Madaktari bingwa wa upasuaji wa China waokoa mkono uliovunjika wa kondakta wa Tanzania, na kurejesha matumaini kwa familia

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,242
Reaction score
1,212


Wiki tatu zilizopita, Ali Hamad Kombo mwenye umri wa miaka 31 aliamini maisha yake ya kazi na kujitafutia riziki kwa ajili ya familia yake yalikuwa ndio basi tena ghafla tu yamefikia mwisho.

Kombo ambaye ni kondakta wa daladala katika wilaya ya Chake Chake Kisiwani Pemba, Zanzibar, anategemea malipo ya kila mwisho wa siku ili kumsaidia mke wake na watoto wake watatu. Ajali ya barabarani ilimfanya avunjike mkono wa kulia, na kumlazimu kuacha kazi na kuifanya familia yake kuwa na maisha yasiyo na uhakika.

"Nilidhani maisha yangu ndio basi tena," Kombo alikumbuka katika mahojiano ya hivi karibuni na Xinhua. "Bila mkono, nisingeweza kufanya kazi, na bila kazi, nisingeweza kuwatunza watoto wangu."

Lakini leo, mtazamo wa Kombo umebadilika kabisa. Kufuatia upasuaji mgumu katika Hospitali ya Abdulla Mzee, sasa anapata nafuu kwa kasi na anatumai kurudi kazini katika wiki kadhaa zijazo. Matumaini yake mapya, anasema, yanatokana na juhudi za pamoja za timu ya 35 ya madaktari wa China huko Zanzibar na madaktari wenyeji.

"Sijui niwashukuru vipi madaktari wa China," Kombo alisema, akikunja tararibu mkono wake unaoendelea kupona. "Hawakuokoa tu mkono wangu baada ya upasuaji mgumu sana, lakini pia waliiokoa familia yangu. Ninatarajia kufanya kazi tena na kujiingizia kipato."

Daktari mwenyeji alisema jeraha la Kombo lilitokana na ajali ya barabarani katika Kisiwa cha Pemba, ambapo barabara nyembamba na idadi inayoongezeka ya magari mara nyingi husababisha ajali kubwa sana, huku rasilimali za matibabu zikiwa chache.

Baada ya matibabu ya awali, madaktari walithibitisha kuwa Kombo alikuwa amevunjika vibaya sehemu ya ndani ya kiwiko, jeraha linalojulikana kwa ugumu wake na kuleta hatari kubwa ya ulemavu wa muda mrefu ikiwa halitatibiwa ipasavyo.

Kwa Kombo, matokeo ya uchunguzi yalikuwa mabaya sana. "Sikuweza hata kushika kikombe," alisema. "Nilichoweza kufikiria ni jinsi gani watoto wangu watapata chakula."

Katika Hospitali ya Abdulla Mzee, daktari bingwa wa mifupa wa eneo hilo Eveline Emmanuel Sikahanga aliangalia picha za Kombo na kuwasiliana na Hou Jianwen, naibu kiongozi wa timu ya madaktari wa China huko Zanzibar na daktari mkuu wa mifupa, aliyepo Kisiwani Pemba kama sehemu ya mpango wa muda mrefu wa usaidizi wa kimatibabu wa China.

Picha hizo zilionesha mifupa ya mkono wake imevunjika vibaya, huku ikivunjika vipande vingi na sehemu ya juu ya kiungo ikiharibika vibaya. "Haikuwa kuvunjika kwa kawaida," Hou alisema. "Mifupa iliyovunjika ilihusisha kiungo, na vipande vingi vilivyohitaji kuunganishwa upya."

Chini ya rasilimali chache za hospitali, changamoto ilikuwa kubwa, kwani hakukuwa na kifaa kijulikanacho kitalaamu kama “C-arm fluoroscopy” ndani ya upasuaji ambacho kinaongoza X-ray kwa wakati halisi.

Upasuaji wa kwanza ulipangwa kufanyika jioni ya Januari 17 na uliendelea hadi usiku mkubwa. Kwa kutumia mbinu ya “olecranon osteotomy” ili kufikia kiungo kilichoharibika, Hou alifanya kazi kwa karibu na Sikahanga katika upasuaji mzima.

Bila fluoroscopy, kila hatua ilitegemea ujuzi wa anatomia, kugusa na uzoefu, kitu ambacho madaktari wa upasuaji wakati mwingine hukiita "upasuaji usioonekana." Kila uwekaji wa skrubu na waya haukuwa na uhakika hadi X-rays aliyopigwa baada ya upasuaji ilipothibitisha matokeo.

"Mfupa uliofunjika ulikuwa katika hali mbaya zaidi kuliko picha zilivyoonesha," Hou alisema. "Kulikuwa na vipande muhimu zaidi ya saba, na kipande kimoja muhimu kilikuwa vigumu kukitambua mwanzoni."

Pamoja na Sikahanga, Hou alitambua kwa uangalifu anatomia, akatuliza vipande vya mfupa, na kuamua pembe sahihi za kurekebisha.

Kadri upasuaji ulivyoendelea, haja ya kupata usaidizi zaidi ikaongezeka. Hou alimpigia simu Zhu Shuangjiu, mkuu wa upasuaji wa jumla katika timu ya madaktari wa China, ili kusaidia kupunguza mvunjiko na kusaidia katika kurekebisha.

"Kukiwa na watu watatu wanaofanya kazi pamoja, kila kitu kilifanyika kwa ufanisi zaidi," Sikahanga alisema. Upasuaji ulimalizika saa 7:00 usiku kuamkia siku iliyofuata.

Kazi ya Hou haikuishia na upasuaji. Kwa kuwa hakuweza kulala, alichora michoro ya kina ya mbinu ya kupunguza na kurekebisha mfupa uliovunjika, baadaye alimpa Sikahanga kama zana ya kujifunza.

"Hivi ndivyo ushauri unavyopaswa kuwa," Sikahanga alisema baadaye. "Sio kuongea tu, bali kusimama na wewe wakati wa nyakati ngumu zaidi na kukusaidia kuelewa kila uamuzi."

X-rays baada ya upasuaji zilizopigwa asubuhi iliyofuata zilionesha kupungua na kuimarika kwa kuridhisha. Mzunguko wa damu na hisia za neva za Kombo zilikuwa sawa, kiashiria muhimu cha mafanikio.

Kwa Kombo, maelezo ya kiufundi hayakuwa na umuhimu mkubwa kuliko matokeo. Anaweza kuchezesha vidole vyake. Maumivu yameweza kudhibitiwa. Na kwa mara ya kwanza tangu ajali hiyo, anaweza kuweka mipango yake ya siku zijazo.

"Nitarudi kazini," alisema huku akitabasamu.

Kwa Hou na wenzake, kupona kwa Kombo kunaashiria kusudi la jukumu lao. Timu za madaktari wa China zimefanya kazi Zanzibar kwa miongo kadhaa, zikitoa huduma, mafunzo na usaidizi katika maeneo ambayo rasilimali ni chache.

"Msaada wa kweli wa kimatibabu sio tu unahusu kutibu wagonjwa," Hou alisema. "Bali unahusu kutoa maarifa, kujenga imani na madaktari wenyeji, na kubeba jukumu kwa pamoja kwa kila uhai wa mtu."
 
Siku zote nimekuwa nikiamini wapo wengi waliokufa katika Dunia hii ya tatu sababu kuu ikiwa ni kukosekana kwa madaktari bingwa na pia wapo wanaopelekwa mochwari wakiwa hawajafa sawasawa.
 
Hawa wachina wameshindwa kuokoa watu maelfu wakifa na drones za Marekani huko Iran.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…