Madaktari: Hakuna anayerudi kazini kesho!

Naungana na wewe mkuu.

naungana na wewe mkubwa,MADAKTARI ENDELEENI NA MGOMO WENU MWANZO MWISHO HAKUNA KULEGEZA KAMBA,MBONA WABUNGE WALIPODAI POSHO ZIONGEZWE MBONA WALIONGEZEWA HARAKA BILA KINYONGO CHOCHOTE.
 
naunga mkono mgomo wenu..chonde chonde msiache kuwapa huduma mama wajawazito,watoto na wagonjwa walio ktk critical condition

all the best
Tatizo ni kwamba wengine tumeshapoteza marafiki zetu mbali na hayo Napinga kwa nguvu zote Posho za vikao iwe kwa wabunge, watumishi wa Umma au madaktari. Siwezi kubalisisha msimamo wangu kwa sababu wabunge wanapewa na nitaendela kuupinga hata kama Chadema wote watabadilika na kuunga mkono posho za vikao. Ujinga huu sintouunga mkono hata kidogo. Kubadilisha msimamo kwa wananchi kunaonyesha wazi tulivyo wanafiki hata ktk maswala muhimu tunayoyapinga toka serikali hii.
 
serikali imetuma watu 3 wamekwenda hoteli ya starlight mahali amabpo madaktari wamekodi ukumbi na kuzuia kuwa kesho hakuna madaktari kukutana hapo na ukumbi kwa sasa uko chini ya serikali.......ukumbi ulikuwa umeshalipiwa.....
 
tumepata taarifa kuna madaktari wafuasi na mashabiki wa ccm wao wanarudi kazini kesho kwa makubaliano ya siri na serikali''ni taarifa tu wakuu
 
serikali imetuma watu 3 wamekwenda hoteli ya starlight mahali amabpo madaktari wamekodi ukumbi na kuzuia kuwa kesho hakuna madaktari kukutana hapo na ukumbi kwa sasa uko chini ya serikali.......ukumbi ulikuwa umeshalipiwa.....

Huu ndio utoto! Bora lipi? kwa kufanya hivyo si ndio wanawapoteza kabisa? wakiwa huku uraini utaongea nao vipi?
 
Jamani naomba niulize,eti ni kweli madaktari wanataka mshahara wao uwe uanaanzia mil 3.5 kwa mtu wa degree??
 
FFU wamefika hapo starlight hotel na watalinda ukumbi huo usiku kucha..ni taarifa nazipata live toka jikon
 
Hapa ndiyo penyewe sasa. Mbona wabunge walipodai ongezeko la posho ya kukaa hapakutolewa amri? Zaidi tulipewa habari za kukubaliwa madai yao kwa kile kilicho elezwa gharama za maisha zimepanda mjini Dodoma.

MaDr. komaeni na msilegeze kamba. Haki haipigiwi magoti.

BRAVO kwa msimamo.

Nawasilisha.

Pinda alikoroga posho za wabunge


na Janet Josiah na Ratifa Baranyikwa
Tanzania Daima



WANANCHI, wanasiasa na wanaharakati wamemjia juu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusu kauli yake ya kuhalalisha nyongeza ya posho za wabunge.

Wakizungumza na Tanzania Daima, jana jijini Dar es Salaam walisema kiongozi huyo ameonyesha namna viongozi walivyoweka mbele maslahi binafsi hasa linapofika suala la fedha.
Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari juzi, Pinda alitetea posho za wabunge akisema kiasi wanachokipata ni kidogo na wengi wao mwisho wa mwezi hawabaki na kitu, kwani fedha zote za mishahara hukatwa kulipia madeni waliyoingia kwa ajili ya kusaidia majimbo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema Pinda atakuwa Waziri Mkuu wa kwanza kuwapotosha Watanzania kuhusu posho.
Alisema posho wanayopewa wabunge ni kwa ajili ya matumizi yao na si kwa ajili ya kuwasaidia wananchi.

“Nimekuwa mbunge kwa miaka 15 sijawahi kutoa fedha mfukoni mwangu kwa ajili ya kumhudumia Mtanzania mmojammoja kama nitatoa ni kwa hiyari yangu.
“Si kweli kwamba mbunge anaishiwa fedha zake zote kwa ajili ya kumhudumia Mtanzania, kwani Watanzania wanao mfuko wao wa maendeleo ambao wabunge hukaa na wananchi kujadili fedha hizo zitumikaje,” alisema Dk. Slaa.

Kwa mujibu wa Slaa, Pinda alipaswa kuzungumza juu ya ugumu wa maisha ya Watanzania yalivyo sasa na namna ya kuwasaidia na si kuzungumzia wabunge peke yao kwa kuwa wao hawana shinda kama ilivyo kwa Mtanzania wa kawaida.

Akitolea mfano, alisema Pinda alipaswa kuangalia makundi yanayolalamika kuhusu malipo yao kama ilivyo kwa madaktari hivi sasa, kuliko kuchukua jukumu la kuwapotosha Watanzania.

“Kila siku ninasema serikali ya CCM imeshindwa kutafuta njia sahihi ya kupunguza ugumu wa maisha kwa Watanzania badala yake inatumia ujanja ujanja kuonyesha kwamba inashughulikia matatizo yao wakati si kweli,” alisema.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Mbarara Maharagande, alisema suala la nyongeza za posho za wabunge si la kuzungumza kwa wakati huu ambapo maisha ya Watanzania yamegubikwa na mfumko wa kutisha wa bei na kupanda kwa gharama za maisha.

Alisema CUF wanahitaji mfumo wa kisiasa ambao utazaa mfumo mzuri wa kiuchumi utakaowatoa Watanzania kwenye maisha magumu.
Alisema posho ya sh 200,000 kwa siku inayotolewa kwa wabunge 328 ni sawa na sh mil. 65.6 ambazo serikali hutoa kwa siku.
Maharagande alisema fedha hizo ni nyingi na kama zingetumika ipasavyo zingeweza kufanya jambo kubwa la maendeleo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijinsia (TGNP) Usu Marya alishangaa serikali na wabunge kushindwa kutambua wajibu wao.

“Sisi kama wanaharakati tunaona kuna tatizo la msingi la dhana nzima ya uwajibikaji, serikali inashindwa kutambua majukumu yake na Bunge pia,” alisema.

Alisema mbunge hapaswi kutoa fedha zake mfukoni kwa ajili ya kusaidia jimbo inayopaswa kufanya hivyo ni serikali na wabunge kazi yao ni kusimamia wajibu huo wa serikali.

“Si kazi ya wabunge kutoa fedha mfukoni kusaidia watu, serikali inapewa dhamana ya kusaidia watu kwa kutoa huduma kwa wananchi kutokana na kodi inazozikusanya…sisi wanaharakati tunaipinga; inakwenda kinyume kabisa, inakuwa kama wabunge wanaihonga serikali.

Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe aliyebobea katika masuala ya uchumi, Prosper Ngowi, amesema Pinda anatakiwa kuelewa kuwa maisha magumu si kwa wabunge peke yake bali ni kwa Watanzania wote.

Alisema alichotakiwa kuzungumza Pinda katika hotuba yake ni kueleza namna serikali itakavyoweza kuwapunguzia ugumu wa maisha Watanzania.
Aliongeza maisha yaliyopanda si katika mkoa wa Dodoma kama wanavyodai wabunge bali ni nchi nzima na hasa watu wenye vipato vya chini.
Mkazi wa mkoa wa Kagera, Yohana Kazimoto, ambaye alipiga simu chumba cha habari cha Tanzania Daima, alisema viongozi wengi wamesahau kutetea maslahi ya wananchi badala yake wanaangalia yanayowahusu.
Naye mkazi wa Yombo Vituka jijini Dar es salaam, Ester Barimi, alisema kama viongozi wa serikali wameamua kujilimbikizia posho, wafanye hivyo pia katika sekta nyingine zikiwemo za afya, elimu na kilimo




 
Madaktari na serikali wote ni vimeo. I hate them.

Nimeonja chungu ya jeuri yao unafikiri Mkuchika, Pinda, Kikwete n.k wanatibiwa humu nchini. Wanaoumia ni tabaka la chini kabisa ambalo pengine hakuna hata wa kuwasemea humu zaidi yangu mimi na wewe ambaye umeipenda comment hii.

Wengi tunaoingia JF tunao uwezo wa kwenda HINDU MANDAL, AGHAKAN, REGENCY n.k Lakini hao ambao wataumia kwa migomo ya madaktari hata uhakika wa milo miwili kwa siku hawana.

Hivi unafikiri kama kuna mtu ndugu yake atakufa; kwa hiyo migomo atawachukuliaje hao madaktari?

Ndiyo hapo walalahoi wengi ambao wanahongwa kanga na ubwabwa na hao wanasiasa wajue thamani ya kura zao.Ili itakapofika muda wanasiasa wanadai kupitishwa wawaulizi wamepata kuchukua hatua gani katika kutetea masilahi yao.
Ni muda mzuri kabisa kwa madaktari kugoma nawashauri sasa muda wa kukutana na Pinda umepita.Kuna taasisi tatu tu ndiyo iliyobaki kukutana navyo ilikuweza kujadiliana(Makamu wa Raisi ,Rais mwenyewe au kamati ya Bunge ya masuala ya jamii ili kikao cha Bunge kijacho PM afuliwe U-PM wake immediately at the first seating of the Parliament maana waheshimiwa Wabunge sisi walalahoi tumewapa Rungu la kuwaadabishwa Viongozi wenye Jeuri kama ya Pinda na wengineo
 
Hiyo kesho ndo tutajua nani ni mkali wa kusimamia misimamo yake, Political Government au Professional Doctors.
 
Cousin unajua serikali at times inapenda sana kudharau carrier za wengine wanaona kuwa kufukuza ndio suluhisho, sielewi wanaposema kuwa hawana hela miaka karibia mitano mfululizo Kikwete ametumia mamia ya hela za walipa kodi kwenda WEF (World Economic Forum) na hatujaona faida yoyote zaidi ya kufuja hela na misafara ambayo hizo hela zingefanyia mambo mengine

Labda tujiulize pia mantiki ya wao kutumia mabilioni mengi ya shilingi kufanya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru huku kukiwa hakuna lolote la maana la kujivunia!!. Nchi gizani, mfumuko mkubwa wa bei kwa mishahara kiduchu, hata msongamano wa magari umetushinda achilia mbali uchafu uliojaa kila mahali. viongozi kila kukicha wanavaa wanaenda ofisini!!, wanafanya nini?. Then tunategemea maendeleo, ndoto!, si kwa aina hii ya viongozi tulionao, wanaoona siasa ndiyo kitu muhimu kuliko vyote, jamani wote hatuwezi kuwa wanasiasa!!. maisha magumu ni kwa kila mtu!!. mkishapiga vimyaka vyenu vitatu (3) virahisi mnaita social nini sijui!!, mnataka kuendesha watu waliopiga five concrete years!. Shame on you vilaza!!.
 
Jamani naomba niulize,eti ni kweli madaktari wanataka mshahara wao uwe uanaanzia mil 3.5 kwa mtu wa degree??

Wee unaona hizo ni Nyingi? unajua inamgarimu huyo Dr miaka mingapi kupata hiyo taaluma? Au unadhani kutibu Mtu ni sawa na kutengeneza Gari?

Mimi ,tu wa IT Navuta zaidi ya 2M na naona bado haitoshi.
 
When the cock stands on the big rock and begins to cock then the darkness disseapears and the sun rises its tantacles to welcome the better hopes,hopes for everyone...madocs naona mko kwenye ncha ya ushindi na umoja wenu ndo ushindi wenu na jukumu lenu kwa sasa ni kupingana na aina yoyote ya lobbying till the sun brings hopes for you

This is your time,do it now!

Well said,the next professor,teach ur students to behave so
 
Mkuu kama nimewaelewa vizuri hawa madaktari ni kwamba tatizo ni mtindo/efficiency ya mawasilano toka serikalini. Taarifa toka kwa Waziri mkuu zikiwataka madaktari wakutane naye (PM) Jumapili (leo) ziliwafikia jana Jumamasi saa 10 jioni! Na waliochosema viongozi ni kwamba kwa muda huo ingekuwa vigumu kuwapata madaktari hao. Pia wakasema wakati huo hata hata mkutano wa viongozi wa madaktari ulikuwa umeshaisha na watu wameshaingia uraini.

Nadhani Wizara ya Afya ndio yenye tatizo hapa. Kwanza kwa kuvurunda na kutoa kauli za kejeli, kauli ambazo ndizo ziliwapandisha maruhani hawa madaktari, na pili kutomshauri vizuri Waziri mkuu namna ya kutatua huu mtafaruku. Kama wangetumia busara kwa kuunda timu ndogo ili kuratibu mawasiliano kati ya serikali na madaktari na hakika barua ya mualiko wa kukutana na waziri mkuu ingefika kwa wakati. Hawajafanya hivyo na sasa mambo yanazidi kuharibika. Kumbuka hii sumu iko karibu nchi nzima kwa sasa. Hospitali nyingene hawasemi lakini huduma zimezorota kabisa. Nadhani wanaita mgomo baridi.
Mkuu nisikilize vizuri, mwajiri wako anapokuita hata ukiwa kitandani unaamka na kwenda kumwona. Heshima kwanza kwa mwajiri wako hakuna habari za kufanya mgomo halafu unaweka masharti wewe kama umeichukua nchi hostage.

Nimekuwa nafuatilia sana mijadala hapa JF na nimeona waziri mkuu akitoa taarifa hizi mapema tu kiasi kwamba hata majibu yao yalikuja mapema wakitaka kukutana Jumatatu na sio Jumapili mara ukumbi gani.. Juzi Ijumaa wakati wanakutana na kina Nkya, tulipata taarifa hawataki kuzungumza na hawa viongozi, jambo ambalo sikuelewa kwa nini halafu wakamtaka waziri mkuu na mapema tulitaarifiwa waziri mkuu atakutana nao, ubishi ukawa wakutane ukumbi gani. Mvutano mkubwa ukawa kuhusu ukumbi gani wakutane na tumeyasoma hapa JF.. Kwa hiyo unachoongea hapa kusema kweli sielewi kama taarifa zinazowekwa hapa ni za uongo au maana hiyo Ijamaa yenyewe walikuwa wakibishana juu ya ukumbi na usalama wa Waziri mkuu leo iwe hawakujua mapema!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Wee unaona hizo ni Nyingi? unajua inamgarimu huyo Dr miaka mingapi kupata hiyo taaluma? Au unadhani kutibu Mtu ni sawa na kutengeneza Gari?

Mimi ,tu wa IT Navuta zaidi ya 2M na naona bado haitoshi.


Haujanijibu swali langu mkuu!!Kama unalipwa zaidi ya mil 2 huku umesoma IT basi nina uhakika wa 100% hufanyikazi serikalini na pia sidhani kama kwenye swali langu niliuliza unalipwaje mkuu!
 
hahaha. karibuni unguja kutibiwa. huku madaktari sio anasa, ni huruma na upendo
 
Huyu Dr Ulimboka mwakingwe kweli noma angekuwa Mgaya wa TUCTA au yule jamaa yenu Kibamba angesema wamepostpone mgomo mpaka watakapo tangaza tena

viva Mwakingwe viva the Late Rwegasira RIP
 
Huyu PM angekuwa na busara angekubali ombi la madaktari kukutana nao kesho, uwaziri mkuu wake usingepungua na labda angejijengea heshima kwenye jamii. Kesho aibu itamshika pale madaktari watakapoendelea na mikutano yao.

...Madakatari wana hiari ya kwenda au kutokwenda kazini, lakini ni wazi kuwa hawataweza kuwa na mikutano kesho, watake wasitake...
 
Mh Pinda huwa ananifurahisha sana

PINDA.2.jpg


12_10_6scme1.jpg


Huyu Mkuu waziri anapenda sana maigizo

IMG_9046.jpg

Heheheheheh....mtoto wa mkulima huyo. Bongo bwana yaani ni usanii kwenda mbele jamaniii...hahahah...nimecheka sana hizo picha. Yani wanatuona sijui wote tuko STD II na hadithi za Manenge na Mandawa.
 
Back
Top Bottom