Madai ya kuwa Polisi ni waonevu Yasipuuzwe, tukio la Hamza lituunganishe zaidi kuliko kutugawa

Ni muhimu zaidi kwani wananchi sasa wameamini kuwa Hamza amekufa na Siri moyoni


Ni kweli.

Unajua tukio la Hamza ni Ambush, na siku zote Ambush haina mbabe, yeyote anapasuka asipokuwa na bahati.

Kama nilivyosema, hapakuwa na mawasiliano baina ya Askari. Hivyo haikujulikana Kama wanamshambulia Hamza ili wamkamate au ili wamuue au vyovyote vile.
 
Hakuna ulijualo. Zingatia kuna hii kitu 'random shooting' yani hapa mapigo ya silaha huwa hayazingatii kulinganisha vilengeo hiki ndicho kilichokuwa kinafanywa na wale polisi wetu ile juzi na hapo hata uwapeleke hao unaowaita jwtz wanakosa 'tageti', hii inasababishwa na mazingira magumu ya kimapigano pia kulinda uhai.Elewa hiyo mzee kwenye mazingira tuli umpe askari hizo risasi usemazo hakuna atakayekosa.!
Hujaelewa nilivosema landam sijasema kupiga risasi nimemanisha kuwa kuwa beba askari bila kupanga kwamba tutamchukua fulani Leo,,,, Pole sana
 
Kwa mada yako si sahihi kumtuhumu Hamza kwa alichofanya bila kuchunguza sababu ya kufanya vile, ikipatikana sababu itasaidia kuzuia matukio kama hayo, na hasa kama alidhulumiwa basi jeshi litaangalia namna ya kupunguza dhuluma kwa watu!
 
Kudhulumiwa madini sio kweli. Kuna video kasikika akisema yuko tayari kufa kumtetea Allah na wako vijana wengi wa kiislamu kutekekeza hilo. Kwamba ndugu zake waislamu wanafungwa na kuonewa na polisi. Hii ni 'excuse' ya magaidi wengi.
Bongo movie wamefeli sinema nyingi lakini tujiulize wale magaidi wa Chadema ambao intelijensia iliwabaini. Intelijensia hiyohiyo imeshindwaje kumgundua gaidi wa CCM mpaka akatuulia askari wetu? Je kwanini hakuua raia au hakwenda kuua watu kanisani kama mtuma hoja unaamini hiyo video?
Je kwanini isiundwe tume huru kuchunguza tukio hili badala ya kutoa hukumu za ramli! (Maana yawezekana alidhulumiwa au yawezekana aliamua kuwa gaidi dhidi ya polisi!) Je kwanini alienda Selender badala ya sehemu nyingine gaidi huyo? Je kwanini hakushambulia magari yaliyokuwa yakipita na baadhi akionekana kuyaongoza? Je afya yake ya akili ni timamu? Je kesi ya Zombe haitoshi kuonesha katika idara hiyo nyeti kuna "majambazi?" Kuna mengi ya kujiuliza na kujifunza katika hili.
Mipayuko na mihemko sidhani kama vina usaidizi wakati huu.
 
Kumekucha!!

Tukio la Hamza ni tukio Baya la kikatili na linalohuzunisha, nimezipitia clip kadha wa kadha za tukio hilo Kwa kweli zinaumiza, zinasononesha na zinatisha mno. Sitaki Kueleza jinsi saikolojia ya Hamza na Wale Askari namna walivyokuwa wanakabiliana huku kila mmoja ikifikia hatua ya kuutetea Uhai wake. Itoshe kusema tukio lile lilikuwa tukio Baya la kihalifu.

Nawapa pole wote kuanzia Familia za Polisi waliouawa, jeshi la polisi pamoja na Familia ya kijana Hamza Kwa kumpoteza mpendwa wao.

