Madai ya kuwa Polisi ni waonevu Yasipuuzwe, tukio la Hamza lituunganishe zaidi kuliko kutugawa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,881
Kumekucha!!

Tukio la Hamza ni tukio Baya la kikatili na linalohuzunisha, nimezipitia clip kadha wa kadha za tukio hilo Kwa kweli zinaumiza, zinasononesha na zinatisha mno. Sitaki Kueleza jinsi saikolojia ya Hamza na Wale Askari namna walivyokuwa wanakabiliana huku kila mmoja ikifikia hatua ya kuutetea Uhai wake. Itoshe kusema tukio lile lilikuwa tukio Baya la kihalifu.

Nawapa pole wote kuanzia Familia za Polisi waliouawa, jeshi la polisi pamoja na Familia ya kijana Hamza Kwa kumpoteza mpendwa wao.

Kilichonifanya niandike hivi leo, ni baada ya kupitia maoni mbalimbali katika mitandao ya kijamii kufuatia tukio la Hamza, pia nilipata nafasi kufuatilia maoni ya Watanzania waliopo kijiweni, Kwa kweli nilishindwa kustaajabu maoni Yao. Maoni mengi ya Watanzania sijajua ni Kwa nini yanaponda Sana ndugu zetu Polisi,
Sio Mtandaoni sio mtaani, wengi wamekuwa wakiponda polisi. Ni wachache Sana waliokuwa wakilisifia jeshi letu la polisi.

Katika nadharia zilizoibuka kuhusiana na Tukio la Hamza, nadharia iliyopata nguvu Kwa watu kwenye jamii ni nadharia ya Dhulma ya Madini aliyofanyiwa Hamza. Ingawaje hakuna ushahidi wa moja Kwa moja katika madai ya nadharia hiyo lakini watu wengi wamesikitishwa na taarifa hiyo ambayo bado haijathibitishwa.

Kwa nini nadharia hiyo imepata nguvu zaidi kuliko nadharia zingine?
Kwa nini isiwe nadharia ya kusema mshikaji alikuwa Gaidi?
Au alikuwa jambazi?
Au alikuwa kichaaa??

Nafikiri majibu ya maswali hayo mengi yalishajibiwa; tukio linakosa sifa ya Ugaidi Kwa sababu Mshikaji hakushambulia Raia, na pia hakutumia nguvu kubwa kujihami. Muda mwingi alikuwa amejiachia uchi pasipo kujali kuwa atapigwa Risasi.

Sio tukio la ujambazi Kwa sababu Mshikaji ukimtazama katika utekelezaji wa shambulizi lake, hakuna dhamira yoyote aliyoionyesha ya kutaka kupora Mali yoyote..
Mshikaji Hakuwa chizi wala kichaa kwani tukio akiwa analitekeleza alionekana kuwa na utulivu zaidi kuliko polisi, Hakuwa na papara, shabaha yake ilikuwa ni polisi pekee, hakuonyesha kuchanganyikiwa licha ya milio mingi ya RISASI iliyokuwa ikimfuata. Hamza kusema ni kichaa au chizi haitaingia akilini Kwa wengi kutokana na umahiri wake wa kutumia silaha.

Alichokosa Hamza ni mipango katika utekelezaji wake. Yaani tukio lile anaonekana Hakuwa amejipanga Kwa siku kadhaa nyuma. Laiti angekuwa amejipanga walau siku tatu nyuma ni hakika matokeo yangekuwa mengine. Tukio lililotokea linaonyesha Hamza Hakuwa amejipanga vyema kilichomsaidia ni kujua vyema matumizi ya silaha lakini Hakuwa amejipanga kutekeleza Kwa ufanisi tukio lile.

Kwa upande wa Askari wetu wanaotulinda;
Tukio hili Askari wetu mnapaswa mjitathmini, nafikiri mnaelewa nazungumzia Jambo gani.

Tukio limetokea mapema kabisa muda wa kazi ingawaje Kwa Askari muda wote ni WA KAZI.
Tukio kutokea Mchana kuna Advantage nyingi kuliko kutokea usiku. Kumaanisha Pambano hili lilikuwa linawapa nafasi nzuri Askari wetu kushinda mapema zaidi isiyozidi dakika 10 kumuangamiza Adui.
Kama nilivyosema Hamza Hakuwa amejipanga na Kama angekuwa amejipanga asingefanya tukio hilo majira Yale, kwani majira Yale yasingemsapoti ukilinganisha na majira ya Jioni ya saa moja, usiku au alfajiri na mapema.

Tukio lolote la namna Ile linalofanyika mida kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 11 jioni linawa-favour zaidi Askari kuliko maadui, hasa adui akiwa mmoja.

Askari wetu mbali na kufanikiwa kudhibiti tukio like la kutisha, lakini walionyesha mapungufu kadhaa katika utekelezaji wao;
Miongoni mwa mapungufu;
1. Hawakuwa na mawasiliano.
Katika kushambulia mawalisiliani kitu muhimu mno. Askari wetu mashambulizi yak Kwa kweli yanatafakarisha mno. Walikuwa wakishambulia hovyo hovyo pasipo weledi. Walikuwa wakipiga piga risasi bila shabaha.
Madhara ya kutokuwa na mawasiliano ni kufanya tukio kuchukua muda mrefu, lakini piah wangeweza kudhuriana Kama sio kupiga wasiohusika.

2. Kutokuwa na Shabaha
Upungufu mwingine ni Askari wetu kutokuwa na Shabaha, adui alikuwa Yu uchi kabisa, mara kadhaa alikuwa hajajificha na anatembea Kwa tambo. Kutokuwa na Shabaha kumesababisha madhara mengi mathalani;
2.1. Tukio kuchukua muda mrefu
2.2. Kupoteza Risasi nyingi
2.3. Kumuua Mhalifu wakati Kwa watu wenye Shabaha Mhalifu asingeuawa, angepigwa Risasi ya Bega, kisha apigwe ya mguuni mchezo kwisha.
Usijeniambia ni nasema kirahisi, najua ni kazi na ndio maana mmeenda kusomea na mnalipwa Kwa kazi hizo.

3. Namna Mzunguko wa kumshambulia Hamza ulivyoundwa.
Mzunguko ule Kwa kweli unaupungufu mkubwa. Askari wetu walikuwa upande huu na upande huu kisha walikuwa wakishambulia pasipo mawasiliano, yaani walimuweka mtu Kati Hamza, kisha walikuwa wakipiga Risasi. Kwa kweli Kwa kukosa Kule Shabaha ule mzungumko waliouunda haukuwa rafiki Sana kwani wangeweza kuuana Askari Kwa Askari.

4. Ushambuliaji
Askari wetu walikuwa wakishambulia hovyo hovyo pasipo kupeana nafasi, hii ni kutokana na kutokuwa na mawasiliano.

Kwa wachukua video sitazungumzia lolote.

Nikirejea kwenye maoni ya watu kuhusiana na Tukio hili;
Masaa machache kabla Hamza hajafahamika watu wengi walikuwa upande wa Polisi na kuwapongeza na kuwapa pole Kwa kazi nzuri waliyoifanya kwani waliamini Mhalifu Yule alikuwa Gaidi. wachache waliponda Askari Kwa kuona wamechukua muda mrefu na kumuua mhalifu pasipo kumkamata mzima mzima.

Baadaye baada ya Mhalifu kufahamika, na nadharia ya kudhulumiwa Madini yake kuzuka, watu wengi waliingiwa na hisia za chuki dhidi ya polisi. Wengi iwe Kwa uzoefu wao binafsi au Kwa kuona Kwa watu wengine wanaliona jeshi la polisi Kama linauonevu na dhulma Kwa wananchi wao.

Tukiwa Kama Watanzania, watu wa nchi moja. Hatupaswi kuyaona mambo haya yanaendelea pasipo kuyafanyia kazi.

Polisi Kama binadamu wanamazuri na mabaya Yao. Mazuri Yao yanasababu Kama ilivyo Kwa mabaya.
Dhulma ya polisi ichunguzwe inatokana na nini, Hata hivyo ipo dhana kwenye jamii kuwa polisi wetu wanapenda Rushwa, pengine sababu ni suala la mishahara yao kuwa kidogo ingawaje siijui.

Hii dhana inayoendelea kuhusiana na Askari wetu tuitafutie ufumbuzi mapema. Polisi ni Watanzania wenzetu, siwezi kuwasema Kwa ubaya Kwa vile sijui yanayowakuta,
Nafikiri hata wanaowasema vibaya hawajui yanayowakuta, pengine kabla hujawasema vibaya polisi ingefaa ukawe polisi hata Kwa miezi sita ili ujue nini kiwapatacho huko.

Hata hivyo hiyo sio sababu ya polisi kujitetea ati waonee na kuwadhulumu watu wanaowalipa mishahara.

