Pinda aliwaambia Madaktari ''Liwalo na Liwe'', baadhi ya madaktari nao siku hizi wanafanya haya kuitikia wito huo:
1/Wanauza damu kama bangi(Wanasema hizo ndio deal za chap chap kwenye mazingira ya kazi yao).
2/Hakuna Emergency tena(Hawako tayari kuhatarisha maisha yao tena).
3/Wanafika kazini saa tatu Asubuhi na wanaondoka saa 6 mchana(Wanasema wanafanyakazi kulingana na malipo wanayopewa).
4/Hakuna huduma za Afya za msingi siku za weekend(Wanasema wako busy na mambo ya kifamilia kwanza).
5/Wameanzisha hospitali
zao(Vijiwe) na vituo vyao vya kupima Afya(Diagnostic centres) ambapo wagonjwa wao wanaelezwa kufika huko ili kupata huduma bora(Wanasema wanaongeza kipato ili kumudu maisha).
6/Wanakula rushwa(CCD) kama mchwa wenye njaa kali(Wanadai mfumo wa nchi yetu ndipo ulipofikia hapo).
7/Wanatoa siri za wagonjwa hadharani hususani magonjwa yenye unyanyapaa kama STI, Psychiatric etc(Wanasema ni adhabu kubwa sana kutunza siri za watu mioyoni mwao).
8/Wamekimbia kutibu na kwenda kusoma zaidi, kwenda kufanyakazi nje ya nchi, kwenda kufanya tafiti au kufanya kazi za kiofisi mahospitalini(Wanasema ni kujitesa kama sio kujiua kukaa Tanzania na kuishi kwa kutibu watu)
9/Wameacha kabisa kazi ya kutibu watu na kwenda kufanya kazi nyingine kama biashara(Wanasema kuna maisha zaidi ya udaktari)
10/Wanatoa tiba haramu tena ndani ya hospitali za Serikali(Abortion, Abusement, Placebo, Fixion, Torture etc)
*Omba Mungu sana usiugue wewe, ndugu yako au Rafiki yako na kisha ukaenda kutibiwa hospitali za umma/serikali, utajuta kwanini ulienda, mimi yalinikuta na sitasahau maisha yangu yote.