Madai ya Waislam juu ya NECTA ni mazito

Status
Not open for further replies.
kiukweli waislamu wanayo haki ya kudai hivyo vitu japokuwa serikali yetu haina dini ila kuna baadhi ya viongozi wameingiza udini ktk kutekeleza majukumu yao na kuonekana kuwa wanamaslahi nayo ktk maisha yao ndio maana wanalilia mfumo wa kuandika majina drs 7 urudie ili waendeleze kuwakandamiza waislamu ktk kupata elimu.


alshabab
 
Kiukweli waislamu wanayo haki ya kudai hivyo vitu japokuwa serikali yetu haina dini ila kuna baadhi ya viongozi wameingiza udini ktk kutekeleza majukumu yao na kuonekana kuwa wanamaslahi nayo ktk maisha yao ndio maana wanalilia mfumo wa kuandika majina drs 7 urudie ili waendeleze kuwakandamiza waislamu ktk kupata Elimu.

Pelekeni watoto shule badala ya vyuo/madrasa ili waelimike,...muuache kulalama ili muonewe huruma na serikali....hii ni dunia ya ushindani sio kutwa kulalama.
 
Mimi naona kwa mtazamo wangu, serikali iachane na hii mitihani ya dini. Sioni umuhimu wa haya masuala katika elimu ya kawaida. Anayeteka kubobea katika dini, aende Universities na shule za kidini! Pia system nzima ya utungazi, usimamizi, usambazaji, usahihishaji na utoaji matokeo ni bomu sana! Syestem nzima lazima itazamwe upya!
 
Mkuu muonamambo naona umeona mambo! Hilo la pili ni chokochoko tu. Tukianza hivyo itakuea tabu kweli kwa Tanzania. Hapa kuna wanawake wanataka asilimia 50; hapo tuna shida tayari. Kesho useme wakristo asilimia 50 na waislamu 50 keshokutwa wasukuma nao watataka asilimia yao! Wakurya nao watake sehemu yao kisha wachagga nao wajimegee sehemu yao kwenye vyombo vya nchi: Tutakuwa na nchi kweli hapo.
Kosa limetokea na Waziri amekiri na kuomba radhi baada ya maelezo lakini naona watu wanataka roho yake!

Umewasahau Wazanzibari wanataka 100% yao! CCM wamekamata 100% serikalini!

Hawa jamaa walianzia mbali, walitaka Mahakama ya "kanzu", ajira ziwe 50% kila sekta na idara. Na sas kwa vile waziri amekiri madhaifu, hawataishia hapo, watataka na shule ziwe zao 50%, Vyuo 50%, mikoa igawanywe 50%, Hospital 50% nk. Hawa jamaa wanatafuta namna ya kuanzisha Boko Halali yao! Time will tell!
 
Tudhulumiwe tukae tunaogopaogopa kuitwa wadini> mtaita wadini mpaka mchoke, nyiyi msio na dini mbona mmewafelisha watoto zetu walio pasi?
hii kesi si ilishatolewa ufafanuzi, ya nini kuendelea na malumbano wakati makosa yameshajulikana na yatafanyiwa kazi..........
 
Hawa jamaa wana matatizo sana basi na waziri wa elimu awajibishwe au kwa kuwa siyo mgalatia?

MAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: HUJUMA ZA BARAZA LA MITIHANI DHIDI YA WAISLAM Kila sifa njema anastahiki Allah, ambaye rehema zake zimeenea katika kila kitu katika ulimwengu bila ya kujali utii ama uasi wa kitu hicho katika amri na sharia zake. Rehema na amani zimuendee kipenzi chetu mtume Muhammad (S.A.W) kwa kuwa kiigizo chema na rehema kwa walimwengu wote. Ndugu waandishi kwa muda mrefu waislam wamekuwa wakiilalamikia suala zima la utendaji wa serikali kuwa umekuwa wakibaguzi kwa kuwapendelea wakirsto kwa kuwapa nafasi mbalimbali muhimu serikalini na katika taasisi zake. Ndugu waandishi na Waislam mnamo tarehe 01/ 05/2012 Baraza la mitihani la Tanzania lilitangaza matokeo ya kidato cha Sita, matokeo hayo yaliwashtua sana wanafunzi waislam waliofanya mtihani wa elimu ya dini ya kiislam (Islamic Knowledge). Takriban asilimia 70 walifeli kwa kupata daraja F, na asilimia 30 ndio waliofaulu tu. Katika hao waliofaulu walipata alama za juu kabisa nchi nzima ni wanafunzi saba tu ambao wamepata daraja D, kwa matokeo haya somo hili likawa somo la mwisho kwa ufaulu nchi nzima (rejea kitabu cha takwimu cha Baraza la mitihani Tanzania April 2012.
Matokeo haya yaliwashtua wazazi na walimu wa somo hili, baadhi ya wanafunzi waliamua kukata rufaa ya kutokubaliana na matokeo hayo.

Waislam kupitia Taasisi mbali mbali za kiislam walimuandikia katibu mkuu wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kumuomba aunde tume huru kuchunguza matokeo ya somo husika.
Kufuatia malalamiko hayo ya baadhi ya taasisi za dini, baraza la mitihani liliyatazama matokeo hayo na kugundua pia walikosea na hivyo Baraza la mitihani likaidhinisha kutolewa matokeo mapya kwa somo hilo.

Mabadiliko hayo ya matokeo ufaulu kwa wanafunzi wale wale ambao awali walifeli kwa asilimia 70, sasa yakabadilika na ufaulu ukaongezeka kwa zaidi ya asilimia 70.
Kwa namna yoyote ile itakavyokuwa dosari kubwa kama hii ni kashfa kubwa kwa Baraza la mitihani Tanzania na Serikali kwa ujumla. Na kwa kutilia maanani muundo na historia ya utendaji wa wa baraza la mitihani la Tanzania kama nilivyoanza kuelezea, Waisla wanayokila sababu ya kuamini kwamba matokeo haya ni uthibitisho tosha wa hujuma ambazo wanafunzi wa kiislam walikuwa wakifanyiwa kwa muda mrefu. Na hii inatupa picha kwamba dosari hizi zilizotokea kwenye somo la maarifa ya kiislam, haziishii kwenye somo hili, bali uchunguzi ukifanyika kwa masomo yote waliofanya wanafunzi wa kiislam itadhihirika kwamba hila na dhulma kama hizi zinafanyika katika masomo mengine.
Kimsingi kwa dhulma hii waliyoifanya baraza la mitihani dhini ya wanafunzi wa kiislam, Bakwata na waislam wote kwa ujumla wamepoteza imani na baraza la mitihani la Tanzania na hasa katibu mtendaji wake . Bakwata, linawapongeza na kuwaunga mkono Taasisi zote za kiislam nchini kwa jitihada ya kuligundua hili na hatua walizozichukuwa dhidi ya baraza la mitihani na kuhufahamisha umma wa kiislam juu ya kadhia hii.
Tunarudia baraza tunawapongeza taasisi zote za kiislam na tunasema katika hili Bakwata tuko nyuma yao kwani kauli yao ndio kauli yetu.

Bakwata, inamshangaa Katibu mtendaji wa Baraza la mitihani (Necta) Dk. Joyce Ndalichako, kwa kauli yake aliyoitoa kupitia vyombo mbali mbali vya habari vya jana tarehe 5/06/2012, akisema hakuna hujuma na mitihani inasahihishwa na walimu wenye sifa,wanachaguliwa na na wakuu wa shule zao, walimu wenye uzoofu na kuna mfumo wa usahihishaji aliohuita “Conveyor Belt”.

Bakwata inasema hapa tatizo la msingi sio mitihani kusahihishwa na walimu wenye sifa,na nani anawachagua walimu hao wenye sifa au huo mfumo wa usahihishaji, tatizo la msingi hapa ni kufelishwa kwa makusudi kwa wanafunzi wetu wa kiislam katika somo husika, wakati nakala za mitihani yao (Scripts) zinaonyesha wamefaulu.
Bakwata, tunahoji kwanini tatizo hili la huo mfumo (Conveyor Belt) litokee mwaka huu, mbona matokeo ya mwaka jana waislam hawakulalamika na kulikuwa hakuna dosari kama za mwaka huu iweje itokee mwaka huu, wakati mfumo ni ule ule?
Bakwata, tunaamini waislam katika hili tumehujumiwa na waislam hawajaridhishwa na majibu ya Dk. Ndalichako, aliyoyatoa kupitia vyombo vya habari vya hapa nchini.

Hiyo mifumo ya usahihishaji sio maneno matakatifu kwamba haiwezi kuchezewa kutokana hila za binadamu ni mifumo iliyowekwa na binadamu, na binadamu huyohuyo anaweza kuibadilishabadilisha vyovyote anavyotaka. Sisi kama Bakwata,tunaamini ili kurudisha imani ya waislam dhidi ya Baraza la mitihani tunataka mambo yafuatayo yafanyike, · Tume huru iundwe la kuchunguza Baraza la mitihani la Tanzania na utendaji wake wa kazi kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.


· Katibu mkuu wa baraza la mitihani (Necta) ajiuzulu mara moja ili kulinda heshima ya serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania na Baraza la Mitihani.


· Watendaji wakuu wa kitengo cha mitihani na wanaohusika na mfumo wa kompyuta ya Baraza la mitihani nao wawajibishwe mara moja. · Hatua za kisheria na kinidhamu zichukuliwe dhidi ya watumishi wa baraza la mitihani watakaothibitika kuhusika na kashfa hii.


· Muundo wa baraza la mitihani uzingatie uwiano wa kidini, kitendo cha chombo nyeti kama hiki kujazana watu wa dini moja kunaliondolea baraza la mitihani sura ya kitaifa, kwani takwimu zinaonyesha makatibu wakuu watendaji na manaibu katibu wakuu wamekuwa wakristo na wenyevyiti wa baraza hilo ni wakristo tangu lilipoanzishwa mwaka 1973, mpaka hii leo na takwimu tunazo.
· Pia tunaiyomba Serikali iwape nafasi wanafunzi wote ambao baada ya matokeo yao kubadilishwa wamekuwa na sifa za kujiunga na vyuo vikuu waruhusiwe kuomba mikopo bodi ya mikopo, tunalisema hili kutokana na muda wa kuomba mikopo kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na elimu ya juu kwisha.
Suala la Sensa ya watu na makazi.
Kama tunavyojua kwa mwaka huu wa 2012, kuna zoezi la sense ya watu na makazi ambayo inatarajiwa kufanyika kuanzia mwezi wa nane, 2012, na kutoka na upotoshaji ulioenea kwenye vyombo vya habari hapa nchini, kalenda iliyochapichwa na ofisi ya waziri mkuu, imetoa takwimu zinazoonyesha idadi ya watanzania ni milioni 43 ambapo kwa mujibu wa dini zao wakristo ni asilimia 52, waislam asilimia 32 na dini zingine ni asilimia 16. Bakwata tunalaani kitendo hiki na tunasema takwimu hizi sio sahihi na zinapotosha wananchi, hii ni kwa sababu katika sense zilizofanyika hivi karibuni ikiwemo sense ya mwaka 2002 kipengele kinachobainisha dini za watanzania kiliondolewa. Kwakuwa taarifa hizi zinaonekana kwenye kalenda zinazoonyesha zimetayarishwa na ofisi ya waziri mkuu, tunaitaka serikali kurudisha kipengele kinachobainisha dini za watanzania katika sense ya mwaka huu ili ukweli ujulikane na kuondoa kabisa sintofahamu hii.
SUALA LA MGOGORO WA HIVI KARIBUNI ZANZIBAR
Ndugu waandishi wa habari naamini nyinyi nyote kama waandishi wa habari mnajua au mmesikia vurugu zilizohusisha imani za dini zilizotokea visiwani humo na kutokana na taarifa nyingi za vyombao vya habari zilizokuwa zikitolewa tangu mgogogro huu uanze kuna kila dalili za kuchukuliwa hatua za haraka haraka na katika mazingira haya wale wote waliohusika na vurugu hizi wasijulikane tena na watu wasio na hatia wakahusishwa na hali ikawa mbaya zaidi kwa hivy o kutokana na kadhia yote hiyo na yote yaliyosemwa na makundi mbalimbali ya waisla na wasiokuwa waislam Sisi kama Bakwata tunasema yafuatayo: Kwanza tunalaani kitendo cha uvunjifu wa amani uliotokea Zanzibar na tunaamini waliofanya vurugu zote zile sio waislam bali ni wahuni tu. Pili tunasema Wazanzibar, wasikilizwe kwa yale ambayo wanayapigia kelele kama malalamiko yao yapo katika muungano Serikali haina budi kuyasikiliza


yale yote yanayolalamikiwa na kuyarekebisha, kwani Muungano sio qur- an useme kilichomo humo hakiwezi kurekebishika. Tatu iundwe tume huru yenye wajumbe kutoka pande zote, makanisa, Serikali na UAMSHO ili zichunguzwe tuhuma hizi kwa undani zaidi maana kwa kweli athari zinaweza zikawa za muda mrefu kwani zinapandikiza kutoaminiana baina ya Wazanzibar hasa wakristo na waislam jambo ambalo halikuwepo hapo kabla na yoyote takae bainika kuwa na hatia sheria ichukue mkondo wake bila ya kujali wadhifa alionao katika chama, dini ama Serikali. Mwisho tunamuomba Allah atupe Imani ya kweli katika nchi yetu na kama kuna fisadi na adui Allah amdhalilishe hapahapa Duniani, amen. Wabillah Tawfiq.
clip_image002.gif
Sheikh Issah Bin Shaabani Simba. Sheikh Mkuu na Muft wa Tanzania
 
Wanataka ndani ya siku saba serikali ya CCM iwe imefanya haya:

1. Ndarichako awe amejiuzulu
2. Uwiano wa wafanyakazi wa NECTA kati ya Wakristo na waislam
3. Kuundwa tume huru kuchunguza kufelishwa kwa wanafunzi wa kiislam
4.........


Consern

Kipi kitafuata?????

Hivi hawa watu huwa wanatumia kiungo gani kufikiri
 
Jaman kwa hili waislam wameonewa kwanin umkate mtoto wa mtu kisa muislam, shangaen kwanin sasaiv baraza tumbo joto, if there z nothng wrong, am real smeling a rat here..
 
Mkuu muonamambo naona umeona mambo! Hilo la pili ni chokochoko tu. Tukianza hivyo itakuea tabu kweli kwa Tanzania. Hapa kuna wanawake wanataka asilimia 50; hapo tuna shida tayari. Kesho useme wakristo asilimia 50 na waislamu 50 keshokutwa wasukuma nao watataka asilimia yao! Wakurya nao watake sehemu yao kisha wachagga nao wajimegee sehemu yao kwenye vyombo vya nchi: Tutakuwa na nchi kweli hapo.
Kosa limetokea na Waziri amekiri na kuomba radhi baada ya maelezo lakini naona watu wanataka roho yake!

Hawa NECTA wamezoea kufanya utumbo kama huu alafu mnasema waislam ni vilaza!!! NA sasa naaanza kuamini kilichotokea Zanzibar ni uchakachuaji wa makusudi.
 
Bakwata, tunahoji kwanini tatizo hili la huo mfumo (Conveyor Belt) litokee mwaka huu, mbona matokeo ya mwaka jana waislam hawakulalamika na kulikuwa hakuna dosari kama za mwaka huu iweje itokee

Mfumo wa mitihani miwili badala ya mitatu umeanza kutumika mwaka huu na ni mpya. Soma habari hapa chini. Kilichokosewa ni kubadilisha computer program code ya kutafuta wastani wa mitihani. Badala ya kugawanya kwa 2 mwaka huu, waliendelea kugawanya kwa 3 kama mwaka jana.

Serikali kuichunguza Necta

...."Mfumo wa mtihani wa Islamic Knowledge ulioanza kutumika rasmi kidato cha sita kwa mwaka huu unatumia mitihani miwili na si mitatu. Hivyo tofauti ya alama iliyobainika imetokana na mfumo wa ukokotoaji kwa njia ya kompyuta kuendelea kutumia mitihani mitatu katika upatikanaji wa wastani wa alama za mwisho," alisema Dk. Kawambwa....
 
Mkuu Kimbunga masomo ya Dini ndo jamaa wanayategemea kwenda UDOM kusoma Bachelor ya Arabic.Ukiyaondoa tu hawana degree inabaki diploma ya Chuo chao Arusha
 
Umewasahau Wazanzibari wanataka 100% yao! CCM wamekamata 100% serikalini!

Hawa jamaa walianzia mbali, walitaka Mahakama ya "kanzu", ajira ziwe 50% kila sekta na idara. Na sas kwa vile waziri amekiri madhaifu, hawataishia hapo, watataka na shule ziwe zao 50%, Vyuo 50%, mikoa igawanywe 50%, Hospital 50% nk. Hawa jamaa wanatafuta namna ya kuanzisha Boko Halali yao! Time will tell!
ishu ni kwamba wameona tumeshawapiga bonge la step sasa wanatafuta njia ya kupata uhiano............wakati mwarabu ametawala akukumbuka kujenga shule wala hospital zaidi aliwafundisha jinsi ya kucheza bao na kukaa vibarazani kunywa kahawa na wanawake kushona ukiri.
wakati mjerumani na mwingereza wao walijenga shule na mahospital ambayo mpaka sasa zinatumika. so wakati wakristu wanasoma wao wako madrasa............na kucheza bao leo hii wanategemea tuwe sawa ni kitu ambacho akiwezekani.....
walipewa chuo cha morogoro uliza sasa hivi kipo katika hali gani ni aibu.............shule ya biafra imeishia wapi......kinondoni muslim. al maini ni nyinginezo.
jipangeni sawasawa kwa kujenga shule zaidi na kuwaelimisha watu wenu kuwa elimu dunia pia ni muhimu otherwise mnataka vidole vyote vilingane while impossible.
 
Mimi naona kwa mtazamo wangu, serikali iachane na hii mitihani ya dini. Sioni umuhimu wa haya masuala katika elimu ya kawaida. Anayeteka kubobea katika dini, aende Universities na shule za kidini! Pia system nzima ya utungazi, usimamizi, usambazaji, usahihishaji na utoaji matokeo ni bomu sana! Syestem nzima lazima itazamwe upya!

:clap2:
 
Samahani sana wakuu sipo hapa kuutukana uislam ila ninasema hivi. Waislam nimesoma nao miaka hiyo kuanzia chekechea, shule ya msingi, secondari na vyuo mbalimbali kwa degree tofautitofauti. Kwa mtizamo wangu ni kuwa kwa jinsi elimu ya Tanzania inahitaji usome kwa mitulinga na kukesha kwa sana kulingana na aina yetu ya ufundishaji hakuna hata siku moja mtu wa jamii ya kiarabu anaweza kumshinda mkristu!!!!!!! Tangu miaka ile tunasoma wakristu walikuwa wanaongoza tu hasa shule zao za seminary. Kama kuna mtu mwenye data ya wakuu na watumishi waliopita NECTA si kuwa ni wakristu wamejaa pale. Ili waislam wafaulu wanavyotaka wao labda wawe wanatungiwa mitihani yao milaini kama chapati za maji, pia wawe na shule zao!!! Ila tu kama watakuwa na shule zao bila kuchanganyika na sisi makafiri ndiyo kwanza watafeli mpake mwiso kabisa. Kwa mantiki hiyo waislam ndiyo wameanza kufeli leo au ni hata mpaka tulipotoka?

Nawashauri ndugu zangu waislam kama hamtaondokana na umwinyi hakuna jinsi mnaweza kuwa katika best education perfomers, nasema hata siku moja haitatokea!!! Kusoma kunahitaki misuli, tena misuli ya nduvu na dedication. Nasema hata nje ya nchi nimesoma na waislam toka nchi zote, west Africa, Uarabuni kwenyewe, n.k lakini hawafui dafu!!! Je kule nchi za nje nako kuna upendeleo? Tena kuna chuo kimoja nilisoma degree yangu ya pili na katika enrollment waislam walikuwa kibao, by the time tunamaliza waislam wote walikuwa wameondoka, nakumbuka walikuwa kama 11 au 12 hivi tulipoanza kwenye field ile but walimaliza wawili tena kwa tabu?!!!! Je kule nje nako wanawachukia waislam!!!

Hebu ndugu zangu kaeni chini mtafakari kabla hamjaongea lolote!!!! Siamini na wala sitaaamini eti kuwa mtu anachukua namba ya mtahiniwa anaanza kupekua udini!!!! this does not click in my head!!! Ondoeni kwanza vizingiti vinavyofanya mfeli ndipo muanze kulaumu!!! Ndiyo maana nasema jamani hata huu Muungano hautakiwi. Acha waislam Zanzibar wabaki wenyewe na mamlaka zao vinginevyo wanatuletea vurugu tu hapa. Halafu kwa kiasi waislam wa Bara wanajitahidi maana umwinyi haujawakaa sana na kwa kuwa wamechanganyika na makafiri katika discussion zao. Kule Zanzibar sidhani kama waislam safi wanachanganyika na makafiri wakati wa discussion!!! Nataka mjue kuwa kufaulu test na mitihani ya darasani kwenu iliyoandaliwa mithili ya castadi si kufaulu kigongo cha National kinachoandaliwa na wataalam. Forget and Tafakari.
 
mbona baada ya kubadilishiwa waliopata F ni wengi tu? Wenye A ya hilosomo hawafiki hata 10.........

Upumbavu wa baadhi ya watanzania ni huu, badala ya kuoigia kelel madini yanavyochitwa na twiga kutoroshwa wanaendekeza udini....

Kwa hiyo baraza waajiriwe kwa kufuata dini na sio uwezo wa watumishi? Na wakishakuwa idadi sawa wawafaulishe hata kama wamefeli?

Badala ya kubiresha shule zao wanang'ang'ania udini, na nafasi sawa.............. Kwahiyo waajiri waweke nafasi sawa za wakristu na waisilamu kwa kuwa nchi hii ina dini mbili tu?

Anayewatumia anajua kwa kuwapata, nyie ng'ang'anieni dini, wenzenu wanakomba rasilimali za nchi..................

Nashauri baraza waweke na somo la kulalamika hilo kuna watu watapata A+...... Inachosha kuona udini unaingizwa kila mahali....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom