Madai ya muda (EoT) kwa Tanroads yanayoongeza gharama za mradi na ucheleweshaji– Ripoti ya CAG

winnerian

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
335
530
Madai ya muda kwa Tanroads yanayoongeza gharama za mradi, ucheleweshaji– Ripoti ya CAG

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wakandarasi na washauri walikuwa na madai ya TZS 1.03 trilioni hadi Novemba 2019 kutokana na kuchelewa kulipwa hati za malipo ya muda.

“Ilibainika kuwa madai hayo yalisababishwa na kutotolewa kwa fedha na Wizara ya Fedha na Mipango; ambayo hatimaye ilizuia Tanroads kuwalipa wakandarasi kwa wakati na hivyo kusababisha kuzorota kwa maendeleo ya kazi pamoja na kupanda kwa gharama za mradi kutokana na tozo za riba,” inasomeka sehemu ya ripoti hiyo.

“Aidha, nina wasiwasi kuwa kutolipwa kwa wakati kwa madai ya wakandarasi na washauri kunaweza kuongeza kiasi cha deni kutokana na tozo za riba jambo ambalo linaweza kufanya miradi husika kukwama au kutokamilika hivyo kuwanyima wananchi manufaa yaliyokusudiwa ya miradi hiyo,” alibainisha CAG.

Muunganiko wa kandarasi na zabuni.
Serikali tunaishauri izingatie sana kulipa madeni yenye riba kwani kwa kufanya hivyo itajiondoa kwenye mzigo wa kulipa madeni ambayo haya tija kwenye miradi yake wala wananchi wake
 
Serikali imeanzisha miradi mingi sana ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali...na ulipaji wake unakuwa mgumu sana mpaka inasababisha miradi mingine kuwa na mwendo mdogo kuliko wa kobe na kuongezeka gharama za mradi kutokana na huo ucheleweshaji wa malipo kwa wakandarasi na wahandisi wasimamizi.
 
Serikali imeanzisha miradi mingi sana ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali...na ulipaji wake unakuwa mgumu sana mpaka inasababisha miradi mingine kuwa na mwendo mdogo kuliko wa kobe na kuongezeka gharama za mradi kutokana na huo ucheleweshaji wa malipo kwa wakandarasi na wahandisi wasimamizi.
Sababu kubwa ya haya yote ni kuwa a Taifa lenye siasa kwenye kila idara muhimu ya serikali. Yaani bila siasa haya yote yangepata dawa na kuishi au kupungua kabisa
 
Back
Top Bottom