Niliwahi kuandika wakati Fulani, kazi zote zinaweza kuwa nzuri ikiwa mfanyaji atajitenga na Dhulma, unyanyasaji na uonevu lakini kazi yoyote inayokufanya udhulumu, unyanyase na kuonea wengine basi kazi hiyo ni laana sio kwako tuu hata Kwa kizazi chako.

Wito wangu:
Polisi na Askari wetu, jitahidini kutenda haki, msidhulumu, wala msionee wala kunyanyasa watu. Toshekeni na mishahara yenu Kama alivyosema Yesu Kristo.

Na Sisi Wananchi, tujitahidi Kushika sheria na kutenda wajibu wetu pasipo kuwakwaza hawa ndugu zetu Katika majukumu Yao.
Tusikwazane, tusiwe mzigo Kwa wengine. Tusiwe mtego Kwa wengine kufanya Maovu.

Ni Yule;
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Siasa za ugaidi tena zile za katiba zimeishia wapi ,hamnaga la maana nyie wanachadema akili za kuku

USSR
 
we nawe muda wote unawaza siasa zenu za ovyoovyo,wenzio wanatoa ushauri mzuri kwa jeshi letu
Aisha, acheni ugaidi hii dini yenu sijui ina tatizo gani. Anzeni nyie kufundishana elimubya dunia huko maskulini na achaneni na elimubya ahera inayofundisha kuua watu!
anzeni nyie pia sio kutegemea wengine vinginevyo mmekusudia kuua kwa kivuli cha allah
 
Aisha, acheni ugaidi hii dini yenu sijui ina tatizo gani. Anzeni nyie kufundishana elimubya dunia huko maskulini na achaneni na elimubya ahera inayofundisha kuua watu!
anzeni nyie pia sio kutegemea wengine vinginevyo mmekusudia kuua kwa kivuli cha allah


Mkuu Mimi sio Muislam lakini siungani na maoni yako.
 
Sirro ajue kabisa vijana wake bado mafunzo na pengine hii inatokana na kuwa matukio kama haya hayajawahi kutokea ila wajipange na wapewe elimu, hili tukio limewaweka wazi sana
Umesema vyema Sana wasipobadilika matukio Kama haya yatakuwa yakijirudia waache uonevu kwa wananchi sikuzote mwisho wa manunguniko na mateso Ni hasira Kali juu yao na kutokea kwa maafa ya kusikitisha.
 
Hili tukio limedhalilisha jeshi la police kwa asilimia kubwa,majirani zetu walituogopa hasa nyakati za mwalimu nyerere nadhani sasa ni wakati maalumu kubadilisha mtindo wa mafunzo uendane na mbinu zakidunia ,haya mambo yakuvunja matofali kwa mkono au kubebana sarakasi n.k,hayatasaidia lazma tutumie technologia inayotumia akili na sio mijinguvu ,tulitamba katika vita vya chini chini ila kwasasa hatuendani na wakati,jeshi letu limejipanga kudhibiti raia ila wakina hamza wapo lazma mikakati thabiti iwepo ni lazma jeshi liwe linafanya maboresho kama kuongeza ujuzi na mafunzo katika nchi nyingine,matumi bora ya Tehama,Drones,nucleus,snipers,bila kusahau Akili
 
Tabia za polisi kwa raia ndio zinawanyima legitimacy ya kueleza yale ya upande wao na kusikilizwa, pamekuwepo na malalamiko ya kudumu toka kila kona ya nchi juu ya madhila polisi wanayoyafanyia raia wasio na hatia, kuchelewesha kesi makusudi ili wapewe rushwa, kubambikia kesi ni baadhi tu, hata Rais kwa ile hotuba yake juzi ni ushahidi tosha.
 
Hili tukio limedhalilisha jeshi la police kwa asilimia kubwa,majirani zetu walituogopa hasa nyakati za mwalimu nyerere nadhani sasa ni wakati maalumu kubadilisha mtindo wa mafunzo uendane na mbinu zakidunia ,haya mambo yakuvunja matofali kwa mkono au kubebana sarakasi n.k,hayatasaidia lazma tutumie technologia inayotumia akili na sio mijinguvu ,tulitamba katika vita vya chini chini ila kwasasa hatuendani na wakati,jeshi letu limejipanga kudhibiti raia ila wakina hamza wapo lazma mikakati thabiti iwepo ni lazma jeshi liwe linafanya maboresho kama kuongeza ujuzi na mafunzo katika nchi nyingine,matumi bora ya Tehama,Drones,nucleus,snipers,bila kusahau Akili


Upo sahihi Mkuu
 
Back
Top Bottom