Kilichonifanya niandike hivi leo, ni baada ya kupitia maoni mbalimbali katika mitandao ya kijamii kufuatia tukio la Hamza, pia nilipata nafasi kufuatilia maoni ya Watanzania waliopo kijiweni, Kwa kweli nilishindwa kustaajabu maoni Yao. Maoni mengi ya Watanzania sijajua ni Kwa nini yanaponda Sana ndugu zetu Polisi,
Sio Mtandaoni sio mtaani, wengi wamekuwa wakiponda polisi. Ni wachache Sana waliokuwa wakilisifia jeshi letu la polisi.

Katika nadharia zilizoibuka kuhusiana na Tukio la Hamza, nadharia iliyopata nguvu Kwa watu kwenye jamii ni nadharia ya Dhulma ya Madini aliyofanyiwa Hamza. Ingawaje hakuna ushahidi wa moja Kwa moja katika madai ya nadharia hiyo lakini watu wengi wamesikitishwa na taarifa hiyo ambayo bado haijathibitishwa.

Kwa nini nadharia hiyo imepata nguvu zaidi kuliko nadharia zingine?
Kwa nini isiwe nadharia ya kusema mshikaji alikuwa Gaidi?
Au alikuwa jambazi?
Au alikuwa kichaaa??

Nafikiri majibu ya maswali hayo mengi yalishajibiwa; tukio linakosa sifa ya Ugaidi Kwa sababu Mshikaji hakushambulia Raia, na pia hakutumia nguvu kubwa kujihami. Muda mwingi alikuwa amejiachia uchi pasipo kujali kuwa atapigwa Risasi.

Sio tukio la ujambazi Kwa sababu Mshikaji ukimtazama katika utekelezaji wa shambulizi lake, hakuna dhamira yoyote aliyoionyesha ya kutaka kupora Mali yoyote..
Mshikaji Hakuwa chizi wala kichaa kwani tukio akiwa analitekeleza alionekana kuwa na utulivu zaidi kuliko polisi, Hakuwa na papara, shabaha yake ilikuwa ni polisi pekee, hakuonyesha kuchanganyikiwa licha ya milio mingi ya RISASI iliyokuwa ikimfuata. Hamza kusema ni kichaa au chizi haitaingia akilini Kwa wengi kutokana na umahiri wake wa kutumia silaha.

Alichokosa Hamza ni mipango katika utekelezaji wake. Yaani tukio lile anaonekana Hakuwa amejipanga Kwa siku kadhaa nyuma. Laiti angekuwa amejipanga walau siku tatu nyuma ni hakika matokeo yangekuwa mengine. Tukio lililotokea linaonyesha Hamza Hakuwa amejipanga vyema kilichomsaidia ni kujua vyema matumizi ya silaha lakini Hakuwa amejipanga kutekeleza Kwa ufanisi tukio lile.

Kwa upande wa Askari wetu wanaotulinda;
Tukio hili Askari wetu mnapaswa mjitathmini, nafikiri mnaelewa nazungumzia Jambo gani.

Tukio limetokea mapema kabisa muda wa kazi ingawaje Kwa Askari muda wote ni WA KAZI.
Tukio kutokea Mchana kuna Advantage nyingi kuliko kutokea usiku. Kumaanisha Pambano hili lilikuwa linawapa nafasi nzuri Askari wetu kushinda mapema zaidi isiyozidi dakika 10 kumuangamiza Adui.
Kama nilivyosema Hamza Hakuwa amejipanga na Kama angekuwa amejipanga asingefanya tukio hilo majira Yale, kwani majira Yale yasingemsapoti ukilinganisha na majira ya Jioni ya saa moja, usiku au alfajiri na mapema.

Tukio lolote la namna Ile linalofanyika mida kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 11 jioni linawa-favour zaidi Askari kuliko maadui, hasa adui akiwa mmoja.

Askari wetu mbali na kufanikiwa kudhibiti tukio like la kutisha, lakini walionyesha mapungufu kadhaa katika utekelezaji wao;
Miongoni mwa mapungufu;
1. Hawakuwa na mawasiliano.
Katika kushambulia mawalisiliani kitu muhimu mno. Askari wetu mashambulizi yak Kwa kweli yanatafakarisha mno. Walikuwa wakishambulia hovyo hovyo pasipo weledi. Walikuwa wakipiga piga risasi bila shabaha.
Madhara ya kutokuwa na mawasiliano ni kufanya tukio kuchukua muda mrefu, lakini piah wangeweza kudhuriana Kama sio kupiga wasiohusika.

2. Kutokuwa na Shabaha
Upungufu mwingine ni Askari wetu kutokuwa na Shabaha, adui alikuwa Yu uchi kabisa, mara kadhaa alikuwa hajajificha na anatembea Kwa tambo. Kutokuwa na Shabaha kumesababisha madhara mengi mathalani;
2.1. Tukio kuchukua muda mrefu
2.2. Kupoteza Risasi nyingi
2.3. Kumuua Mhalifu wakati Kwa watu wenye Shabaha Mhalifu asingeuawa, angepigwa Risasi ya Bega, kisha apigwe ya mguuni mchezo kwisha.
Usijeniambia ni nasema kirahisi, najua ni kazi na ndio maana mmeenda kusomea na mnalipwa Kwa kazi hizo.

3. Namna Mzunguko wa kumshambulia Hamza ulivyoundwa.
Mzunguko ule Kwa kweli unaupungufu mkubwa. Askari wetu walikuwa upande huu na upande huu kisha walikuwa wakishambulia pasipo mawasiliano, yaani walimuweka mtu Kati Hamza, kisha walikuwa wakipiga Risasi. Kwa kweli Kwa kukosa Kule Shabaha ule mzungumko waliouunda haukuwa rafiki Sana kwani wangeweza kuuana Askari Kwa Askari.

4. Ushambuliaji
Askari wetu walikuwa wakishambulia hovyo hovyo pasipo kupeana nafasi, hii ni kutokana na kutokuwa na mawasiliano.

Kwa wachukua video sitazungumzia lolote.

Nikirejea kwenye maoni ya watu kuhusiana na Tukio hili;
Masaa machache kabla Hamza hajafahamika watu wengi walikuwa upande wa Polisi na kuwapongeza na kuwapa pole Kwa kazi nzuri waliyoifanya kwani waliamini Mhalifu Yule alikuwa Gaidi. wachache waliponda Askari Kwa kuona wamechukua muda mrefu na kumuua mhalifu pasipo kumkamata mzima mzima.

Baadaye baada ya Mhalifu kufahamika, na nadharia ya kudhulumiwa Madini yake kuzuka, watu wengi waliingiwa na hisia za chuki dhidi ya polisi. Wengi iwe Kwa uzoefu wao binafsi au Kwa kuona Kwa watu wengine wanaliona jeshi la polisi Kama linauonevu na dhulma Kwa wananchi wao.

Tukiwa Kama Watanzania, watu wa nchi moja. Hatupaswi kuyaona mambo haya yanaendelea pasipo kuyafanyia kazi.

Polisi Kama binadamu wanamazuri na mabaya Yao. Mazuri Yao yanasababu Kama ilivyo Kwa mabaya.
Dhulma ya polisi ichunguzwe inatokana na nini, Hata hivyo ipo dhana kwenye jamii kuwa polisi wetu wanapenda Rushwa, pengine sababu ni suala la mishahara yao kuwa kidogo ingawaje siijui.

Hii dhana inayoendelea kuhusiana na Askari wetu tuitafutie ufumbuzi mapema. Polisi ni Watanzania wenzetu, siwezi kuwasema Kwa ubaya Kwa vile sijui yanayowakuta,
Nafikiri hata wanaowasema vibaya hawajui yanayowakuta, pengine kabla hujawasema vibaya polisi ingefaa ukawe polisi hata Kwa miezi sita ili ujue nini kiwapatacho huko.

Hata hivyo hiyo sio sababu ya polisi kujitetea ati waonee na kuwadhulumu watu wanaowalipa mishahara.

Niliwahi kuandika wakati Fulani, kazi zote zinaweza kuwa nzuri ikiwa mfanyaji atajitenga na Dhulma, unyanyasaji na uonevu lakini kazi yoyote inayokufanya udhulumu, unyanyase na kuonea wengine basi kazi hiyo ni laana sio kwako tuu hata Kwa kizazi chako.

Wito wangu:
Polisi na Askari wetu, jitahidini kutenda haki, msidhulumu, wala msionee wala kunyanyasa watu. Toshekeni na mishahara yenu Kama alivyosema Yesu Kristo.

Na Sisi Wananchi, tujitahidi Kushika sheria na kutenda wajibu wetu pasipo kuwakwaza hawa ndugu zetu Katika majukumu Yao.
Tusikwazane, tusiwe mzigo Kwa wengine. Tusiwe mtego Kwa wengine kufanya Maovu.

Ni Yule;
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Maneno yako ni sahihi.
Jamaa alitembea kutoka salender Bridge mpaka akafika pale ubalozi wa Ufaransa karibu nusu saa.
Hakuna defender ya polisi ilofika wala makamanda. ijapokuwa makao makuu yapo karibu sana..
Gari lapolisi lilifika bada mtuhumiwa kuuliwa.
Kuna askari alikwenda kumpokonya bunduki na baada ya kumpokonya akamuengeza marisasi. kwanini.?
Ikiwa kafika karibu na kumpokonya silaha kwanini asimkalie juu yake na kumdhibiti.
Risasi nyingi alipigwa baada ya kuangukua au kupigwa. kama kesha pigwa kwa nini wakamuengeza marisasi.?

Kuna gari la maji ya kuwasha lingeweza kumdhibiti.
Hakuna hata mazungumzo baina yule jamaa na polisi kumwambia weka silaha chini au kitu chochote. Hakuna hata kipaaza sauti kilichotumika

Kuna masuali mengi na ukweli ukiangalia video utaona risasi zinavyolega mbali kabisa.

Tunatumai ukweli utatoka.
Ilo baki sasa polisi wanejenga hoja kuwa ni gaidi na anapaswa kuuuliwa kuficha walofanya.
 
Mkuu andiko lako tunaweza sema ni ‘Case Study’ kama kuna wahusika wanapita hapa wachukue haya madini maana ume balance story yako kati ya jamii na walinda amani wetu
IGP ameshahukumu mjadala umefungwa wazazi tuchunge watoto wetu
 
Maneno yako ni sahihi.
Jamaa alitembea kutoka salender Bridge mpaka akafika pale ubalozi wa Ufaransa karibu nusu saa.
Hakuna defender ya polisi ilofika wala makamanda. ijapokuwa makao makuu yapo karibu sana..
Gari lapolisi lilifika bada mtuhumiwa kuuliwa.
Kuna askari alikwenda kumpokonya bunduki na baada ya kumpokonya akamuengeza marisasi. kwanini.?
Ikiwa kafika karibu na kumpokonya silaha kwanini asimkalie juu yake na kumdhibiti.
Risasi nyingi alipigwa baada ya kuangukua au kupigwa. kama kesha pigwa kwa nini wakamuengeza marisasi.?

Kuna gari la maji ya kuwasha lingeweza kumdhibiti.
Hakuna hata mazungumzo baina yule jamaa na polisi kumwambia weka silaha chini au kitu chochote. Hakuna hata kipaaza sauti kilichotumika

Kuna masuali mengi na ukweli ukiangalia video utaona risasi zinavyolega mbali kabisa.

Tunatumai ukweli utatoka.
Ilo baki sasa polisi wanejenga hoja kuwa ni gaidi na anapaswa kuuuliwa kuficha walofanya.

Madai yote yatolewa ufumbuzi
 
Kutumia makalio ni kuamini cha upande mmoja ili usitumie makalio sikiliza pande zote kisha tafakari kwa nini Hamza hakuwaua Raia wa kawaida?
Hivi wale jamaa wa Kibiti waliokuwa hawauwi raia wa kawaida na badala yale wakawa wanawaua viongozi na maaskari hawakuwa magaidi? Nimesahau hivyo tukumbushane.
 
Back
Top Bottom