasi fulani ambazo huwa ni zake kabla ya mwenye nyumba/chumba hajakabidhiwa kitita chake kama pesa ya kodi.

2. Kwa kuwa hadi sasa hakuna taratibu zozote zile za kushughulikia masuala ya madalali wa nyumba naomba mnijuze 'great thinkers' kinachofanywa na hawa madalali wa nyumba ni sahihi?

The listener
 
kama upo nje ya nchi ujiandae kwa life ya kupanga before hujafisadi fedha za umma na kujenga kibanda chako
 
For great thinkers only

Hivi sasa niko katika kijihatua cha awali kabisa kuinua kibanda changu cha kujihifadhi na mama watoto wangu pamoja na wanangu wawili J and E. Nimeishi katika nyumba ya kupanga kwa muda sasa. Leo nitazungumzia zaidi madalali wa nyumba zaidi ya wenye nyumba wenyewe.

1. Udalali wa nyumba siku hizi imekuwa ni kazi inayowaingizia kipato baadhi ya watu na hivyo kuwa sehemu ya kuendesha maisha yao ya kila siku. Mimi sipingani kabisa na kazi hii kwani wapo watu wengi tu wanaofanya kazi rasmi lakini wanavurunda zaidi ya kawaida. Kinachoniudhi ni huu utarartibu wa madalali wengi kuongeza pesa kiasi fulani ambazo huwa ni zake kabla ya mwenye nyumba/chumba hajakabidhiwa kitita chake kama pesa ya kodi.

2. Kwa kuwa hadi sasa hakuna taratibu zozote zile za kushughulikia masuala ya madalali wa nyumba naomba mnijuze 'great thinkers' kinachofanywa na hawa madalali wa nyumba ni sahihi?

The listener
 
Habari ya mda. Hivi kwanini madalali wanafanya mtu apate ugumu wakati anatafuta gari/nyumba/chumba ya kununua au kukodisha?...unakuta bei ya ile unacho tafuta ni ndogo but kwasababu ya hawa watu,inapanda ghafla. Sawa,commission utapewa but that should not be set by you!...au kwasababu umetumia vocha ya elfu 2 na siku tatu unataka ulipe laki 5 katika mauzo ya gari na kodi ya mwezi mmoja kwa chumba/nyumba. If that is the case na nyie mlipe TRA kodi,because you are earning money wakati huna kampuni au ofisi. Naomba maoni yenu katika swala hii.

Asanteni.
 
Hivi ukikataa kuwalipa,wana nguvu yeyote kisheria?,nilipangisha nyumba siku nalipwa dalali anataka nimpe feza,niliwatoa mbio.
 
ndio wamefanya maisha yapande gharama.... nyanja nyingi za hela za uraiani... hukosi dalali...
 
Tunarudi tena pale pale tatizo sio dalali ila ni mfumo wa sheria, Udalali ni kazi kama kazi yoyote na anatakiwa alipe kodi kama mlipa kodi yeyote ni lazima awe na ofisi ambayo utakwenda kuangalia kama ni gari, nyumba, warehouse, kiwanja, shamba, na kama ni asilimia mbili au tatu ya thamani anakula kwani wapo jurahisisha kazi ya mtu badala ya kuhangaika huku na huko.
Hawa madalali wakiona nyumba inauzwa mil100 tayari tamaa na uchu unamtoka akijua hili tajiri na Sio tu iwe ghali hivyo hata shamba la 4m atakuambia 5 sasa anakula m kwa mtindo gani? Hapo lazima sheria iwepo najua ipo lakini haifanyiwi kazi
 
ni kazi km kazi nyngne..c amekufanyia kazi?wanasaidia sna kurahisisha kazi.japo wanakera
 
Hawa viumbe ni hatari sana, wote wana vitambi na nyumba ndogo maana hawana uchungu na hela kabisa. Ila hela yao kama ya maruhani vile, sinaona wengi wao wakiwa na maisha ya maana sana (hapa nazungumzia wale wa kikwetu wa viwanja, mashamba, magari, nyumba za kupanga/kuuza, n.k) Si wa dili kubwa kama za Richmond, Radar na wengineo.
 
Tena sikuhizi wanataka uwape 10% ya bei ya kitu unachonunua,washenz sana hawa watu hela ntafute mie we kuzunguka tu na kutumia vocha na unkwapue hivo… .sio watu kabisa hawa
 
Hawa watu ni wabaya kabisa. Mimi nikisikia biashara inamhusisha dalali, basi uwa najitahidi kuachana nayo kwani hawa jamaa wanawaharibia si tu wanunuaji/wapangaji bali pia wenye kuuza kwa tabia yao ya kuongeza bei. Badala ya nyumba kuuzwa haraka inakaa muda mrefu bila kuuzwa eti kwa kuwa dalali kapandisha bei!!! Nyumba za kupanga vile vile, zinakaa muda mrefu bila wapangaji kwa kuwa tu dalali anataka cha juu. Siwapendi kama nini hawa jamaa.

Tiba
 
Madalali ni middle men wapo duniani pote sema kibongobongo wamekaa kimagumashi ndiyo maana kazi yao ni unprofessional!
usilogwe kumdhurumu dalali wale watu wanaushirikiano wa kimbwambwa. Nafkri mnaikumbuka ile scenario ya mama aliyeuza uwanja bahari beach, kilichomtokea wanakijua madalali! Pia scenario ya Visran dalali maarufu alivuna mabilioni ya rada la BaE system kwenye deal na tz gvt!
Hawafai bt wataendelea kuwepo!
 
hadi kwenye maduka siku hizi kuna madalali,ukifika wanakushika wanakupeleka mkifika dukani unaona anawahi kutamka bei kabla ya mwenye duka,mfano kitu ni elfu 60 anasema elfu 90 au yoyote kubwa juu ya elfu 60,then wanajuana na mwenye duka later,so kuweni makini ndugu
 
Halafu katika upangaji huo hakuna hata mmoja mwenye nyumba anayelipa kodi ya kupangisha tra au aliyesajiri biashara hiyo tra yaani nchi inapoteza mapato mengi kwenye hii biashara.
 
Back
Top Bottom