Madai ya Uchochezi na Masalio ya Fikra za Kikoloni ndani ya Watawala na Watawaliwa

NN, mbona hiki nilichosema bado ni kweli na kila neno bado nalisimamia. Mbona sijabadilika chochote. Binafsi naona fahari kuwa nilichokisema bado kinasimama na tulikuwa na nafasi ya kukifutilia mbali mwaka jana lakini ndiyo hivyo tena... Lakini siwezi kuimba wimbo tu ilimradi ijulikane naijua tune.
Mzee naona hapo umemnukuu asiye!

Hata hivyo unajua nini? Kwa haya yanayoendelea sasa hivi na hii 'radio silence' toka kwako, unawapa watu mawazo ya labda unaunga mkono kila kitu.

Ndo maana unaona unakuwa hueleweki.

Si lazima ukubaliane na Magufuli kwenye kila jambo kwa asilimia 100.

Sasa kama hukubaliani na hizi habari/ visingizio vya uchochezi, kwa nini huo ukimya ilhali zamani hukuwa mkimya hivyo? Kwanza ukimya si hulka yako kivile....kwa kadri nijuavyo!

So why this radio silence my man?

Do you lend countenance to everything that's going on?
 
MM angalau bado anajenga hoja kwa anachokisimamia. Ninashangazwa na hawa ambao wamemfanya role model waliyemwita fisadi mkuu nchi hii. Hakuna falsafa wanayosimamia zaidi ya kutafuta matukio na kudhalilisha wanaopishana nao mawazo. Zimebaki siku 2 jua kupakatwa na mwezi
 
Mwanakajiji anaposimamia ukweli..yuko tayari kurudi nyuma na kuangalia wapi tulikosea.........

kuwa alikuwa mkoloni, akaja Nyerere na leo CCM hawa wametufikisha hapa tulipo.........na misheria hii ya ajabu ajabu

Thanks
hata wewe mkuu siku hizi unatuita sisi nyumbu. Dah binadamu bana.

Njaa mbaya
 
So why this radio silence my man?

Do you lend countenance to everything that's going on?

Swali zuri; kwa mkongwe kama wewe unajua kabisa nikiwa kimya manake nini. Ni rahisi sana kwa mtu kufanya haraka ya kuzungumza ili aonekane amezungumza; wakati mwingine ni vigumu kwa mtu kutumia muda kusikiliza na kufikiri vizuri ili mtu azungumze vizuri. So the silence in public doesn't mean I'm silent within myself but when that end well..
 
Umeona eeh! We acha tu Mkuu, mtu anaweza kuijenga reputation yake kwa miaka mingi sana na watu kutokea kumpenda na kumthamini mtu huyu kwa kuwa kile anachokisema wanakiunga mkono na ni ukweli wa hali halisi. Halafu mtu huyu anaamua kubadilika bila sababu yoyote ile ya msingi na kile alichokisema kwa miaka mingi sasa ameamua kupingana nacho. Chezeya kiumbe kinaitwa binadamu!!

Ni rahisi kudai ni vigumu kuthibitisha madai... sasa sijui ni nani amebadilika hasa...
 
Utajibaraguza vile upendavyo lakini wino haudanganyi, hawakukosea wale waliosema tusiandikie mate na wino upo. Maandishi yako unatamani kuyakimbia lakini huna jinsi. Sasa unafiki wako hadharani. Umelipwa kiasi gani mpaka kubadili msimamo wako na wale uliowapinga sasa umeamua kuungana nao?

Ni rahisi kudai ni vigumu kuthibitisha madai... sasa sijui ni nani amebadilika hasa...
 
MM asee siamini ila ndo binadamu si mara zote tutafikiri the same.. Ila umebadilika pakubwa sana
 
Utajibaraguza vile upendavyo lakini wino haudanganyi, hawakukosea wale waliosema tusiandikie mate na wino upo. Maandishi yako unatamani kuyakimbia lakini huna jinsi. Sasa unafiki wako hadharani. Umelipwa kiasi gani mpaka kubadili msimamo wako na wale uliowapinga sasa umeamua kuungana nao?

Baadhi ya wale niliowapinga ni kina Lowassa; nani kaungana nao sasa? Na sijawahi kuwa na kumpinga mtu kama mtu; ile makala yangu ya Kiingereza ya "why we oppose them" ukiisoma ingeliweza kukusaidia kuelewa kuwa kinyume na wewe mimi siongozwi na ugomvi dhidi ya mtu, wala sidhanii kuwa anayenipinga amenunuliwa au anatumiwa na watu nje yake.

Ninaamini katika watu kuwa na maoni yao na kuyasimamia kwani ni muumini wa kweli wa demokrasia. Mwenzangu na wewe na wengine kadhaa humu mnayepingana naye ni mgomvi wenu, asiyepiga magoti kuwaheshimu anakuwa hasimu na asiyeitikia wimbo mnaouimba basi amekuwa mnafiki... alama za kweli za mwanademokrasia mmezipoteza mmebakia watu wa visasi, kejeli, ugomvi, n.k Kama kawaida mkishashindwa hoja...
 
MM asee siamini ila ndo binadamu si mara zote tutafikiri the same.. Ila umebadilika pakubwa sana

Ukiulizwa nimebadlika nini hasa utashindwa; nilisema Lowassa hafai na alipoenda CHADEMA nilisema hafai; wao walisema hafai alipokuwa CCM na baadaye alipoenda CHADEMA wakasema anafaa; ni yupi kati yetu amebadilika? NIna uhakika hautakuwa na ujasiri wa kujibu swali hili dogo tu la kuonesha 'mabadiliko'.
 
Sikuingia CHADEMA kwa sababu ya yoyote yule. Na yalikuwa makosa makubwa kumkaribisha Lowassa na kama ingekuwa ni amri yangu asingeingia CHADEMA. Simuungi mkono kwa sababu bado kuna maswali chungu nzima kuhusu Richmond/Dowans na mabilioni aliyogawa nyumba za ibada ameshindwa kuyajibu. Nitakuwa wa kwanza kushangilia siku akitangaza kaamua kurudi CCM kwa sababu moyo na akili yake bado viko huko.

Mie siyumbishwi kama wewe mganga njaa umewekewa bulungutu mezani na kuamua kuasi yale yote uliyoyaamini na kuyatetea kwa miaka chungu nzima.

Hebu tuambie ni milioni ngapi zilizowezesha uamue kuwa mnafiki na kuungana na fisadi dikteta uchwara
.

Ukiulizwa nimebadlika nini hasa utashindwa; nilisema Lowassa hafai na alipoenda CHADEMA nilisema hafai; wao walisema hafai alipokuwa CCM na baadaye alipoenda CHADEMA wakasema anafaa; ni yupi kati yetu amebadilika? NIna uhakika hautakuwa na ujasiri wa kujibu swali hili dogo tu la kuonesha 'mabadiliko'.
 
Ukiulizwa nimebadlika nini hasa utashindwa; nilisema Lowassa hafai na alipoenda CHADEMA nilisema hafai; wao walisema hafai alipokuwa CCM na baadaye alipoenda CHADEMA wakasema anafaa; ni yupi kati yetu amebadilika? NIna uhakika hautakuwa na ujasiri wa kujibu swali hili dogo tu la kuonesha 'mabadiliko'.
Thread yako inahusu uhuru wa vyombo vya habari na uchochezi jikite hapo..Hayo mambo yaowasa yametoka wapi?
 
mzee wakijiji anakula matapishi hahahaaaaa jamani hamisheni uzi wake wa udikteta ujea apa kila mwana jf ajue unafki wa uyu mwandishi bandia ambaye anapingana na kalamu yake
 
Mzee mwanakijiji acha kujichanganya kuwa hujabadirika. Mfano hili andiko lako ulizungimzia vizuri sana hiki kinachoitwa ni uchochezi kinachotumiwa na serikali hii ya ccm. Je baada ya Lowasa kuhama kimeisha you? Je unataka kutuaminisha kuwa kumbe wewe mambo yote uliyokuwa unayakosoa ccm ilikuwa ni sababu ya Lowasa tu? Swali la mwisho kwako, je maandamano ya hapo sep mosi ya UKUTA ni ya uchochezi?
 
Ukiulizwa nimebadlika nini hasa utashindwa; nilisema Lowassa hafai na alipoenda CHADEMA nilisema hafai; wao walisema hafai alipokuwa CCM na baadaye alipoenda CHADEMA wakasema anafaa; ni yupi kati yetu amebadilika? NIna uhakika hautakuwa na ujasiri wa kujibu swali hili dogo tu la kuonesha 'mabadiliko'.
Umeng'ang'ani EL na Move toka CCM to CDM. Umsahau kujibu maswali unayoulizwa.

Kosa lao halihalalishi kosa lako mkuu. Two Wrongs Dont Make It Right.

Jitetee wewe tuliekuamini, usijifananishe na wao.
 
Na uki-Qoute post, Qoute yote sio vimstari tu unavyoona rahisi kujibu. Ili ukijibu kesho urudi kujionea mwenyewe ulichojibu kama kinaendana na ulichoulizwa.

Kuna saa nawazaga labda wewe sio wewe
 
Back
Top Bottom