asakuta same
JF-Expert Member
- Mar 1, 2011
- 14,829
- 5,041
unazungumzia mauaji yanayofannywa na chadema au nini unachotaka kuuliza
mpuu.zi wewe nani kazungumzia ccm au chadema hapa. siyo lazima kila thread uchangie ,kaa kimya kuficha upumba.vu wako.
unazungumzia mauaji yanayofannywa na chadema au nini unachotaka kuuliza
Kuna jambo najiuliza hapa. Hivi kwani hao wabunge wanalipwa mshahara au hizo allowance ndiyo mshahara? Na je vikao huwa wanahudhuria kwenye muda wa ziada auNdio maana nikasema siasa iliingizwa ktk hilo. kumbuka sitting allowance ya mbunge ni tshs 70,000 na sio hicho mlicholishwa, ingawa ktk malipo kwa siku pia hulipwa posho ya kujikimu na posho hizo kumbuka hawalipwi kiholela isipokuwa pale tu wanapohudhuria vikao bungeni. zingatia idadi ya wabunge na jumla ya vikao wanavyokaa kwa mwaka. kwa kuonesha kujali serikali iliongeza kiasi cha malipo kwa madaktari ingawa sio kwa kiwango walichokuwa wanadai.
Kwa yeyote aliyekuwa akishabikia ule mgomo bila shaka alikuwa upande wa shetani ambaye aliuratibu ili kupoteza roho za watu wasio na hatia. Laiti kama ungepoteza ndugu au mtu wa karibu kwa sababu tu madaktari wamegoma bila shaka ungejua athari na ubaya wa ule mgomo. Kwa umuhimu wa kazi zao mgomo sio njia sahihi kwani roho zinazopotea pale haziwezi kufidiwa hata kama watalipwa zaidi ya wanachokidai. Siasa inaingia hasa pale unapotaka wachukuliwe kama ni bora sana kuliko watumishi wengine na kudai mambo ambayo kinadharia unayemdai hawezi kuyatimiza halafu silaha kubwa ni mgomo ambao unagharimu maisha ya wananchi wa hali za chini. Kamwe sitaunga mgomo wa madaktari kwa kuwa kufanya hivyo ni kushangilia vifo vya wananchi wasio na hatia tena wenye hali za chini kama mimi.
Matendo yao ndio yanathibitisha hayo. Angalia baada ya wanasiasa kukaa kimya kuhusu hilo kimeendelea nini zaidi ya baadhi ya madktari kuanza kuilamba serikali miguu kuhusu leseni zao na ajira zao?
Kwa yeyote aliyekuwa akishabikia ule mgomo bila shaka alikuwa upande wa shetani ambaye aliuratibu ili kupoteza roho za watu wasio na hatia. Laiti kama ungepoteza ndugu au mtu wa karibu kwa sababu tu madaktari wamegoma bila shaka ungejua athari na ubaya wa ule mgomo. Kwa umuhimu wa kazi zao mgomo sio njia sahihi kwani roho zinazopotea pale haziwezi kufidiwa hata kama watalipwa zaidi ya wanachokidai. Siasa inaingia hasa pale unapotaka wachukuliwe kama ni bora sana kuliko watumishi wengine na kudai mambo ambayo kinadharia unayemdai hawezi kuyatimiza halafu silaha kubwa ni mgomo ambao unagharimu maisha ya wananchi wa hali za chini. Kamwe sitaunga mgomo wa madaktari kwa kuwa kufanya hivyo ni kushangilia vifo vya wananchi wasio na hatia tena wenye hali za chini kama mimi.
Kwa yeyote aliyekuwa akishabikia ule mgomo bila shaka alikuwa upande wa shetani ambaye aliuratibu ili kupoteza roho za watu wasio na hatia. Laiti kama ungepoteza ndugu au mtu wa karibu kwa sababu tu madaktari wamegoma bila shaka ungejua athari na ubaya wa ule mgomo. Kwa umuhimu wa kazi zao mgomo sio njia sahihi kwani roho zinazopotea pale haziwezi kufidiwa hata kama watalipwa zaidi ya wanachokidai. Siasa inaingia hasa pale unapotaka wachukuliwe kama ni bora sana kuliko watumishi wengine na kudai mambo ambayo kinadharia unayemdai hawezi kuyatimiza halafu silaha kubwa ni mgomo ambao unagharimu maisha ya wananchi wa hali za chini. Kamwe sitaunga mgomo wa madaktari kwa kuwa kufanya hivyo ni kushangilia vifo vya wananchi wasio na hatia tena wenye hali za chini kama mimi.
wamegundua kuwa walikuwa wanatumiwa kisiasa sasa wameamua kuzingatia maadili yao na kuweka siasa pembeni.
taarifa zilizotelewa na serikali bungeni mara mbili ni kuwa mgomo haukuwa na athari zozote ...vifo vilivyotekea Muhimbili kipindi cha mgomo na kabla ya mgomo hakukuwa na tofauti...hansard
tumia hekima.. kuna watu wengi wanakufa mikononi mwa madaktari wakiwa katika jitihada za kuokoa maisha yao. na hilo linauma na source of flustration. Which is better acha watu wafe and act like nothing is wrong au goma kwa siku chache watu wachache wafe ili uweze kusave maisha ya watu wengi zaidi?!!
Nenda hospitali yoyote kubwa kachukue data za watu wanaokufa kutoka na kukosa huduma stahiki utalia... hawa waliokufa kwenye mgomo ni wachache mnno na ni sawa na jone la maji kwenye ndoo..
Watu wengi wanaharakishwa kufaa na hata viongozi wetu wanalijua hiloo ndio maana wakiugua wanakimbilia njee.. Madai ya madaktari yalikuwa rahisi sanaa ''serikali iboreshe huduma za afya kwa kuhakisha vifaa, dawa na miondombinu inaboreshwa ili kuwezesha madakatri kuokoa vifo vinavyozuilika na la mwisho ni kuboreshwa mishahara.
Pili watumishi hatuko sawa na ni ukweli usiopingika kila mmoja ana umuhimu wake na wengine ni bora kuliko wengine. Kama unabisha mbona serikali inalipa mishahara tofauti kwa kada tofauti?! Je mlinzi aliyepo ikulu analipwa sawa na mlinzi wa manispaa?!!
Acha kujidanganya. binadamu hatuko sawa, ila tuna mahitaji ya msingi ambayo ni sawa. Na suala la mshahara ni majadilianao kati ya mtumishi na mwajiri na ndio maana ukienda kwenye baadhi ya taasisi utakuta watu wawili wameajiriwa post moja lakini wana-mishahara tofauti na hii inatokana na wewe mwenyewe. Mwajiri anakuuliza nikulipe Tsh ngapi unasema laki nne na anakulipa mwenzako anaulizwa anasema milioni moja analipwa sasa kosa la nani?!.
Mmebatiza kazi ya udaktari ni wito na hawatakiwi kugoma halafu mnasahau kuwaongezea masilahi yao wakigoma shida, sasa why didnt you pay them better on the first place?!!
Nakuomba sanaa na pia ni kujithalilisha kutaka kujifananisha wewe na daktari au mwalimu au mkulima wakati wewe ni engineer?! Daktari ni daktari na mwalimu ni mwalimu na enginer ni enginer. na hizi ni professions. kila mtu ana kazi yake na kila mtuu ana umuhimu wake na haitakaa daktari alipwe sawa mhasibu eti kwa sababu wote wana first degree?!! No way.
Mfumo wetu wa kulipana mishahara ni mbovu na hauzingatii ugumu wa kazi, risk, initial capital iliyowekezwa kuwapata hao watumishi. Tumekuwa viazi na wavivu wa kufikiri wewe unasema serikali haina hela lakini hiyo hiyo serkali inawaambi madaktari haina helaa wikii hiyo hiyo ina hela inatangaza kupanda kwa posho za vikao vy wabunge, walipata wapii hiyo helaa. Waziri mkuu pinda ni mmoja kati ya watu waliouchochea sanaa mgomo wa madaktari kwa undumila kuwili wake.
Daktari ni mfanyakazi kama mfanyakazi mwingine anastahi vitendea kazi vya kutosha kama ilivyo lazimz kila waziri apate landcruiser V8 basi kila hospitali ipata vifaa stahiki kulingana na level yake. Na kama ilivyo haki kwa kila mwanasiasa kulipwa posho ya kukaa bungeni vilevile ni lazima kulipwa daktari posho yake ya kukesha akiokoa maisha ya wananchi wapiga propaganda kama wewe.
Endelea kufikiri hivyo.... Hivi umeshafanya tathmini ni madaktari wangapi wameondoka nchini baada ya ule mgomo tena waliosoma kwa kodi za watanzania sasa wanawatumikia wengine kwa serikali kushindwa kuwalipa???? No research no right to speak
Kuwa na majibu yasiyo na kujeli ndugu, unless huyo shetani unamchukulia kirahisi rahisi tu.
Kuna jambo najiuliza hapa. Hivi kwani hao wabunge wanalipwa mshahara au hizo allowance ndiyo mshahara? Na je vikao huwa wanahudhuria kwenye muda wa ziada au
muda wa kawaida wa kazi? Je vikao si ni sehemu ya majukumu yao ya kila siku? Sasa ni kwnini wanalipwa?
Sina maana kwamba madaktari hastahili malipo mazuri, lakini rejea madai yao kumi na moja kati ya hayo madai manane yalilenga maslahi na matatu yakalenga kuboreshwa kwa mazingira ya kazi kwenye huduma ya afya, unaweza kujua mzani ulilenga wapi kati ya hayo mawili.
Nakubaliana na hoja kuwa kila kada inastahili maslahi yake na mshahara ni makubaliano kati ya mwajiri na mwajiriwa, ikiwa hilo wanalielewa kulikuwa na haja gani ya kuendelea kulumbana na mwajiri ikiwa mshahara unaotaka hakulipi na mwajiri hakubalini na matakwa yako, njia ya uungwana ilikuwa kuandika barua ya kuacha kazi na si kugoma.
Kwa hoja hiyo hiyo ya kila kada na maslahi yake inaweza kukufanya ukose nguvu ya kujadili au kuhoji maslahi ya mawaziri ikiwa wewe sio waziri au waalimu wakati wewe sio mwalimu au wabunge wakati wewe sio mbunge au madaktari wakati wewe sio daktari.
Mkuu sina maana ya kukejeli, ninachokijua roho ya uuaji inatoka kwa shetani na shetani anapotaka kuua humuingia mtu yoyote na mtu huyo kufanya mauaji kutekeleza kazi ya shetani. sasa kama kutakuwa na wanolaani mauaji hayo ya watu wasio na hatia atakuwa anampinga na lumlaani shetani na kwale watakoshabikia watakuwa upande wa muuaji ambaye ni shetani.
Napenda sana unielewe kwa kile nisemacho na sio unavyotatafsiri wewe.
......unajua watanzania tuna Ushamba flani hivi wa KUJIDAI tunajua vitu...kumbe HAMNA KITU.....nani alikuambia DAKTARI anaweza kushawishiwa na MWANASIASA....tuaache huu ujuaji usiokuwa na msingiMatendo yao ndio yanathibitisha hayo. Angalia baada ya wanasiasa kukaa kimya kuhusu hilo kimeendelea nini zaidi ya baadhi ya madktari kuanza kuilamba serikali miguu kuhusu leseni zao na ajira zao?