Madaktari kuuza damu kwa wagonjwa mahututi ni ubinadamu?

Siyo damu pekee mkuu, hata dawa utaambiwa haipo na kuelekezwa maduka ya kununua yanayomikiwa na hao Madaktari

Wang'ayo elewa kuwa HIZI NI ZAMA ZA RUSHWA NA POSHO!, makanisani, misikitini, majumbani, vijijini...jamii nzima imeathirika!

Kuhusu kumwelekeza mgonjwa wapi anaweza pata huduma au dawa,kama dakitari anamiliki kihalali,sioni ubaya wa kumwelekeza mgonjwa kununua dawa au kupata huduma ktk duka/hospital binafsi hata kama anamiliki au anifahamu vizuri kuwa huduma au propduct zake ni bora, ni sawa na dawa anayoandikiwa mgonjwa umejiuliza ni vigezo gani dokta anavitumia kuchagua dawa ktk kundi la dawa nyingi zinazofanana ufanisi wake? je inamaanisha anakuwa ameipendelea au kuitafutia soko kampuni iliyotengeneza dawa hiyo?
kuhusu kutoa mlungula kwa huduma ya damu au tiba nyinginezo, wanaosababisha ni nyinyi/sisi wenyewe, hakuna hatua zozote tunazozichukua bali kulalamika tuuu, na mara nyingi rushwa zinachochewa na wagonjwa na ndugu wa wagonjwa, kwa kutaka kukwepa taratibu zilizowekwa, kwa ujumla hiki ni kizazi cha rushwa na posho. Watanzania wengi wanaamini kuwa bila kutoa mlungula hawezi pata huduma nzuri, na wengi huanzisha wenyeewe kabla hawajaombwa, na hata kazini kikao au mafunzo kufanyika bila kulipwa posho eti watu wanagoma, nilishangaa hii tabia imeenea hata vijijini eti kuwaita wajumbe wa kamati fulani ili kuwaelekeza mambo ya maendeleo kwa faida yao kwanza wanauliza posho na kama hakuna wanagoma kushiriki, hiyo ni rushwaaa!
 
Mkuu unajua Madaktari wa sasa wanafikiri kwamba taaluma hiyo sasa ni ya kuabudiwa. Siyo damu pekee mkuu, hata dawa utaambiwa haipo na kuelekezwa maduka ya kununua yanayomikiwa na hao Madaktari. Hivi tukisema mazingira mabaya wanayajenga wao wenyewe tutakosea? Wauze damu, wahamishe madawa na vifaa vingine bado wanadai mazingira mazuri yapi hayo?
we tema povu tu ila mgomo upo pale pale kikubwa ni kutatua tatizo sio argument kama hii ambayo haina mashiko.
 
blood bank Incharge sio Dr...wananchi wetu wana uelewa mdogo sana sana sana...wakiona mtu yuko hospital kavaa koti refu jeupe waadhani ni Dr.
nadhani elimu inahitajika....tusimlaumu aliye post hi I mada . tumpe elimu
 
Hivi ukiambiwa kumtolea ndugu yako damu kwa nini iwe shida? Ni mambo mangapi serikali wanasema ni bure wakati watu wanalipia. Si tulisikia madaktari wakimwambia Pinda siku waliyokutana nao pale muhimbili kuwa serikali inajidai huduma bure wakati wakienda hospitali wanaambiwa wabebe cloves zao, syringe zao na madawa yao. Mnawasingizia hao madaktari kwa kuwa wao ndio wanaoonana ana kwa ana na wagonjwa hivyo kubebeshwa lawama. Sasa wamesema LAWAMA BASI, mnahangaika!

Kama kweli ulienda hospitali ukatozwa rushwa ni wajibu wako kuripoti na kumuwajibisha aliyekutoza rushwa ( Sasa unataka madaktari wawasaidie kugoma kwa sababu wanatoza rushwa). Fanya sehemu yako ya wajibu kuwawajibisha wala rushwa wote na wote wasio na tija kwa Tanzania.

kama hujailewa mada ni lazima uchangie?
 
Madaktari wetu ni wakatili aisee ukishaingia kwenye himaya yao lazima wakutoe upepo. Na hili sio swala la malipo ni swala la ethics kwa sababu naamini wanajua situation kwenye sekta ya afya kabla hawajaingia huko.

Tunatolewa upepo na DOWANS bil 111, kagoda Bil 40, Chenge Bil 40 za rada, Meremeta zaidi ya Bil 150, EPA bil 133. Deepgreen...... ukishatoka huko nenda kacheck bei na matumizi ya maVX ya mawaziri na wakurugenzi, wakuu wa mikoa na wakurugenzi wao, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wao. hizi za madaktari zipo kotekote - TRA, TANESCO, hata kutafutiwa faili tu maofisini. kwa mwenye akili anajiuliza chanzo cha haya yote ni nini? na kisha ananza kuhangaika na chanzo. Madaktari wanalijua sana hili la kudeal na chanzo maana asilimia kubwa ya kazi yao inabezi kwenye Symptoms, then signs, then hawaishii hapo na kuanza kutibu bali wanafanya investigations maabara kujua kilichosababisha hizo symptoms na signs ni nini (i.e DIAGNOSIS), wakishakijua ndipo hutoa tiba ambayo inaelekezwa kwenye diagnosis na zingine kidogo kama panadol na asprin ili kutoa relief ya symptoms. Sasa hizo stage zote wameshapita na wamefikia diagnosis. Mnachosuggest akina mamaporojo ni kuwa waachane na kutibu diagnosis ila wajikite kwenye tiba ya kutoa unafuu wa symptoms. Ni ngumu sana kwa madaktari kuwaelewa zaidi sana wanawashangaa tu.
 
blood bank I charge ni laboratory technician au lab technologist...Dr,kazi yake ni kuomba damu kwa hizi department ili mgonjwa awekewe....damu ni tatizo kubwa NA ndio maana kuna wajanja wachache wanatumia hii mwanya kuchukua rushwa.
cha msingi report kwa administration ya hiyo hospitali Ili hiyo muuza damu akamatwe......
kwa kutuma ngugu zako wakachukue hela nyumbani that's means umebariki hiyo rushwa,...
tufunguke watanzania.....tuko nyuma sana kudai haki zetu za msingi....Rushwa NA upendeleo ni adui WA haki NA amani ya NC I.
Good afternoon
 
blood bank Incharge sio Dr...wananchi wetu wana uelewa mdogo sana sana sana...wakiona mtu yuko hospital kavaa koti refu jeupe waadhani ni Dr.
nadhani elimu inahitajika....tusimlaumu aliye post hi I mada . tumpe elimu

Rushwa ina channel anayepokea wagonjwa anaweza kuwa anaunganisha line na incharge wa blood bank. Kumbuka incharge wa blood bank haonani na wagonjwa moja kwa moja hivyo daktari au muuguzi ndio makamanda wa mbele kumwambia mgonjwa damu ipo benki lakini inahitajika fedha.
 
Ndugu yangu alikufa kwa kukosa fedha ya kulipia damu Muhimbili sitasahau siku hiyo, tulimtuma ndugu mmoja kwenda kuchukua fedha akachelea lakini mgonjwa wetu alikufa tukimwangalia.

Pole sana,naweza kusema wananchi wa Tanzania tumezoea kupelekwa pelekwa katika kila idara.Na laiti sisi wenyewe tungekuwa na ushirikiano nchi nzima kama nchi zingine serikali ingetia adabu.Ok,ndio uzalendo.
 
Damu ya kuongeza wagonjwa mahututi inauzwa ingawa kanuni ya tiba inakataza kufanya hivyo kwani hata wanaojitolea damu hawauzi damu yao kwa hospitali husika. Benki ya damu ni kwa ajili ya dharura lakini ukifika na mgonjwa madaktari watakuambia lipa mathalan elfu 50,000 ili mgonjwa wako aongezewe damu kama huna fedha unatakiwa kwenda kutafuta ndugu na jamaa wa kujitolea damu hata kama ipo lakini wakati huo mgonjwa kabakiza muda wa nusu saa damu itakwisha mwilini na asipopata damu daktari anakuambia atakufa. Ukitoa fedha damu inaletwa mara moja.

My take: - mazingira ya kugoma kwa maelezo kwamba serikali iboreshe mazingira ya kazi ni kweli?

- Kama wanaojitolea damu bure wangekuwa wanauza bei yake ingekuwa ya juu kupita kiasi
tusingeiweza wengi na tungekufa.

- Je mazingira bora ya kazi ni tiketi ya pekee ya mgonjwa kupata huduma bora?
Je huduma bora ni vifaa vya kazi pekee au inaambatana na roho ya daktari na muuguzi?

Daktari anahusikaje kuuza damu. unaonekana hata hujui daktari anafanyaje kazi - Daktari anayemuona mgonjwa mara nyingi hutoa orders tu mfano, mgonjwa anahitaji damu units 3 kama vile anavyoprescribe vidonge. Daktari haendi pharmacy kumchukulia vidonge mgonjwa, wala haendi blood bank kumchukulia damu mgonjwa unless kuna tatizo la logistics. Hivyo hakuna mazingira yanayomfanya daktari amuuzie mgonjwa damu. kama ukinunua basi kuna wahusika wengine kabisa, ila kwa kuwa upeo wenu wa uelewa kikomo chake ndo hapo basi mnajua ni daktari ndiye aliyewauzia.
 
...not everybody can be a doctor, hata tukilipwa hela ndogo, tukiwa maskini...still, not everybody can be a doctor! You will hate that fact for the rest of your miserable life!

Kwani ulilazimishwa kufanya kazi serikalini? si ungeenda kuomba kazi Agha Khan kama ulikuwa unataka maslahi?
 
Rushwa ina channel anayepokea wagonjwa anaweza kuwa anaunganisha line na incharge wa blood bank. Kumbuka incharge wa blood bank haonani na wagonjwa moja kwa moja hivyo daktari au muuguzi ndio makamanda wa mbele kumwambia mgonjwa damu ipo benki lakini inahitajika fedha.

nnachosema hapa ni kwamba yawezekana mazingira ya rushwa yakawepo...Ila tukubali kuwa both mtoa NA mpokeaji ni wakosaji ...kama umeombwa rushwa I li upewe damu nawe ukatoa that means umebariki...
mtu pekee anayeweza badili upepo ni mtoaji NA sio mpokeaji....report
 
damu ya kuongeza wagonjwa mahututi inauzwa ingawa kanuni ya tiba inakataza kufanya hivyo kwani hata wanaojitolea damu hawauzi damu yao kwa hospitali husika. Benki ya damu ni kwa ajili ya dharura lakini ukifika na mgonjwa madaktari watakuambia lipa mathalan elfu 50,000 ili mgonjwa wako aongezewe damu kama huna fedha unatakiwa kwenda kutafuta ndugu na jamaa wa kujitolea damu hata kama ipo lakini wakati huo mgonjwa kabakiza muda wa nusu saa damu itakwisha mwilini na asipopata damu daktari anakuambia atakufa. Ukitoa fedha damu inaletwa mara moja.

My take: - mazingira ya kugoma kwa maelezo kwamba serikali iboreshe mazingira ya kazi ni kweli?

- kama wanaojitolea damu bure wangekuwa wanauza bei yake ingekuwa ya juu kupita kiasi
tusingeiweza wengi na tungekufa.

- je mazingira bora ya kazi ni tiketi ya pekee ya mgonjwa kupata huduma bora?
Je huduma bora ni vifaa vya kazi pekee au inaambatana na roho ya daktari na muuguzi?

propaganda mbaya. Mawaziri wamechaguliwa kwa ama kulipa fadhila, ama kuweka uwiano sawa, ama kunyamazisha watu wanaopinga ufisadi ama kiushikaji, meritocracy was not there. Katiba mpya ije iondoe hizi regularities tuone kama hao madakitari watauza damu tena
 
Pole sana,naweza kusema wananchi wa Tanzania tumezoea kupelekwa pelekwa katika kila idara.Na laiti sisi wenyewe tungekuwa na ushirikiano nchi nzima kama nchi zingine serikali ingetia adabu.Ok,ndio uzalendo.

that's true.....Tue wazalendo WA ukweli
 
Damu ya kuongeza wagonjwa mahututi inauzwa ingawa kanuni ya tiba inakataza kufanya hivyo kwani hata wanaojitolea damu hawauzi damu yao kwa hospitali husika. Benki ya damu ni kwa ajili ya dharura lakini ukifika na mgonjwa madaktari watakuambia lipa mathalan elfu 50,000 ili mgonjwa wako aongezewe damu kama huna fedha unatakiwa kwenda kutafuta ndugu na jamaa wa kujitolea damu hata kama ipo lakini wakati huo mgonjwa kabakiza muda wa nusu saa damu itakwisha mwilini na asipopata damu daktari anakuambia atakufa. Ukitoa fedha damu inaletwa mara moja.

My take: - mazingira ya kugoma kwa maelezo kwamba serikali iboreshe mazingira ya kazi ni kweli?

- Kama wanaojitolea damu bure wangekuwa wanauza bei yake ingekuwa ya juu kupita kiasi
tusingeiweza wengi na tungekufa.

- Je mazingira bora ya kazi ni tiketi ya pekee ya mgonjwa kupata huduma bora?
Je huduma bora ni vifaa vya kazi pekee au inaambatana na roho ya daktari na muuguzi?
Kwani hayo mazingira mabaya yameonekana siku hizi!.Yasiku hizi ni salama kiasichake kuliko ya miaka ya nyuma.HAPO MKUU MASLAHI KWANZA UBINADAM KAPUNI.
 
Kwani ulilazimishwa kufanya kazi serikalini? si ungeenda kuomba kazi Agha Khan kama ulikuwa unataka maslahi?

Nilishaacha kufanya kazi serikalini tangu 2006, and believe me...am so much better and happy first for my decision to quit practising clinical medicine (wakati ni specialist surgeon), and second for where I am right now! lakini siachi kujiuliza iwapo kila daktari ataacha clinical work hospitali akaja huku niliko mimi...nani atatibu mama/baba/dada/kaka/sshangazi/mjomba/babu/bibi zetu? mara zote naheshimu na kwatetea kwa nguvu zote maDaktari wenzangu ambao hawakuchukua uamuzi wa kuacha kutibu kama mimi na kubaki mahospitalini wakitibu...I have been there long enough to know hard hard/frustrating/hopeless it is kuwa katika hospitali ya serikali ukitibu waTanzania masikini (sio wewe keyboarder mbofya bofya tu hapa JF kutukana madaktari kisha ukiugua unakimbilia Aga Khan)...wanaopata huduma huko Muhimbili/Temeke/Amana/Mwananyamala wanajua...
 
Tunatolewa upepo na DOWANS bil 111, kagoda Bil 40, Chenge Bil 40 za rada, Meremeta zaidi ya Bil 150, EPA bil 133. Deepgreen...... ukishatoka huko nenda kacheck bei na matumizi ya maVX ya mawaziri na wakurugenzi, wakuu wa mikoa na wakurugenzi wao, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wao. hizi za madaktari zipo kotekote - TRA, TANESCO, hata kutafutiwa faili tu maofisini. kwa mwenye akili anajiuliza chanzo cha haya yote ni nini? na kisha ananza kuhangaika na chanzo. Madaktari wanalijua sana hili la kudeal na chanzo maana asilimia kubwa ya kazi yao inabezi kwenye Symptoms, then signs, then hawaishii hapo na kuanza kutibu bali wanafanya investigations maabara kujua kilichosababisha hizo symptoms na signs ni nini (i.e DIAGNOSIS), wakishakijua ndipo hutoa tiba ambayo inaelekezwa kwenye diagnosis na zingine kidogo kama panadol na asprin ili kutoa relief ya symptoms. Sasa hizo stage zote wameshapita na wamefikia diagnosis. Mnachosuggest akina mamaporojo ni kuwa waachane na kutibu diagnosis ila wajikite kwenye tiba ya kutoa unafuu wa symptoms. Ni ngumu sana kwa madaktari kuwaelewa zaidi sana wanawashangaa tu.

Kaka mkubwa,

Ukiendesha gari ukapita taa nyekundu trafiki akikumata akiomba 10,000 kama huna utaandikiwa kulipa notification au gari italala kituoni. Lakini daktari akitaka 50,000 wakati mkeo mjamzito anatakiwa operation na hiyo pesa huna hapo unapoteza mke na mtoto chance kubwa sana. Kagoda, EPA nk pamoja na kuwa mabilioni ya shillingi lakini bado hazitishii maisha yangu moja kwa moja kama huyu daktari anayeniomba sh 5000 wakati mimi nipo hoi bin taaban nimepata ajali nimefikishwa hospitali na wasamaria wema saa 7 usiku.
 
Swali dogo la kujiuliza: WHO RUNS THE BLOOD BANK? Yeyote anayejua hospitali yoyote Tanzania ambapo daktari ndio in-charge wa blood bank aseme hapa! Maana sio kila mfanyakazi hospitalini basi ni daktari! Wakati niko Muhimbili nimeshaona mara kibao watu wanakuja muulizia mfagia ward (sio hata nurse) wakiulizia dokta fulani! Sasa hu6yu mtu akifanya ujinga wowote ule, basi ni dokta kafanya...hata akifumaniwa mtaani huko kwenye uwazi wataandika daktari bingwa kafumaniwa!
.....Its a fact that not everybody can be a doctor; and its also true that not every doctor can be A Real doctor..the one whom you can trust and professinally upright, the one who can not mistakenly operate on a feet instead of a head, the one whose main goal is to save life and not to cause death..Now we are made to understand that we have just a pocket of Real docs remaining..the rest are just wachumia tumbo, synonymous to those sleeping fellows in the august house, who are dying to have their 'sleeping allowances' tripled in the expence of the lives of their voters! Shame on you. The unfolding episode reminds me of a dedicated doctor simply known as 'Dr Waya' of Litembo Hospital whose dedication to save humanlives remains immeasurable now and then! and for that matter her popularity in southern region is unquestinable!
 
Nilishaacha kufanya kazi serikalini tangu 2006, and believe me...am so much better and happy first for my decision to quit practising clinical medicine (wakati ni specialist surgeon), and second for where I am right now! lakini siachi kujiuliza iwapo kila daktari ataacha clinical work hospitali akaja huku niliko mimi...nani atatibu mama/baba/dada/kaka/sshangazi/mjomba/babu/bibi zetu? mara zote naheshimu na kwatetea kwa nguvu zote maDaktari wenzangu ambao hawakuchukua uamuzi wa kuacha kutibu kama mimi na kubaki mahospitalini wakitibu...I have been there long enough to know hard hard/frustrating/hopeless it is kuwa katika hospitali ya serikali ukitibu waTanzania masikini (sio wewe keyboarder mbofya bofya tu hapa JF kutukana madaktari kisha ukiugua unakimbilia Aga Khan)...wanaopata huduma huko Muhimbili/Temeke/Amana/Mwananyamala wanajua...
Wewe ulifanya mawazo ya busara kwakuwa ulishajiona kwamba huna wito,motivation yako ilikuwa ni gain zako binafsi sio kusaidia wananchi wa nchi yako waliopigika. Mimi nina matatizo na hawa wenzako wanaojifanya kama wana interest za wananchi at heart halafu wanafanya vitu completelly opposite. Ni bora wangeondoka kama wewe wakabaki wale ambao kweli wapo tayari kufanya kazi kwa ajili ya wananchi kuliko kuwaomba kitu kidogo wananchi choka mbaya na kuwauzia dawa na huduma nyingine ambazo walistahili kupata bure.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom