Je ni dhambi kufanya kazi ya udalali?

Je ni dhambi kufanya kazi ya udalali?

john achila mukumwa

Senior Member
Joined
Jan 4, 2024
Posts
137
Reaction score
273
Je ni dhambi kufanya kazi ya udalali?

Udalali ni nini

Dalali ni mtu anayeuza kitu kwa niaba ya mwingine na kisha kuchukua asilimia fulani ya faida ya kile kilichouzwa. Dalali pia anaweza kuwa mtu mwenye kutafuta soko la bidhaa ya mtu mwingine na kisha kuchukua asilimia ya faida inayopatikana.

Hata ununuaji wa bidhaa kiwandani na uuzaji masokoni kwa namna moja au nyingine ni “udalali”, kwani utanunua kwa gharama ndogo na kuuza kwa gharama kubwa na kisha kuchukua ile faida. Hapo tayari umeshakuwa dalali wa wenye kuitengeneza ile bidhaa.
Kwa maana ya maelezo hayo ya udalali, mtu akiifanya siyo dhambi.

Kwa hiyo udalali si dhambi ikiwa tu haujahusisha mambo yasiyofaa.

Mambo yasiyofaa ni pamoja na yale yaliyooneshwa hapa chini.

UWONGO NA UDANGANYIFU

Kwa mfano, kama umepewa kazi ya kutafuta mteja wa bidhaa husika, halafu ukampata na kumwekea kiwango cha juu sana, nje na mapatano na yule aliyekupa bidhaa. Lengo la kufanya hivyo ni ili wewe upate faida kubwa. Au, mteja amehitaji bidhaa au nyumba na wewe ukamlaghai kwa uwongo na kumpa kitu ambacho kiko chini ya viwango, huku ukijua kabisa kuwa kitu hicho hakistahili hiyo gharama. Huo wote ni uwongo au udanganyifu (Kutoka 20:16).
Tukumbuke kuwa kusema uwongo kwenyewe ni kutenda dhambi (Kutoka 20:16, Kumb. Torati 5:20), hivyo moja kwa moja, hata udalali unaofanyika kwa kusema uwongo, ni haramu.

DHULUMA
Dhuluma (Kutoka 20:16) ni kumdhulumu mtu fedha au mali au bidhaa yake, aidha kwa kumlipa kisasi au kwa sababu nyigine yoyote. Udalali huo ni haramu. Hii ni kwa sababu msingi wenyewe wa udalali, umejikita kwenye dhuluma, ambayo ni tendo la dhambi.

Shughuli zikifanyika ndani ya nyumba ya Mungu
Ilivyo, kanisa si sehemu ya minada, na udalali, ni sehemu ya ibada takatifu ya roho na kweli.
Bwana Yesu aliwafukuza wale madalali wote waliokuwa wanabadili fedha ndani ya nyumba ya Mungu:
Yohana 2:15 “Akafanya kikoto cha kamba, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao".
Hivyo, udalali unaofanyika ndani ya nyumba ya Mungu ni haramu.

Sadaka ya fedha zinazotokana na udalali
Pamoja na maelezo haya, kama udalali haujahusisha mambo hayo hapo juu, fedha iliyopatikana inaweza kutolewa sadaka ikiwemo zaka, na ikakubalika mbele za Mungu.

Kwa ujumla, kufanya kazi ya udalali ni halali, na si dhambi, kama inafanyika bila matendo yasiyofaa. Udalali unaotokana na kutenda dhambi ni dhambi; hauwezi kuhalalisha udalali huo kuwa sahihi. Badala yake unaufanya uwe haramu.

Je mkristo anaweza kufanya kazi ya udalali

Biashara halali yo yote ni kazi kama kazi zingine. Udalali pia ni sehemu ya kazi ya biashara.
Mkristo anaweza kufanya udalali, ikiwa hatatumia uwongo, dhuluma, rushwa, kuifanya ndani ya kanisa la Mungu, au kutumia njia au kitendo cho chote ambacho, kwayo ni dhambi.
 
DC836C3C-9AE7-4C14-8F67-9FEE6E8459D8.jpeg

😩
 
Mtu umechukua kazi ya kunadi kitu kwanini usimwambie anayekutuma kuwa thamani ya kitu chako ni 400 sisi watu na soko tutauza 450

Ili mlaji ajue bei elekezi ni 450 haipandi wala haishuki soko linyooke kama rula.!

Kwani kama inchi hatuna uelekezi wa kisheria ni asilimia ngapi dalali anapaswa kupata baada mchakato.!?

Kuna mzee kitaa aliwapa madalali wa bongo kazi ya kuuza nyumba yake akawapa na bei elekezi million 35 ile anataka auze arudi shamba akalime

Vile madalali wanamchukulia poa mzee hawakumpanga

Mzee wanakuta kwenye hati ya makabidhiano ni million 70.! 😎

Akaghairi kuuza nyuma katikati ya mchakato. 🤭
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom