Ndugu Mgaya, Madaktari wanaonyesha njia. Kati ya kada inayodhalilishwa ni pamoja na hii ya ualimu. Utadhani viongozi wa serikali yetu hawakupitia kwa Mwalimu. JK akiongea na vizee vya magamba (ccm) ambavyo vilisombwa na mafuso na kupewa fedha kidogo za ugoro aliwashambulia walimu waliotishia kugoma na kweli mkafyata mkia.
Jana mtoto wa mkulima aliye-Pinda alimshambulia Dr. Ulimboka na kuwaamuru Madaktari kurudi kazini bila kushughulikia matatizo yao.
Sasa Mgaya, wewe una kundi kubwa kuliko makundi mengine ya watumishi wa umma. Waamshe walimu wako nao waendelee kudai haki zao. Si umeona waheshimiwa wa mjengoni walivyodai kuwa Dodoma hakukaliki sharti waongezewe posho kutoka 70,000/- (ambayo hata hivyo hawaistahili) hadi 200,000/= kwa ajili ya kusingizia kwenye viti vinavyozunguka kubembeleza usingizi wao. Wamepewa bila shida. Si unajua tena ndugu aliye-Pinda naye aliongezewa kitita hicho hicho na hata akachukua fedha haramu iliyokusanywa na Katibu Mkuu wa Nishati na Madini ya kulainisha upitishaji wa bajeti. Waunge mkono madaktari, kweli huu ni mwanzo wa ukombozi..