Madaktari kugoma nchi nzima!

Mzee wa Kaya natumaini ujumbe huu atakuwa ameshapelekewa na timu ya Salva Rweyemamu. Kazi ipo mwaka huu Poleni wa Dr. wa ukweli kwa matatizo mnayoyapata. Haki haiombwi bali inapiganiwa

Sana sana huyo "kubwa jinga" wa Ikulu aliyeamua kusaliti fani yake atakuja na press release itakayosema
kwamba mgomo wa madaktari unahamasishwa na kuratibiwa na CDM. Mark my words!
 
Komaeni madaktari, cheo ni dhamana. Siasa imekuwa kama ndio fani muhimu sana nchi hii. Saa imefika kumaliza hii hali. Eti mbunge kukaa tu anapewa 200,000. Mbaya eeeeeee.:juggle:
 
WAZIRI MPONDA, BLANDINA NYONI NA WEWE MSALITI MTASIWA...................ANGALIENI SAANA SUALA HILI MIMI BINAFSI NAAMINI HADI HAPO MLIPO MNAZO AKILI TIMAMU NA NDIYO MAANA MKAWEKWA KWENYE NYADHIFA KAMA HIZO..............KUWA KWENYE WADHIFA HUO SI KWAMBA WEWE UMEKUWA JAJI WA HAKI ZA WATU.

KILA MMOJA KWA NAFASI YAKE AFUMBE MACHO NA AUSHIRIKISHE UBONGO WAKE KUCHAMBUA HILI. KUBWA ATAKALOLIONA KWENYE TASWIRA NI KUWA KILA MGONJWA ANAYEHANGAIKA HUKO HOSPITALINI NA BAADAE KUKATA ROHO KWA KUKOSA UANGALIZI WA DAKTARI...........MKONO/MAAMUZI YAKE YAMESHIRIKI KUUA..............MUOGOPENI MUNGU.

KAMA KUNA MATATIZO NA HAO MADAKTARI HAKUNA MUAFAKA WA WATUA WAZIMA KAMA NYINYI KUKAA PAMOJA NA KUKUBALIANA JAMBO MOJA..................SWALI...Je, madai haya ya Ma daktari ni mapya??? Hayafahamiki???? Je, Madaktari hawa wameanzisha shari hii ama ni Wizara kutojipanga imechelewesha haki zao????? Na kama kila mtu kwa nafasi yake anaelewa kuwa yeye ndiye sababu ya jambo kama hili kutokea kwa nini asingetumia hata hivyo vyombo vya habari kuomba muda kurekebisha na baadae kuliweka sawa jambo kama hili.

NYUNDO YENYE NGUVU YA KUFUKUZA MADAKTARI (AMBAO KILA SIKU SERIKALI INASEMA HAWATOSHELEZI) IMETUMIKA KWA SABABU ZIPI..............BUSARA IKO WAPI???? MLIWAHI KUKAA KIKAO NA KUJIULIZA MARA MBILI KUWA UAMUZI HUO UNAWEZA KUWA NA MADARA GANI!! MLIPATA MUDA WA KUJIANDAA NA MBADALA KABLA YA KUTOA BARUA HIYO!!! ukitangaza vita ni vizuri kuwa na uhakika na silaha ulizonazo na kuzifahamu vyema silaha alizonazo adui yako......................Ndiyo maana Hayati Baba wa Taifa alipotutangazia kuwa tunaingia vitani na Uganda alisema maneno yafuatayo..........SABABAU YA KUMPIGA NDULI TUNAYO.............UWEZO WA KUMPIGA TUNAO. Hakukurupuka alikaa na wataalamu wake wa kijeshi wakamuelekeza uwezo alionao adui na mbinu watakazotumia kumtandika. hakuridhika aliwatembelea pia huko mstari wa mbele kujihakikishia yale walioyasema huku vita ikiunguruma akajiridhisha kuwa nduli ataondoka tu.

Mwisho nawaambia nyie kina Mponda, Nyoni, Mtasiwa na wengine wote wanaochezesha suala hili..................kumbukeni kuna Ndg zenu pia nao wataungana na sisi kufa kama huduma za madaktari hazitakuwepo..............Mungu ndivyo alivyo utaitwa kwenu huko ama utataarifiwa msiba wa nduguyo ambaye atakuwa amekosa huduma sahihi ya Daktari huko Ruvuma ama Bukoba kwa uzembeUjanja wenu wa kutokukubali kuwajibika.................Ni aibu kushiriki kifo cha nduguyo wa damu kwa kukosa kuwajibika mungu mwenye haki atawahukumu kwa hilo......................Nimesema ukweli wangu toka rohoni naweza kupumua sasa na kama kuna mtu anaweza kumfikishia mmojawapo wa hao ujumbe huu kwa naman anayofahamu anisaidie kufanya hivyo
 
Wizara ya afya kama zilivyo wizara zote za serikali hutegemea fungu lao toka hazina; pale hazina yetu inapokauka kwa sababu viongozi wetu matumizi yao mabaya, unategemea katibu mkuu atawalipa wafanyakazi mishahara yao toka wapi? Lawama ziende kwa viongozi wanaoweka vipaumbele vya sherehe za kisiasa na kudharau malipo stahiki ya wafanya kazi. Hatuwezi kuwalaumu makatibu wakuu kwa mapungufu haya!!
 
utasikia tu kuna mkono wa chadema...kazeni uzi hawa magamba wanakera sana....wanasinzia bungeni wanaingiza 200,000/=
 
wenzako wanachangia point wewe unachangia pumba. Ufala.
Madaktari nawaunga mkono 100%, kazeni buti, msilegeze kamba hata kidogo. Tunaweza kuanza ni wizara kwa sasa lakini ikibidi, hata Rais apigiwe kura na bunge ya kutokuwa na imani nae, kwani haya yanayofanyika anayaona na yeye kama msemaji wa mwisho huwa haoneshi concern yoyote. JK OUT!
 
Kikao cha mkutano mkuu wa dharura wa chama cha madaktari Tanzania (MAT) kilichofanyika leo siku ya jumamosi, tarehe 14/01/2012 ukumbi wa JAFFARY COMPLEX kimejadili kwa kina yafuatayo:

1.
Kwamba, chama cha madaktari Tanzania kimejadili na kuazimia kutoa masaa 72 kwa serikali kuwa “Intern doctors” wote waliohamishwa warudishwe Muhimbili mara moja wakamalizie muda wao. Na kwamba ifahamike kuwa interns huomba kwenda kufanya internship katika hospitali Fulani kutegemeana na malengo ya baadaye waliojiwekea. Na pili kuna baadhi ya vifaa vipo mf. Muhimbili na huko kwingine haviko. Madaktari wemesikitishwa sana na uamuzi huu kwa vile haieleweki ni kwa nini “intern doctors” waadhibiwe wakati walidai walipwe mishahara yao tu na serikali ilikiri kosa hilo. Wanachama wangependa kuona waliofanya uzembe huo wanawajibishwa mara moja na sio kuachwa waendelee kuwaadhibu madaktari wasio na kosa.

2. Kwamba, kwa kuwa Intern doctors wamekuwa wakifanya kazi bila malipo kwa muda mrefu na hali hiyo ikapelekea kusitisha kazi ndipo serikali ikaamua kuwalipa mishahara yao. Kufuatia kuendelea kusababisha adha kwa madaktari na wataalamu wengine wa afya na hatimaye kusababisha huduma mbovu kwa wagonjwa, Chama cha madaktari kimeona kimshauri Mh. Rais atafute ajira nyingine kwa ajili ya maafisa waandamizi wafuatao:
a. Katibu Mkuu, wizara ya Afya , Ms. Blandina Nyoni b. Mganga Mkuu wa serikali, Dr. Deo Mtasiwa
3. Kwamba waziri wa afya Dr. Hadji Mponda (MB) afute kauli yake inayoashiria kwamba “intern doctors” ni wanafunzi wa udaktari wa mwaka wa 5. Ieleweke kwamba ni madaktari kamili, waliohitimu mafunzo yao na kula kiapo rasmi cha udaktari. Na chama cha madaktari kimesikitishwa sana na upotoshwaji huuu wa mara kwa mara. Kutokana na hayo hapo juu basi chama cha madaktari Tanzania kina msamehe kwani inaonekana hajui atendalo. Ijulikane kwamba mjadala wa hivi ulishawahi kuibushwa mwaka
2005 na waziri wa afya kipindi hicho alikiri bayana kwamba intern ni daktari kamili aliyefuzu.

4. Kwamba, chama cha madaktari Tanzania kimeamua kumsimamisha uanachama wa chama hiki Dkt. Deo Mtasiwa, ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Serikali (CMO), kwa kosa la kusaliti fani ya udaktari na pia kwa kushindwa kumshauri waziri wa afya vizuri kuhusiana na mambo yanayohusu fani ya udaktari Tanzania. Mkutano huu unamsimamisha rasmi Uanachama huo kwa kipindi cha mwaka mmoja. Taratibu za kumrejesha zitajadiliwa kwenye Mkutano mkuu wa kawaida wa chama. Hii itakuwa fundisho kwa madaktari wengine wote nchini.

5. Kwamba chama cha madaktari Tanzania (MAT) kimeazimia kuitisha mkutano mwingine mkubwa wa wanachama wote siku ya jumatano tarehe
18/01/2012, kuanzia saa tatu asubuhi na kuendelea kwenye ukumbi
utakaotangazwa. Agenda za mkutano huo, pamoja na mambo mengine, zitakuwa zifuatazo:
i. Hatma ya heshima ya fani ya udaktari na mustakabali wa huduma za afya kwa watanzania
ii. Kwa nini serikali haijaanza kulipa posho ya kazi muda wa ziada (on call allowance) kama ilivyopitishwa mwaka 1990 na kufanyiwa maboresho mwaka 2008.
iii. Mshahara mpya wa daktari unaoendana na elimu, ujuzi, umuhimu, hadhi, majukumu, na hali ya uchumi wa sasa na mfumuko wa bei.
iv. Maslahi mengine ya madaktari kama nyumba, posho ya mazingira magumu, ufadhili wa masomo ya elimu ya juu na posho ya kufanya kazi kwenye mazingira hatarishi( Risk allowance).
v. Kuhamishwa hovyo hovyo kwa madaktari bingwa 61
vi. Mengineyo (kwa idhini ya mwenyekiti)
IMETOLEWA​

DR. NAMALA MKOPI
RAIS – CHAMA CHA MADAKTARI TANZANIA (MAT)
huu ubaya wa kuingiza siasa ndani ya taaluma
 
huu ubaya wa kuingiza siasa ndani ya taaluma

Na wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri ndugu kwania ulichoandika ni tofauti na maada
hebe correct me labda sijaelwa unamaanisha nini hapo.......????
 
Chama cha madaktari (MAT) kinaendelea sasa hivi na mkutano mkubwa sana Dar es Salaam na mpaka sasa maazimio yaliofikiwa Mojawapo ni 'TOOLS DOWN' kuanzia kesho! Kaeni chonjo..habari zinaendelea kuja!:canada:
 
Nawaunga mkono, nimefuatilia speech ya Dr Nkyaa nae hakuna cha maana alichoongea zaidi ya kubit around da bush na kuwakebehi maDr. wawaboreshee maslahi yao bana wasilete longolongo
 
Chama cha madaktari (MAT) kinaendelea sasa hivi na mkutano mkubwa sana Dar es Salaam na mpaka sasa maazimio yaliofikiwa Mojawapo ni 'TOOLS DOWN' kuanzia kesho! Kaeni chonjo..habari zinaendelea kuja!:canada:




mmenyanyaswa sana,mmeonewa sana,mmetukanwa sana nadhani kuna kitu mnatakiwa kugrand si kingine ni kugoma tu
 
things falling apart ,blandina and co must go!

Nina imani kuwa mgomo huu ntatokea kweli,kwani upeo na mwamko wa madaktari si sawa na wakina Mkoba wa CWT, sipati taswira kama jukwaa la katiba nao wakiamua kungnga na wa kwao.j( nchi inamshinda vibaya,much beter akajiuzulu tu!
 
Chama cha madaktari (MAT) kinaendelea sasa hivi na mkutano mkubwa sana Dar es Salaam na mpaka sasa maazimio yaliofikiwa Mojawapo ni 'TOOLS DOWN' kuanzia kesho! Kaeni chonjo..habari zinaendelea kuja!:canada:

Hakika amewakosea madaktari. Inabidi Awaombe radhi.

Kusema madaktari wawe na uzalendo wakati hata yeye Mwenyewe Hana Chembe ya uzalendo ni matusi.
 
Back
Top Bottom