NdasheneMbandu
JF-Expert Member
- Jan 2, 2012
- 940
- 308
Muziki umeanza. Ni wakati wenu madaktari kugangamala. Vinginevyo, mtaendelea kudharauliwa siku zote. Ushauri wangu ni kwamba msilegeze kamba.
Hii kali Waziri wa Afya hajui kama Interns Doctor kama ni daktari kamili ama bado mwanachuo!! Ametolewa wapi huyu? Vigezo gani vilitumika kupewa uwaziri ktk wizara muhimu kama hii?
Subiri kidogo, Katibu Mkuu na Mganga Mkuu ni wateule wa Rais na MAT haiwezi kuwakataa, kwani Rais anapowateua watu hakuna debate so wao kumkataa haina Tija. Kwa mujibu wa sheria Madaktari hawaruhusiwi kugoma. Ushauri wangu wa Kijinga wanaweza kuunda kamati ndogo ikaenda kunywa chai pale Magogoni na kupiga picha Kama walichofanya watu Fulani baada ya kuzira mjadala wa mswada wa Katiba ya CCM. Sijatambua Kama ni kwa kiasi gani wamefanikiwa au waanze mikutano yao isiyoisha. But because Watz wengi mishahara ni midogo mno na hawana akiba then sitarajii kuona mgomo endelevu wenye tija katika uhai wangu! Do you know why 80% wanategemea kuapata hizo tips za kukimbiza mafaili ya watu tu. Hata vyama vya wafanyakazi havitengi strike
funds za kuwalipa wanachama wao wakifanya mgomo Halali! Mdaktari na Polisi ngoma draw kugoma ni marufuku sijui watatumia sllaha gani huishia kumwomba kila mtu kitu kidogo!:A S 465:
Mzee wa Kaya natumaini ujumbe huu atakuwa ameshapelekewa na timu ya Salva Rweyemamu. Kazi ipo mwaka huu Poleni wa Dr. wa ukweli kwa matatizo mnayoyapata. Haki haiombwi bali inapiganiwa
mhh serikali imeingia katika vita ambayo siku zote tunajua mshindi ni nani..? :biggrin:
Kwa kweli mimi sifahamu tunakoelekea kama Taifa, hii migogoro kati ya madaktari na serikali kila mwaka imekuwa na athari kubwa sana kwa watanzania na hasa wa vipato vya chini, na ndio maana leo hii madaktari wamekuwa hawawajibiki tena wanapokuwa kwenye vituo vyao vya kazi wanababaisha then wanakuelekeza kwenda kwenye hospitali zao binafsi ambazo ni ghali sana, Serikali angalieni hii mambo bhana wananchi tunaumia.:shock:
Hii serikali yetu ni pambaf kabisa mwaka huu wametenga Shilingi bilioni 13 kwa ajili ya kutibia watu wenye matatizo ya moyo nje ya nchi na kila mwaka mambo ni haya haya
kwa nini wasiboreshe huduma hapa nchini hawa watu wakatibiwa nchini na hizi pesa zikasaidia watu wengi zaidi mimi naamini kuna watu wanabenefit na huu mfumo wao waliouandaaa.Kwa nini Dr Masau wa THI(Tanzania Heart institute ) amejaribu kusaidia katika hii sector lakini picha ninayoipata serikali inamsabbotage hata kama hana vifaa vya kutosha kwa nini tusijazie pale aliposhindwa
Kwa ujumla mtazamo wangu wanasiasa/serikali hawana machungu na ubovu wa wa hii sekta ya afya kwani wao wanajua wakiugua watatibiwa wapi ndio maana wanaiacha hii huduma iendelee kudorora wala hakuna juhudi za dhati kujaribu kuboresha
Sasa hivi nchi nyingi zinapiga hatua sana katika huduma za jamii kwa ujumla mfano
Rwanda kwa sasa huduma ya afya imepiga hatua kubwa sana na mambo iiyofafanya ni kuhakikisha budgetary allocation ya funds to health sector inatosheleza kununua vifaa,madawa na pia kulipa wafanyakazi vizuri Madaktari hawa tunaowabeza hapa wapo huko wanachapa kazi vizuri sana tu,kama vile pia Lesotho, Namibia, Botswana ambako pia hawa wataalamu wa afya nurses na Madaktari wanafanya kazi nzuri kwenye nchi hizi za wenzetu.
Na kwa sasa nasikia Zambia wanapiga hatua eti daktari wa kawaida analipwa take home si chini ya tanzania shilingi milioni 3.6 tanzania wanalipwa sijui laki ngapi lakini am sure haifiki milioni
Sasa sijui hivi vvinchi vingine ni nchi tajiri au zina nini cha ajabu.
Napata shida kidogo hapa naomba ufafanuzi kwa hili,huyu mganga mkuu wa serikali kama amefutiwa uanachama na MAT ina maana kwamba sasa hivi hatambuliki kama daktari na kama ni hivyo basi hana mamlaka ya kutekeleza majukumu ya kidaktari ktk kipindi hicho alichofungiwa sasa hiyo nafasi yake ya CMO anaachia ngazi ama inakuwaje?