Madai ya Uchochezi na Masalio ya Fikra za Kikoloni ndani ya Watawala na Watawaliwa

Mwanakijiji wewe tunakujua ni mtu uliyekata tamaa baada ya kujikuta umekosa nafasi kwenye serikali, kifupi wewe ni muasi kwa hiyo unaamua kuandika makala za kichochezi kuwashawishi wananchi wawe na chuki na serikali yao waliyoiweka madarakani wao wenyewe kwa njia ya kura.

Huwezi kufananisha uongozi wa sasa na ule wa kikoloni hata kidogo labda uwe unaishi ughaibuni (muasi kama wewe).

Ni vyema ukarudia kuisoma historia ya tanzania ukiwa umetubu na ukiwa hauna jazba kama wakati ulipokuwa unaandika makala yako hii ambayo haina ukweli wowote katika maisha ya mtanzania wa sasa.

Unataka kujenga jamii ya watu walalamikaji lalamikaji na yenye kulaumu badala ya kuhamasisha watu kufanya kazi. Wewe ungekuwa mzalendo ungebaki hapa nchini ukashiriki kujenga nchi kikamilifu badala ya kuangalia mechi kwenye TV na kukosoa.

Kifupi HUNA MPYA vijana wanasema UMECHOKA.
 
yeye mtoto ndio anaitwa RAshid Baghdella - tena tumewasiliana juzi tu - na mzee ndiyo Kheri. Nadhani kwenye makala niliwachanganya kidogo. Sasa Pasco, wenzetu mnaposhtuka leo hii miye binafsi nashangaa na hasa mnapotubeza sisi tulio nje ya nchi kuwa hatujui nini kinatokea nchini au nilazima kuwemo nchini ili kufanya harakati. Nadhani muda umefika tuwaache tu watutawale wapendavyo yaishe.
 
Mwanakajiji anaposimamia ukweli..yuko tayari kurudi nyuma na kuangalia wapi tulikosea.........

kuwa alikuwa mkoloni, akaja Nyerere na leo CCM hawa wametufikisha hapa tulipo.........na misheria hii ya ajabu ajabu

Thanks
 
Kilichotufanya tukubali sheria kandamizi wakati wa Nyerere ni nini?
Sheria hutungwa kulingana na mahitaji ya wakati huo na dhamira ya kweli ya kulinda na kutetea maslahi ya nchi. Sheria zinapotungwa hatuulizwi wananchi isipokuwa WABUNGE wetu ambao tangu wakati huo hadi leo ni watiifu kwa CHAMA chao na serikali yao kwanza.
 
wewe umewafuata wakoloni huko ulaya,sasa umeshiba vyao unaanza kutukana na kunyea nyumbani kwenu.dhambi ya kuzaliwa itakutafuna.
 
wewe umeungana na wakoloni huko unataka kutudanganya sisi huku utuvurugie harakati zetu za kupambana na umaskini...nasema MM,kwa sasa HATUDANGANYIKI,labda BAADAYE.
 
Sheria hutungwa kulingana na mahitaji ya wakati huo na dhamira ya kweli ya kulinda na kutetea maslahi ya nchi. Sheria zinapotungwa hatuulizwi wananchi isipokuwa WABUNGE wetu ambao tangu wakati huo hadi leo ni watiifu kwa CHAMA chao na serikali yao kwanza.

Sheria hizo hizo zilikuwapo wakati wa Nyerere na zipo sasa, lakini sasa tunapiga kelele kuwa hatuzitaki japo zimewekwa na Bunge. Ni nini kilichotufanya turidhie sheria hizo kandamizi wakati wa Nyerere?

*Naandika haya nikiweka hypothesis kuwa maneno ya Mwanakijiji haya hayana shaka
Ninachotaka kusema kwa kifupi ni kuwa hakuna uchochezi na kama hakuna uchochezi hakuna uhaini kwani uhaini ni kusimama kinyume cha taifa lako na kutaka kuliangamiza.
 
Sheria hizo hizo zilikuwapo wakati wa Nyerere na zipo sasa, lakini sasa tunapiga kelele kuwa hatuzitaki japo zimewekwa na Bunge. Ni nini kilichotufanya turidhie sheria hizo kandamizi wakati wa Nyerere?

*Naandika haya nikiweka hypothesis kuwa maneno ya Mwanakijiji haya hayana shaka
Juzi tu tumeridhia sheria ile ya kuunda tume itakayoratibu maoni kuhusu KATIBA mpya. Kuna vifungu mle ni kandamizi sana na adhabu imewekwa kabisa kwa watakaovikiuka. Sheria kandamizi zitaendelea kutungwa tu endapo mahakama zetu zitaendelea kukaa kimya bila kufanya kazi yao ya msingi ya KUTAFSIRI kwa lugha rahisi ili sisi WANANCHI tuzikatae.
 
yeye mtoto ndio anaitwa RAshid Baghdella - tena tumewasiliana juzi tu - na mzee ndiyo Kheri. Nadhani kwenye makala niliwachanganya kidogo. Sasa Pasco, wenzetu mnaposhtuka leo hii miye binafsi nashangaa na hasa mnapotubeza sisi tulio nje ya nchi kuwa hatujui nini kinatokea nchini au nilazima kuwemo nchini ili kufanya harakati. Nadhani muda umefika tuwaache tu watutawale wapendavyo yaishe.
Mkuu Mwanakijiji asante kwa ufafanuzi wa jina.
Hili la kushtuka sasa ni kawaida kwenye miti hakuna wajenzi. Matukio haya pia ndio yanatufungua macho kumbe hatuna kabisa 'nil' vyama vya kutetea wanahabari.
MCT ni kibaraka wa serikali dhalimu ya Tanzania!. Jukwaa la Wahariri na Moat they are dancing to the tune of who pays the piper!. Tamwa sasa ni chama cha wanahatakati, TAJA died long time ago not sure if it exit hata vitabuni!.

Usijibizane na hao wanaokuita mchochezi au kuhusu kutokuwepo nchini, hao ni vichaa, na kuwa kichaa sio mpaka uokote makopo!.

Ila pia its about time to start thinking kuyasogeza mashambulizi to ground zero. Long distance missiles zimesha fanya kazi ya kutosha, sasa tuyasogeze majeshi yetu mstari wa mbele tayari kwa mashambulizi.

Hata mimi niliweka silaha chini na kujishughulisha na mengine, ila kinachoendelea kinanipandisha hasira, napanga kuvaa combat kuingia uwanja wa mapambano before 2015!.

Tanzania ni nchi yetu sote, haiwezekani wote tukae kimya wakati shamba la baba limevamiwa na ngendere, tena ngedere ukiwachekea utavuna mabua!. Tuendelee kuwachekea tuvune mabua au tuwakome giladi bila kuwaangalia usoni?!.

Uamuzi ni wetu individually ikibidi wote kuonekana wachochezi na tuonekane!.
 
Jamaa haeleweki kabisa.

Hapa Kazi Tu imegeuka na kuwa Hapa Magufuli Tu.

Wengine wote kaeni kimya. Ole wenu mfungue midomo.
Kitu cha kushangaza zaidi kila anaposhika mic anasema "niombeeni kwa Mungu" au "muendelee kuiombea nchi amani". Kwa kweli nashindwa kushangaa, hivi haoni kauli, maigizo na matendo ya polisi dhidi ya upinzani yanahatarisha amani ya nchi? Hivi hafahamu ugumu wa maisha aliowazidishia walalahoi unawafanya kulaani utumbuaji wa maisha yao, utumbuaji wa sauti zao?

Jirani walianza na kitu kama hii na waliishia kutumbuana. sasa mkulu, yeye "kutumbua" ndio msamiati wake.

Huu ung'ang'anizi wa madaraka wa naofanya fisiem utaleta majanga. Majanga ya viwanda na maisha bora ya mwendokasi.

Hivi wastaafu wa jeshi na polisi kweli wameanza kujiunga na ujambazi?
Maumivu ya kichwa huanza ..........
 
MM leo hii makala anaikimbia kama ukoma, lakini sisi hatuna lengo baya, tunamkumbusha tu kwamba kile alichokiandikia miaka sita nyuma, ndcho hiki tunaendelea kukidai leo
 
MM wa sasa amepofuka hawezi andika kama zamani kweli njaa imeathiri akili anacheza mziki asioupenda bila kujali kuwa anapishana na mdundo.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nonda

NN, mbona hiki nilichosema bado ni kweli na kila neno bado nalisimamia. Mbona sijabadilika chochote. Binafsi naona fahari kuwa nilichokisema bado kinasimama na tulikuwa na nafasi ya kukifutilia mbali mwaka jana lakini ndiyo hivyo tena... Lakini siwezi kuimba wimbo tu ilimradi ijulikane naijua tune.
 
MM leo hii makala anaikimbia kama ukoma, lakini sisi hatuna lengo baya, tunamkumbusha tu kwamba kile alichokiandikia miaka sita nyuma, ndcho hiki tunaendelea kukidai leo

Yaani, kile cha watu kusema Lowassa hafai halafu kusema leo anafaa na bado watu wanaamini wana legitimacy. Hivi mimi leo nikisema napinga hoja ya uchochezi (na kama watu wamenisoma wataona nimesema hivyo) nani atakuwa na legitimacy zaidi?
 
Umeona eeh! We acha tu Mkuu, mtu anaweza kuijenga reputation yake kwa miaka mingi sana na watu kutokea kumpenda na kumthamini mtu huyu kwa kuwa kile anachokisema wanakiunga mkono na ni ukweli wa hali halisi. Halafu mtu huyu anaamua kubadilika bila sababu yoyote ile ya msingi na kile alichokisema kwa miaka mingi sasa ameamua kupingana nacho. Chezeya kiumbe kinaitwa binadamu!!

Aisee!

Ama kweli binadamu ni viumbe changamani sana!
 
Back
Top Bottom