Madalali Dar, walalama wachina kuingilia kazi zao

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
3,712
Reaction score
11,611
Madalali wanaofanya shughuli zao katika maeneo ya Masaki na Oysterbay, Dar es Salaam, wameiomba Serikali iingilie kati kutokana na kuingiliwa kwa biashara yao na raia wa kigeni, hasa Wachina, wanaodaiwa kufanya biashara ya udalali wanapoingia nchini.

Akizungumza na Swahili Times, Kaimu Katibu wa Madalali katika maeneo hayo, Ally Kasi, ameeleza kuwa raia hao wa kigeni husaidiwa na baadhi ya Watanzania wakiwemo madereva na wakalimani, jambo linalorahisisha shughuli zao zisizo rasmi katika soko la upangishaji wa nyumba.

“Anaweza akaja kwangu akanambia anahitaji nimwoneshe nyumba zinazopangishwa, namzungusha, na anaweza akakwambia hii nyumba mbaya hatuitaki, kumbe jioni karudi pale kampa mlinzi elfu 10 au 20, inategemeana na mtu aliyemkuta. Anachukua namba ya mwenye nyumba halafu anaongea na mwenye nyumba,” amesema.

Ameongeza kuwa baadhi yao huongeza bei ya upangishaji kwa makusudi ili kupata kamisheni ya siri. "Kwa mfano, nyumba ni dola 5,000 [TZS milioni 13] kwa mwezi, yeye anamwambia mwenye nyumba 'nakuja na mchina mwenzangu, mwambie ni dola 5,500 [TZS milioni 14.2], hiyo 500 [TZS milioni 1.3] kila mwezi itakuwa yangu mwaka huu, mwakani utachukua wewe.'"
 
Hata nyie madalali Watanzania ni matapeli tu. Kama mnataka heshima na haki fungueni rasmi real estate offices ili mtambulike na Mamlaka kama BRELA na TRA.

Kinyume cha hapo, nawaomba Wachina wakamatie hapo hapo mpaka mjifunze kufanya biashara rasmi
 
Kama wale waliokula cha juu Dipii wodi
 
Madalali ni matapeli waliohalalisha wizi wao kwa hiyo kama wamekutana na watabe zaidi yao. Wacha wanyolewe para kwa chupa, sina huruma nao
Sema tena na tena. Hawa madalali ni mashetani na ndiyo wanafanya maisha ya kupangisha na kununua nyumba au viwanja yawe magumu. Natamani angetokea mtu mmoja atengeneze website ya kuchukuwa commision ndogo kwa wateja wanaotafuta nyumba au viwanja.
 
Makampuni yaliyosajiliwa yanafanya kazi kwa misingi ya kamisheni wanayokubaliana na wenye mali. Hawa wa mitaani wanataka wapate zaidi ya wamiliki wa nyumba, viwanja au mashamba.
 
Madalali wanaofanya shughuli zao katika maeneo ya Masaki na Oysterbay, Dar es Salaam, wameiomba Serikali iingilie kati kutokana na kuingiliwa kwa biashara yao na raia wa kigeni, hasa Wachina, wanaodaiwa kufanya biashara ya udalali wanapoingia nchini.

Akizungumza na Swahili Times, Kaimu Katibu wa Madalali katika maeneo hayo, Ally Kasi, ameeleza kuwa raia hao wa kigeni husaidiwa na baadhi ya Watanzania wakiwemo madereva na wakalimani, jambo linalorahisisha shughuli zao zisizo rasmi katika soko la upangishaji wa nyumba.

“Anaweza akaja kwangu akanambia anahitaji nimwoneshe nyumba zinazopangishwa, namzungusha, na anaweza akakwambia hii nyumba mbaya hatuitaki, kumbe jioni karudi pale kampa mlinzi elfu 10 au 20, inategemeana na mtu aliyemkuta. Anachukua namba ya mwenye nyumba halafu anaongea na mwenye nyumba,” amesema.

Ameongeza kuwa baadhi yao huongeza bei ya upangishaji kwa makusudi ili kupata kamisheni ya siri. “Kwa mfano, nyumba ni dola 5,000 [TZS milioni 13] kwa mwezi, yeye anamwambia mwenye nyumba ‘nakuja na mchina mwenzangu, mwambie ni dola 5,500 [TZS milioni 14.2], hiyo 500 [TZS milioni 1.3] kila mwezi itakuwa yangu mwaka huu, mwakani utachukua wewe.'”

Kasi amesema tayari wameshawasilisha malalamiko hayo kwa baadhi ya viongozi wa Serikali, akiwemo Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo, na wameahidiwa kuwa suala hilo linafanyiwa kazi.

Madalali Dar walalamikia Wachina kuingilia kazi za udalali - SwahiliTimes Madalali Dar walalamikia Wachina kuingilia kazi za udalali
 
So wote hawalipi kodi. Shida iko wp?
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom