#COVID19 Madaktari waishauri Serikali chanjo ya Corona kuwa ya lazima

Sasa kama wao wamechanjwa na wanaambukizwa na kufa,sasa sisi tuchanje ili iweje tena??
 
Inasikitisha sanaaa. Watu wengi wamekufa na serikali haitaki kukiri. Hili suala la chanjo ya majaribio ni hatari sana. Linaua kuliko hata covid yenyewe.
 
twendeni polepole
 
Iko sheria mtu akitaka kujiua mfano kujinyonga kwa kamba/kanga/ sarawili kwa kujitundika mtini au darini na bahati mbaya mpango huo ukabuma na akagundulika hushitakiwa kwa kosa la kutaka kujiua kwa kukusudia.

Wako wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa yanayo tesa na kufikia mahali kukutaa dawa za kutibu au kuupoza ugonjwa na hatimaye kuhatarisha maisha yao. Sijawahi kusikia pahala wameshitakiwa au iko sheria inayo taka walazimishwe kutumia dawa au washitakiwe kwa kukusudia kujiua kwa kukataa matibabu. Wako wengi tu wanaotembea na ukimwi wakijua au hawajui na kuendekea kuambukizana HIV. Lakini serikali hailazimishi kila mtu kwenda kupima HIV na madaktari hawalalamiki kuambukizwa ukimwi kwa kujichoma/ kujikata kwa bahati mbaya wakiwahudumia. Tunachosikia ni kampeni za kutumia gloves, kondomo dume na jike. Corona watumie kondomu zake ambazo ni barakoa na satinaiza waachane na hizi hoja za kujivunjia heshima mbele ya jamii inayo waheshimu tena sana tu.

Serikali kama inavotoa takwimu za walio chanjwa ingetoa na takwimu za wanaokufa kwa sababu za kuchanjwa na walio ambukizwa na walio chanja. Hii ingesaidia kuwahamasisha wasio chanja kuchukua tahadhari za umakini zaidi ya hii ya kukataa chanjo. Hili la kulazimishia chanjo ni kutafuta kukwaza wananchi wake na kuifanya ichukiwe nao bila sababu ya msingi.


Atakaye chukiwa zaidi ya wote hawa ni Mh Rais, sijui wenye huu mpango wa kulazimishana chanjo wanachuki gani na Rais mpaka kumchonganisha na anao waongoza. Mimi ni ulize inakuaje madaktari ambao mwanzoni walishauri chanjo iwe hiari leo wageuke kula matapishi yao eti chanjo iwe ni lazima? Tukisema hawana uhakika na utafiti wao tutakosea?
 
Umejichanganya...hebu soma tena kwa umakini ulichoandika.
 
Na swali jingine lakuuliza ni kwanini madakatri wao wanakufa sana kwa corona na uku wameshachajwa?
 
Chanjo bado zipo nyingi nenda kachanjwe.
 
Wametumwa si bure
 
Wakichanja wao kuna shida gani? hao watakuwa wanatumiwa na mabeberu kuweka kizuizi cha watu ambao hawajachanjwa kovid kunyimwa huduma za kiafya, tumeshashuhudia kule ufaransa kuna maandamano kwa sababu ya mambo kama haya, watu wananyimwa kuingia mahali kupata huduma kisa hawana cheti cha korona, Mwenyezi Mungu anawaona kwa kushiriki uovu......
 
Inasikitisha. Kuna watu wengi wamekufa kutokana na chanjo. Ushahidi upo mwingi mno, kila mtu anajua. Waache kujipendekeza, hakuna mtanzania atakaye jipeleka kwenye kifo.
Kwa hiyo upo kinyume na mwenyekiti wa ccm ambaye ni Rais wako? na kwa maana hiyo unaungana na Gwajima na polepole?
 
Kwa hiyo upo kinyume na mwenyekiti wa ccm ambaye ni Rais wako? na kwa maana hiyo unaungana na Gwajima na polepole?
Msimlishe Mwenyekiti wetu maneno. Yeye alishasema ni hiari. Kama kuna watu wamekufa kutokana na chanjo nani aendelee kuchanjwa???
 
Za kuambiwa changanya na za kwako

Mtumishi alihoji
Ukichanjwa unapona? Unaweza kupona au usipone
Ukichanjwa huambikizwi virusi? Unaambukizwa
Ukichanjwa Huambukizi wengine virusi? Unaambukiza
 
Sasa mtu anachanjwa kinga, halafu mgonjwa akija hiyo kinga haifanyi kazi mwilini, then anachoma ili imlinde na nini?!

Ni sawa na kulala kwenye chandarua chenye matundu makubwa yanayopitisha mbu, sasa unalala kwenye hicho chandarua kwa ajiri ya kupata ulinzi gani au kwa ajiri ya kutimiza wajibu wa kulala katika chandarua?!


COVID-19 ni ufala wa karne...ha ha ha ha ha. Sichanji Mimi.
 
Inasikitisha. Kuna watu wengi wamekufa kutokana na chanjo. Ushahidi upo mwingi mno, kila mtu anajua. Waache kujipendekeza, hakuna mtanzania atakaye jipeleka kwenye kifo.
Na mmoja ndugu yangu anahangaika na hali yake baada ya chanjo
 
Kwa watu wanaotumia akili zao za kuzaliwa , tayari wameshastuka kuwa hii ni miradi ya watu.
 
Mkuu hapo unakuwa unampoteza mbu maboya aanze kujiuliza mara mbili mbili, hivi hiki ni chandaruaaaa au nyavu ya kuvulia samaki.......wakati anabung'aa bung'aa kujiuliza anapigwa mweleka.
 
Madaktari wameishauri Serikali chanjo ya Corona iwe lazima.
===
Madaktari gani, wa wapi, waliishauri serikali lini, wakiwa wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…