Madaktari chonde chonde

Madaktari wana haki ya kudai madai yao......lakini kugoma tena,watu wa chini watakuwa wanaumia sana,nafkiri watafute njia nyingine mbadala ya kudai madai yao..

Panga la shaba, huo ndio ukweli na wanatakiwa kuwa na utu na kutambua kuwa wanaoumia katika migomo yao ni wananchi wa kawaida mama na baba zao wakiwemo.
 
Nilitegemea kuona michango ya watu kuitaka serikali na madaktari wafikie mwafaka lakini cha ajabu michango ya watu wengi hapa wanataka madaktari wagome....sidhani kama nyie kweli mna uchungu na madai ya madaktari kuliko ndugu zenu watakaokufa mahospitalini kama ilivyokuwa katika mgomo wa awali.

Mkuu nchi hii haiendi bila migomo, na ukweli wa hii maneno iko wazi kuanzia vyuoni hadi serikalini. Kimsingi migomo ndiyo suluhu pekee kwa watawala wa nchi hii
 
Mkuu nchi hii haiendi bila migomo, na ukweli wa hii maneno iko wazi kuanzia vyuoni hadi serikalini. Kimsingi migomo ndiyo suluhu pekee kwa watawala wa nchi hii

Hebu jiulize kama kila idara ya serikali watumishi wote wakigoma itakuwaje? unataka kuniambia watumishi wengine siyo muhimu na hana madai isipokuwa madaktari tu? Wasitumie kigezo cha kwamba wakigoma lazima watakufa na hivyo wao kubembelezwa .... wanatuumiza watanzania wenzao bhana!
 
Wewe unayeshangilia watu wafe ndiyo unajiona una akili?

Try to think broadly and with depth - hivi watu wameanza kufa hospitalini baada ya madaktari kugoma? Wale ambao miaka yote wamekuwa wakikosa basic services na kuishia kufa ni kwa sababu ya mgomo wa madaktari? Mojawapo ya madai yao ni kuboreshwa kwa huduma za wagonjwa na mazingira ya tiba, kudai mambo haya nako ni upuuzi?
 
Madaktari wana haki ya kudai madai yao......lakini kugoma tena,watu wa chini watakuwa wanaumia sana,nafkiri watafute njia nyingine mbadala ya kudai madai yao..
sioni njia mbadala zaidi ya mgomo. Ukiona rais anasamehe wezi wa EPA, Richmond/dowans haijui tena anaongea bila aibu, hakika selikali yenye viongozi type hiyo bila migomo hawaendi mkuu!, can you imagine time lapse tangu mgomo usitishwe wameachieve nini? Nafasi ambayo selikali makini ingeitumia effectively kutatua mgogoro huo!
 
Rais amesamehe wezi kwani yeye judge? Au mnataka awe anaingilia uhuru wa mahakama?
 
Hebu jiulize kama kila idara ya serikali watumishi wote wakigoma itakuwaje? unataka kuniambia watumishi wengine siyo muhimu na hana madai isipokuwa madaktari tu? Wasitumie kigezo cha kwamba wakigoma lazima watakufa na hivyo wao kubembelezwa .... wanatuumiza watanzania wenzao bhana!

Hao watumishi wengine kama wamekubali kupoteza haki zao kwa kuogopa na kukaa kimya ni shauri yao; kila mtu anatakiwa kujipigania pale alipo, ukikaa kimya usimlaumu mtu.
 
Hawa madaktari wanaogoma ingekuwa kipindi cha nyerere mnachukua majina halafu utekelezaji unafuata...
 
Nimesikia kwa vyombo vya habari kuwa next wiki madokta huenda wakagoma ati kwa kuwa bado wizara inaongozwa na mawaziri wale wale waliosababisha mgomo wa awali kitu ambacho serikali kupitia kwa PM ilikuwa imeahidi itakishughulikia.
Kuna tetesi nimezipata kuwa Dr Mponda aliandika barua ya kujiuzuru kwa raisi naye JK akamwambia kuwa " wewe bado u mchanga kwenye siasa, huo ni upepo tu utakwisha, chapa kazi achana na mambo ya kujiuzuru".
Kwa maono yangu madokta mkigoma mtakuwa mnawaumiza raia wasio na hatia kwasababu serikali hii chini ya JK haitakaa iwasikilize kwa maana ya kutatua mgogoro huo. Napendekeza mgomo na maandamano yenu yaelekezwe katika kuupinga utawala mzima wa JK na wateule wake vinginevyo mnajilisha upepo, JK will never respond to your cry!!
Nawasilisha

Una uhakika kuwa JK aliandika haya?. Kama ni kweli basi anacheza politics na maisha ya watu. Ninavyojua mimi JK hawezi kumtoa pale kwa sasa itaonekana kuwa ni shinikizo na hivyo kuacha precendent mbaya kama wanavyoamini. Mimi ninaamini kabisa kuwa kama mawaziri wangekuwa huru na kuachwa wafanye kazi zao bila kuingiliwa na JK basi mgogoro ule wa madaktari usingefika pale ulipofikia.

Nina hakika kabisa 100% kuwa report ya kudanganya dhidi ya madaktari aliyosoma Mponda bungeni haiukuwa ya kwake, aliletewa na Ikulu aisome, ndiyo maana JK hawezi kumwachisha kazi kwani anajua kuwa ni yeye ndiyo aliyempatia KASA (sumu) kama ambavyo alivyompatia Pinda KASA ya kuwatisha kuwafukuza kama hawatarudi kazini kabla ya kipigishwa about turn na kupewa desa jipya.

Kuwa waziri katika serikali ya si dili sana maana unakuwa unafanya kazi kimsukulemsukule. Unakuwa huna final say kwani ukiweka wazi mawazo yako unakuja pingwa hadharani na kuwa mdogo kama piriton, kumbuka Maghufuli?, kumbuka Mwandosya? et al. Mawaziri wanachokifanya hizi sasa ni kusubiri mishahara minono tu na maagizo toka IKULU. They have been denied authority to work independently.
 
Mau. Sikulaumu msimamo wako. Everyone has the right to his own opinion.

Lau ungefahamu kiini cha tatizi labda ungeside na madocta. Maskini hujijui kuwa unacho stahili kwenye tiba ni zaidi ya unacho kipata sasa.

Madai ya madaktari yanahusu msaada na haki kwa wagojwa ambazo hivi sasa hawazipati. Wa kwanza kulalamika punde CT scan ikikosekan ni wananchi. Watadai hati mtambo umenunuliwa hata mwaka bado umeharibika !!!!!!! Kumbe mtambo umeletwa 2nd hand kwa bei ya mpya. Madawa yakikosekana, wananchi wanadai madokta wanaiba.

Daktari naye ni mwanadamu. Ana mahitaji kama mfanya kazi mwingine yeyote. Madocta hawataki kuoba rushwa kwa wagonjwa. Lakini kama mshahara ni mdogo. Anamtoto anahitaji karo na malezi unafikiri atatoa wapi pesa?

Daktari wanomba wapatiwe nyenzo za tiba za kisasa ambazo hazija pitwa na wakati. Wanadai madawa yaliokuwa katika viwango na sio belw standard. Wanadai mshahara mzuri na allowance za haki ili asiwe na haja ya kwenda kufanya kwenye private hosp anapotoka kazini kwake. Mbona mie naona vyote hivi ni kwasaidia wagonjwa pia? TAFAKARI.
 
Hebu jiulize kama kila idara ya serikali watumishi wote wakigoma itakuwaje? unataka kuniambia watumishi wengine siyo muhimu na hana madai isipokuwa madaktari tu? Wasitumie kigezo cha kwamba wakigoma lazima watakufa na hivyo wao kubembelezwa .... wanatuumiza watanzania wenzao bhana!
Ishinikize selikali iwafukuze kazi basi!. "mimi mgonjwa mtarajiwa, nabariki mgomo wa ma dr.,"
 
sioni njia mbadala zaidi ya mgomo. Ukiona rais anasamehe wezi wa EPA, Richmond/dowans haijui tena anaongea bila aibu, hakika selikali yenye viongozi type hiyo bila migomo hawaendi mkuu!, can you imagine time lapse tangu mgomo usitishwe wameachieve nini? Nafasi ambayo selikali makini ingeitumia effectively kutatua mgogoro huo!
Tatizo la Tanzania ni kwamba, kupata uongozi ndio mafanikio makubwa ya mtu kufurahia. na si kujivunia umefanya nini kwenye nafasi hiyo uliyofikia. ndio maana viongozi wengi wame relax kwenye vyeo walivyonavyo. hii ndio sababu unaona hakuna hata tatizo moja hapa tanzania limetatuliwa na kuisha kabisa.
 
Nimesikia kwa vyombo vya habari kuwa next wiki madokta huenda wakagoma ati kwa kuwa bado wizara inaongozwa na mawaziri wale wale waliosababisha mgomo wa awali kitu ambacho serikali kupitia kwa PM ilikuwa imeahidi itakishughulikia.
Kuna tetesi nimezipata kuwa Dr Mponda aliandika barua ya kujiuzuru kwa raisi naye JK akamwambia kuwa " wewe bado u mchanga kwenye siasa, huo ni upepo tu utakwisha, chapa kazi achana na mambo ya kujiuzuru".
Kwa maono yangu madokta mkigoma mtakuwa mnawaumiza raia wasio na hatia kwasababu serikali hii chini ya JK haitakaa iwasikilize kwa maana ya kutatua mgogoro huo. Napendekeza mgomo na maandamano yenu yaelekezwe katika kuupinga utawala mzima wa JK na wateule wake vinginevyo mnajilisha upepo, JK will never respond to your cry!!
Nawasilisha

Nawaunga Mkono Madaktari kwa move zote wanazozifanya. Ila kwa hili la kuipa tena Serikali siku tatu ten, nadhani kidogo mmeteleza, kulikuwa hakuna haja, mngetangaza mgomo huo kuanza kesho hadi hapo hao wahusika watoke Wizarani, then, mngerudi kazini na kuendelea na mazungumzo na Serikali. Mmesha ingia vitani, kumpa adui mwanya wa siku moja tu anaweza kukushangaza.
 
jamani wote tulisikia ahadi za pinda tarehe tisa feb.mpaka leo hakuna cha maana kilichotekelezwa,kuna mambo yanahitaji muda mfupi,wa kati na muda mrefu.sasa tujiulize tunahitaji muda au fedha kiasi gani za kuwawajibisha hawa wanasiasa?kama watendaji wakuu wa wizara wamewajibishwa sasa kuna ugumu gani kwa hawa wawili?
 
Try to think broadly and with depth - hivi watu wameanza kufa hospitalini baada ya madaktari kugoma? Wale ambao miaka yote wamekuwa wakikosa basic services na kuishia kufa ni kwa sababu ya mgomo wa madaktari? Mojawapo ya madai yao ni kuboreshwa kwa huduma za wagonjwa na mazingira ya tiba, kudai mambo haya nako ni upuuzi?

Sisemi kwamba hayo yasifanyike, hapana...hoja yangu hapa ni jinsi wanavyoyadai hayo...sasa kama huduma duni zilizopo bado watu wanakufa...je na madaktari nao wakigoma inakuwaje? Waachane na migomo, mazungumzo yalishaanza ni kwa nini wasiwe na moyo wa subra...then nyie mnashabikia wagome ili hali iendelee kuwa mbaya zaidi mahospitalini. Our fello Tanzanian will suffer missalably and evencually they will die.
 
Nilitegemea kuona michango ya watu kuitaka serikali na madaktari wafikie mwafaka lakini cha ajabu michango ya watu wengi hapa wanataka madaktari wagome....sidhani kama nyie kweli mna uchungu na madai ya madaktari kuliko ndugu zenu watakaokufa mahospitalini kama ilivyokuwa katika mgomo wa awali.

Sasa kama serikali iliyokaa nao inaanza mambo ya kitoto tuwashauri nini madaktari?

Watafikiaje muafaka wakati ule wa kwanza waliofikia wakati wa kuahirisha mgomo umetelekezwa?

Kama serikali imeshindwa kutekeleza makubaliano yao ya awali basi madaktari hawana jinsi...

Babu DC!!
 
Sasa ukikuta ajenda hazieleweki ndio utoe lame excuses? Hapo madaktari wamechemsha na wamejidhalilisha. Na wakigoma this time wajue wananchi hawatalaumu serikali.

usijadili kitu ambacho hujakifanyia utafiti na kujua ukweli wake. Wale walioitwa kwenye kamati ya pinda walikuwa ni tana ambao mwakilishi ni kanali wa jeshi,watu wamaabara,mwakilishi wao alikuwa mtumishi wizarani. Toka lini kanali wa jeshi akatetea wananchi? Badala ya kuzungumzia maboresho ya wizara wakaishia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom