Madaktari chonde chonde

Sasa ukikuta ajenda hazieleweki ndio utoe lame excuses? Hapo madaktari wamechemsha na wamejidhalilisha. Na wakigoma this time wajue wananchi hawatalaumu serikali.

wameomba kikao cha doctors na waziri mkuu wanakuja na watu wa mambo ya ndani kwani kuna vita pale? Suala ni kuamba yule mwandishi wa prime alikurupuka kukimbilia kwenye vyombo vya habari ili kupotosha umma. Madaktari walijitoa kutokana na kukosa imani na ujumbe wa serikali uliokuja na watu hata wasiohusika. Tatizo linarudi mwanzo ambapo madaktari walikuwa wanaomba kuongea na wizara na wizara inakimbilia kwenye vyombo vya habari,hawa ndo negotiators.? Kwanza jiulize,kuna madai ya doctors hawa wengine wanaenda kujadili madai yapi? Wana mgogoro gani na serikali? Tuwe wakweli na tuache unafiki toka mwanzo walikaa kimya kwa nn sasa? Hawajui kwamba wanataka kutumika kuharibu maboresho ya wizara ya afya yanayokaribia kufanyika. Tutashinda hii vita,hata kama watakaofaidi ni wachache. Kwani waziri kujiuzulu ni gharama gani?
 
The moment madaktari wali kubali kurudi kazini,
wali kubali kudhalilishwa na kunyimwa madai yao.

Next time mkigoma tegemeeni kuchapwa fimbo tu.

Hakuna mgomo wala nini hapa,ingawa mngeweza kugoma mngekua na
support yangu.
 
Liyumba hakshitakiwa, jeetu patel hakushitakiwa, maranda hakushitakiwa? Lukaza hakushitakiwa? Balali hakuondolewa? Si ndio EPA hao au mlitaka rais awaweke kizuizini bila kuwapitishia mahakamani?

Acheni kuongea kama watu msiojua sheria na taratibu.
 
Rais amesamehe wezi kwani yeye judge? Au mnataka awe anaingilia uhuru wa mahakama?

Kweli upeo wako wa kufikiri ni mdogo!Rais alitangaza kuwa yeyote aliyeiba pesa kupitia EPA arudishe na hatashitakiwa.Orodha ya wezi na ushahidi vilikuwepo BOT,hii ni nini kama siyo kuingilia majukumu ya polisi na mahakama?
 
Sasa ukikuta ajenda hazieleweki ndio utoe lame excuses? Hapo madaktari wamechemsha na wamejidhalilisha. Na wakigoma this time wajue wananchi hawatalaumu serikali.
tatizo unasikiliza propaganda za serikali.Toka mwanzo walijaribu kuzima mgomo kwa propaganda na vitisho wakashindwa.sasa ofisi ya waziri mkuu ikajaribu kurudia njia zile zile chafu badala ya kukaa na ma daktari na kupata ufumbuzi wa kudumu.kwa kugundua hilo ndio maana madaktari walisusia hicho kikao cha alhamis. Kwa taarifa yako,kamati ya waziri mkuu ilijishtukia kua ilikosea,then wakapanga kikao kingine ambacho kilifanyika ijumaa. ktk kikao cha ijumaa,wakakubaliana kua kwa kua makubaliano yeyote yatakayofikiwa ya kuboresha utoaji huduma ya afya Tanzania yatahitaji utekelezaji wa wizara ya afya,ambayo kwa sasa inaongozwa na watu ambao kwa kiasi kikubwa ndio waliochangia kutokea kwa mgomo wa jan-feb,lazima hao waondolewe kwanza kama alivyo ahidi PM ndipo majadiliano memgine yaendelee.Nafkiri umepata picha
 
Liyumba hakshitakiwa, jeetu patel hakushitakiwa, maranda hakushitakiwa? Lukaza hakushitakiwa? Balali hakuondolewa? Si ndio EPA hao au mlitaka rais awaweke kizuizini bila kuwapitishia mahakamani?

Acheni kuongea kama watu msiojua sheria na taratibu.

Hata kama ulinufaika na wizi huo haiwezi kubadili ukweli!Liyumba hakushitakiwa kwa EPA,alishitakiwa kwa matumizi mabaya ya pesa ktk ujenzi wa majengo pacha ya BOT.Rajabu Maranda na Farjani Rajabu(binamu yake) kesi yao ni wizi wa Tsh 200mil.Ukijumlisha jumla ya pesa wanazotuhumiwa kuiba wale wote waliofikishwa mahakamani ni less than 2bil out of 133bil zilizoibiwa.JK alisema zimerudishwa 69bil lkn waliorudisha imebaki kuwa siri yake kwa kuwa ni yeye na rafiki zake.Kuondolewa kwa Balali aliyesingiziwa wizi uliofanywa na CCM na baadaye akasingiziwa kifo kulilisaidia nn taifa kama siyo kupoteza ushahidi dhidi ya JK na wezi wenzie?
 
Pesa zimeibwa kipindi cha Mkapa na wizi chini ya Ballali ambaye alitolewa Washington na Mkapa akaletwa sasa kikwete anahusika vp na huo wizi?

Je unajua Jeetu karudisha sh ngapi na wahindi wenzake? Unajua hao kina Lukaza wameleta sh ngapi? Au unajua za maranda tu? Unajua hao changanyikeni nao walileta ngapi?

Sawa tuseme wizi umefanywa na CCM lakini Ballali kama proffessional kuidhinisha malipo yasiyo halali ni makosa. Mimi siwezi kuona signature yako wewe halafu ukanambia eti ulishurutishwa kusaini.kwahiyo ya kusema Ballali kasingiziwa mi nakataa. The guy is dead tumuombee apumzike salama basi.
 
Hawa madaktari wanaogoma ingekuwa kipindi cha nyerere mnachukua majina halafu utekelezaji unafuata...

umeshasema ungekuwa wakati wa nyerere..understand this,nyakati hizi ni tofauti,sidhani kama hata nyerere angechukua hatua unazo zisema..
 
Madaktari wakirudi kazini wakati madai yao hayajasikilizwa itakuwa utoto, kwanini waliacha watu wakafa mwezi Januari?
Mi nasema tuone kama Jk ni roho ngumu kiasi gani akiona watu wakifa, ilhali anauwezo wa kutekeleza madai ya madaktari na hataki. Eti ni upepo tu, utapita? Madaktari gomeni. Tuone huo upepo utapitia upande gani. Watu watakufa, lakini haki yenu ikipatikana itawaokoa wengi zaidi.
 
Hivi rais anashindwa nini kuwatimua hawa mponda na mwenzake?
Madaktari wako serious kweli nimependa msimamo wao,na jumatano mbali wangeanza jumatatu!
 
Nimesikia kwa vyombo vya habari kuwa next wiki madokta huenda wakagoma ati kwa kuwa bado wizara inaongozwa na mawaziri wale wale waliosababisha mgomo wa awali kitu ambacho serikali kupitia kwa PM ilikuwa imeahidi itakishughulikia.
Kuna tetesi nimezipata kuwa Dr Mponda aliandika barua ya kujiuzuru kwa raisi naye JK akamwambia kuwa " wewe bado u mchanga kwenye siasa, huo ni upepo tu utakwisha, chapa kazi achana na mambo ya kujiuzuru".
Kwa maono yangu madokta mkigoma mtakuwa mnawaumiza raia wasio na hatia kwasababu serikali hii chini ya JK haitakaa iwasikilize kwa maana ya kutatua mgogoro huo. Napendekeza mgomo na maandamano yenu yaelekezwe katika kuupinga utawala mzima wa JK na wateule wake vinginevyo mnajilisha upepo, JK will never respond to your cry!!
Nawasilisha

Wewe ushauri wako ni wa nguvu ya soda, madaktari kitu wanachotaka ni kusaidia (raia wa chini) wasiendelee kuumia na kufariki kwa kukosa dawa na vitu kama hivyo, sasa kama wakiendelea na kazi wakati hamna dawa wala vifaa vya kazi watakuwa wanafanya nini si ni kazi bure! Cha msingi ni serikali kusikiliza madai ya Madaktari kwa umakini na kwa masirahi ya taifa hili, siyo wachukulie kama nazo ni siasa. Kifo cha mtu mmoja kinaweza kukomboa vifo vya watu wengi.

