Madaktari kugoma nchi nzima!

Madaktari kugoma nchi nzima!

Tunaotegemea hospital za Serikali mbona cha moto tutakina!
Lakini mbona pesa za posho za wabunge ziapatikana lakini pesa za madaktari ndio ishu!!?
 
Imeandikwa na Theopista Nsanzugwanko; Tarehe: 18th January 2012 @ 14:50

MBUNGE wa Nzega, Dk. Hamisi Kigwangalla (CCM), amehamasisha madaktari wagome bila kuogopa wanapoamua kuweka vifaa chini.

Amesema ili kuhakikisha Serikali inachukua hatua mapema kuhusu malalamiko yao alitaka waweke chini vifaa kabla ya mazungumzo na Serikali.

Kigwangalla, alitoa kauli hiyo jana Dar es Salaam, kwenye mkutano wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) waliojadili uamuzi wao baada ya Serikali kutorudisha walioondolewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mkutano huo uliojumuisha madaktari wa kada mbalimbali ulijadili uamuzi wa muda mfupi baada ya Makamu Mwenyekiti wa MAT, Dk. Primus Saidia na wengine wawili kwenda Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kwa nia ya kumwomba Waziri aende kuzungumza nao.

Mbunge huyo aliwataka madaktari kutorudi nyuma bali kusonga mbele, huku akiwataka kuacha woga na kuwa majasiri katika kusimamia maslahi yao kwa umoja.

Alisema wakikosa ushirikiano katika uamuzi wao hususan wa kuweka vifaa chini kushirikisha madaktari, wauguzi na wafamasia ili kuwe na matokeo ya uwekaji vifaa hivyo.

Aliwambia kama kutakosekana ushirikiano miongoni mwao, ndio utakuwa mwisho wa mapambano yao kwani uamuzi huo umefanywa katika ngazi kubwa ya MAT, hivyo hakutakuwa na pengine pa kukimbilia, kwani chama hicho ndiyo ngazi ya juu ya uamuzi.

“Ikiwa tutakubaliana kuweka vifaa chini, lazima kuona athari ili tusidharaulike, kwa kuwa na mikakati ya pamoja ya kushirikisha wote, kwani ikiwa uamuzi huo utafikiwa na katika huduma ziendelee hospitalini mtakuwa mmejimaliza,” alisisitiza Kigwangalla.

Mbunge huyo alisema madaktari waliofika katika mkutano huo ni wachache (250) wakati kuna zaidi ya madaktari 500 Dar es Salaam, hivyo lazima kuwe na mikakati ya kuhamasisha wengine kushiriki katika kufikia uamuzi huo.

Alisema ikiwa lengo lao halitafanikiwa, itawachukua miaka 10 kulalamikia maslahi yao na kufanyiwa kazi huku akisisitiza kuwa yeye sasa si daktari kwani mbali na uanasiasa, ana shughuli zake nyingine na watakaoathirika ni walio kazini.

Alishauri kuwa katika malalamiko yao madaktari watake mshahara wa Sh milioni 3.5 huku posho iwe Sh 200,000 kwa madaktari wanaofanya kazi za ziada.

Hata hivyo Mwenyekiti wa MAT, Dk. Namala Mkopi alipinga kiwango hicho cha posho na kusema wao wanataka nusu ya posho ya siku ambayo ni Sh 40,000.

“Wabunge wanadai posho ya Sh 200,000 kwa ajili ya posho ya saa nane, kwa nini madaktari wasipewe posho hiyo kwa kazi ya saa 36?”Alihoji.

Katika kikao hicho kilichoanza saa nne asubuhi, madaktari hao walishauriana kutotoa uamuzi huo hadi waonane na Waziri wa Afya na kuwatuma wawakilishi watatu kwenda wizarani.

Akitoa taarifa baada ya kurejea kutoka wizarani, Dk. Saidia alisema walikutana na Naibu Waziri wa Afya, Dk. Lucy Nkya, aliyewaahidi kufika katika mkutano huo baada ya saa moja yaani saa 10.

