Visenti
JF-Expert Member
- Jul 24, 2008
- 1,025
- 327
Siyo damu pekee mkuu, hata dawa utaambiwa haipo na kuelekezwa maduka ya kununua yanayomikiwa na hao Madaktari
Wang'ayo elewa kuwa HIZI NI ZAMA ZA RUSHWA NA POSHO!, makanisani, misikitini, majumbani, vijijini...jamii nzima imeathirika!
Kuhusu kumwelekeza mgonjwa wapi anaweza pata huduma au dawa,kama dakitari anamiliki kihalali,sioni ubaya wa kumwelekeza mgonjwa kununua dawa au kupata huduma ktk duka/hospital binafsi hata kama anamiliki au anifahamu vizuri kuwa huduma au propduct zake ni bora, ni sawa na dawa anayoandikiwa mgonjwa umejiuliza ni vigezo gani dokta anavitumia kuchagua dawa ktk kundi la dawa nyingi zinazofanana ufanisi wake? je inamaanisha anakuwa ameipendelea au kuitafutia soko kampuni iliyotengeneza dawa hiyo?
kuhusu kutoa mlungula kwa huduma ya damu au tiba nyinginezo, wanaosababisha ni nyinyi/sisi wenyewe, hakuna hatua zozote tunazozichukua bali kulalamika tuuu, na mara nyingi rushwa zinachochewa na wagonjwa na ndugu wa wagonjwa, kwa kutaka kukwepa taratibu zilizowekwa, kwa ujumla hiki ni kizazi cha rushwa na posho. Watanzania wengi wanaamini kuwa bila kutoa mlungula hawezi pata huduma nzuri, na wengi huanzisha wenyeewe kabla hawajaombwa, na hata kazini kikao au mafunzo kufanyika bila kulipwa posho eti watu wanagoma, nilishangaa hii tabia imeenea hata vijijini eti kuwaita wajumbe wa kamati fulani ili kuwaelekeza mambo ya maendeleo kwa faida yao kwanza wanauliza posho na kama hakuna wanagoma kushiriki, hiyo ni rushwaaa!