johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 84,035
- 142,131
Hiyo ndio taarifa ya Dkt. Mchomvu wa Kairuki hospital
Anasema juzi asubuhi Membe alifika hospital hapo kwa ajili ya check up na alikuwa kawaida kabisa anatembea mwenyewe, anaongea na kucheka kufanya utani kama kawaida
Baada ya check up alirudi nyumbani kwani hakuwa na tatizo lolote lakini alfajili ya leo(jana) aliletwa akiwa mahututi na Moja kwa Moja akapelekwa ICU na likaitwa Jopo la Madaktari kumhudumia, amesema Dr Mchomvu
Madaktari tuna kazi ya kuokoa maisha lakini Swala la kifo ni la Mungu mwenyewe hakuna awezaye kuzuia, amesema.
---
DAKTARI WA MEMBE AFUNGUKA KILICHOMUUA MEMBE.
Daktari wa Familia na Daktari wa Muda Mrefu wa Bernard Membe amesema Membe alikuwa mzima na alikuwa na afya imara wakati wote wala hakuwahi kuwa na tatizo lolote sugu kama magonjwa ya kisukari wala Moyo.
Amesema Siku ya Jana alipata homa ndogo ya kifua, akapata shida ya kukohoa na kubanwa kifua na usiku wa kuamkia leo alishindwa kupumua ghafla akakimbizwa Hospitali
Ameongeza kuwa maradhi hayo yanatokana na virusi ambavyo vinazunguka vinaingia kwa njia ya hewa, vinasababisha mgando kwenye mfumo wa mapafu, damu inakuwa nzito na hicho ndicho kimesababisha kifo cha Membe
Source: Wasafi