Lakini kabla ya muda huo kufika, Dk. Saidia alisema alipigiwa simu na Naibu Waziri akiomba radhi kuwa hatafika kwani amekutana na wasaidizi wake lakini hakuwa amepata jibu la moja kwa moja kuhusu madai yao.

Hivyo, kutokana na hali hiyo, aliomba akutane nao wote leo saa nane mchana katika ukumbi utakaotafutwa na Wizara, jambo ambalo madaktari hao walilikubali, lakini wakataka ukumbi watakaoutafuta wao.

Baadhi ya madaktari waliohamishwa Muhimbili, walilalamika kutopokewa katika hospitali walizopangiwa na Wizara kwa sababu mbalimbali.

Dk. Frank Mgaya alisema yeye na wenzake waliopangiwa Amana, hawajapokewa kwa madai hospitali hiyo haijapata barua ya Wizara na kuwataka kutoa nakala za barua zao na kuziacha hospitalini hapo na kurudi jana.

Alisema lakini jana asubuhi walipigiwa simu kuwa kikao hakijafanyika hivyo wasiende huku akisisitiza kuwa katika hospitali hiyo, kuna madaktari bingwa watatu, huku walio katika mazoezi ni 51, jambo ambalo ni vigumu kujifunza.

Alisema waliokwenda Lugalo walikuwa saba na walipokewa wanne na Aga Khan walitakiwa kurudi mwisho wa mwezi huu na kabla ya kupokewa watafanyiwa mtihani wa majaribio.

Hivyo, alisisitiza kuwa si kweli kuwa hawajaripoti walikopangiwa, ila hawapokewi kwa sababu mbalimbali na kuiomba Wizara kufuatilia suala hilo.

Madaktari hao waligoma hivi karibuni wakidai posho zao za mazoezi kwa vitendo ambazo walilipwa Sh milioni 826 na kisha Serikali kuwasambaza katika hospitali mbalimbali za wilaya.

Baada ya uamuzi huo, madaktari walipinga na kuipa Serikali saa 72 (zilizomalizika jana), kutaka warudishwe wote kuendelea na mafunzo Muhimbili huku wakiwa na madai mengine.

Kigangwalla ana backup ya Kikwete? always anakwenda njia tofauti na wenzake wa CCM
 
Lucy Nkya(8).jpg

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya

Siku chache baada ya Chama cha Madaktari nchini (MAT) kutangaza mgogoro na serikali na kuipa saa 72, serikali imetangaza kuwa ipo tayari kukaa nao meza moja na kuzungumzia masuala ya sekta ya afya.

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya, alitoa kauli hiyo jana na kusema kuwa serikali ipo tayari kukaa na MAT kuzungumza kama watakuwa tayari.
Dk. Nkya alisema sakata la madaktari 1,994 waliokuwa katika mazoezi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili waliamua kutoendelea na ratiba zao za mazoezi kwa vitendo baada ya kucheleweshewa posho zao za kila mwezi.

Alisema baada ya kuchelewa kutolewa kwa fedha za posho, wizara ilifanya jitihada ya kuhakikisha fedha hizo zinapatikana haraka.

Alisema serikali ilikuwa ikitoa taarifa katika taasisi walizokuwa wakifanyia kazi kuhusiana na jitihada zinazofanywa ili kutatua tatizo hilo.
“Ieleweke kwamba wataalamu hawa huingia mikataba na hospitali husika na mkataba wanaoingia umeainisha hawatakiwi kugoma au kuanzisha mgomo,” alisema Dk. Nkya.
Dk. Nkya alisema pamoja na wizara kufanya jitihada hizo kuwa suala lao limefanyiwa ufumbuzi, lakini bado walishikilia msimamo wao wa kutorudi vituoni hadi wapokee fedha na kwamba jambo hilo halikuwa la kiungwana.

Alisema baada ya kuona hivyo, wizara ilipeleka wataalamu 51 waliokuwa wakisubiri kuanza mafunzo Januari mwaka huu ili kuchukua nafasi za wataalamu waliokataa kurejea katika hospitali hiyo kwa ajili ya kuzuia athari ambazo zingeweza kujitokeza kwa wagonjwa. Hata hivyo, alisema katika mgomo huo kuna wenzao 60 ambao hawakugoma.

“Baadhi ya wataalamu waliokuwa wakifanya mazoezi katika vituo kama vya Hospitali ya KCMC, Mount Meru, Bombo, Bugando na Manispaa za Dar es Salaam walitambua jitihada za wizara za kushughulikia tatizo hilo na waliendelea na ratiba yao ya mazoezi kwa vitendo,” alisema.

Alisema waliogoma uongozi wa Muhimbili uliwachukulia hatua na kuwaandikia barua kuwarudisha wizarani na kutaka wapatiwe wataalamu hao.
“Ili kuhakikisha wataalamu hao wanafikia malengo ya mazoezi ya vitendo wizara imeamua kuwapanga katika hospitali mbalimbali ikiwemo Muhimbili, Temeke, Mwananyamala, Aga khan, Amana na Lugalo kwa kuzingatia uwezo wa hospitali,” alisema.
Alisema Januari 16, mwaka huu wataalamu 194 walikuwa wamepewa barua na wameripoti katika vituo walivyopangiwa.

Alisa wizara yake imepata taarifa kupitia vyombo vya habari kuwa MAT imewapa saa 72 iwarudishe madakatari hao katika hospitali ya Muhimbili pamoja na kutaka kuondolewa kwa baadhi ya viongozi wa wizara.

Hata hivyo, alisema tamko hilo halijawasilishwa rasmi wizarani na kusisitiza kuwa madakatari hao hawajafukuzwa kufanya mazoezi bali wamepangiwa vituo vingine.

Akizungumzia uamuzi wa MAT kumvua uanachama Mganga Mkuu wa Serikali, Deo Mtasiwa, Dk. Nkya alisema chama hicho hakiwezi kumchukulia hatua bali chombo chenye mamlaka ni Wizara.
Rais wa MAT, Dk. Namala Mkopi, alisema suala hilo watalizungumzia leo na kwamba tamko walilolitoa Jumamosi sio lazime lipelekwe wizarani ndio maana walitoa taarifa kupitia vyombo vya habari.

CHANZO: NIPASHE
 
Shida ya serikali kuongozwa na siasa badala ya taaluma. Sasa hapo napo mseme ni CDM wanaasisi mgomo wa Madaktari
 
Kigwagala ni upambanaji, lakini shombo la Magamba anakopigia kura za ndiyoooooooo!!!!!! Bungeni linamfanya anuke vibaya mbele ya wapambanaji wenzake.:biggrin::biggrin::biggrin::biggrin::biggrin::biggrin::biggrin::biggrin:
 
Unamfahamu Kigwangala kweli wewe au ndo mwendelelezo wa ushabiki wa kisiasa?
 
Madaatari wanatakiwa kuwa kama watumishi wa vyombo vya usalama. Sidhani ethics za taaluma ya udakatri zinawafavour kugoma. Mgomo kwa mdaktari hautakiwi kuwa kuw option hata ya tatu kama kwa wanafunzi au walimu au marubani au etc.

Otheriwise pamoja kwamba tunajua mattizo yao but migomo ya holela ya mdaktari ni uthibitisho wengi waliingia fani wa kufuata mkumbo. sina uhakia lakini kwa logic niiyonayo sidhani hata nchi za nje na zilizoendelelea madktari wana option ya kugma katika ku boycot
.

Kifupi madaktari waache uselfish. I think .They should know a better way ya kudeal na wanasiasa badala ya kuwakomoa wananchi.
 
Kigwagala ni upambanaji, lakini shombo la Magamba anakopigia kura za ndiyoooooooo!!!!!! Bungeni linamfanya anuke vibaya mbele ya wapambanaji wenzake.:biggrin::biggrin::biggrin::biggrin::biggrin::biggrin::biggrin::biggrin:

Anakubali muongezeko wa pesa za kula za Wabunge, yeah alitetea Mgodi wa Dhahabu ulioko Nzega

Kigeugeu?
 
Madaatari wanatakiwa kuwa kama watumishi wa vyombo vya usalama. Sidhani ethics za taaluma ya udakatri zinawafavour kugoma. Mgon kwa mdaktari hautaiwi kuwa kuw aopton hata ya tatu kama kwa wanafunii au walimu au marubani au etc.

Otheriwise pamoja kwamba tunajua mattizo yao but migomo ya holela ya mdatari ni uthibitisho wengi waliingia fani wa kufuata mkumbo. sina uhakia lakini kwa logic niiyonayo sihani hata nchi za nje na zilizoendelelea madktari wana option ya kugma katika ku boycot
.

Kifupi madaktari waache uselfish. I think .Thye shuld know a better way ya kudeal na wanasiasa badala ya kuwakomoa wananchi.

Umenishangaza sana kwa mawazo yako haya. Unataka kusema Madaktari hawana haki ya kulipwa stahili zao eti kwa kuwa wanatakiwa kuhudumia wananchi? Unaweza kufanya kazi ukiwa na njaa? Madaktari wana familia zinazowategemea na kwa bahati mbaya wanafanya kazi kubwa sana tena kwa mazingira magumu. Tafadhali sana, usidharau taaluma ya watu.

Wanasiasa hawana la maana wanalofanya lakini hata kabla ya kuidhinishwa walijiongezea posho kufikia 200K kwa siku, we unaona ni sawa.
 
Jamani Dr. Kigwangala hakuunga mkono bajeti ya Wizara ya Afya ya mwaka 2011/12? Najua aliunga mkono. Mbona hakuongelea posho na mishahara ya Madaktari?
 
Imeandikwa na Theopista Nsanzugwanko; Tarehe: 18th January 2012 @ 14:50

MBUNGE wa Nzega, Dk. Hamisi Kigwangalla (CCM), amehamasisha madaktari wagome bila kuogopa wanapoamua kuweka vifaa chini.

Amesema ili kuhakikisha Serikali inachukua hatua mapema kuhusu malalamiko yao alitaka waweke chini vifaa kabla ya mazungumzo na Serikali.

Mbunge huyo aliwataka madaktari kutorudi nyuma bali kusonga mbele, huku akiwataka kuacha woga na kuwa majasiri katika kusimamia maslahi yao kwa umoja.

Alisema wakikosa ushirikiano katika uamuzi wao hususan wa kuweka vifaa chini kushirikisha madaktari, wauguzi na wafamasia ili kuwe na matokeo ya uwekaji vifaa hivyo.

Aliwambia kama kutakosekana ushirikiano miongoni mwao, ndio utakuwa mwisho wa mapambano yao kwani uamuzi huo umefanywa katika ngazi kubwa ya MAT, hivyo hakutakuwa na pengine pa kukimbilia, kwani chama hicho ndiyo ngazi ya juu ya uamuzi.

"
Ikiwa tutakubaliana kuweka vifaa chini, lazima kuona athari ili tusidharaulike, kwa kuwa na mikakati ya pamoja ya kushirikisha wote, kwani ikiwa uamuzi huo utafikiwa na katika huduma ziendelee hospitalini mtakuwa mmejimaliza," alisisitiza Kigwangalla.

Hapo kwenye wekundu naona kama Mh. Hamis Kigwangala anachochea mauaji. Hivi athari anazozisema Kigwangala ni zipi? Siyo watu kufa baada ya madaktari kuweka vifaa chini? Kauli zingine hizi ni za hatari, tunaweza kushtukia Ocampo yupo Dar kuchunguza kauli hizi hasa kama Madaktari wataitikia wito wa Kigwangala na matokeo yake wananchi wakapoteza maisha!

Kigwangala akawaambie Madaktari wa Hospitali zote za Nzega wagome na kuonyesha athari kwa wananchi wake wa Nzega.
 
Ieleweke kwamba ni madaktari kamili, waliohitimu mafunzo yao na kula kiapo rasmi cha udaktari.

DR. NAMALA MKOPI
RAIS – CHAMA CHA MADAKTARI TANZANIA (MAT)

Hicho kiapo cha Madaktari kinasemaje?
 
Fanyeni kama kenya
hawawezi kuwafanya
kitu chochote
 
Fanyeni kama kenya
hawawezi kuwafanya
kitu chochote

Ukikamata kichwa cha nyoka kwa mukono wako basi hakikisha humwachii mpaka pale umemtoa meno kama wewe ni mwanamazingira... Natoa hongera kwenu madaktari na kazeni uzi mpaka kieleweke
 
kwa mtazamo wangu mimi madaktari ni muhimu kuliko hao wabunge wanaoongezewa posho tena kwa haraka haraka kuliko maelezo, kwa nini tusiwafikirie hawa wataalam ambao mchango wao ni mkubwa kuliko hao walala usingizi kwenye vikao? ebu angalieni ugumu wa kazi na mazingira ya madaktari, waurumieni jamani au kwa sababu hao waheshimiwa wakiumwa wao na familia zao wanakwenda kutibiwa india?
 
Madaatari wanatakiwa kuwa kama watumishi wa vyombo vya usalama. Sidhani ethics za taaluma ya udakatri zinawafavour kugoma. Mgon kwa mdaktari hautaiwi kuwa kuw aopton hata ya tatu kama kwa wanafunii au walimu au marubani au etc.

Otheriwise pamoja kwamba tunajua mattizo yao but migomo ya holela ya mdatari ni uthibitisho wengi waliingia fani wa kufuata mkumbo. sina uhakia lakini kwa logic niiyonayo sihani hata nchi za nje na zilizoendelelea madktari wana option ya kugma katika ku boycot
.

Kifupi madaktari waache uselfish. I think .Thye shuld know a better way ya kudeal na wanasiasa badala ya kuwakomoa wananchi.

Umeandika nini penye red?
 
Here I smell magamba magamba..green flag blood..very bad odour
 
Rias, mawaziri, manaibu mawaziri, makatibu wakuu wote, makatibu wakuu wasaidizi , wakurungezi, wabunge wote, wakuu wa mikoa na wilaya na wenye nazo wote wakiuugua wao ni kwenda kutibiwa India. Kwa hiyo hawana uchungu wo wote na hudumu za afya nchini na wanajua wakiugua wana pa kukimbilia.

Kuna wakati fulani Blandinyo Nyoni alienda Uswiz kwenye hospitali fulani ya Uswiz akaanza kuisifia kwa kusema Hospitali hiyo ni nzuri sana kama hoteli ya nyota tano.

Eti hospitali zimepandishwa uboro na kuwa za rufaa! Rufaa mavi. Hali za hospitali zetu ni hovyo sana kila kitu ni siasa tu la maana hakuna. Ipigwe marufuku hakuna mwanasiasa yeyote kukimbilia nje ya nchi punde anapougua, atibiwe hapahapa nchini ndiyo atayajua machungu yanayowapata walala hoi. Shenzi type.

Sorry, hapo kwenye bould sijaelewa? nieleweshe.
 
Wanatishia serikali nyau?? Hivi hayo masaa 72 bado tu??.................Mbona nasikia kuna madaktari na maprofessor wengi tu huko bungeni na serikalini wanaoweza kujaziba hilo pengo. Mfano Prof. Maji Marefu, Dr. Nchimbi, Dr. Mathayo, Dr. Lyatonga Mrema, Dr. Brandina Nyoni, Dr. Lucy Nkya, Dr. Magufuri, Dr. Bilali...... list ni ndefu siwezi kuwataja wote!!!
Pia nasikia Babu wa Loliondo na wanajeshi wako standby kuipiga serikali tafu!!!
 
Back
Top Bottom