"Chagua kati ya kuishi kwa mateso au kufa"
 
Madaktari wakirudi kazini wakati madai yao hayajasikilizwa itakuwa utoto, kwanini waliacha watu wakafa mwezi Januari?
Mi nasema tuone kama Jk ni roho ngumu kiasi gani akiona watu wakifa, ilhali anauwezo wa kutekeleza madai ya madaktari na hataki. Eti ni upepo tu, utapita? Madaktari gomeni. Tuone huo upepo utapitia upande gani. Watu watakufa, lakini haki yenu ikipatikana itawaokoa wengi zaidi.

J.k siyo wa kujaribiwa kiasi hicho, anauwezo hata wa kuwaacha watanzania milioni mkafa na asifanye chochote, kwa hiyo yeye haoni hatari hata watu wakifa, ilimradi Mwanaisha na Riz1 wanaishi yeye yuko poa. Kwa hiyo usitegemee kama mkifa atasikitika au kuchukua hatua yoyote. Ndiyo alivyozaliwa yeye akisha kula akashiba masufuria yote anayatoboa na misumali.
 
Eti upepo tu wa kisiasa, kweli mjomba kauzu! Kumbe ata lawama kashazoea itakuwa, teh teh!
 
usijadili kitu ambacho hujakifanyia utafiti na kujua ukweli wake. Wale walioitwa kwenye kamati ya pinda walikuwa ni tana ambao mwakilishi ni kanali wa jeshi,watu wamaabara,mwakilishi wao alikuwa mtumishi wizarani. Toka lini kanali wa jeshi akatetea wananchi? Badala ya kuzungumzia maboresho ya wizara wakaishia

Yule kanali wa jeshi taaluma yake ni muuguzi. Ni mchumia tumbo vibaya mno. Kuna ka-mchakato anataka kukaanzisha ili wauguzi wakatwe asilimia fulani kwenye mishahara yao moja kwa moja kutoka hazina ili 'kutunisha' mfuko wa TANA. Ana tabia ya ubabe,utemi...nilishasema hapa matatizo waliyonayo wauguzi ni mengi sana na hawatakiwi kudandia hoja za madaktari.
 
Pesa zimeibwa kipindi cha Mkapa na wizi chini ya Ballali ambaye alitolewa Washington na Mkapa akaletwa sasa kikwete anahusika vp na huo wizi?

Je unajua Jeetu karudisha sh ngapi na wahindi wenzake? Unajua hao kina Lukaza wameleta sh ngapi? Au unajua za maranda tu? Unajua hao changanyikeni nao walileta ngapi?

Sawa tuseme wizi umefanywa na CCM lakini Ballali kama proffessional kuidhinisha malipo yasiyo halali ni makosa. Mimi siwezi kuona signature yako wewe halafu ukanambia eti ulishurutishwa kusaini.kwahiyo ya kusema Ballali kasingiziwa mi nakataa. The guy is dead tumuombee apumzike salama basi.
Mkuu naona ufaham wako kuhusu EPA ni mdogo au umeamua kuwa mbishi tu au nawe ni mnufaika wa pesa hiyo. Pesa iliyoibwa ni nyingi kuliko iliyo rudi, jumla pesa zinazodaiwa kukwapuliwa na waliofunguliwa kesi ni ndogo kuliko kiasi kilicho rudishwa. Makosa yakifanyika na awamu ya nyuma haimpi waranti raisi ajaye kusamehe kihuni kama alivo fanya. Je, hao "changanyikeni" ni akina nani?.
 
Hata mkigoma hamtapewa kila kitu. Waziri wa afya siyo waziri wa madaktari pekee. Nyie gomeni hamna jipya!
 
naunga mkono mgomo wa madaktari kwa asilimia mia mbili,hii nchi bila hakuna kinachofanyika....
 
mazingira ya kazi hayajaboreshwa

mponda na nkya hawajawajibishwa

hakunawaraka wowote kutoka serikalini unaoelekeza juu ya mabadiliko ya maslahi ya madaktari.pinda amedanganya tena!!kamati yake imeshakula perdiems,kamati ya bunge ya huduma za jamii imeshavuta perdiems,tunasubiri vifo vingine ndo tuamue???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom