Madaktari chonde chonde | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari chonde chonde

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by oba, Mar 3, 2012.

 1. oba

  oba JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nimesikia kwa vyombo vya habari kuwa next wiki madokta huenda wakagoma ati kwa kuwa bado wizara inaongozwa na mawaziri wale wale waliosababisha mgomo wa awali kitu ambacho serikali kupitia kwa PM ilikuwa imeahidi itakishughulikia.

  Kuna tetesi nimezipata kuwa Dr Mponda aliandika barua ya kujiuzuru kwa raisi naye JK akamwambia kuwa " wewe bado u mchanga kwenye siasa, huo ni upepo tu utakwisha, chapa kazi achana na mambo ya kujiuzuru".

  Kwa maono yangu madokta mkigoma mtakuwa mnawaumiza raia wasio na hatia kwasababu serikali hii chini ya JK haitakaa iwasikilize kwa maana ya kutatua mgogoro huo. Napendekeza mgomo na maandamano yenu yaelekezwe katika kuupinga utawala mzima wa JK na wateule wake vinginevyo mnajilisha upepo, JK will never respond to your cry!!
  Nawasilisha
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo waendelee kufanya kazi wakati walidanganywa na Pinda?

  Na wakifanya hivyo watakuwa kama watoto wanaodanganywa kwa pipi na kufanyishwa kazi za ajabu ajabu!!

  Babu DC
   
 3. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  Gomeni tu madokta hadi kieleweke. Siasa zimezidi sana nchi hii kuliko utaalaam.
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Wakiendelea kufanya kazi katika mazingira ya ubabaishaji na kudanganywa tutawashangaa sana!!

  Babu DC!!
   
 5. Dr. Wansegamila

  Dr. Wansegamila JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 1,230
  Likes Received: 815
  Trophy Points: 280
  tumechoka kufanywa watoto wadogo, na tumechoka kupewa ahadi za uongo kama jk alisema kweli kuwa huo ni upepo tu kwa kweli alikosea sana, madaktari wana hasira sana juu ya jabo hili na hata morali yao ya kazi ipo chini sana. Tusubiri tuone
   
 6. C

  Chain Smoker Member

  #6
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu yangu acha kuwadanganya madaktari.... Madocta gomeni mpaka kielewe(leaders have never been accountable for mistakes which emerges in their hands). Serikali yetu ina viongozi jeuri,wababe,wajivuni kana kwamba ni miungu flani. Njia pekee ni madocta wanayodemonstrate. Watanzania acheni woga tukiendea kusubiri hivi vitume vya uchunguzi mara cjui kamati ya madudu gani hatutapata suluhu ya queries zetu. Na mnajua kiongozi wa nchi yetu si mtu wa kufanya maamuzi sahihi kwa muda muafaka. Hili linapaswa kuigwa na sekta zote hususan ndugu zangu walimu.
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Mar 3, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Madaktari gomeni tu, sisi wananchi tupo tayari ku suspend kuugua mpaka jawabu lenu lipatikane. Mungu yu upande wetu.
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Dr Hadji Mponda, akili za kuambiwa changanya na zako! Kindly save life of innocent Tanzanians by tendering resignation.
   
 9. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Tulishaunga mkono hoja hii,ma dr mna haki zote
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Viongozi wa CCM ni watu wabaya sana hawana UTU. SO doc do whatever suits you!
   
 11. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,519
  Likes Received: 10,436
  Trophy Points: 280
  kwa kiburi cha hii serikali bora mgome tu.
   
 12. Panga La Shaba

  Panga La Shaba JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 209
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Madaktari wana haki ya kudai madai yao......lakini kugoma tena,watu wa chini watakuwa wanaumia sana,nafkiri watafute njia nyingine mbadala ya kudai madai yao..
   
 13. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hao madokta nadiriki kuwaita hayawani, nadhani wamerukwa na akili. Wamegoma kujadili kwenye kikao kisa kuna wauguzi , watu wa maabara na wafamasia kwahiyo wao wanajiona ni bora kuliko tAaluma za wenzao. Kama wanampango wa kugoma bora wagome tu lakini wajue wanao suffer ni kina baba kabwela.
   
 14. MZEE WA ROCK

  MZEE WA ROCK JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 623
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  gomeni tu rais wetu si anataka tufee,nyie acheni tufe ili akose wa kumpigia kura
   
 15. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wewe unayeita madaktari mahayawani,yawezekana serikali yako hii unayoitetea kila siku humu jamvini ndo hayawani number moja kwa nini iwaajiri watu ambao wewe unawaita hayawani badala yako wewe mwenye akili nyingi.Period
   
 16. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hahaha mimi nitawaita hayawani mara 1000. Na ningependa wapimwe akili kama mrema alivyopimwa KCMC kipindi cha Mkapa. Haiwezekani wewe daktari ukatae kujadili kisa eti madai yao wao SPESHO mi naona ni upuuzi wa hali ya juu. Kwa watu waliobahatika kufuatlia huduma za afya US na Canada utakuta Nurse ni mtu muhimu sana pengine hata kuliko daktari.

  Hii ni selfishness of the highest magnitude na hao jamaa naona wana lao jambo na kama wana malengo ya kisiasa bora waseme mapema maana wanao suffer ni wajomba zao na shangazi zao wanaotokea mbwinde.
   
 17. vimon

  vimon Senior Member

  #17
  Mar 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45

  Hivi wewe unaleta propaganda zako ha JF unafikiri watanzania tumelala hii nchi inahitaji mabadiliko madaktari hawajabagua mtu wao walikwenda kuchukuwa majibu wakakuta mkutano ambao ajenda hazijulikani sasa ulitaka waingie kichwa kichwa,acha upumbavu usitumie masaburi kufikiri
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nilitegemea kuona michango ya watu kuitaka serikali na madaktari wafikie mwafaka lakini cha ajabu michango ya watu wengi hapa wanataka madaktari wagome....sidhani kama nyie kweli mna uchungu na madai ya madaktari kuliko ndugu zenu watakaokufa mahospitalini kama ilivyokuwa katika mgomo wa awali.
   
 19. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Sasa ukikuta ajenda hazieleweki ndio utoe lame excuses? Hapo madaktari wamechemsha na wamejidhalilisha. Na wakigoma this time wajue wananchi hawatalaumu serikali.
   
 20. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  akili yako bado haina akili!
   
Loading...