Kenya 2022 Madai ya Odinga kuhusu Ruto kuchakachua matokeo ni ya kijinga sana kwa sababu hizi

Kenya 2022 General Election

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,834
18,836
Hawa jamaa wa Raila ni wajinga kwelikweli, eti team ya Ruto wali hack matokeo?

Ni uongo kwa sababu hizi

Matokeo yote kutoka vituo vya kupigia kura ambayo yanajazwa kwenye fomu ziitwazo fomu 34A yote yalisainiwa na mawakala wa kila upande kabla ya kuwekwa kwenye mtandao wa IEBC

Kisha hizo fomu original za vituoni yaani hizo 34A zilijumliswa kupata matokeo ya jumla ya jimboni, na mawakala wa pande zote wakiwepo pia, matokeo ya jumla ya vituoni yanajazwa kwenye fomu nyingine inayoitwa 34B na kusainiwa na mawakala wa pande zote

Hizo fomu 34B zinapelekwa makao makuu ya kuhesabu, yaani Bomas na kuhakikiwa na Tume na mawakala wa pande zote pia

Katika kuhakiki fomu za 34B ni lazima majumuisho yake yafanane na matokeo yaliyoandikwa kwenye fomu 34A ambazo zilipakiwa mtandaoni na kila mtu kuziona na pia lazima zifanane na fomu original za 34A ambazo maafisa wa tume kutoka majimboni wanakua nazo

Baada ya uhakiki huu ambao ndio umechukua muda mrefu, fomu zilizohakikiwa za 34B nazo huwekwa mtandaoni

Sasa ili mtu achakachue matokeo inabidi a hack mtandao wa IEBC na kubadilisha zile fomu za 34A zilizopo na public ilishaziona na kisha kubadili pia zile fomu original za 34A ambazo maafisa wa tume wapo nazo na kubadili pia zile hesabu za kwenye fomu 34B ambazo zni mjumuisho wa matokeo ya kwenye fomu 34A na zilishainiwa na mawakala wa pande zote

Sasa mpinzani atakuwa vipi na nguvu za kufanya hayo yote?

Hata serikali yenyewe haiwezi kuchakachua sababu waki hack server na kubadilisha matokeo ya fomu 34A tayari wapinzani watajua sababu matokeo wanayo, yaliwekwa public mara tu zoezi la kupiga kura lilipo isha
 
Wameongea kishabiki tu sababu wana mrengo wa kisiasa.

Sasa pale wametoa sababu gani ya maana? Wangeelezea kwa kina kuwa kuna nini kimefanyika
Kama umesikiliza vizuri wamesema hawako tayari kusema chochote mpaka wakati muafaka.
Kumbuka huyu ni makamu mwenyekiti na makamishina wenzie watatu huku mwenyekiti Chibukati akibaki na makmishina wawili tu.
 
Hawa waliteuliwa ba Uhuru mwaka 2021 kumzuia Ruto , ila ndio imetoka mzee
Ushawahi kuona wapi Serikali inaibiwa kura?

IMG_20220815_192254.jpg
 
Tume ya uchaguzi kugawanyika siyo jambo jepesi kama unavyofikiria ya mwaka 2017 yanaweza jirudia.
Twaweza kusema lolote kuhusu tume kugawanyika. Tusisahau kuwa tume iliruhusi vyombo vya habari kufanya tallying kutoka matokeo yaliyobandikwa ktk vituo vya kupigia kura. Ile tallying ya TV zote ilionyesha Ruto aliongoza. Tofauti ilikuwa kwa idadi ya vituo vilivyoingia ktk kila chombo cha habari, TV nk. Sasa matokeo ya tume ni sawia na tallying ya vyombo vya habari. Raila na hao wa tume wanaomsapoti wana hoja gani?
 
Tume ya uchaguzi kugawanyika siyo jambo jepesi kama unavyofikiria ya mwaka 2017 yanaweza jirudia.
Mkuu labda ulikuwa hufuatilii uchaguzi na mchakato mzima ulivyokuwa, yaani kila kitu kilikuwa wazi na mshindi alikuwa anafahamika tangia tarehe 10, sababu kila kitu kilikuwa wazi, ngoja wafungue kesi halafu uone, hawana hoja yoyote,
 
Wewe ni staff wa IEBC?

Kama siyo, basi kaa kwa kutulia

Back
Top Bottom